Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

Hivi wananchi kweli tunashindwa kuwaadhibu hawa watu mwakani kweli?
Hili ni swali zuri sana ambalo wengi wetu tunasubiri jibu lake.

Kwa upande wangu, kama waTanzania wataona ni sawa tu, na hakuna chochote kinacho wastua na utawala huu, nitajuwa kwamba nchi yetu hii ipo chini ya laana. Ngoja tuvute subira.
 
Sijui wananchi watatumia mbinu gani nyingine, lakini 2025 lazima waendelee kushikilia dola na hawajawahi kuwa na nia ya kuibadilisha nchi hii kimaendeleo.
Umekuwa 'jumla' mno, kiasi kwamba umepitiliza na kuyafanya yaliyo kweli ndani ya andiko lako, nayo yakose uzito.

Wananchi wakipewa elimu, na kuongozwa vema, yote uliyo yaorodhesha kufanywa na CCM wananchi wana uwezo nayo sana..
Siyo kweli kuwa "...hapajawahi kuwa na nia ya kuibadili nchi hii kimaendeleo." Zungumzia haya tunayo yashuhudia sasa.
 
Ukimsikiliza vizuri Spika point yake ni kwanini aende kwenye media wakati spika ndio ameitisha huo ushahidi, sasa kanuni za bunge zinamfunga mpina hata kama anaweza kuwa na Ushahidi sahihi dhidi Ya Bashe
Hizo kanuni zinazomfunga Mpina alizitaja Spika? Mbona hiyo ingekuwa kazi ndogo tu ya kuifanya badala ya kueleza yaliyo njea kabisa ya jambo husika, kama kuelezea mapungufu ya Mpina alipokuwa waziri wa Uvuvi. kulikuwa na sababu zozote za maana kwa spika kuibua hayo?
 
Na ambavyo hutaweza kuamini waziri ukimskiliza ni kama alikua na uchungu kweli na kwamba ana nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi ndio mana akatoa vibali kwa watu nje ya wale walio kwenye takwa la sheria kumbe wapi ndugu ni kuwahadaa chenga ya mwili tu
bashe ni mwigizaji mzuri sana. Usipo kuwa mwangalifu anakupoteza haraka sana ndani ya kichaka..
Uliona alivyo kuwa akipaza sauti Bungeni? Maigizo matupu!

Uzuri wake, anajuwa kupangilia hoja, hata kama ni uongo.
 
What Mpina did is called OUTSMART😀 mbele ya Tulia kakosea, mbele ya wananchi katukosha saana 🤝. Bunge lipo kwaajili ya wananchi na wananchi tunamshukuru Mb. Mpina kutufikishia hili maana kama ushahidi ungepelekwa kwa spika it's obviously kuwa ungezimwa na wananchi tusingejua.
Sasa ni muda wa wananchi kufanya tathmini juu ya hawa wawakilishi wetu, tunaowapa dhamana mpaka ya kuunda serikali waendelee kuwepo katika hizo nafasi huku wakiendelea kuifisadi nchi kwa mgongo wa upole wa watanzania? Embu tuangalie wakenya wametuzidi nini kufanikiwa kulitikisa Bunge lao mpaka kubadirisha kanuni na sheria kandamizi juu yao?
Watanzania tuamke
 
Watu wa CCM wamekaa kimichongo michongo issue kama hii wao wanachukulia business as usual. Kifupi wanaona matumbo yao yanathamani kuliko wanaowaongoza
 
Hujaelewa hapa angalia utaona vibali vilicheleweshwa maksudi kwa viwanda vinavyozalisha sukari,pia utaona Moja ya kampuni ilisajiliwa ndani ya mwezi mmoja huko mzenjibar na ikahamia apo Daslam na kupewa tenda
Sema mkuu.
Naomba 'hardbody' na wasomaij/wachangiaji wa mada yake wakusikilize kwa makini.

Mwishowe itabainika Bashe ni 'Bangusilo' tu.
 
Bashe umetukosea sana watanzania. Tunataka ujiuzuru huo uwaziri kwa manufaa yako na Taifa kwa ujumla. Kama uliagizwa na sasa unabebeshwa lawama itajulikana tu. Hili la kampuni kusajiliwa ndani ya mwezi mmoja Z'bar na kupewa tenda kubwa kama hii bara tunalichungiza zaidi.
 
Hili sakata wakati nasoma uzi humu kwa mara ya kwanza nilikuwa sijalielewa lilivyo. Nikasema acha nizame U-tube kujua likovipi ndio nikapata kuelewa mwanzo, kati na mwisho ulivyo hebu twende pamoja kwa ambaye hajaelewa kama mimi kwa Lugha nyepesi

Iko hivi waziri wa kilimo wakati anawasilisha bajeti yake ya wizara, kwenye sakata la sukari alisema ametoa vibali kwa makampuni ya wafanyabiashara kuagiza sukari kiasi cha Tani 410 elfu kufidia upungufu uliopo wa sukari

Pia akashusha lawama kwamba kulingana na kanuni zilivyo, vibali ilitakiwa vitolewe kwa viwanda vinavyozalisha sukari ndio viweze kuagiza nje kama kuna upungufu lakini hivo viwanda ambavyo ni Mtibwa sugar, Kagera Sugar, Bagamoyo etc vimeshindwa kuimport hata kilo moja ya sukari kwa mda wa miezi 3 na kusababisha tatizo la upungufu wa sukari kuwa kubwa kama ilivyo sasa

Sasa Mpina yeye akampinga waziri kwamba taarifa yake ni ya uongo, Ikabidi spika wa bunge amwambie awasilishe taarifa kuhusu uongo wa waziri. Mpina akawasilisha taarifa iliyoeleza mambo mengi kusuhu uongo wa waziri Bashe ambayo siwezi kueleza yote humu ila mwishoni ntaweka video ili kwa ambaye hakupata nafasi ya kusikia awasilize wote kwa makini na kuelewa vizuri

Sasa kilichotikisa zaidi katika taarifa ya Mpina ni Jinsi Waziri Bashe alipotoa vibali kwa Makampuni yenye kujihusisha na Mambo tofauti kabisa na kilimo wala sukari kupewa vibali vya kuingiza sukari tena zingine zikiwa na Mitaji midogo ya hadi Tshs mil 1. Mfano kuna Kampuni inajihusisha na Stationary ina hisa 1000 zenye thamani ya mil 1 lkn imepewa kibali cha kuingiza Tani 2 elfu zenye thamani ya Tshs Bil 6.6😂

Kampuni nyingine Itel (kampuni ya simu na vifaa vya kielektronic) imepewa kibali cha kuingiza Tani 60 elfu yenye thamani ya Tshs Bil 160 wakati mtaji wa kampuni ya itel ni Tshs mil 50

Kwahiyo kwa kifupi inaonekana kuna makampuni yalikua hayana sifa ya kupewa vibali vya kuingiza sukari lakini kwa matakwa flani flani na kwa masilahi ya wachache yakaweza kupatiwa hizo dili.

MY TAKE: Spika Aunde tume ifanye uchunguzi wa sakata hili maana kuna harufu ya rushwa, uhujumu uchumi, ufisadi na makosa mengine kibao Kama kuna ukweli juu ya hili basi wote waliohusika wafukishwe kwenye vyombo vya sheria hii si sawa nchi inapigwa kizembe namna hii Watanzania tusikubali aisee tupaze sauti kukemea hili

Sakata lilianza hapa


Hapa ndio mpina akaitisha press na kufichuo uozo wa waziri

Pia soma:Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Ila spika tunae. Yaani anamuamini waziri, hamuamini mbunge, bunge linaisimamia aje Serikali kwa mtindo huu!
 
WADANGANYIKA tuko kimya! Kama mbuzi, kondoo au kuku wanaosubiri kuchinjwa!
Tuamke kama manyang'au!
 
Akili ikiwa 'njiwa', hata ukiambiwa hasara huwezi kuelewa.
Kwako, hasara ni mpaka serikali itoe pesa ndipo ujue imepata hasara?
Sawa mimi nimekiri sijui ni hasara gani wewe mtaalamu nifahamishe serikali imepata hasara ipi ?!
 
Hapa kuna vitu viwili muhimu vya kutafakari
1:Ushahidi wa Luhaga Mpina kuthibitisha Bashe alidanganya bunge

2;Luhaga Mpina kuvunja kanuni za bunge

Ukifuatilia kwa makini la kuchukua nafasi kujadiliwa ni (Ushahidi wa Luhaga Mpina dhidi ya Bashe)

Lakini watanzania tulivyo wajnga tunamjadili Luhaga Mpina badala ya kujikita kweny maudhui ya Ushahidi aliotoa.

Hata spika katumia muda mwingi kumsema Luhaga Mpina badala ya kilichowasilishwa
Acha uongo basi
 
mimi sijawahi kuwa 'kondoo' hata kwa sekunde moja, naomba usinijumuishe humo.

Sawa.

Wewe usiye Kondoo. Na mwenye Ujasiri wa Simba, chonde tuongoze sisi Kondoo ili kuwafurumisha Hawa mumiani waliogeuza Nchi yetu kuwa ni Miliki Yao...
 
Bunge la ccm... Wabunge wote ni ccm... Spika ni ccm... Mafisadi na wezi ni ccm... Wananchi wamesinzia wanasogezwa kama kete za draft!
 
Sema mkuu.
Naomba 'hardbody' na wasomaij/wachangiaji wa mada yake wakusikilize kwa makini.

Mwishowe itabainika Bashe ni 'Bangusilo' tu.
Huu ni mchongo hao viongozi wa serikali hawajui yaliyojaa kwenye mioyo ya watanzania walio wengi wamezoea na kuona wao ni royal empire ila tutashuhudia kipindi Cha KAMPENI mambo yatakuwa magumu kuliko miaka yote ambayo wamekalia hivyo viti ,watu wanashadadia yanayofanyika huko Kenya ila Wakati wetu tz wabunge watafanya KAMPENI chumbani ,we are still learning!
 
Back
Top Bottom