Sakata la Mauaji ya Rais wa Haiti lachukua sura mpya

Sakata la Mauaji ya Rais wa Haiti lachukua sura mpya

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Kukamatwa kwa mfanyabiashara mwenye uraia wa Haiti ambaye anaishi Florida ambaye vyombo vya usalama vinadai kwamba ni mhusika mkuu wa mauaji ya aliyekuwa raisi wa Haiti, kunazidi kuongeza maswali kwenye hili sakata ambalo tayari limeacha mawasli mengi.

Vyombo vya usalama vya Haiti vinadai kwamba mtuhumiwa anayejulikana kama Emamanuel Sanon, mwenye umri wa miaka 62, ambaye hapo kabla alionyesha nia ya kuongoza nchi ya Haiti katika video aliyoipakia kwenye mtandao wa YouTube. Hata hivyo, mwanaume huyu siyo mashuhuri katika wanasiasa wa nchini Haiti, na watu wake wa karibu wanadai kwamba mwanaume huyo ametupiwa zigo na wale wahusika halisi wa mauaji hayo ya Raisi Jovnel Moise katika shambulizi lililofanyika juma lililopita ambapo risi aliuawa na mkewe kujeruhiwa.

Rafiki mmoja wa Bwana Sanon anayeishi Florida aliliambia shirika la The Association Press kwa sharti la jina lake kutowekwa wazi kuwa, Sanon ni mchungaji wa kanisa la kilokole na ni daktari mwenye leseni huko nchini Haiti, lakini leseni yake haifanyi kazi nchini Marekani. Pia alidai kwamba, Sanon alimwambia kuwa alifuatwa na na watu waliodai wanatoka kwenye serikali ya Marekani na kitengo cha haki, ambao walimwambia kuwa wanataka kumfanya awe raisi wa Haiti.

Anasema mpango ulikuwa ni kumkamata Moise na siyo kumuua. Anasema kama Sanon angejua kuwa wanaenda kumuua Moise basi ana uhakika asingeshiriki.

"Nina uhakika juu ya hili," kilisema chanzo hicho. "Hii ilipaswa kuwa ni misheni ya kuiokoa Haiti kutoka jehanamu, kwa msaada wa serikali ya Marekani."

Pia Rev. Larry Caldwell ambaye ni mchungaji huko Florida anaunga mkono maelezo hayo. Yeye anadai kuwa amefanya kazi na Sanon katika kufungua makanisa na vituo vya afya nchini Haiti kati ya mwaka 2000 mpaka 2010. Haamini kuwa Sanon angehusika katika tukio lolote la vurugu.

"Ninajua haiba ya huyu mtu," Alisema Caldwell. "Unamkamata mtu kama huyo na kudai kwamba amehusika katika kosa la mauaji, wakati akijua kwamba kujihusisha na mauaji kutampeleka jehanamu?" .... Kama kuna mtu ambaye yuko tayari kusaidia nchi yake, basi ni Sanon."

Mkuu wa Polisi wa Haiti, Leon Charles anadai kuwa wauaji wa Moise walikuwa wanamlinda Sanon, na anadai kwamba ni Sanon aliyepanga mauaji ya raisi.

Charles anadai kwamba walipata kofia yenye nembo ya Kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya cha Marekani, maboksi 20 ya risasi, vipuri vya bunduki, namaba nne za usajili wa magari kutoka nchi ya Domicican, magari mawili na vifaa vingine katika nyumba ya Sanon iliyoko nchini Haiti.

Watu 26 waliokuwa wanajeshi wa Columbia wanakisiwa kuhusika katika mauaji hayo na 23 kati yao wameshakamatwa, pamoja na raia wa Haiti watatu. Charles anadai watuhumiwa watano bado hawajakamatwa na watatu wameuawa.

"Ni watu hatari sana," alisema. "Ninazungumzia makomando, wanajeshi wa kitengo maalum."

Wakati huo, Mkuu wa Polisi wa Colubmia, Jorge Luis Vargas, anasema kuwa Kampuni moja iliyoko Florida ijulikanayo kama CTU Security, ilitumia kadi yake ya bank kununua tiketi 19 za safari ya ndege kutoka Bagota mpaka Santo Domingo kwa ajili ya watuhumiwa 19 raia ya Columbia. Wengi wao waliwasili nchini Dominican Juni, na walisafiri kurlrkra haiti ndani ya majuma machache, alisema vergas.

Pia alisema kuwa dimitri Herard, Mkuu wa Ulinzi wa Ikulu ya Haiti, alisafiri kwa ndege mpaka Columbia, Ecuador, na Panama miezi kadhaa kabla ya mauaji hayo, na jeshi la Polisi la Columbia linachunguza kama ana ushirika wowote na hao wanajeshi wa kukodi. Huko nchini Haiti waendeshamashitaka wanampango wa kumfanyia mahojiano Herard kuhusiana na mauaji hayo.

Charles pia alisema kuwa Sanon alikuwa akifanya mawasiliano na kampuni ya CTU Security na ni kampuni hiyo iliyo watafuta na kuwaajiri wale waliofanya mauaji. Anaendelea kusema kuwa Sanon aliwasili Haiti mwezi wa Juni kwa kutumia ndege binafsi huku akiambatana na baadhi ya waliohusika na shambulio hilo.

Kazi ya mwanzo ya watuhumiwa hao ilikuwa ni kumlinda Sanon, ila baadae walipokea amri ya kumkamata raisi, alisema Charles.

"Misheni ilianzia hapo," aliongeza kuwa, watuhumiwa wengine 22 walijiunga na hilo kundi.

Charles anadai kwamba baada ya mauaji ya Moise, muaji mmoja alimpigia simu Sanon, ambaye naye aliwasiliana na watu wengine wawili ambao nao inasadikika kuwa ni kati ya waliopanga mauaji hayo. Hakutaja wasifu wa watu hao au kusema kama polisi wanawafahamu.

Rafiki yake Sanon anadai kwamba aliudhuria mkutano siku za karibuni huko FLlorida ambapo aliongozana na Sanoni na watu wengine zaidi ya 12, akiwemo Antonio Enmanuel Intrigo Valera, mhamiaji kutoka Venezuela anayeishi MIami ambaye ndiye kiongozi wa CTU Security. Anadai kwamba katika mkutano huo mpango ulionyeshwa ambao ulikuwa ukibainisha jinsi fani nchi ya Haiti itajengwa upya, ikijumuisha mfumo wa maji, kubadili takataka kuwa chanzo cha nishati na kurekebisha barabara.

Sanon aliuliza, ni kwanini wanausalama wanaomsindikiza Haiti wote wana uraia wa Columbia. Sanon alijibiwa kwamba, raia wa Haiti hawaaminiki na serikali inanuka rushwa. Anadai kwamba Sanon alimpigia simu akiwa Haiti siku kadhaa kabla ya kutokea mauaji na kumwambia kuwa hao raia wa Columbia hawaonekani wameondoka bila kumuaga.

"Nimebaki peke yangu. Hawa watu ni akina nani? Sijui ni nini wanafanya." Mtoa taarifa ananukuu alichosema Sanon.

"Sanon ni mchuzi wa kafara," aliongeza mtoa taarifa "Maskini anadhani Mungu atarekebisha kila kitu."

Sanon ameishi kwenye kitongoji cha Broward huko FLorida, na Hilsborough huko Gulf Coast. Kumbumbukumbu zinaonyesha kuwa pia ameishi mji wa Kansas, Missouri. Mwaka 2013 alitoa taarifa kuwa kafirisika na kujitambulisha kama daktari kwenye video aliyopakia YouTube akiipa jina "Uongozi kwa ajiliya Haiti."

Hata hivyo, kumbukumbu zinaonyesha kuwa Sanon hajawahi kupewa kibari cha kufanya kazi ya udaktari au shughuli nyingine yoyote na Kitengo cha Afya cha Florida.

Katika kumbukumbu za kimahakama kutoka kwenye karatasi alizopeleka mahakamani kuhusiana na kufirisikakwake mwaka 2013 huko Florida zinaonyesha kuwa alikuwa daktari na mchungaji katika Kanisa la Kilokole huko Tabarre Haiti. Pia alidai kuwa ana anamiliki taasisi na makampuni mbalimbali ikiwemo Taaisi ya Rome Haiti, ambayo aliitambulisha kama Shirika lisilo la kiserikali, kituo cha redio huko Haiti na majengo ya vituo vya afya huko Haiti na Dominican.

Wakati akitoa tamko la kufirisika kwake, yeye na mke wake walikuwa wanakipato cha $5,000 kwa mwezi, nyumba huko Brandon, Florida iliyokuwa na thamani ya kiasi cha $143,000. Baadaye ilibainika kuwa walificha kuorodhesha eneo lenye kiasi cha hekari 35 huko Haiti, ili lisijulikane kwa watu na taaisi zilizokuwa zikiwadai.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Sanon alianzisha biashara zaidi ya 12 katika kipindi cha miaka 20, ambazo zote hazikufanya vizuri.

Mwaka 2011 kwenye video ya YouTube Sanon alisikika akisema kuwa serikali ya Haiti imejaa wala rushwa, na aliwatuhumu kwa kuiba mariasili za Wanahaiti. "Hawajali kuhusu nchi, wala watu."

Pia alipotosha kuwa Haiti ina madini ya Uranium, visima vya mafuta na mariasili nyingine ambazo viongozi wa serikali wamejimilikisha.
 
Asante sana mkuu kwa kutuhabarisha maana redio zetu na television zinaonyesha udaku na mambo ya kipuuzi mda mwingi.Ila huyo rais nae angeachia madaraka mapema haya yote yasingemkuta .Kakomaa kukaa madarakani kwa mabavu watu wamempiga za mbavu so sad[emoji24][emoji24].Tuna la kujifunza hapa watu wakikuchoka jiondoe mapema tu.
 
Pia alidai kwamba, Sanon alimwambia kuwa alifuatwa na na watu waliodai wanatoka kwenye serikali ya Marekani na kitengo cha haki, ambao walimwambia kuwa wanataka kumfanya awe raisi wa Haiti.
Hiki kitengo cha haki ndiyo walihack kale kamashine ka moyo ka bwana yule aliekuwa anatutukania Mama zetu pamoja na dada zetu na hatimae Taifa likapona.Mungu ibariki sana Marekani.
 
Back
Top Bottom