Sakata la Mtoto wa Rose Nungu (MunaLove), Linaumiza Sana Moyo


Nakuunga mkono hakukuwa na sababu ya yeye kusema mtoto ni wa nani kwa kipindi hiki saa ingine na busara itumike tu mdomo siku zote unaponza kichwa. Yeye a focus kwenye msiba wa mwanae na sio kuanza kujibu walimwengu kwenye social network haimsaidii kitu zaidi ya kumdhalilisha tu na kumuongezea machungu at the end hata u explain vipi people believe what they want to believe
 
Mkuu,utajilazimisha kuwa baba wa mtoto ambaye mama yake amekwambia wewe sio baba wa huyo mtoto?
Mkuu, mwanamke akikwambia neno siyo unalichukua 100 percent na kuact kama yeye alivyotaka wewe uact, sometime unatakiwa kuonesha ukomavu kwa sababu siku zote utabaki kuwa kichwa cha familia, Zacharia hata kama si biological father wa huyu mtoto, ameonesha ukomavu. Huwezi kususa maiti kisa mama kasema mtoto hakuwa wako!
 
Ila kiukweli huyu jamaa hata kama ikionekana mtoto sio wake lakini ame-play part yake kama mzazi kama yote aliyozungumza yana ukweli kuanzia kutoa huduma za kifedha n.k ...mambo mengine ya migogoro ya familia hiyo tunaachia
 
Huyo Zacharia atawashinda kabisa na huo mwili kamwe hautozikwa mpaka mahakama ifanye maamuzi....mtoto alizaliwa ndani ya ndoa na baba amekuwa akimuhudumia kabisa...
Hapa Zacharia lazima awashinde na mimi namshauri akaweke zuio mahakamani Muna asizike kabisa.....
Nitamshangaa sana Zakaria akikubali Muna azike mtoto ,atumie njia yeyote ile mtoto asizikwe mpaka ukweli ujulikane...ikiwezekana ni kuanzisha mtiti kama njia ya mahakama itashindikana....Hii itakuwa fundisho kwa wanawake wanaopenda kuuza miili yao bila kujali kitakacho tokea mbele....
 
Kama alizaliwa ndani ya ndoa huyo ni wa kwake....
Hili jambo likipelekwa mahakamani Zacharia anaweza kuwashinda kabisa....
Jambo liko serious sana......... kuwa baba wa mtoto hakuishii kwenye kutoa mbegu tuuu
Kweli kabisa mkuu, na hata exhumation order inatoka kabisa kama atazikwa kinyume na matakwa ya baba, hili siyo suala dogo ujue!
 
Pumzika kwa amani baba.Siku zote mototo hana hatia kwa tofauti za wazazi,cha msingi wampumzishe wanetu bila malumbano.
 
hapa Muna atumie tu busara ashirikiane na mumewe wamzike mtoto.....kama nguo imeshamvuka kinachofuata ni kuchutama tu
 
hapa Muna atumie tu busara ashirikiane na mumewe wamzike mtoto.....kama nguo imeshamvuka kinachofuata ni kuchutama tu
Umenena vyema, hiyo ndiyo njia pekee ya kusolve hii crisis
 
Sasa wanaume na wanawake tutatofautishwa kwa mavazi...yaani sakata la muna liniumize moyo mimi huku Kimara? Katafute kazi ya kufanya utajikuta mambo ya watu wengine wala hayakusumbui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…