The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Msemaji wa serikali ndg Gerson Msigwa akitoa mrejesho wa kinachoitwa kikao cha serikali na TUCTA leo tarehe 26/7/2022
Lugha gongana. Msemaji wa serikali anasema hivi, TUCTA wanasema vile. Ni kama kuna kurushiana mpira. Gerson Msigwa anaongea kana kwamba TUCTA ndiyo mwajiri na mlipa mshahara wa watumishi wa umma. Wasikilize TUCTA hapa, kisha msikilize Gerson Msigwa. Total lugha gongana..!
.............................................._________________
Binafsi baada ya malalamiko ya wafanyakazi wa umma wa nchi hii yaliyotokana na "tafsiri ya nyongeza ya 23.3%" kuwa kinyume na matarajio yao...
Basi kila mtu alitegemea serikali ije na kauli mojawapo kati ya hizi mbili kuwaambia watumishi wa umma wote, kwamba;
1. Mlichokiona kwenye mishahara yenu ya July, 2022 ndicho hicho hicho, na ndiyo maana ya 23.3%, ya nyongeza yenu, hakuna kingine zaidi. FANYENI KAZI...!
AU
2. Serikali inawaomba radhi watumishi wa umma wote kwa kuwa kulifanyika makosa ya kiufundi ktk mfumo wa kikokotoo cha mishahara. Serikali inarekebisha makosa hayo kuanzia August, 2022. HUU NDIO UUNGWANA.
Lakini huu mchezo unaoendelea kati ya TUCTA na serikali ni siasa za kijinga sana na ni kuwadhihaki wafanyakazi wa umma na kuwafanya hamnazo.