Sakata la mfanyabiashara Deo Bonge kutekwa, Spika Tulia afunguka "Sio Msaidizi Wangu"

Wakuu,

Baada ya tukio la jaribio la kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo, maarufu kama Deo Bonge, lililotokea eneo la Kiluvya hivi karibuni, picha za watuhumiwa zilisambaa na kuibua mjadala mtandaoni. Mmoja wa watuhumiwa alidaiwa kuwa msaidizi wa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, hali iliyosababisha taharuki.
Kutokana na madai hayo, Spika Tulia aliibuka kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) na kutoa ufafanuzi akisema, "Huyo pichani si Michael msaidizi wangu, wamemfananisha. Naamini wote waliohusika watapatikana na kuchukuliwa hatua stahiki."
Sakata hili limezidi kuzua mijadala huku wengi wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika ili kuhakikisha haki inatendeka na wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Haya wafukunyuzi wa mambo tuleteeni picha tuone kama sio yeye

Soma, Pia:

Mh Spika na Rais wa IPU amekuwa muungwana kujibu kuwa si msaidizi wake
 
Huyo ni msaidizi wake bi Kiroboto. Aache kujishebedua antoe mhalifu akashtakiwe.
 
Deo, mke wa mtu sumu
Hayo mengine sisi hatuyajui. Tunachotaka ni walengwa wakamatwe wawajibishwe. Hii nchi ni ya wote kile kitendo ni cha kulaani leo kwake kesho inaweza kuwa kwako pia.
 
Deo Bonge atakuwa alidhulumu mpunga wa watu ,mbona kwenye interview na Ayo amekuwa muoga kufunguka?
Kufunguka kunategemea na watakaochukua hatua kama una uhakika watafanya hivyo.vinginevyo unaweza ukafunguka alafu ukajikuta uko mwenyewe.vinginevyo labda uamue liwalo na liwe.
 
Majibu ya spika yako vizuri na yamenyooka.Ila sasa ndo ajue kua haya mambo yasipozibitiwa hakuna ambaye atakua salama.Mtu yoyote anaweza akaingia kwenye kadhia kwasababu ya ujinga wawatu wachache.
 
Kuna Wakati Picha ya Patrick Chokala akiwa Msemaji wa Ikulu ilifananishwa na ya mchungaji Mtikila 😂😂

Zikawekwa picha za Wawili hao tukajua ni kweli mchungaji Mtikila amefananishwa na Chokala 🤣
 
Wewe ni Sadist hata kama alidhulumu, kwako hiyo NDIYO njia sahihi ya kurecover kwa jamii iliyostaaribika inayojinasibu kufuata utawala wa Sheria? Kama Ndio hivyo kazi ni kubwa!
Ndg yangu kuna biashara nyingi za sirini, siyo kila deni unaweza kulidai kisheria, madeni mengine mnadaiyana nje ya mfumo wa kisheria!!
 
Kufunguka kunategemea na watakaochukua hatua kama una uhakika watafanya hivyo.vinginevyo unaweza ukafunguka alafu ukajikuta uko mwenyewe.vinginevyo labda uamue liwalo na liwe.
Afanye kama yule mfanyabiashara wa magari aliyesema wazi kwamba muliro anatumika ,aliitisha press conference akamwaga mboga.
 
Kuna Wakati Picha ya Patrick Chokala akiwa Msemaji wa Ikulu ilifananishwa na ya mchungaji Mtikila 😂😂

Zikawekwa picha za Wawili hao tukajua ni kweli mchungaji Mtikila amefananishwa na Chokala 🤣
Njiti anafuga genge la watekaji huoni sura yake ilivyokomaa utafikiri anakula sementi.
 
Back
Top Bottom