Kusema ukweli hii sababu imewakera wadau wengi wa michezo. Na nina imani hata shabiki wa simba mwenye akili timamu, hawezi kukubaliana na huu upuuzi.
Maana kwa taarifa zilizopo ni kwamba Yanga kwenye mechi iliyopita, haikuruhusiwa kuingia siku ya mwisho kufanya mazoezi kwenye huo uwanja! Lakini haikuja na hili wazo la kitoto la kugomea mechi!
Ila kwa simba limekuwa ni wazo sahihi, na Bodi ya ligi imebariki, pasipo kuangalia hasara na usumbufu kwa mashabiki na wadau wengine waliowekeza raslimali zao za kila aina kuelekea kwenye huu mchezo. This is not fair at all.
Yaani ni kwamba simba ni wageni wa uwanja wa Mkapa, kiasi cha kulazimisha kufanya mazoezi siku ya mwisho kabla ya mchezo! Na kwa nini hawakutoa taarifa mapema kwa wasimamizi wa uwanja, ili maandalizi yafanyike? Au walikuwa wanatafuta tu kisingizio cha kugoma?