The Khoisan, nyongeza ya 23.3% wala sio mbaya na siyo ndogo hata kidogo iwapo tu kanuni sahihi ya kuitawanya kwa kila mnufaika ingetumika...
Obviously, kuna uhuni umefanyika katika distribution ya kiwango hicho cha nyongeza kuanzia wa mshahara ngazi ya chini hadi yule wa ngazi ya juu kwa kila kada ya utumishi...
Ni kuwa, huyu Mwigulu Nchemba na wenzake pale wizara ya fedha + wizara inayoshughulikia mambo ya utumishi, walitumia kanuni ya maamuzi yao kichwani...
Mbona miaka yote especially ile ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (2005 - 2015) nyongeza za namna hii zilitoka mara kwa mara, lakini kanuni ya kumpatia kila mtumishi haijawahi kulalamikiwa kama ya sasa...??
Mimi naamini ishu siyo uhaba wa fedha wala nini bali ni uhuni tu wa baadhi ya viongozi wasaidizi wa Rais Samia...
Nina hakika Rais hata yeye anashangaa na lazima kawaweka kiti moto wahusika wa utekelezaji wa hili...!!
I believe something is wrong somewhere...