Uchaguzi 2020 Sakata la Sheikh Ponda na "masheikh rasmi"

Mimi kinachoniuma Sheikh Kipozeo yupo Bakwata!
Huwa napenda kuangalia clip zake japo mi mkatoliki
Sheikh Ponda anajielewa sana yule Baba.Mungu ampe maisha marefu.
Huna lolote
 
Wamekandamizwaje
 
mapico naheshimu sana mawazo yako kaka ila kwa hili la zanzibar kuhusu kuwatesa wakiristo kipindi cha mfungo sio kweli,kuna maeneo maalum yamewekwa kwa ajili ya watu kupata chakula ,kula hadharani kwa watu waliofunga ambao asilimia 98% ni waislam hii ni kuwadhihaki na kutoiheshim imani yao.
napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kaka yangu mapico
 
Ona sasa,kwa mfano huyo Lipumba asingerekodiwa ina maana ungekataa kuwa Lipumba hakuwahi kumpigia kampeni Kikwete kwa sababu hakuna video kumuonesha Lipumba akifanya hivyo. Na hapo ndipo lilipo tatizo,kwa sababu mfano huku misikitini yanatokea mengi tu ila hayarekodiwi hata huyo Lipumba mara nyingi tuanafanya siasa msikitini ila hakuna video wala audio.
 
Naona unajizungusha tu na hii ni kwa sababu siku hizi imekuwa tatizo sio ccm bali Magufuli.
 
Upo nchi gani ndugu, unajifanya huelewi kabisa kama vile umeweka pamba masikioni. Ngoja nikujibu hapa hapa.

Kuna orodha ya mashekh na Viongozi wengi wa dini ya Kiislamu wanaimba chagua Magufuli, Chagua Magufuli. Hao haujawaona eeeh?

Hivi unajua msimamo uliotolewa na viongozi wa BAKWATA ni kuona waislamu wanamchagua Magufuli.

Hivi unajua maaskofu wengi wakubwa wa madhehebu ya Kikristo kuanzia Pentekoste, Sabato, Lutheran, Anglicana, Katoliki wapo bega kwa bega kuwaambia wakristo wamchague Magufuli.

Kabla hujamkosoa Ponda kwa kitendo chake cha kuwaomba waislamu wampe kura Lissu, basi anza kwanza kuwaza kinachofanywa na viongozi wengine wa dini.
 
Kafir ni neno la kiarabu lenye maana ya mpingaji. Katika muktadha wa dini ya kiislamu, kafir ni yule anayepambana kuupinga uislamu hususani kwa njia za hila na udhalimu. Uislamu hauna tatizo na uwepo wa dini zingine au uwepo wa ubagani, maana dini hizo zilikuwepo na zitaendelea kuwepo regardless ya uwepo wa uislamu.

Na hapa narudia tena kusema, Bakwata ni kikundi cha makafir. Wako pale kulinda matumbo yao huku wakijivika kilemba cha unafiki wa dini ya kiislamu lakini kiuhalisia hawana uchungu wowote na uislamu au waislamu.

Ulishaona wapi masheikh wanakunywa pombe, wanakula kiti moto au wanaomba dua kwa jina la Yesu? Njoo Bakwata utawakuta.
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako) kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?
Wafanye tu ndiyo demokrasia
 
Serikali ya ccm haiwezi kukwepa lawama hii ya kuliingiza taifa kwenye mpasuko mkubwa sana.

Kuna vitu mmevilea na sasa vinataka kulivuruga taifa.

Naona mpambano wa "wakristo"(waprotestanti) wakiungana na waislamu dhidi ya mfumo wanaoamini ni "mfumo katoliki".

Nikitazama kauli za viongozi wengi wanoheshimika wa madhehebu ya kiprotestanti na uislamu,ndani ya miaka hii 5 wamekuwa very negative na uongozi uliopo.

Na mwenendo wa kampeni hivi sasa unadhihirisha mpasuko huu.

Sikuwaza kabisa kuwa huenda uchaguzi huu ukawa mgumu hivi!

Haya mazimwi mliyatengeneza na kuyatumia dhidi ya upinzani miaka ya nyuma,sasa yanataka kuwatafuneni wenyewe.Mungu atunusuru,yawatafune peke yenu na kutuachia taifa letu salama.

Ila namtahadharisha Lissu asiingie makosa ya wakina Mzee wetu (namheshimu sana) Nyerere.

Viongozi wengi wa taifa hili wamekuwa wakitumia makundi fulani yenye nguvu (kama ukristo au uislamu) kisiri kupata majority.Halafu baada ya kupata uongozi wanayaswaga makundi hayo na yanawaletea shida baadae.

Mfano mzuri ni Nyerere na waislamu waliomsaidia sana wakati wa kupigania uhuru wa nchi.

Hadi leo vilio vya waislamu hao bado vipo,mwandishi wa uzi huu ni mfano mzuri.Makala zake nyingi zinajieleza zenyewe.

Kama Lissu anasimamisha sheikh kumuombea kura za waislamu,aelewe kuwa atakapopata kiti cha urais,ana deni nao na anapaswa kudeal nalo bila kuathiri wale wengine.
Kwa ufupi atakumbwa na mtihani wa kuunganisha taifa kutoka katika makundi ambayo yeye pia amefaidika nayo.

Hili ni suala gumu,Lissu pamoja na Magufuli,yeyote atakayeshinda uchaguzi huu,anapaswa kuhakikisha kufikia 2022 makundi haya either yameungana au yanaheshimiana na kukubaliana kwa amani na pia kuanzia 2025 watanzania wahamasike kupiga kura kama watanzania,na sio kama waislamu,wakristo,wasukuma,wachaga,maskini,matajiri etc.

Ila kwa hili ccm mtuombe msamaha,mmetutia kwenye wakati mgumu kama taifa.Haikuwa lazima kutufikisha huku na muda wa kutosha mmekuwa nao madarakani.
 
Lissu awachezesha "Makirikiri" CCM huko Ruvuma
 
Naomba neck wamzuie huyu shehe ponda,,anakera sana,,ikibidi mali zake zote zitaifishwe na afungwe...
 
Mkuu nichangie kidogo. Bakwata wao watangaze hadharani na mufti wao eti mitano tena. Akija huyu akisema mitano kwanza ndio nongwa. Nahisi wanaogopa km Tundu Lissu akichukua nchi wao na familia zao watakua hawana vibarua wachumia tumbo hawa.

Mwisho kabisa wewe ni verified member na kuna wachangiaji naona km wanakujua wengine wanakuita mzee. Waweza weka picha yako nikuone? Asante na samahani lkn.
 
Mie bila kuingilia dini kinachonichekesha Mashekh walioko Bakwata wakimpigia Debe Magufuli ni Sawa. Ponda kachagua upande wake WA haki imekuwa Nongwa.
 
Sheik ponda ameamua kuimalizia heshima ndogo aliyobaki nayo kwa kulamba matapishi yake

Sheikh ponda uzee unamuendea vibaya
 
Nimekosoma vyema na kukuelewa vizuri. CCM ndio adui mkubwa wa nchi yetu, anapenda kutugawa ili aweze kututawala. Kwa sasa mpango ni mmoja tu, watanzania tunapaswa kuweka tofauti zetu za kidini, kiitikadi au kikabila pembeni, tuwe kitu kimoja ili tuitoe CCM madarakani. Baada ya hapo tufanye maridhiano, tujenge upya mifumo yetu.

Kama haujui tu, ni CCM ndio iliyowagawa waislamu, na inafurahia hilo. Mivutano iliyopo miongoni mwa makundi ya kiislamu ni mikubwa sana kuliko baina ya waislamu na dini zingine.

Ni CCM ndio ilipeleka siasa kwenye nyumba za ibada. (Yaani umekuwa ni utaratibu rasmi kwa viongozi wa kisiasa (kiserikali) kuwa wageni rasmi kwenye maadhimisho ya kidini, na huko wanazitumia kama majukwaa ya kisiasa).
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako) kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?
Kwani hawajatangaza bado? Hivi Askofu kwenda kwenye kampeni za Magufuli na kutangaza huyu ndio anayefaa kuchaguliwa, si ndio Kama alivyofanya Ponda?
 
Umetoa mada nzuri sana. Labda kwa kuongezea, waislam wa Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa wakiongozwa kama ng'ombe. Ng'ombe ukiwatia kwenye zizi moja ni rahisi kuwadhibiti.

Tofauti na wakristo, wao wanaongozwa na makanisa mengi tofauti na si rahisi kuwaswaga kama ng'ombe.
 
Maisha yataacha kwenda kwako wakati unatembelea VX la serikali? Maisha yanakwamaje kwako kwa mfano?
Madaraja ni sehemu ya maisha na hayakuja kuondoka ili watu wote tulingane,Cha msingi pambania maisha yako achana na siasa uchwara.Hata hao unaowapigania waingie madarakani nao wanatembelea VX na wana maisha mazuri,Ila Shida yao ni wanafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…