Sakata la 'Plea Bargain': Wadau wamwandikia barua Rais Samia kutaka amuondoe Biswalo Mganga

Sakata la 'Plea Bargain': Wadau wamwandikia barua Rais Samia kutaka amuondoe Biswalo Mganga

Hii nchi yetu tunaongozwa kama vile hatuna vichwa.

Tunaishi kwa matakwa ya aliyepo madarakani.

Hatutaendelea kamwe kwa staili hii.

Tunapaswa kuwa na taasisi imara na sio kuongozwa na matakwa ya mtu.
 
Wewe unahemka bila kuijua sheria au katiba 8nasemaje kuhusu jaji wa Mahakama.

Kuna nafasi amvazo Rais anaweza kuteua lakini hawezi kutengua.
Acha kuwa mjinga soma vizuri. Nimesema utaratibu unafuatwa ambao ni tume ya kijaji ya majaji 3 toka nchi za madola kuchunguza na zikiona anastahili kuondolewa basi Rais anamuondoa. Ni nini hujaelewa hapo?
 
Anayewateua ni nani ? halafu labda kwa faida yako na mamluki wengine kama wewe ni kwamba hatujawahi kuogopa vitisho vya kibwege , nakupa onyo la mwisho , usijaribu tena kunitisha .
Wewe cheza mbali.......................onyo?!!!!! Haya tuone
 
Naona Raia mwema ni gazeti la udaku lililopooza...linajitahidi kutumia nguvu nyingi kuziba gape lililoachwa na magazeti ya Musiba..
itaandika hizi issue ht mwaka mzima na hakuna kitu itafanyika...kukaa na kujadili udaku km huu ambao hautakuja kufanyiwa kazi ni matumizi mabaya ya muda na Ubongo.
bado unaamini ni udaku ?
 
Duh!
hii ni aibu na fedheha kwa Majaji wetu, maana Majaji hawatakiwi kuwa na madoa ya uchafu.
 
MBOWE KWA SASA TUNALAMBA NAYE ASALI.... HATAKI HATA KUMTINGISHA MAMA. "MJINI HAPA KAA KIMASTER"
 
Bwana Bams, Jaji hakamatwi kizembe bila kufuata utaratibu maalumu. Hata marehemu Jaji Moses John Mwakibete alivyovuliwa ujaji kwa tuhuma za rushwa hakukamatwa kizembe kama ambavyo wengi mnapendekeza. Katiba iko wazi kabisa kuhusu utaratibu wa kumuwajibisha Jaji wa mahakama kuu. Haya mengine ni mihemko ya kisiasa na hasira zisizokuwa na matokeo mazuri.....
Kwahyo umemaliza au umetupa taarifa za mwakibete

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Kwahyo umemaliza au umetupa taarifa za mwakibete

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Nimefanya vyote: Nimewapasha taarifa za utaratibu wa kikatiba uliotumika kumwondoa Mwakibete, na kumalizia kuwaambia ukweli mchungu kwamba Jaji haondolewi kizembe bila kufuata utaratibu. Aidha ajiuzulu mwenyewe, au katiba ifuate mkondo wake. Hizi nyingine ni upepo wa siasa ambao utapita tu.....
 
Back
Top Bottom