Sakata la Mbowe kuwa na tuhuma za ugaidi isiwe sababu ya kutaka Watanzania tuamini anaonewa. Tuache mahakama iamue.

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kila mwanaChadema anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Mbowe amebambikizwa shitaka la ugaidi. Mbowe anaonewa maana sasa amewekwa kwenye sero ya wafungwa wa kunyongwa. Sawa, mnaweza kuwa sawa lakini suala lipo mahakamani.

Ibara ya 13 ya JMT ipo wazi kabisa kuwa hakuna mtu atakuwa na hatia mpaka mahakama imtie hatiani.

Sasa kama mahakama ndio chombo cha kumtia mtu hatiani mbona mnataka watanzania waingilie suala amabalo lipo mahakamani? Kama hana kosa basi acheni mahakama iamue,sio kutaka watanzania waingilie suala ambalo lipo ndani ya mahakama.

My take; Kulazimisha wananchi waamini kuwa Mbowe kaonewa is wastage of time.
 
Iwapo kama visa hivyo ni vigeni miongoni mwa Watanzani,mawazo au hisia hizo zisingekuwepo.
 
Mpaka leo unashindwa kujua kesi ya kihalali na ya kupikwa?, .Walisema mamemchunguza kwa muda mrefu na wanao ushahidi , vipi wanavojikanyaga mpaka hakimu anajitoa . Remember justice delayed is justice denied
 
IGP alishahukumu hii kesi tayari lakini.
 
Bahati mbaya Tanzania hatuna mahakama inayoweza kuitwa mahakama kwa maana ya mahakama.

Marehemu aliua mahakama, akaigeuza kuwa taasisi yake kwa nia ya kuwatesa wasiomshangilia. Aliwateua wasiojulikana kuwa majaji, akawajaza mahakamani. Msajili wa mahakama ni afisa wa wasiojulikana. Ndiye anayeamua kesi gani ipelwkwe kwa jaji, na ipi apewe asiyejulikana ili kumkomoa mtuhumiwa, kama walivyofanya kwa Mbowe. Baada ya njama kugundulika, amejitoa mapema.
 
Issue sio ugaidi ni katiba mpya.....watake wasitake katiba haiepukiki
 
Ungejua kuwa huna cha msingi cha kuongea ungeisha nyamaza.
 
Chadema mpaka damu ziwatoke maskioni
 
Na miaka wameshaamua apate mingapi jela ila CCM ni wapuuzi Sana anyway kwa Ku share nami chochote Private message iko wazi
 
ni kweli lakin wewe ni mwiongoni msioipenda tanzania.unataka tuendelee kulumbana alafu muendelee kuiba tumewastukia
 
Pole ndugu,
duniani kuna wengi wenye uwezo wa kawaida wa kuelewa vizuri mambo yanayo wazunguka katika maisha yao, na penye hitaji, hawa huweza kusaidiwa wakabadilika na kuwa wazuri, wema na wenye utu na hamu ya maendeleo ya kweli kwao.
Lakini pia, kuna ambao wanazidi kupoteza uwezo wa hata kusoma mazingira na zaidi umuhimu wa mabadilikojami chanya kwao, wewe u mmoja wao. Nyie ndio zao kuu la awamu ya kipindi cha giza cha Nabii Walwa Njozi wa Burigi. Kwa kurithi takataka zote za ukatili na udhalimu mmekuwa ni hasara kubwa kwa TAIFA.
Kipindi cha kuyaong'oa haya magugumaji sasa kimeshafika. AMEN
 
Watanzania tunaonewa kwa CCM kufanya ufisadi katika nchi hii kama Rais anavyokiri hapa nchi kufanyiwa ufisadi na CCM.

Huu ndiyo uonevu unaotakiwa uulaani.Uonevu kwa chadema haukuhusu.
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu mbona una thread nyingi kuhusu Mbowe? Si utulie tushamweka ndani? Au wataka na roho yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…