Sakata la Mtakaba wa DP World ni mtihani mkubwa

Kwa kweli ni mtihani mkubwa sana..., hawa wahuni walisaini mkataba bila kuusoma..., waliposikia tu Asalaaam Aleykum, wakamwaga wino kama vichaa....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Ukitaka kujua akili za wachangiaji basi angali michango kati ya wanaopinga na wanaounga mkono mkataba, ni dhairi kabisa utagundua kuna kundi moja hapa limepewa pesa na kuna watu wengine wasiyokuwa na akili za kwenda shule wao kazi yao ni kuwafuatata viongozi wao walichosema, na kuna kundi linalosimama kwa kigezo cha dini ya Uisilamu, yaani mtu akimuona muharabu anajua tayali ni Uisilamu wenyewe

Kwa waisilamu wanaojitambua Uisilamu umefafanua vizuri kabisa, mbora kwa Mwenyezi Mungu ni yule anayezifuata amri za Mungu na akazishika na sunna za Mtume Muhammad (S.A.W) na wala haungalii kipato cha mtu, Kwangu mimi hawa DP world wawekezaji kama kweli wangekuwa waungwana basi wangekuja na masharti mazuri ya uwekezaji kama Uisilamu wenyewe unavyofafanua
 
its not being 'crazy' but a simple debatable question? can you please elaborate the difference seen between the two contracts?
Wa TICTS ulikuwa na kikomo na haukuuza nchi nzima.....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Hakuna anaekula nyuma ya pazia zaidi Fisi meuh na mitoto yake Fisi beuh

hoja yako ni toothless
 
Makuhadi wa uchumi wetu wanaendelea kuuza raslimali zetu kila uchao!
madini walishauza
vitalu vya gas
sasa bandari!
 
Mleteni hapa Yuda atueleze kwanini alifanya hivyo, ona sasa wanakalibia kuparurana makucha usoni.
 
Membea na OAC umesahau?
 
'USALAMA WA TAIFA' - can you please explain in what context will our country be compromised?

why didn't anyone complain about TICT's which has been running the port for the past 20 years?
How can it be TICT ' s business ?!
 
hili ni pisi la kimba litakalowasumbua sisiemu kwenye uchaguzi wa 2025 na hawana hata la kujibu. aliye karibu nao awashauri waliondoe mapema, litawanukia hadi wakome.
 
Mkataba wa TICTS unafanana na wa DPW? weka hapa mkataba TICTS tuone.Na ulishasikia ticts anataka kwenda mahakamani kwa kustishwa mkataba? Jua kwamba kwa dpw hilo jambo la kusitisha mkataba halitokuwepo ukijaribu tu jua nchi umeliwa.
 
Huo mkataba wa uendeshaji bandari uko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…