Tetesi: Sakata la Mo Dewji, mambosasa, DCI Boaz Watenguliwa

Tetesi: Sakata la Mo Dewji, mambosasa, DCI Boaz Watenguliwa

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Wakuu kuna tetesi zilianza kusambaa kwamba kufuatia sakata la kutekwa kwa bilionea Mohamed Dewji, kuna mabadiliko ya nafasi za baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi nchini ambapo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz wamepangiwa majukumu mengine.

Taarifa hizo zilidai kwamba Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii, Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, SACP Ramadhan Mungi akiwa kamanda mpya wa kanda maalum ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, jeshi la polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa imekanusha taarifa hizo na kueleza kwamba zinaenezwa na watu wenye maslahi yao binafsi. Kwa kifupi ni kwamba hakuna mabadiliko yaliyofanyika na Mambosasa na Boaz wanaendelea kushikilia nafasi zao.
4eb9e0fb-2a83-42cf-b6ca-d692fa2f1d3d.jpg
 
Hawawezi tena umeshampangia, ila kwa maoni yangu naona Zirro ndio alipaswa kuondolewa. Mambosasa namuelewa sana anazijua vizuri siasa ila Zirro haziwezi atolewe tu, atakuja kumess up makubwa zaidi
Cha kushangaza huyo munayemuita zero humu humu JF ndio mlimpendekeza na Jiwe akafuata ushari wenu.
Leo anatumika ipasavyo na jiwe mnamuona zero.
Hahahhaha.
 
Wakuu kuna taarifa za mabadiliko ya nafasi za baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi nchini ambapo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz wamepangiwa majukumu mengine.
Inaelezwa kwamba Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii, Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, SACP Ramadhan Mungi akiwa kamanda mpya wa kanda maalum ya Dar es Salaam.
Wa makosa ya jinai kosa liko wapi kama hizi taarifa ni za kweli?
 
Hawawezi tena umeshampangia, ila kwa maoni yangu naona Zirro ndio alipaswa kuondolewa. Mambosasa namuelewa sana anazijua vizuri siasa ila Zirro haziwezi atolewe tu, atakuja kumess up makubwa zaidi
Ziro yupo kwenye UAIJIPII sababu ya DAB, na DAB ndo yupo nyuma ya hii Drama ya MOO, na DAB anasiri nyingi za SISITIMU na JIWE, kwa konekshen hiyo usitegemee Ziro au DAB kuguswa. Ila kafara is a must, kuna watu lazima wang'oke, ni kina nani let's wait!
 
Back
Top Bottom