Sakata la Makonda limeonyesha wengi wetu hatupo tayari kwa utawala wa kisheria

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nawasalimu kwa jina chama pendwa, CCM.

Leo nami natumia haki yangu ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba ya JMT. Tangu jana mitandaoni suala kubwa lililoibuka ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar Ndugu Makonda kudai kuna vitisho dhidi ya maisha yake. Watu wengi sana wameongelea kuhusu Makonda kiasi kwamba hadi wale waliokuwa wakimuita LE COMMANDANT FIELD MARSHALL wametoa maoni hasi kabisa. Usaliti wao kwa le commandant Paul Makonda ni zaidi ya ule wa Yuda kwa kristo. Binafsi nasikitika kuona kwamba awamu iliyopita ilizalisha wanafiki wengi mno.... watu maarufu waliokuwa karibu sana na Makonda leo hii ndo wamekuwa wa kwanza kumsema vibaya mitandaoni. Hili ni janga kubwa la kitaifa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba ukisoma maoni ya wengi ni kwamba watanzania wengi hawajali kabisa utawala wa sheria (rule of law). Maoni mengi yanaonyesha watu wako tayari kuona Makonda akichukuliwa sheria mkononi bila kupitia mahakamani. Hili ni jambo la kusikitisha mno. Kama wananchi wengi tumekuwa tukilaumu viongozi kutofuata sheria basi na sisi tujitazame kama kweli nafsini mwetu tuna nia ya dhati kabisa kwenye kufuata sheria? Au tunataka sheria ifuatwe na Mama Samia tu huku sisi wakati mwingine tukichoma moto wasiokuwa na hatia kwa kisingizio cha wizi??

Sikatai kwamba Makonda ana tuhuma ambazo zina ushahidi mwingi na anastahili kuadhibiwa. Ila tukisema tunalipiza kisasi nje ya mahakama tutakuwa tu sawa na yeye na automatically tutakuwa wahalifu wapya. Kuna mataifa ya Africa tangu uhuru wao ni kupinduana tu madarakani kwasababu tu pale mwanzoni walikosea kwa kutotafuta maridhiano mapema huku nchi ikiendeshwa bila kujali katiba na sheria.

Mimi nadhani tuige mfano kwa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia ambaye anawanyoosha washenzi wa utawala uliopita kimyakimya kupitia mahakama. Ikumbukwe utawala uliopita wa Zambia chini ya Rais Edgar Lungu ulikuwa wa mkono wa chuma kama ilivyokuwa hapa kwetu. Makada wa chama tawala cha PF walikuwa na nguvu kuliko hata polisi wakati fulani. Hata Rais Hichilema alionja joto ya jiwe kwa kupewa kesi ya uhaini huku ikiambatana na mateso huko mahabusu kwa zaidi ya miezi mitatu. Hapo pichani ni aliyekuwa waziri wa kilimo Mh. Michael Katambo akiwa kapiga magoti wakati akiongea na Rais Edgar Lungu. Rais HH alivyoingia madarakani alitangaza ni mwanzo mpya na hakutakuwa na haja ya kulipizana visasi. Ila wajanja wanaona HH kupitia mahakama na vyombo vya dola akikamata washenzi mmoja baada ya mwingine na kuwapa kesi. Mimi naona yuko smart sana.

Nahitimisha kwa kuisihi serikali iharakishe kumpeleka Bashite mahakamani ili kuepusha mabaya yanayoweza kumtokea kwa jinsi wananchi walivyoonyesha kukasirishwa.

IMG_20220413_190039.jpg
 
View attachment 2186339
Sisi kufuata sheria na kutofuata sheria inategemea ni nani yaliyomkuta 🤣

Mahakama ikimhukumu mtu ambaye anapendwa utaskia haikutenda haki hiyo hiyo mahakama ikimhukumu mtu ambaye hapendwi utaskia sasa huyu hakimu ni wa ukweli hayumbishwi.

Kuhusu makonda wakitaka kumshughulikia hawakosi pa kuanzia lazima kuna madudu yake tu ya upigaji wanayoweza kutumia.
 
Tatizo ni kubwa. Hata mtaani mtu kasingiziwa mwizi tayari kauawawa.
 
Back
Top Bottom