Sakata la picha chafu: Wema, mama Wema kusoma albadili

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
SIKU chache zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu.

Wawili hao wako kwenye mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni, Risasi Jumamosi linakumegea.

Picha hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na kichwa cha mama Wema.

Lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si yeye na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku watu wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika.

KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye kufedhehesha.

"Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.

"Wiki iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili.

"Wamesema kwanza kabla ya tukio hilo la Abdadili wametoa siku saba kwa yeyote anayejijua amehusika na picha zile za kutengeneza aende mwenyewe kwa mama Wema, nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar) ili kuomba msamaha.

"Kama zitapita siku saba na hakuna atakayejitokeza, Albadili itasomwa na mmoja baada ya mwingine watakufa.

Tayari wameshawasiliana na mashehe ambao watasoma Albadili hiyo," kilisema chanzo hicho.

WEMA AYEYUKA HEWANI

Baada ya kusikia kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika, juzi Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo lakini muda mwingi wa maandalizi ya habari hii, simu yake haikuwa hewani!

MAMA WEMA SASA

Baada ya kumkosa Wema, Risasi Jumamosi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.

KUHUSU ALBADILI

Akizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema: "Ni kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili.

Haiwezekani watu wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo."

KUHUSU MASHEHE

"Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa.

Kama hakuna atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema."

NENO LAKE KWA WAHUSIKA
"Nawaambia wale wote wanaojijua walihusika na ile picha ya uongo, ya kutumbukiza kichwa changu kwenye picha nyingine na wale waliohusika kuitupia kwenye mitandao, waje waniombe radhi kabla siku saba hazijaisha, sitanii jamani."

UKWELI WAKE

"Mimi ni Muislamu safi, nasema sijawahi kupiga picha za namna hiyo katika maisha yangu tangu nizaliwe mpaka utu uzima wangu huu na wala sijawahi kufikiria.

 
Unapofanya jambo ambalo unajua litadhuru watu unatofauti gani na uchawi kama sio mshirikina? Jambo lenyewe lishatokea mwezi umepita leo ndo wanajifanya kusoma albadili, huo uchawi tu mi naona

Waoo waende kwa waganga tuuu
 
Hamna cha Albadili wala nini...Hayo ni matisho mbuzi

Anamtisha nani wakat watu washajionea mpododo huo aka kipwapwiso, akasome tu albadili asije tu kushangaa inampata mwanae wema maana na yeye hata haaminiki usikute zile picha kasambaza yeye ili aongelewe zaidi maana kwa wema kila kitu kinawezekana mbele ya umaarufu
 
bwahahahaha, eti watakufa!1..hahahhahaha1..hivi yule dogo alikojoleaga buku la dini alikuwa?
wekeni picha tufaidi jamani!
 
hv jamani huyu mama anajua thamani ya umama kwell?anafahamu hadhi ya uanamke au kuitwa bibi?kwa ninj ana act km mtoto mdogo lakini?hv hao global wanamlipa sh.ngapi labda mpaka anakubali kujidevalue kias hikk?mbona mmwe was respectable person?kwa nini hatunzii heshma mabinti zake wengine?ana mapepo or laana?how do u fill to have such kind of mama?nimeimia kama namjua vile kwa sababu mimi ni mama wema anaweza akawa mama yangu kabisamana ana
mabinti mi mdogo sana kwako!hajui km kukaa kimya ndo jibu la mjinga.....!hv kuna supa staa mwenye skendo km uwoya mbona mzazi wake hatumsikii,wolper je?na wengineo...please mama tulia na ujane wako unadhalilisha sana jinsia yetu na km kuna wanaokuunha mkono ni wehu sana!mi team wema mniite hater tu kwa kweli but km kuna wanaokuunga mkono hao wana madegedege wote.....!
 

Eeee nyoka atazaa nyoka siku zotee WEMA kamrithi mama yakee kila kituuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…