Hawa watoto watu mnatakiwa muwe makini nao sana,mimi binafsi nimewahi kua mwalimu wa bweni shule flani ya binafsi,kesi Kama ya huyo binti ilikuja ikamkuta msaidizi wangu ambaye ni mwalimu pia wa kiume,kidogo aende jela,inshu ikaja kuishia mahakamani.Ila hadi kipindi kesi iko mahakamani,binti alikua anasisitiza kabakwa na alikua analialia kinoma,watu wa haki za wanawake kilamara wakawa wanatembelea shule kuja kunihoji,muda huo jamaa yuko mahabusu anateseka.Mwisho wa siku akaja akaonekana yule mwalimu hana hatia.Namuonea huruma sana huyo mwalimu Jimmy,ukute aliombwa akamsaidie mwalimu kuondoa wachelewaji,maeneo ya bwenini,akasingiziwa kama abavyosingiziwa.