Sakata la Martin Saanya na Nguvu za Wachambuzi Wa Soka Bongo

Sakata la Martin Saanya na Nguvu za Wachambuzi Wa Soka Bongo

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Iwapo Kamati ya Maamuzi Ingekaa mara tu baada Ya Dk 90 za mtanange Wa Simba na Geita, huyu Refarii Uwezekano mkubwa Asingepona kufungiwa. Martin Saanya Sasa ni Kama amesafishwa na Upepo umebadilika.

Kwamba alitoa maamuzi sahihi. Faulo ya Geita halali.!

Japo Wachambuzi wengi Wanaitwa Wachambuzi 'Uchwara' na Wakati mwingine Wameitwa takataka..!

Nguvu Ya Wachambuzi imeoneonekana kwenye kipute hicho, Wamepindua Upepo na Refa huyu anaweza Kuonekana heroes huku Wengine wakionekana Wanadandia taaluma zisizo wahusu ambazo hawana Utaalamu nazo.

Ndo hivyo tu... Kamati zinazohusika zitoe ufafanuzi Mapema kabla Watu hawajatiana Vidole vya Macho.
 
Lile ni goli halali na Simba ili bebwa na ni kawaida kwa mpira wa Bongo. Leo Simba kesho Yanga. Hakuna mpira unaochezwa bila kugusana Ila Kapombe kajiongeza.
 
Lile ni goli halali kwa maana halisi ya neno hilo. Mpira wa miguu ni mchezo wa kugusana na hakuna mchezaji hapo anayecheza na mama mkwe wake uwanjani, watu waache ushabik wa kijinga.

Mapungufu yoyote ya waamuzi ktk ligi hii kwenye mechi zinazohusu Yanga na Simba dhidi ya timu zingine lazima yazinufaishe tu hizo timu mbili na sio kinyume chake.

Mpira wa nchi hii utaendelea kurudi kinyume nyume kama treni ya Godegode.
 
Kinachozungumzwa hapo ni Kugusana Kikawaida na Kugusana Kusiko Kawaida....!
Kiswahili acha kabisa..!
Kosa ambalo Sanya alitoa adhabu kwa Geita ni George kumsukuma Kapombe. sio kumgusa Kapombe. George amekuja kukiri kuwa alimsukuma 'kidogo', sio sana. Wanaotazama clip wanadai hakumsukuma wala hakumgusa kabisa. Sasa tumuamini nani, wanaoangalia clip, George au Sanya?
 
Back
Top Bottom