Hardbody
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 4,139
- 4,640
Hili sakata wakati nasoma uzi humu kwa mara ya kwanza nilikuwa sijalielewa lilivyo. Nikasema acha nizame U-tube kujua likovipi ndio nikapata kuelewa mwanzo, kati na mwisho ulivyo hebu twende pamoja kwa ambaye hajaelewa kama mimi kwa Lugha nyepesi
Iko hivi waziri wa kilimo wakati anawasilisha bajeti yake ya wizara, kwenye sakata la sukari alisema ametoa vibali kwa makampuni ya wafanyabiashara kuagiza sukari kiasi cha Tani 410 elfu kufidia upungufu uliopo wa sukari
Pia akashusha lawama kwamba kulingana na kanuni zilivyo, vibali ilitakiwa vitolewe kwa viwanda vinavyozalisha sukari ndio viweze kuagiza nje kama kuna upungufu lakini hivo viwanda ambavyo ni Mtibwa sugar, Kagera Sugar, Bagamoyo etc vimeshindwa kuimport hata kilo moja ya sukari kwa mda wa miezi 3 na kusababisha tatizo la upungufu wa sukari kuwa kubwa kama ilivyo sasa
Sasa Mpina yeye akampinga waziri kwamba taarifa yake ni ya uongo, Ikabidi spika wa bunge amwambie awasilishe taarifa kuhusu uongo wa waziri. Mpina akawasilisha taarifa iliyoeleza mambo mengi kusuhu uongo wa waziri Bashe ambayo siwezi kueleza yote humu ila mwishoni ntaweka video ili kwa ambaye hakupata nafasi ya kusikia awasilize wote kwa makini na kuelewa vizuri
Sasa kilichotikisa zaidi katika taarifa ya Mpina ni Jinsi Waziri Bashe alipotoa vibali kwa Makampuni yenye kujihusisha na Mambo tofauti kabisa na kilimo wala sukari kupewa vibali vya kuingiza sukari tena zingine zikiwa na Mitaji midogo ya hadi Tshs mil 1. Mfano kuna Kampuni inajihusisha na Stationary ina hisa 1000 zenye thamani ya mil 1 lkn imepewa kibali cha kuingiza Tani 2 elfu zenye thamani ya Tshs Bil 6.6😂
Kampuni nyingine Itel (kampuni ya simu na vifaa vya kielektronic) imepewa kibali cha kuingiza Tani 60 elfu yenye thamani ya Tshs Bil 160 wakati mtaji wa kampuni ya itel ni Tshs mil 50
Kwahiyo kwa kifupi inaonekana kuna makampuni yalikua hayana sifa ya kupewa vibali vya kuingiza sukari lakini kwa matakwa flani flani na kwa masilahi ya wachache yakaweza kupatiwa hizo dili.
MY TAKE: Spika Aunde tume ifanye uchunguzi wa sakata hili maana kuna harufu ya rushwa, uhujumu uchumi, ufisadi na makosa mengine kibao Kama kuna ukweli juu ya hili basi wote waliohusika wafukishwe kwenye vyombo vya sheria hii si sawa nchi inapigwa kizembe namna hii Watanzania tusikubali aisee tupaze sauti kukemea hili
Sakata lilianza hapa
Hapa ndio mpina akaitisha press na kufichuo uozo wa waziri
Pia soma:Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia