Sakata la Mdee na Wenzake: Yule anayejisifu kusoma sheria na kupata A hamuwezi kumuona akichambua uamuzi wa Spika kuwalinda Mdee na Wenzake

Katiba ya chama inamzuiya mwanachama kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya kumfukuza?
Kama haizuii basi subirini tusubiri maamuzi.
 
Huyu ni Pascal Mayalla kwanini usimtaje moja kwa moja tu...?

Hawezi. Huyu ni mwana propaganda "mbuni" wa CCM achimbiaye kichwa chini ya ardhi huku kiwiliwili chake chote kikiwa nje..

Yeye hoja na kauli zake kuu kuhusu haya mambo huwa ni "..CHADEMA kwisha habari yake.." au "...CHADEMA ni Kangaroo court" huku yeye akiwa ni "mbuni" aliyeficha kichwa huku kiwiliwili kikiwa wazi kikichomwa na jua jangwani...

Huyo ndiye Pascal Mayalla "msomi wa sheria" aliyepata A kwenye course ya "..Kangaroo court law.."
 
Kuna wakati huwa najiuliza hata nchi zilizoendelea wanafiki kama hao uwepo.
 
Kwa kweli hichi kinachoendelea kwenye huu ni kujidhalilisha jamii forums....ni kujidhalilisha CHADEMA..........

Kwanini kuikosoa CHADEMA inakuwa ni kosa la jinai ambalo hukumu yake kudhalilishana na kuvuana nguo kiwango......??

Sasa kuna tofauti gani kati ya Jf na kijiwe cha wavuta bangi.........

JF inaaminika kuwa ni uwanja wa watu wenye bongo zinazochemka na kuibua mijadala yenye tija kwa taifa.......kwanini tunataka kuipoteza sifaa hii kwa kushindwa kudhibiti mihemko yetu..........

Ni Demokrasia ipi inayohubiriwa na CHADEMA......Ni uhuru upi wa kutoa maoni unaopiganiwa na CHADEMA......??

Kwanini demokrasia ni kuisifia CHADEMA tu na sio kinyume chake.......???

Sasa kwa mtiririko huu kuna tofauti gani kati ya nyie na utawala wa MAGUFULI....??

Wandugu kuna maisha mengine nje ya siasa na wanadamu hatuwezi kuishi na mawazo yanayofanana hata watoto wako wa tumbo moja hutofautiana mawazo.....Hilo ni jambo la kawaida na ni maumbile ya kibinadamu....hakuna dawa juu ya hili zaidi ya kuvumiliana
 
Tatizo asipochambua jinsi unavyotaka wewe lazima utaghadhabika. Sasa kwaninini unaitafuta hasira kwa lazima?
 
Hiki chama kina madikteta hatari mno. Sema CCM inawanyoosha. Watanzania wasiwe na hofu wako salama na kamwe Chama Cha Mbowe hakitaingia ikulu.
 
Uko sahihi, ila Paskali apunguze ujuwaji, si lazima kila jambo ujifanye unalijuwa wewe, mbona hata Jaji Werema ni member humu lakini huwezi kumuona akirukia kila jambo la kisheria kujifanya yeye ndio mjuwaji.

Unapochezea hisia za watu utalajie haya yote, kiukweli ni mchambuzi mzuri wa siasa ila ujuwaji umezidi sana na ukimsoma huku ukiwa na akili timamu unaelewa ana ajenda zake binafsi anazozingiiza kwa kutumia kalamu.

Kwanza since Pasco amegombea ubunge kupitia ccm wajumbe wakapiga spana amepoteza moral authority ya kuhesabika kama mchangiaji huru, ni chawa wa Lumumba tu hakuna kingine na hawezi kuitakia mema Chadema hata sekunde moja.

Kwanza hiyo kampuni yake ya PPRA kuweza kusurvive wakati wa Magufuli na kuendelea kupewa tender za Sabasaba basi elewa wazi huyu ni insider.
 
Kwa nini hampendi kuambiwa ukweli?
Ukweli upi,? Kwamba Mbowe kafoji barua ya kuwateua, au kigogo wa Cdm! na kuwatoa baadhi wao magerezani wakasafirishwa usiku wa manane kwenda kuapishwa ubunge. Ingekua hivyo tusingefika hapa, subiri vyuma visuguane mwanga utayokea soon
 
Chadema mtagombana na nchi nzima sasa.

Sio kwa Povu hili.

Kila siku mnaongeza idadi ya maadui wapya.

Kwenu haki ni pale inapowapa favour nyinyi na vinginevyo sio HAKI.


MBOWE Alisema.......ACHENI UHUNI BHANA!
Wahuni wahuni hivi
 
Mambo ya hovyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…