Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,142
Wakuu kuna tetesi zilianza kusambaa kwamba kufuatia sakata la kutekwa kwa bilionea Mohamed Dewji, kuna mabadiliko ya nafasi za baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi nchini ambapo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz wamepangiwa majukumu mengine.
Taarifa hizo zilidai kwamba Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii, Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, SACP Ramadhan Mungi akiwa kamanda mpya wa kanda maalum ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, jeshi la polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa imekanusha taarifa hizo na kueleza kwamba zinaenezwa na watu wenye maslahi yao binafsi. Kwa kifupi ni kwamba hakuna mabadiliko yaliyofanyika na Mambosasa na Boaz wanaendelea kushikilia nafasi zao.