Elections 2010 Sakata la mauaji ya Dereva wa CCM Maswa na hatima ya Shibuda

Duh!Habari hii inatisha!tunashukuru kwa taarifa!
 
Ndugu naona na wewe uko kwenye kampeni jinsi ulivyo present habari yako imekaa kishabiki kwa kuchukuwa upande mmoja tu wa maoni yaani shibuda -- kwa kuwa umewahi kuendesha vipindi vya televisheni haswa vya kukalisha wagombea na wanasiasa mbalimbali nilidhani unauzoefu wa kuchukuwa habari na maoni pande zote mbili -- umechukuwa moja ukaja kuweka hapa
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa. Ngoja tusubiri ya mtaa wa pili pia kwani sisi ni waungwana labda tuchokozwe!
 

Heshima kwako Pasco,

Mkuu napenda kusoma mabandiko yako huko balanced sana.

Ukiona hivyo ujue CCM maji yako shingoni hawana ustaharabu hata chembe.Inashangaza kidogo hapa Arusha Dr Batilda anapewa upendeleo wa kijinga,akimaliza mkutano anasindikiwa na msafara wa magari mengi hakuna polisi wa kumzuia,Lema akisindikizwa inakuwa nongwa.Mji wa Arusha hauna barabara za kuhimili misafara ya wagombea ubunge laiti polisi wangezuia misafara ya wagombea wote ningewaelewa.
 
Hukubali ujinga kwa kumwaga damu ya mtuuuuuuuuuuuu????

Ditopile alikuwa chama gani alipouwa? Na akawa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji kupata dhamana.....wanaweza kuwa wameua kwa utashi wao na wala sio kwa maagizo ya CHADEMA kama wewe unavyotaka kushabikia
 

Heshima kwako shy,

Mkuu soma tena na tena bandiko la Pasco halafu omba radhi.
 

hapo kwenye pink sijakusoma.
 
-- kwa kuwa umewahi kuendesha vipindi vya televisheni haswa vya kukalisha wagombea na wanasiasa mbalimbali nilidhani unauzoefu wa kuchukuwa habari na maoni pande zote mbili -- umechukuwa moja ukaja kuweka hapa

Name Calling!
 
Sijaita jina nimesema kwa kuwa aliwahi kuwa mwendeshaji wa vipindi vya televisheni alitakiwa kuwa mzoefu wa kuandika na kutoa maoni yake si ya upande mmoja kama hivyo anavyofanya ni mbaya sana - asiwe kama hassan ngeze wa rwanda aliyekuwa jela sasa hivi
 
Radhi siombi msimamo wangu ni huo aandike habari zake kwa umakini sio kwa ushabiki yeye ni mzoefu wa haswa televisheni anajua anachofanya
 
Pole kwa wafiwa, na hili liwe fundisho kwa serikali na vyombo vyake vya uhasama (usalama?)
 
Mh hii mbaya sana, sheria ichukue mkondo wake
 

another controversial statement
 

shy jamaa kasema huo ni upande mmoja wa shilingi anafatilia wa pili
 


Shy usiwe na haraka subiri bado hajaimalizia story yake soma maandiko mekundu
 
Dereva umeuwawa ni kwa ajili ya KIHEREHERE CHAKO
 
Hili ni lazima litolewe ufafanuzi wa kutosha. Nilikwisha andika na ninarudia tena kuwa CHADEMA wawe waangalifu na hujuma za kijasusi zinazofanywa na CCM dhidi yao.

Hii ni mipango ya kitaalam sana ya kijasusi ambapo wana CCM wanaotumwa kuanzisha vurugu hawajui kuwa wanatumwa kama mbuzi wa kafara. Wao wauawe, CCM ipate 'public sympathy' halafu wanachi waichukie CHADEMA na kuiona ni chama cha magwanda kinachoashiria vurugu na sasa zinathibitika.

Tangu shirika la kijasusi la nchi fulani kubwa lichukue tenda ya kusaidia JK aingie madarakani suala hili limeendelea kujitokeza na cha ajabu limetokea hata maeneo ambayo vurugu huwa si jambo la kawaida.

Hivi leo hii mimi nikute watu wako kwenye mkutano wa CCM halafu nipite katikati ya huo mkutano na mavazi ya CHADEMA au nikipepea bendera ya CHADEMA nakuwa natafuta kitu gani. Majasusi hawa wanajua kitu kinaitwa 'mob psychology'. Wanaelewa akilianzisha mmoja basi akili ya mtu mmoja inagawanyika na idadi ya mob yaani mfano 1/100,000. kisha 'fraction' hii ndio hufanya maamuzi, kupiga, kuvunja mbavu n.k.

Naona taratibu baada ya CCM kujua kwa uhakika kuwa wamepoteza uchaguzi huu, wanaanza kuleta mbinu za Burkina faso, Ivory Coast, Sierra Leone, Somalia na Sudan.

'Provoke them, let them seem dangerous to rule, destroy their public image, gain public sympathy'.

CCM hata mkiishiwa sera, tafadhali msimwage damu zetu na kusingizia CHADEMA. Hawa green guard na wengineo mlio nao wanayoyafanya ni sawa na suicide bombing.

Mfano kama green guard wangekuja kunivamia mimi, nisingekubali kupoteza maisha au afya yangu kwa kuwatazama tu, ningeweza kupiga mtu risasi ya kichwa, lakini mimi ndio ningeonekana muuaji.

Please please CCM huku mnakoenda sasa ni usengeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…