Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

Kwanza sheria inasemaje kuhusu nani anatakiwa kuagiza sukari ikitokea hali kama hiyo? Pili kwanini Msukuma Aje kwenye media kutoa ushahidi wakati Spika alimwambie apeleke Kwakwe, kanuni za zinasemaje kuhusu alivyofanya Mpina? Hili swala ukiingia harakaharaka utalaumu au kumuona Spika mbaya ama Mpina yupo sawa lakini ukweli ni Kubwa Na Mpina amekosea kwenye kwa
M
Shida iko wapi ikiwa ushahidi huo huo Mpina alioupeleka kwa umma kwa sehemu akaamua kuupeleka kwa Spika?

Kwani ushahidi huwa ni jambo la siri lisilopaswa kujulikana kabla na watu wengine?

Spika na bunge walisema Mpina apeleke ushahidi kwao, sasa wamepelekewa ushahidi, waupitie huo ushahidi lakini wasilazimishe Mpina kutokujieleza kwa umma kwa jambo ambalo umma una maslahi nayo?

Kwanini Spika na bunge liingilie uhuru wa Mpina wa kujieleza nje ya bunge?
Mpina ni mtoto wa mjini ni mzalendo alijua kabisa ushahidi huu angeupeleka kwa spika ungeishia kuwekwa kwenye makabati tu sasa yy kalisanua wenye akili tu ndo watamuelewa mpina.
 
Kwanza sheria inasemaje kuhusu nani anatakiwa kuagiza sukari ikitokea hali kama hiyo? Pili kwanini Msukuma Aje kwenye media kutoa ushahidi wakati Spika alimwambie apeleke Kwakwe, kanuni za zinasemaje kuhusu alivyofanya Mpina? Hili swala ukiingia harakaharaka utalaumu au kumuona Spika mbaya ama Mpina yupo sawa lakini ukweli ni Kubwa Na Mpina amekosea kwenye kwa Media
Jikite kwenye mada kuu ya mleta uzi
 
Hivi wananchi kweli tunashindwa kuwaadhibu hawa watu mwakani kweli?
Wanaiba mchana kweupe, wanaingiza kura haramu mbele ya vyombo vya dola. Askari anakimbia na sanduku la kura mchana kabisa. Msimamizi anatangaza matokeo yake aliyokuja nayo, matokeo ya baadhi ya majimbo huwa yanazidi hadi idadi ya waliojiandikisha. Sijui wananchi watatumia mbinu gani nyingine, lakini 2025 lazima waendelee kushikilia dola na hawajawahi kuwa na nia ya kuibadilisha nchi hii kimaendeleo.
 
Kwahiyo kosa nii kwenda. Kwenye media. Je wakilisho lake liko sahihi?
Ukimsikiliza vizuri Spika point yake ni kwanini aende kwenye media wakati spika ndio ameitisha huo ushahidi, sasa kanuni za bunge zinamfunga mpina hata kama anaweza kuwa na Ushahidi sahihi dhidi Ya Bashe
 
Shida iko wapi ikiwa ushahidi huo huo Mpina alioupeleka kwa umma kwa sehemu akaamua kuupeleka kwa Spika?

Kwani ushahidi huwa ni jambo la siri lisilopaswa kujulikana kabla na watu wengine?

Spika na bunge walisema Mpina apeleke ushahidi kwao, sasa wamepelekewa ushahidi, waupitie huo ushahidi lakini wasilazimishe Mpina kutokujieleza kwa umma kwa jambo ambalo umma una maslahi nayo?

Kwanini Spika na bunge liingilie uhuru wa Mpina wa kujieleza nje ya bunge?
Hawalazimishi bali Kanuni ndio zinambana Mpina, ni sawa wewe uwe mgombea halafu ujitangazie matokea ya Kura Mapema Kabla ya Tume,, Mpina Hakupaswa kuja kwa Media angetulia kwanza
 
Unajua waandishi wetu wengi sana ni Bogus
Hapa ingekuwa wenzetu hiyo Stationary na kampuni ya simu tayari ingejukina na kuwekwa wazi hata kama ni ya Waziri, Rais au yeyote

Kama kuna freedom of information basi wayaweke bayana
 
h
Ukimsikiliza vizuri Spika point yake ni kwanini aende kwenye media wakati spika ndio ameitisha huo ushahidi, sasa kanuni za bunge zinamfunga mpina hata kama anaweza kuwa na Ushahidi sahihi dhidi Ya Bashe
hata sheria za makaburu zilikuwa sahihi wakati ule ila zilikuwa batili!!Hii ni sawa na kusema mwanachama wa chama cha siasa akiwa na mgogoro na uongozi wa chama hapaswi kwenda mahakamani akienda ndo amejifuta uanachama!!

Sheria m za namna hyo hatuzitaki.Sisi ndio umma na tunahaki ya kujua sio tu vitu vidogo kama hivi hata mikataba anayosaini mama we have to know basi angalau hata kupitia bunge!
 
Hapa kuna vitu viwili muhimu vya kutafakari
1:Ushahidi wa Luhaga Mpina kuthibitisha Bashe alidanganya bunge

2;Luhaga Mpina kuvunja kanuni za bunge

Ukifuatilia kwa makini la kuchukua nafasi kujadiliwa ni (Ushahidi wa Luhaga Mpina dhidi ya Bashe)

Lakini watanzania tulivyo wajnga tunamjadili Luhaga Mpina badala ya kujikita kweny maudhui ya Ushahidi aliotoa.

Hata spika katumia muda mwingi kumsema Luhaga Mpina badala ya kilichowasilishwa
Spika anamshambulia muwasilishaji ili iwe ngao ya kupotezea kilichowasilishwa,
 
Kwanza sheria inasemaje kuhusu nani anatakiwa kuagiza sukari ikitokea hali kama hiyo? Pili kwanini Msukuma Aje kwenye media kutoa ushahidi wakati Spika alimwambie apeleke Kwakwe, kanuni za zinasemaje kuhusu alivyofanya Mpina? Hili swala ukiingia harakaharaka utalaumu au kumuona Spika mbaya ama Mpina yupo sawa lakini ukweli ni Kubwa Na Mpina amekosea kwenye kwa Media
Ameenda kwa media kwa sababu anajua kutakuwa na twists na turns nyingi na mwisho wananchi(ambao ndio wamemuweka mjengoni) hawatajua ukweli.
 
Kuhusu hili suala la sukari ni jambo kubwa sana ambalo kimsingi Ni suala nyeti ambalo limaonyesha kiwango cha ufisadi kilivyo kithiri nchini
Na ambavyo hutaweza kuamini waziri ukimskiliza ni kama alikua na uchungu kweli na kwamba ana nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi ndio mana akatoa vibali kwa watu nje ya wale walio kwenye takwa la sheria kumbe wapi ndugu ni kuwahadaa chenga ya mwili tu
 
Wanaiba mchana kweupe, wanaingiza kura haramu mbele ya vyombo vya dola. Askari anakimbia na sanduku la kura mchana kabisa. Msimamizi anatangaza matokeo yake aliyokuja nayo, matokeo ya baadhi ya majimbo huwa yanazidi hadi idadi ya waliojiandikisha. Sijui wananchi watatumia mbinu gani nyingine, lakini 2025 lazima waendelee kushikilia dola na hawajawahi kuwa na nia ya kuibadilisha nchi hii kimaendeleo.
Ni ujinga wetu tu wananchi tukiamua kweli kweli haishindikani mkuu
 
Back
Top Bottom