my friend, kama unachoongea ni cha kweli, basi Mungu ataingilia kati. ila kama unachoongea hauna uhakika nacho, umejipanga kuwachafua tu hao jamaa, madhara unayosababisha kwao na kwa waumini wao yatakurudia wewe mwenyewe mara mia. Mungu akusaidie upate ufahamu huo.
binafsi yangu, nilishawahi kusali makanisa hayo yote katika maisha yangu kwasababu mimi ni mlokole (if i am to declare my interest). sadaka wanazotoa pale kwa gwajima waumini walivyo wengi na pale mwenge kwa huyo mtume unayemsema, ni nyingi sana kiasi kwamba wasingehitaji hata kuwa na biashara ya sembe. ni hela nyingi sana kwa jumapili moja hata hutahitaji kuingia kwenye sembe. na kwa majengo yao ya kuishi yale waliyojenga hakika yake kwa sadaka zinazotolewa na vitabu wanavyouza na mafungu ya kumi etc ni mengi sana kiasi cha kumfanya mtu asione umuhimu wa kuingia kwenye iyo sembe. si kila mtu anayefanikiwa anapitia kwenye sembe...
vilevile, identity yako inajulikana, wewe ninahisi ni mbasha. kwasababu kwenye barua yako ile ya kwanza uliandika kuhusu gwajima na kuwa unataka kumshitaki, ulisema kuwa gwajima anauza sembe, hivyo ni wewe mwenyewe.
unachotakiwa kujua, watumishi wa Mungu si malaika, ila wakikosea si sawa na wewe ukikosea, wao huhukumiwa na Mungu mwenyewe, who are you to judge the saints of the Lord? Mungu pekee ndiye anawahukumu, ukiwahukumu wewe Mungu ni mwenye wivu atakurarua hata kama wamekosea. hujui wametoka mbali vipi na Mungu hadi walipofikia hapo, hujui wamevumilia mangapi kwaajili ya Mungu, hujui wamepitia mangapi and how much God values them due to what they have passed through.
kuhusu mbasha, it is unfortunate kwamba asilimia kubwa inaonyesha alikuwa anafanya ngono na yule binti. simhukumu, ila kutokana na ushahidi hasa wa DNA inaonekana alifanya ngono na under-age. hiyo ni statutory rape hata kama binti alikubali, miaka 30 ileile iko palepale tu. kuna ile clip ya audio mbasha aliongea kuomba msamaha kwa yule binti akaongea na story ndeefu kuhusu ndugu zake wa mwanza hadi mzee kulola, kwa aliyesikiliza clip ile atajua hakuna ubishi ngono ilifanyika. na kama ilifanyika, na binti akajulikana ni under 18yrs, basi hakuna ubishi kwamba mbasha alibaka na atastahili kufungwa, na asilimia za kufungwa ni kubwa sana kulingana na jinsi mbasha alivyojichanganya.
binafsi simhukumu mbasha kwa alichokifanya, ninamuonea huruma kwasababu hata mimi si malaika kwamba sijawahi kuzini ktk maisha yangu, nilishazini sana nashukuru Mungu alinisamehe. ila sidhani kama anachokifanya mbasha kinasaidia hasa kiroho kwasababu. angeyamaliza haya mambo chinichini ingemsaidia na angepata watu wanaomsapoti kwenye iyo kesi.