Uchaguzi 2020 Sakata la Sheikh Ponda na "masheikh rasmi"

Madaraja ni sehemu ya maisha na hayakuja kuondoka ili watu wote tulingane,Cha msingi pambania maisha yako achana na siasa uchwara.Hata hao unaowapigania waingie madarakani nao wanatembelea VX na wana maisha mazuri,Ila Shida yao ni wanafiki.

Sawa kabisa, ila tunataka wanaotembelea VX sasa na kuharibu biashara zetu, na wao waje mtaani wafaidi kazi ya mikono yao.
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako) kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?
Hao wote mbona inajulikana wapo CCM ndugu au wewe upo Nchi gani ??
 
..mimi kitendo cha kusalimia "Bwana Yesu Asifiwe" na " Asalaam Aleykum" ktk shughuli za kiserikali naona tayari ni UDINI.

..Na jambo hili lilianza kidogo-kidogo awamu ya Mzee Kikwete, lakini likashika kasi kubwa kabisa ktk awamu ya Raisi Magufuli.

..Magufuli alianza kualika viongozi wa Dini ktk kila shughuli za Kiserikali, kitu ambacho huko nyuma hakikuwa kikifanyika.

..Sasa kama Magufuli amekuwa akijihalalisha kupitia viongozi wa dini, basi lazima wapinzani wake nao watajaribu kupita humohumo alikopita yeye.

..Kama kila shughuli au tukio la kiserikali iliyoko madarakani linahusisha viongozi wa dini, kwanini walioko nje na wanaotaka kuunda serikali nao wasihusishe viongozi wa dini ktk harakati zao?

..Lakini kibaya walichokuwa wakifanya viongozi wa dini waliokuwa wako karibu na Magufuli ni kuleta element za kiimani ktk maamuzi ya serikali. Yaani walikuwa wanahubiri kwamba anayoyafanya Magufuli na serikali yake yanaongozwa au yanahalalishwa na maandiko matakatifu ktk misahafu.

..Aliyetufikisha hapa ni Magufuli, na tatizo lake ni kwamba hana kipaji cha kuongoza, na kujenga hoja zenye ushawishi kwa wananchi. Hali hiyo ndiyo inayomsababisha awatumie viongozi wa dini kama "bakora" ya kusimama, vinginevyo atadondoka kisiasa.
 
Ni vizuri umetambua hilo.
Sio nimetambua bali nimeonesha tatizo,kwa sababu bila ccm huyo Magufuli asingekuwa hapo alipo na watu wameanza kulalamikia ccm kabla ya Magufuli,sasa nashangaa sasa hivi watu hasira zote zimeamishiwa kwa Magufuli tu wakati wanajua tatizo ni ccm.

Hata suala la masheikh wa uamsho walikamatwa na serikali hii ya ccm chini ya JK ila lawama anabebeshwa Magufuli.
 
Sheikh Ponda angekuwa anatueleza waislamu ni faida zipi ambazo tutazipata sie kama waislamu kwa kumpigia kura TunduALissu.
 
Sasa unamtenganisha vipi Magufuy na ccm? Mbona mazuri yote anasema ni yeye ndio amefanya na amevunja rekodi?

Iweje kwenye mabaya hasiusike yeye? Au yeye ni wa mazuri tu mabaya ya kina Mbowe?
 
Kwa kukusaidia, nenda Facebook search Mohamed Said utamkuta huko utapata maarifa makubwa na ufahamu kupitia kalamu yake.
 
na hapo wamekosa la kusema coz shekhe Ponda anamtetea mkristu ingekuwa muislam ndo wangemzushia kedekede,hakika awamu hii yamewakuta
 
kwanza hakuna kiongozi wa kikristo anayekubalika na wakrsto halafu akasema eti mchague magufuli
 
Hayo unayoeleza yamepitwa na wakati. Yoote yalishaelezwa enzi za Mkapa na Kikwete na wakati huo yaliigawa nchi (hasa mitandaoni) katika makundi ya chuki. Kubenea na yule mwalimu wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na wewe pia walikuwa wakuu kupenyeza hizi chuki kwa Watanzania. Sasa naona na wewe unaanza kupenyeza hizi chuki za kuwagawa Watanzania. Ebu tueleza Ponda kafanikisha kipi ambacho Wailslam hawakuwa nacho kama sio kula hela ya kikundi cha Kiislam cha Saudi Arabia kinachoitwa Wahhabi. Tunajuwa kikundi hicho na mrengo wake wa Wahhabism kina pesa nyingi za kuwapa wake na Ponda kwa ajili ya destabilzation siyo wasiyowaislamu tuu, bali hata kwa Waislamu wenzao. Ponda na kundi lake hupata nguvu za kipesa kutoka huko kueneza chuki kati ya Waislamu na Waislamu na pia kati ya Waislamu na wasio waislamu na naona ndiyo wimbo unaimba wewew sasa hivi. Achana na fikra za kuwagawa Watanzania. UKITAKA HAMIA SAUDI ARABIA UJIUNGE NA WAHHABBI, LAKINI NASIKIA HWAMKARIBISHI JITU JEUSI KAMA WEWE.
 
na hapo wamekosa la kusema coz shekhe Ponda anamtetea mkristu ingekuwa muislam ndo wangemzushia kedekede,hakika awamu hii yamewakuta
Hamtetei mkristu wala Muislamu, anatetea umbo lake. Anajaribu kuonyesha pesa ya Wahhabbui haijapotea inatumika vizuri.
 
Hao wakatoliki na walutheri ni wa Tanzania hii au nchi nyingine.Hivi Katika Tanzania kuna mtu au jamii ambayo haijapitia chungu ya shubiri ya Huyu mungu wa chato?
Mimi sijapitia na sijaiona
 
Kwa kukusaidia, nenda Facebook search Mohamed Said utamkuta huko utapata maarifa makubwa na ufahamu kupitia kalamu yake.
Poa poa

Aaah nimeenda Mohamed Said wako kibao. Who is who God knows.
 
That is very true

Nyie wenzetu mnaweza kuisema serikali na kuikosoa sisi tunatakiwa kuisifia kila siku na hili halikubaliki.
 
Jambo moja tu mimi ninalolielewa Waislam awamu hii wanakwenda na Lissu full stop!
 
Waislamu tunajua ni nani mtetezi wetu, nani wa kumwamini na ni nani msanii; sijui kwa nini mashekh wote wa Tz wamepanic again Sheikh Ponda.
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako) kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?
Kwani nani alikwambia kuna mtu kwenye dini ana influence kura zetu.

Hivyo wewe anayekuambia cha kufanya ni mchungaji, sheikh au padri?!

Hata Pope akipanda jukwaani aseme asemacho kura ni kwa Lisu na chadema tu.

HAKI utangulia kabla ya amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…