Sakata la Mbasha mkubwa laanikwa

Sakata la Mbasha mkubwa laanikwa

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Naomba nifunguke kidogo nielezee kile ninachokifahamu kuhusu ili sakata!!
Mgogoro katika ndoa ya Mbasha na Florah ulianza kushika kasi mwaka jana mara baada ya Florah na Mumewe kuhamia kuanza kusali kanisani kwa GWAJIMA (ufufuo na Uzima - kawe) wakitokea kanisa la MITO YA BARAKA (kariakoo)! Inasemekana kuwa mara baada ya kuhamia kanisani hapo kwa mualiko wa Gwajima (aliwaombe waje kusali kwake), mchungaji Gwajima alimfanya florah kama kiongozi wa Ibada ya SIFA na KUABUDU katika mikutani yake!! Kama ni mfuatiliaji wa haya mambo utakumbuka kuwa mwaka jana Florah alizunguka Tanzania nzima akiwa na Gwajima wakifanya mikutano ya Injili!!

Baada ya Muda kidogo Mchungaji Gwajima alimpeleka Florah London kwaajili ya masomo kitendo ambacho inasemekana kilipingwa sana na mumewe Mbasha! Ikumbukwe kuwa GWAJIMA haiwezi kupita miezi miwili pasipo kwenda UK coz amefungua kanisa kule (GLORY OF CHRIST - UK)!! So katika kipindi ambacho florah alikuwa London walikuwa wanaonana mara nyingi sana na GWAJIMA.

Baada ya Florah kurudi Tanzania ndipo akaanza hii ziara ya kuzunguka mikoani na GWAJIMA.. inasemekana kuwa katika kipindi hiki ndipo mahusiano ya kindoa kati ya forah na mumewe yalizorota zaidi... baada ya ziara kuisha Florah arirudi nyumbani lakini she wasn't the same (nisiseme zaidi)!

Baada ya mikwaruzano ya hapa na pale ndipo Florah akaenda kukaa hotelini na inasemekana hoteli ilikuwa inalipiwa na mchungaji GWAJIMA, ikumbukwe kuwa ni swala la kawaida kwa Gwajima kuwalipia bills mbalimbali viongozi wake wa huduma hapo kanisani kwa mfano anamchngaji anaitwa MAXMILLIAN MACHUM amempangishia nyumba ya ghorofa pale ubungo na wachungaji wake wote wapatao thelethini amewanunulia magari!! Lakini hata hivyo hii hatua yake ya kumpangia hoteli mke wa mtu ilizua maswali mengi sana.

NAOMBA TUDIGEST HII KWANZA ALAFU NTARUDI HAPA KUELEZEA YAFUATAYO

1. Kisa cha mbasha "kubaka"

2. Milioni 10 alizotoa GWAJIMA kwenye msiba wa kulola

3. Mungu akinipa ujasiri nitamtaja kabisa mtu aliye nyuma ya pazia ya hii sinema..
-----------------------------------------
Iko hivi wakuu.

1. Kisa cha mbasha "kubaka"
(Sitatoa kila detail ili kulinda identity yangu)

Kabla sijaanza kueleza kisa hiki ni vizuri niwaeleze kidogo kuhusu Intellijensia ya Gwajima jinsi ilivyo... pale kanisani kwake wanavitengo mbali mbali amabvyo wenyewe wanaviita ‘ministries' na katika ministry hizo zipo mbili ambazo ni muhimu zaidi i) Media ministry ii) Security ministry (hii huwa wanaiita ‘mashujaa' wa Daudi).

Media - Ministry kazi yake ni kulitangaza kanisa mitaani na kwenye vyombo vya habari, kueneza ‘propaganda' ya kanisa na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Security Ministry - kazi yao ni kumlinda Gwajima.! Kama umewahi kufika pale kanisani utakuwa umewahi kuwaona huwa wanavaa suti nyeusi na miwani nyeusi (kama secret service wa marekani).

Wale jamaa usiwachukulie poa, majamaa wale ni wanajeshi na polisi wastaafu na wengine bado wapo kazini.

Sasa huduma hizi mbili zinaunda kitu kama "USALAMA WA TAIFA" wa kanisa la Gwajima.
Turudi kwenye topic sasa.

Ni ukweli ambao ulikuja kubainika hivi karibuni kuwa Mr. Mbasha ana mahusiano ya kimapenzi na shemeji yake (kwa muda mrefu kidogo) na habari hii ikamfikia mpaka florah.. kipindi hiki florah bado anakaa hoteli!

Suala hili florah aliwaeleza watu wachache sana wakaribu na likabakia kuwa siri.. lakini sisi wengine tikuwa tunalifahamu muda mrefu tu!
Kuna watu wakamshauri florah amuhoji mmewake na florah akauchukua huo ushauri akaenda kumuhoji Mr. Unaambiwa jamaa aling'aka balaa na akakataa kata kata kuwa hana mahusiano na shemejiye!

Basi katika majibizano mara jamaa akaropoka kuwa mbona hata yeye anafahamu kuwa florah anamahusiano na Gwa**** lakini hasemi chochote! Weeeeee ilikuwa balaa maana hicho kilikuwa kijikikao fulani hivi na ndugu kadhaa walikuwepo basi kila mtu akashikwa na bumbuwazi!!! Unaambiwa Florah hakusema chochote akaanza kulia akainuka akaondoka!!
Na baada ya hapo hata simu za mbasha akawa hapokei.

Inasemekana taarifa zikamfikia mchungaji wao Gwajima, basi Gwajima akamuita ofisini jamaa akakataa kwenda!
Sasa katika hizo purukushani za kuwasuluhisha jamaa kuna siku akatishia kuwa atavujisha ushahidi wa mahusiano ya huyo mchungaji na mkewe florah!! Nahisi hapo ndipo alipojiroga.

KESI YA KUBAKA
baada ya mrafaruku kutokea jamaa akawa dizaini kama amesitisha mahusiano na shemejiye na hapa kati alikuwa hakai nyumbni kwa florah.. lakini inavyoonekana mchungaji alitishwa sana na mkwara wa jamaa kuwa atavujisha ushahidi wa mahusiano yake na mkewe... binafsi nahisi mipango ikaanza kusukwa na binti akasetiwa kwa ajili ya ‘operation tokomeza.

Juzi juzi hapa kabla ya tukio kutokea ndio huyu binti amerudi kwa florah akijua wazi kabisa dada take hayupo! Na kama ujuavyo muonja asali aonji Mara moja, jamaa kuona mzigo umerudi basi ikabidi wakumbushie enzi!
Sitaki kumaliza huondo wote lakini tujiulize maswali haya:

1. Hivi kubaka ndio inakuwa hivi? Ni ijumaa mko nyumbani peke mnamaliza kula mchana mnakaa sebuleni mnapiga stori ‘mizuka inapanda mnaamua kuibanjua amri ya sita! Kesho yake jumamosi anakuja mgeni mnakuwa wapole tu, mnavunga mnaitana shemeji!

Alafu kesho kesho yake Jumapili mnatengeneza mazingira ili muondoke peke yenu wawili! Mnafika mahali fulani ubungo mnapaki gari mafichoni mnaanza kuibanjua amri ya sita.

Mnatoka hapo mnaenda kanisani mnatabasamu kabisa, ibada ikiisha mnatengeneza tena mazingira ili muondoke peke yenu!

Mnafika kisehemu chenu mnapaki tena gari mnabanjuka! Halafu eti amebakwa?

2.Kwanini huyu binti baada ya tukio kutokea akawapigia simu bodyguards wa Gwajima ambao walienda kumchukua na kurudi nae nyumbani kwa gwajima?
Alafu eti hawa bodyguards ndio wanaanza kuwapa taarifa ndugu za florah!! Kwanini apige simu kule?
Kwanini hakuwapigia simu ndugu zake kwanza?

3.Kwanini hii ishu wameipeleka fasta kwenye media! Yani binti yuko polisi anaandika maelezo wao wameshawapigia simu waandishi wako nje wanawasubiri kumuhoji!

Binadamu huwa wepesi kutangaza habari njema zinazotuletea sifa! Inakuwaje habari mbaya na kudhalilisha familia kama habari hii wao wanakuwa wepesi kiasi hicho kuipeleka kwenye media?

Alafu kama hiyo haitoshi wanamrekodi mbasha na kuivujisha audio kwa makusudi kabisa ili iweje!

Kama kweli jamaa amebaka mbona wanatapatapa kutafuta huruma ya wananchi na media?
Kwanini wabehave namna hii?
-----------------------------------------------------
Jamani sitaki kumtaja mtu jina naomba mjiongeze wenyewe! Mtu akitaja jina mie simo.

Ila kwa kifupi hapa namuongelea mchungaji mmoja maarufu sana hapa town, anasukuma ndinga ya maana (hummer), ana mjengo wa maana wa ghorofa nne mbezi beach, na ana hela mpaka hajui azifanyie nini, ana mtoto wa kike anasoma high school nchini Switzerland, na juzi juzi amenunua magari 32 yenye jumla ya thamani ya zaidi ya milioni 250 ameyagawa kwa wasaidizi wake kanisani kwake!

USHIRIKI WAKE KWENYE BIASHARA YA SEMBE.
Huyu mtumishi ana dada zake wawili wote wameolewa na wachungaji wake wasaidizi hapo kanisani kwake, mmoja anaishi ubungo mwingine anaishi kibaha kwa Mathias.!

Hapa nataka kumuongelea huyo anayeishi kibaha kwa Mathias, yeye na mme wake wamejaliwa kupata watoto wawili, na mumewe ni Kiongozi kanisani kwao (kanisani kwa kaka yake) upande wa ulinzi na usalama.
Anahusika moja kwa moja na ulinzi wa mchungaji wetu tunayemuongelea hapa (mzee wa humer na misukule)! Kwa kifupi jamaa yuko katika ‘inner circle' ya mzee wa hummer na misukule!

Sasa huyu jamaa (shemeji/mlinzi wa mzee wa Hummer) mwaka jana alimleta binti kutoka kijijini kwao akasema kuwa ni mtoto wa shangazi yake!!

Baada ya miezi kadhaa mkewe akagundua kuwa jamaa anammega yule binti, basi kukawa na ugomvi mkubwa sana, mpaka mzee wa hummer ikabidi aingilie!! Baada ya kuingilia na kumtetea dada yake, shemeji mtu akamaindi sana kiasi ambacho akaacha hata kwenda kusali kule kanisani na mpaka cheo chake cha chief security officer wa mzee wa hummer akakipiga chini! (Huyu jamaa ni mwanajeshi kikosi cha hapa kigamboni)
Kupitia huyu bwana ndio tukanyetishwa hili suala ntalolielezea hapa.

Mwaka jana mwezi novemba kuna gazeti moja la global liliandika habari kuwa mzee wa hummer amelishwa sumu na askofu watu wakaponda kuwa ni uongo ila mzee wa hummer anataka kujipa promo! Ile ishu ilikuwa ni kweli coz hata mimi mwenyewe niliifahamu karibia miezi minne kabla haijatoka kwenye gazeti ila nilikuwa sikujua why askofu alimlisha sumu, na sababu ambayo baadae global waliitoa ilikuwa ya kijinga mno eti jamaa wenzake wanamuonea wivu!

Sasa huyu mnyetishaji wangu ndo amenifumbua macho.. ishu iko hivi!!
Jamaa anasema kuwa katika sekta ya hawa ‘watumishi wa mungu' kuna CARTEL ya watu sita ikiwajumuisha mzee wa hummer, mchungaji mmoja wa kike ana kanisa mikocheni B pamoja na mwingine ana kanisa kubwa sana Mwenge (sio kakobe) huyu anajiita ‘mtume na nabii!

Anaendelea kusema kuwa hawa wawili (mama wa mikocheni na mtume wa mwenge) wao ni wazoefu sana lakini huyu mzee wa hummer ni wa juzi tu kwenye mtandao ila ni mjanja mni coz ameweza kujenga mtandao mpana sana na amekuwa akiwazunguka wenzie!

Sasa anadai kuwa mwaka jana ugomvi wao ulifikia pabaya zaidi kiasi kwamba wenzie walidhamiria hasa kumuua!! Mwaka jana pekee mzee wa hummer alivamiwa mara mbili nyumbani kwake na watu wasiojulikana na hawakuiba chochote inasemekana kuwa walikuwa wanamsaka mzee wa hummer bahati nzuri hakuwepo (hili Mimi mwenyewe binafsinimelithibitisha kupituia kwa ndugu zake wa karibu)
(Mwishoni ntaeleza connection iliyopo na tukio la Mbasha)
Itaendelea...
-----------------------------------------------
 
Daaa hii ni noma, hii dunia siyo kama tunavyodhani, ni zaidi ya fikra zetu za kibinadamu.
 
Two wrongs....

Mbasha kabaka...maanake ni cheater...

Mkewe naye cheater mwenzie...

Tofauti ni kuwa mkewe hawezi kushitakiwa...(at least kibongo bongo)

Ila yeye miaka 30 inamuhusu...
 
my friend, kama unachoongea ni cha kweli, basi Mungu ataingilia kati. ila kama unachoongea hauna uhakika nacho, umejipanga kuwachafua tu hao jamaa, madhara unayosababisha kwao na kwa waumini wao yatakurudia wewe mwenyewe mara mia. Mungu akusaidie upate ufahamu huo.

binafsi yangu, nilishawahi kusali makanisa hayo yote katika maisha yangu kwasababu mimi ni mlokole (if i am to declare my interest). sadaka wanazotoa pale kwa gwajima waumini walivyo wengi na pale mwenge kwa huyo mtume unayemsema, ni nyingi sana kiasi kwamba wasingehitaji hata kuwa na biashara ya sembe. ni hela nyingi sana kwa jumapili moja hata hutahitaji kuingia kwenye sembe. na kwa majengo yao ya kuishi yale waliyojenga hakika yake kwa sadaka zinazotolewa na vitabu wanavyouza na mafungu ya kumi etc ni mengi sana kiasi cha kumfanya mtu asione umuhimu wa kuingia kwenye iyo sembe. si kila mtu anayefanikiwa anapitia kwenye sembe...

vilevile, identity yako inajulikana, wewe ninahisi ni mbasha. kwasababu kwenye barua yako ile ya kwanza uliandika kuhusu gwajima na kuwa unataka kumshitaki, ulisema kuwa gwajima anauza sembe, hivyo ni wewe mwenyewe.

unachotakiwa kujua, watumishi wa Mungu si malaika, ila wakikosea si sawa na wewe ukikosea, wao huhukumiwa na Mungu mwenyewe, who are you to judge the saints of the Lord? Mungu pekee ndiye anawahukumu, ukiwahukumu wewe Mungu ni mwenye wivu atakurarua hata kama wamekosea. hujui wametoka mbali vipi na Mungu hadi walipofikia hapo, hujui wamevumilia mangapi kwaajili ya Mungu, hujui wamepitia mangapi and how much God values them due to what they have passed through.

kuhusu mbasha, it is unfortunate kwamba asilimia kubwa inaonyesha alikuwa anafanya ngono na yule binti. simhukumu, ila kutokana na ushahidi hasa wa DNA inaonekana alifanya ngono na under-age. hiyo ni statutory rape hata kama binti alikubali, miaka 30 ileile iko palepale tu. kuna ile clip ya audio mbasha aliongea kuomba msamaha kwa yule binti akaongea na story ndeefu kuhusu ndugu zake wa mwanza hadi mzee kulola, kwa aliyesikiliza clip ile atajua hakuna ubishi ngono ilifanyika. na kama ilifanyika, na binti akajulikana ni under 18yrs, basi hakuna ubishi kwamba mbasha alibaka na atastahili kufungwa, na asilimia za kufungwa ni kubwa sana kulingana na jinsi mbasha alivyojichanganya.

binafsi simhukumu mbasha kwa alichokifanya, ninamuonea huruma kwasababu hata mimi si malaika kwamba sijawahi kuzini ktk maisha yangu, nilishazini sana nashukuru Mungu alinisamehe. ila sidhani kama anachokifanya mbasha kinasaidia hasa kiroho kwasababu. angeyamaliza haya mambo chinichini ingemsaidia na angepata watu wanaomsapoti kwenye iyo kesi.
 
Two wrongs....

Mbasha kabaka...maanake ni cheater...

Mkewe naye cheater mwenzie...

Tofauti ni kuwa mkewe hawezi kushitakiwa...(at least kibongo bongo)

Ila yeye miaka 30 inamuhusu...

Acha mahaba, mbasha hatafungwa hata wiki moja
 
Kweli mtu anapovutwa miguu na ibilisi haendi peke yake. Weye wadhani kuwa kumdhalilisha Mtumishi wa Mungu ili kuhalalisha uovu wako kutakusaidia?? Nakusihi ndg yangu. Kama una ushahidi mzuri tu wa Mtumishi yeyote anayeuza unga, ukiuandika humu JF ni kupoteza ushahidi. Unastahili kufuatiliwa na kufungwa. Usijiongezee balaa. Peleka ushahidi wako kwenye vyombo husika na kama unaona hawatamshika, nenda pamoja na Press na makamera makuubwa urekodiwe. Uma utakuwa nyuma yako wala si humu JF.
Kuhusu Mbasha, kama si roho ngumu, alitakiwa mapema sana amwangukie shem magotini. Amalizane naye kiume nje ya pilato. Nyiye msiompenda mnamdanganya hatafungwa. Nakwambieni, Segerea kunamhusu, mvua 30. Na dhambi ya kumnenea mabaya Gwajima inamngoja. Akitoka humo aje kumwomba tena radhi. Kama ni kuchapiwa anakolialia sasa ndo atachapiwa kweupeeee
 
Back
Top Bottom