Sakata la Mbasha mkubwa laanikwa

Hahahaha nakumbuka wapenda umbea tulivyokesha siku ile kufatilia story hii... Na uliivalia njuga hii story khaa kama sikosei na wewe ulipata hadi PM za kutokueleweka concerning that issue

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

nilizipata nyingi sana na nina source yangu moja ya kunipa kinachojiri kwa mbasha
 

ndugu mtumishi sidhani kama kuna mantiki ya kumhisi mtu,kusema eti ni mbasha coz kasema jamaa anahusika na sembe,hoja yako haina mashaka,unawajua wangapi wenye kumtambua gwajima kama mzee wa sembe?

pili,tukivaa viatu vya mbasha,Mungu ametuamrisha kusamehe mara sabini ila ktk hali ya ubinadamu "human inborn traits" tumeumbwa na viashiria vya hasira na chuki,kwa issue ya gwajima kuhusishwa na kuteteleka kwa ndoa ya mbasha ni dhahiri jamaa lazima amchukie!!

tatu,ndg mtumishi,naamini fungu la kumi lina matumizi mengi kuliko kujenga mijengnw mingi ya gharama na kununua miji gari ya kifahari,hv ungejisikiaje kama ungeona sadaka yako imetumika kumlipia ada yatima aliefiwa na wazazi wote wawili? au mama aliekosa gharama za uzazi hospitali? naamin kuna haja ya kufuata mafundisho ya yesu kwa vitendo na si kwa maneno.

mwishowe alienacho hutaka zaidi hyo ni habit ya binadamu sisemi asilimia 100% kwamba uhusishwaji wa gwajima na sembe ni sahihi ila lisemwalo lipo,matajiri hupenda ku maximize wealth hata kwa njia za panya.

mwishowe kama ulivyosema,tumuachie mungu afanye maajabu yake lkn tuwe huru kwenye kuutafuta ukweli coz the "so called mitume na manabii wa siku hz ni watu tu kama mimi na wewe" wanaweza kujifanya watumishi wa mungu to conceal their true identity!!


fin.....
 
nilizipata nyingi sana na nina source yangu moja ya kunipa kinachojiri kwa mbasha

Hahaha shosti uwe unanikumbuka basi kwenye ufalme wako wa hizo updates, I beg u uuuh (umbea utaniua khaaa)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hahaha shosti uwe unanikumbuka basi kwenye ufalme wako wa hizo updates, I beg u uuuh (umbea utaniua khaaa)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

duuh ndugu yangu ni mambo nyeti sana
 
Mkuu The bold sijui aliishia wapi!? Sijui ile simu ya Australia ilimfanya hadi abadili ID? Mkuu The bold hebu njoo huku!
 
Last edited by a moderator:
Nmependa sana maneno yako, maana yamejaa busara na hayapo upande wowote
 

Umenena vyema kbs sadaka co kwa ajili ya kujineemesha wao na suala la sembe lipo linazungumzwa kila leo viongoz wa dini na vyama wamekuwa wakijineemesha wao ss kwann wasizungumzwe ili watu ambao hawajui wawatambue kuwa wanaongozwa na watu wa aina gani
 
Team gwajima..mambo!msalimieni wana media ministries

chipa; ungejua kuwa miye hata huyo Gwajima simfahamu ungeshangaa sana. Miye nipo kukupa kaushauri tu kuhusu hatari iliyopo kwa kuwanena watumishi wa Mungu aliye hai. Hilo huamsha hasira yake tena mara moja. Biblia ambayo miye naiamini saana imejaa mifano mingi tu ambapo watu waliwanena watumishi wa Mungu huyu aliye hai na mwisho wao ukawa mbaya sana.
Mfano ni Kitabu cha HESABU 12: 10
Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
Huu ni mfano mmoja tu nimetamani uusome weye na hao wenzio wanaopenda kuwanenea watumishi wa Mungu. Ukitaka soma vizuri biblia yako tangu mwanzo wa sura hii ya 12. Utaona kuwa Miriamu na Haruni, hawakusema lolote la uongo kumhusu Musa lakini kile kitendo tu cha kumsema wakiwa faragha mbali na Musa, kilimwudhi Mungu wa Musa. Ogopa kushabikia vijineno neno vinavyowahusu hao watumishi. Kama wamefanya maovu, sio kazi yangu kuwatangaza humu JF. Mungu asiyeweza kuwakemea watumishi wake, huyo nadiriki kumsema kuwa ni Kipofu, Kiziwi, na mdhaifu saana tu. Huyo anatuhitaji tumtetee. MUNGU ALIYE HAI HAYUKO HIVYO.
 
Eti wa watumishi wa Mungu wakati wengi wao ni wezi tu. Na mwingine hapo juu anatetea hawa jamaa kujijengea majumba binafsi kwa sadaka za watu. Shame!!

crocodile;
Surely yu are a crocodile. So what are yu doing in jf while yu know this is not your proper place?? Nafasi yako ni mtoni. Unayajua sana mambo ya mtoni. Weye kuwabeza hao watumishi wa Mungu hakuwaondolei utumishi wao. Full Stop.
Kama unamfahamu yeyote ambaye ni mwizi, mpeleke polisi wamkamate wampeleke mahakamani, na mahakama ikimpata na hatia, haijalishi cheo chake. Atafungwa aondoke huku uraiani.
Weye huoni vibaya kupiga kelele za dharau humu wakati raia wema wanaibiwa na mtu unayemjua?? Weye ni mtu wa ajab saana tu.
 

Pamoja na utetezi wakomkwa watumishi wa Mungu, mbona huna uhakika na unachokisema? Kama wamtuhumiwa kuuza sembe, basi unapowatetea uje na ushahidi kwamba hawauzi, siyo kusema tu sadaka. You better be quite.
Kuhusu identity ya Mbasha napo huna uhakika, ila ujue hata kama ni yeye basi anaonyesha uchungu kwa mke wake. Hivi wewe mke wako ahisiwe kutembea na mchungaji wako, utakaa kimya tu? Simtetei kwa dhambi anayotuhumiwa (ubakaji). Narudia tena you better be quite.
Siyo kila mchungaji, askofu, mtume na nabii ameitwa na Mungu. Ndiyo maana Biblia imeturusu kutoaminimkila roho, bali tuzijaribu.
 
Hakika wewe nimmoja wao. Ni suala la muda tu mtaona hasira yake yeye aliye juu

Mbasha hafungwi hata robo siku!!!

Eti wa watumishi wa Mungu wakati wengi wao ni wezi tu. Na mwingine hapo juu anatetea hawa jamaa kujijengea majumba binafsi kwa sadaka za watu. Shame!!


ndugu zangu mabibi na mabwana, kwanza kabisa nilisha declare interest kwamba, nilishawahi kusali kwa gwajima mara nyingi tu, na kwa huyo wa mwenge mara nyingi tu. kwa upande wangu, nililishwa Neno la Mungu na Bwana aliongea nao kupitia wao hadi nikabadilika maisha yangu sana. kama nyie mnao ushahidi kwa hayo mnayoyasema wekeni ushahidi hapa. nijuavyo kwa gwajima ile hummer alipewa Japan alipoenda kuhubiri, alipewa magari mengi tu mengine aliwagawia watumishi wengine, na alipotoka japan na ile hummer alikuja kutangaza kanisani kuhusu kupewa gari hiyo na wajapani, na wajapani wenyewe walikuwepo wengine hadi waliolewa palepale kwa blacks...kipindi hicho lile kanisa lilikuwa pale ubungo. alihamia kawe. pale mwenge nilisali sana pia, nilimwona Mungu. mnachotakiwa kujua ni kwamba kila kanisa linalo sheria zake katika kutumia mafungu ya kumi. kibiblia wana wa Walawi (ambao ni kabila moja la waisrae ambao Mungu aliliteua kuwa ni kabila la makuhani hadi leo hii) wao hawakuruhusiwa kufanya kazi, kazi yao ilikuwa ni kutumika hekaluni tu, na waisrael walitakiwa/wanatakiwa kutoa moja ya kumi ya kila wanachopata ili kuwapa hawa walawi wasiofanya kazi wanaopoteza muda wao hekaluni kusaidia ili kuwahudumia wao wengine kiroho. huu ndio msingi wetu sisi walokole hadi leo hii, fungu la kumi ni la mtumishi wa Mungu na halitakiwi kuliwa na yeyote kibiblia, the more you have many members in your church the more fungu la kumi you will get (tithe). hii ndio sababu utakuwa watumishi wa kilokole wanakuwa na pesa kwasababu ya mafungu ya kumi wala si sadaka nyingine, na wameruhusiwa na biblia kuzitumia. sadaka nyingien ndiu huenda kwenye mambo mengine, huo ndio msingi wa fungu la kumi kibiblia. atakayekwambia vingine ni mwongo.

sasa, kama watumishi hao wanashinda kanisani wanahudumia waumini kila siku hawafanyi kazi nyingine, wanapewa mafungu ya kumi na wakati mwingine wanapewa zawadi, hasa hao wanaosafiri nje kama gwajima kwenda japan, korea etc wanazawadiwa sana kwaajili ya familia yao, kwanini wasijenge mijengo? kwanza kwa jinsi ninavyowajua, naona hawajajenga sana kwasababu walitakiwa kujenga zaidi ya hapo kwasababu Mungu anawabariki kutokana na bidii yao madhabahuni.

kuhusu mbasha, mwanzoni mimi nilikuwa namhurumia na kumtetea. ukiangalia post zangu utaelewa. lakini nilibahatika kufahamu hii issue kiundani sana, kwanza kuhusu DNA aliyopimwa yule mtoto kutokana na tendo, ile clip ya audio mbasha anaomba msamaha, na jinsi alivyolishughulikia hili kiasi kwamba walokole wamemwacha amebaki peke yake kwasababu ya kulishughulikia vibaya, amekosa sapoti. tujifunze katika maisha namna ya kuhandle vitu. yeye alikimbilia kumlaumu gwajima kwa suspicion zake kuwa atakuwa anatembea na mkewe bila hata ushahidi kuwa nao. kwetu sisi wanasheria, suspension however strong, cannot be used as evidence to prove any criminal matter.

ninaamini kabisa, kama kweli gwajima angekuwa ametembea na flora, mbasha asingenyamaza namna hii hadi kusubiri apate kesi ndio aibue. labda kama hana uchungu na mke. alihisi tu. kwani flora mbona kama anasema uingereza alienda na mbasha mwenyewe, na gwajima akienda uingereza mbona inasemekana huwa anaenda na mkewe? tusiwachafue watumishi wa Mungu kwa vitu tusivyovijua. Mungu amsaidie mbasha apone na 30years segerea, na ninashauri asiendelee sana kwenda kimwili alishughulikie kiroho ili pengine neema ya Mungu iingilie kati. la sivyo, watu hawataamini macho yao siku ya hukumu.
 
Hakika mpaka uandikiwe kuwa baba yako mzazi kabaka kuku ndo uta uthibitishia umma kuwa magazeti ya udaku yana andika ukweli.Si mtetei Gwajima ila kama nikioneshwa uwongo na ukweli naweza kubaini.kwa ufupi Gwajima kila sehemu na kila mahali huwa anaongozana na mkewe Esther pamoja na ma bodyguard wake.sasa sijaelewa kidogo naomba nijulishwe huo muda wa Gwajima kuwa na uhusiano na mapenzi na florah inawezekanaje.Afu isitoshe huyo mbasha mwanaume amewai kumbwa na kesi za ubakaji mbili akiwa sekondari.Ni mahesabu ya haraka nimepiga kujua nn kinaendelea.asante
 
Duuu mungu ana wivu????
yap, Mungu ana wivu sana kwa watu wake. ukitaka kujua kuwa Mungu ana wivu jaribu kugusa watu wake utaona atakavyokushughulikia. wivu wa Mungu upo maeneo mengi, wivu mwingine wa Mungu ni kwamba, God never shares his glory with humans. utukufu wa Mungu ni wa Mungu mwanadamu akiiba utukufu wa Mungu Mungu ana wivu huwa anamrarua. pia, watu wa Mungu hata kama wamekosea Mungu huwa anapenda kujitukuza kupitia kwao na kuonyesha kuwa yeye ni Mungu wa rehema na neema. ukisoma kitabu cha Yoel, utaona jinsi Mungu anavyowararua maadui wa israel pamoja na kwamba waisrael walimkosea, walipomrudia kwa kufunga na kulia aliwasamehe, akawarudishia miaka yao yote iliyopotea, akawageukia maadui zao akawalisha nyama zao wenyewe. Neno la Mungu linasema 'watu wangu hawatatahayarika/my people shall never be ashamed" akimaanisha kuwa Mungu hufuta aibu kwa watu wake ili adui yao aiwaaibishe. Mungu atakusambaratisha hata wewe kama unagusa watu wa Mungu (awe muumini awe mchungaji etc, maadam ni mtu wa Mungu usimguse, utakwisha, kama hauamini jaribu).
 
Ndo maan serikali inabidi iingilie kati,makanisa yalipe kodi hamna anchofanya hatoi huduma za jamii kazi kununua mahelcopta... Aende mbali ibilisi huyo kazi kula wake za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…