Sakata la mfanyabiashara Deo Bonge kutekwa, Spika Tulia afunguka "Sio Msaidizi Wangu"

Sakata la mfanyabiashara Deo Bonge kutekwa, Spika Tulia afunguka "Sio Msaidizi Wangu"

Wakuu,

Baada ya tukio la jaribio la kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo, maarufu kama Deo Bonge, lililotokea eneo la Kiluvya hivi karibuni, picha za watuhumiwa zilisambaa na kuibua mjadala mtandaoni. Mmoja wa watuhumiwa alidaiwa kuwa msaidizi wa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, hali iliyosababisha taharuki.
Kutokana na madai hayo, Spika Tulia aliibuka kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) na kutoa ufafanuzi akisema, "Huyo pichani si Michael msaidizi wangu, wamemfananisha. Naamini wote waliohusika watapatikana na kuchukuliwa hatua stahiki."
Sakata hili limezidi kuzua mijadala huku wengi wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika ili kuhakikisha haki inatendeka na wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Haya wafukunyuzi wa mambo tuleteeni picha tuone kama sio yeye

Soma, Pia:

Ndio maana nikimuona mwana siasa anamtaja Mungu au yesu au mtume muhamad mm huwa napandwa na hasira zile za kuinua uchungu mwingi
 
Back
Top Bottom