Sakata la Mh Mpina ni kidhihirisho Tosha kwa Watanzania kuhusu umuhimu wa kuwa na Bunge lenye Uwakilishi wa Vyama Vingi (Bunge Mseto)

Sakata la Mh Mpina ni kidhihirisho Tosha kwa Watanzania kuhusu umuhimu wa kuwa na Bunge lenye Uwakilishi wa Vyama Vingi (Bunge Mseto)

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Ndio! lilianza sakata la report ya CAG-mabilioni yamepigwa na uthibitisho wa ukaguzi ukawekwa wazi, bunge wawakilishiwetu wakanyamaza. Kama haitoshi wakamuita CAG kwenye wanayoiita mahakama yao kujibu hoja kwa nini ameibua madudu yao na anasema ukweli kuhusu udhaifu wao hadharani, CAG akanyamazishwa wote tunajua kilichomtokea baada ya hapo

Likaja Sakata la DP-world kupewa kama bure tu Bandari zetu sio tu za baharini pia na nchi kavu pamoja na baadhi ya mapori makubwa kwa miaka 100. Wawakilishi wetu wakakalishwa chini na kamati ya chama, wakalishwa Nta na asari, midomo, akili na bongo zao zikapakwa gundi, wakaacha kufikiri, wakaacha kuongea;wakaka kimya, hata walipopewa contract na wakaambiwa hii si contract wakasema sawa kabisa hii sio contract wakavaa ukipofu wa ghafla na kujitoa akili.

Kizuri kwenye DP world hapa wananchi na wanaharakati wakapaza sauti, ndipo kidogo miaka ya contract ikapunguzwa mpaka therathini na ushee ila vipengere vingine vikabaki palepale,dhuluma ikabaki na hilo likapita

Suala la Loliondo lilikuwa ni suala hatari sana hasa kwa wao kama wawakilishi wa wananchi, tulitegemea watapaza sauti at least kuwatetea wananchi waliowaweka hapo Bungeni, wananchi wakatimuliwa kama wavamizi kwa mitutu ya Bunduki na wanajeshi, kama vita vile, kwa mara nyingine tena wananchi wakanyimwa haki yao ya kuishi, kulindwa na kupewa huduma za kijamii na serikali yao,

Wengine wakahamishwa na kupelekwa mkoa wa Tanga, tunajua kilichowapata huko sema hakiandikwi tu basi, wengine mpaka leo wanaishi kama wakimbizi nchini kwao. Mbali ya wawakilishi wao kujua, wamekaa kimya, Hii ni mara nyingine ikionyesha jinis Bunge lilivyoshindwa kutimiza wajibu wake wa kutetea wananchi waliowachagua.

Sasa suala la Mpina ni kidhihirisho tosha cha tatizo la wawakilishi wetu kutoweka maslahi ya waliowachagua , kushindwa kutuwakilisha vyema.

Mbali ya Mh Mpina kutoa ushahidi na vielelezo sasa anatishwa, kaitwa kwenye kamati ili ashughulikiwe, na wametumwa watu kumchafua kwa kuibua kashfa za kubambikiza, wengine wamekwenda mbaili eti huyu ashughulikiwa kwa kushindwa kufuata mtindo uleule wa uzezeta, kwa kutaka kuwatetea wananchi badala ya chama, wanasema sasa kwa pamoja asurubiwe, asurubiwe badala ya Bawaba (Aliyedanganya)

Mambo haya yasingetokea kama tusingekuwa na Bunge la chama kimoja, yasingetokea kama tungekuwa na wabunge wengi wa vyama pinzani. Ukitaka Bunge lifanye kazi yake kwa umakini, liwawakilishe wananchi vizuri na kulinda na kueteta maslahi ya wananchi na taifa lazima liwe na wawakilishi wa chama kisichomadarakani walio wengi na walio makini.

Ni ngumu sana kumpinga anayekupa tonge na mwenye uwezo wa kuamua kesho kukunyanganya hilo tonge. Kinachotokea kilitegemewa na wanazuoni walikwisha tahadhalisha kwamba hili Bunge litakuwa Bunge la kwanza kufanya vitu vya ajabu na sasa tunashuhudia. Waswahili wanasema kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ndilo kosa kubwa.Je sisi tunasemaje huku nje tutaendelea kufanya makosa ya waziwazi

Whites people have a saying "you are the victim of your own decisions; your own choices". Now we have seen and being infringed and bloody traumatized by the consequences of our own decisions, our own choices, the choices we made or they forced us to make. Do you still want to continue being the same victim ,victim of your own choice while you can become a hero from the other choice. Time to make correct decision is now. Do not say I did not worn you.
 
Wabunge wenye akili...sio wa upinzani.
 
Wabunge wenye akili...sio wa upinzani.
Ukisoma vizuri ndani ya habari nimetamka kabisa wabunge wa vyama tofauti na chama tawala pia wabung makini. Ila the bottom line ni hata kama mbunge ana akili na kujitambua ni ngumu kufurukuta kwenye uwakilishi kama wa sasa. Ni ngumu kumkalipia aliyekupa Tonge na ana uwezo wa kukunyang'anya hilo Tonge hata leo. Ndio maana tunasema kwanza vyama tofauti ,pili wabunge hao wawe makini. Soma makala yote imejibu hoja zote na kufafanua nini cha kufanya
 
Ndio! lilianza sakata la report ya CAG-mabilioni yamepigwa na uthibitisho wa ukaguzi ukawekwa wazi, bunge wawakilishiwetu wakanyamaza. Kama haitoshi wakamuita CAG kwenye wanayoiita mahakama yao kujibu hoja kwa nini ameibua madudu yao na anasema ukweli kuhusu udhaifu wao hadharani, CAG akanyamazishwa wote tunajua kilichomtokea baada ya hapo

Likaja Sakata la DP-world kupewa kama bure tu Bandari zetu sio tu za baharini pia na nchi kavu pamoja na baadhi ya mapori makubwa kwa miaka 100. Wawakilishi wetu wakakalishwa chini na kamati ya chama, wakalishwa Nta na asari, midomo, akili na bongo zao zikapakwa gundi, wakaacha kufikiri, wakaacha kuongea;wakaka kimya, hata walipopewa contract na wakaambiwa hii si contract wakasema sawa kabisa hii sio contract wakavaa ukipofu wa ghafla na kujitoa akili. Kizuri kwa hapa wananchi na wanaharakati wakapaza sauti, ndipo kidogo miaka ya contract ikapunguzwa mpaka therathini na ushee ila vipengere vingine vikabaki palepale,dhuluma ikabaki na hilo likapita

Suala la Loliondo lilikuwa ni suala hatari sana hasa kwa wao kama wawakilishi wa wananchi, tulitegemea watapaza sauti at least kuwatetea wananchi waliowaweka hapo Bungeni, wananchi wakatimuliwa kama wavamizi kwa mitutu ya Bunduki na wanajeshi, kama vita vile, wananchi wakanyimwa haki yao ya kuishi, kulindwa na kupewa huduma za kijamii na serikali yao, wengine wakahamishwa na kupelekwa mkoa wa Tanga, tunajua kilichowapata huko sema hakiandikwi tu basi, wengine mpaka leo wanaishi kama wakimbizi nchini kwao. Mbali ya wawakilishi wao kujua, wamekaa kimya, Hii ni mara nyingine ikionyesha jinis Bunge lilivyoshindwa kutimiza wajibu wake wa kutetea wananchi waliowachagua.

Sasa suala la Mpina ni kidhihirisho tosha cha tatizo la wawakilishi wetu kutoweka maslahi ya waliowachagua , kushindwa kutuwakilisha vyema. Mbali ya yeye kutoa ushahidi na vielelezo sasa anatishwa, kaitwa kwenye kamati ili ashughulikiwe, na wametumwa watu kumchafua kwa kuibua kashfa za kubambikiza, wengine wamekwenda mbaili eti huyu ashughulikiwa kwa kushindwa kufuata mtindo uleule wa uzezeta, kwa kutaka kuwatetea wananchi badala ya chama, wanasema sasa kwa pamoja asurubiwe, asurubiwe badala ya Bawaba (Aliyedanganya)

Mambo haya yasingetokea kama tusingekuwa na Bunge la chama kimoja, yasingetokea kama tungekuwa na wabunge wengi wa vyama pinzani. Ukitaka Bunge lifanye kazi yake kwa umakini, liwawakilishe wananchi vizuri na kulinda na kueteta maslahi ya wananchi na taifa lazima liwe na wawakilishi wa chama kisichomadarakani walio wengi na walio makini.

Ni ngumu sana kumpinga anayekupa tonge na mwenye uwezo wa kuamua kesho kukunyanganya hilo tonge. Kinachotokea kilitegemewa na wanazuoni walikwisha tahadhalisha kwamba hili Bunge litakuwa Bunge la kwanza kufanya vitu vya ajabu na sasa tunashuhudia. Waswahili wanasema kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ndilo kosa kubwa.Je sisi tunasemaje huku nje tutaendelea kufanya makosa ya waziwazi

The whites have a saying "you are the victim of your own decisions; your own choices". Now we have seen and being infringed and bloody traumatized by the consequences of our opwn decisions, our won choices we made or they forced us to make, do you still want to continue being the same ,victim of your own choice while you can become a hero from your own choice. Time to make correct decision is now. Do not say I did not worn you.
Kwamba Vyama vingi ndio Wana Haki ya kukiuka taratibu au? Si walikuwa wanatimuliwa kama pimbi wakizingua au wewe ni WA juzi?
 
Kwamba Vyama vingi ndio Wana Haki ya kukiuka taratibu au? Si walikuwa wanatimuliwa kama pimbi wakizingua au wewe ni WA juzi?
Soma hoja vizuri andiko husichukue vitukio viwili kama sababu ya kupinga faida kubwa. Kuna mambo mengi mazuri wakati wa vyama vingi yalifanyika kwa sababu ya uwepo wa wapinzani na kuna mambo ya kijinga sana na ya kutia aibu yanafanyika sasa kwa sababu tu ni Bunge la watu walewale na chama kinadictate nini kifanyike Bungeni. Hao wapinzani waliokuwa wakitolewa Bungeni ni kwa sababu walisimamia sheria na haki ila kwa sababu uongozi wa Bunge ulikuwa ni watawala wakizidiwa hoja wanaleta hasira na kutumia nguvu. Labda wewe ndio wa juzi, hujui kwa hoja zipi wale wabunge wa upinzani walikuwa wakitolewa nje.

Personally sipendi siasa nachokiongea ni ukweli husiopingika. Je wewe unafurahia jinsi Bunge letu linavyoendeshwa na jinsi mambo muhimu yanavyopitishwa, kama jibu lako nio ndio basi jitafakari sana kuna kitu hakiko sawa....Tena sijui umesoma chapisho limeorodhesha baadhi ya matukio ya aibu
 
Back
Top Bottom