FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
Dogo ungemaliza kwanza stori zako zingine ambazo hazijaisha. Sioni kama ni busara kujaza ma hadithi kibao ambayo yapo robo robo!Kama wewe ni mpenzi wa simulizi kali sana za kijasusi na kipelelezi, kama unapenda simulizi zinazohusu michezo ya siasa na namna watu wanavyo iishi siasa kikatili.
Kama wewe ni mpenzi wa simulizi ambazo nafsi moja inaishi kwa watu zaidi ya mmoja.
Kama wewe ni mpenzi wa simulizi kali za mapigano na stori kali sana.......BASI UWANJA NI WAKO TWENDE SAWA KWENYE MOJA YA SIMULIZI BORA SANA AMBAZO UTAFUNGA NAZO MWAKA HUU.
SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU.
Kwenye kalamu ni mimi mwenyewe FEBIANI BABUYA.
Wao wapenda kuniita Bux the storyteller.
Wasalaam.
View attachment 2818481View attachment 2818482
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
EheSIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA KWANZA
Ndani ya ofisi moja kubwa sana, alikuwa anaonekana tajiri mmoja ambaye bila shaka umri wake ulikuwa umeenda kiasi cha kutosha. Mzee huyo mwenye kitambi cha wastani ambacho kiliashiria ukwasi ambao alikuwa nao, alikuwa ameketi kwenye meza yake ghorofa ya juu zaidi ndani ya ofisi yake hiyo.
Meza yake upande wa mbele ilikuwa imeandikwa CHAIRMAN kwa maandishi makubwa kisha likafuatia jina lake ambao lilisomeka kama Apson Limo, bila shaka yeye ndiye ambaye alikuwa mmliki wa hizo ofisi kama sio kampuni kwa namna ilivyokuwa inaonekana humo ndani. Ofisi ilikuwa imepambwa kwa vitu vya gharama sana huku ukutani kukiwa na picha kubwa mbili ambazo zilionekana kwa usahihi sana.
Kulikuwa na picha moja ya kawaida ya muasisi wa taifa la Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere lakini pia upande wake wa juu palikuwa na picha kubwa sana ambayo bila shaka ilikuwa ni ya familia. Kwenye picha hiyo alikuwa anaonekana yeye, mama mmoja ambaye bila shaka alikuwa ni mkewe lakini pia walikuwa wanaonekana watoto watano ambapo kati ya hao watoto watano, mmoja tu pekee ndiye alikuwa ni mtoto wa kiume kati yao. Ni picha ambayo ilikuwa inaonyesha namna familia hiyo ilivyokuwa kwenye furaha kubwa sana maana wote walikuwa ndani ya tabasamu zito mno ambalo usingeweza hata kujisumbua kulielezea kwani mtu angeiona tu picha hiyo angeelewa ni kwa namna gani familia hiyo ilikuwa kwenye hiyo furaha kubwa.
Upande wa mkono wa kulia mwa ofisi hiyo ukutani, kulikuwa na maneno makubwa ambayo yalikuwa yanang’aa sana yakiwa yapo chini ya nembo ya kampuni hiyo yakiwa yanasomeka LIMO INVESTMENTS. Ofisi hiyo kubwa ilikuwa pia imenakshiwa kwa vito vya thamani sana ikiwemo na samani za kutosha huku ikiwa na sehemu nzuri sana ya wageni kuweza kukaa na sehemu ya kufanyia mazungumzo ambayo yangekuwa ya mhimu na kumfanya mhusika aongee na tajiri huyo moja kwa moja.
Mzee huyo akiwa ametulia kwenye hilo eneo anaangalia kwa umakini sana jina la kampuni yake ukutani na kuwaza namna alivyoweza kutoka mbali na kampun hiyo mpaka ikaja kusimama vyema na kuwa moja kati ya makampuni makubwa sana nchini, simu yake ya mezani ilimshtua kutoka kwenye mawazo baada ya kuanza kupiga kelele kwa nguvu, akaipokea.
“Mruhusu aingie” ni kauli moja tu ambayo aliitamka bila shaka aliipokea simu ya ugeni kutoka kwa katibu wake ambaye alimpa ruhusa kuweza kumruhusu mtu ambaye alikuwa amefika hapo. Ndani ya muda mfupi mlango ulifunguliwa, aliingia mwanaume mmoja ambaye naye umri ulikuwa umemtupa mkono kidogo akiwa ndani ya suti ya gharama mno na fimbo yake mkononi bila shaka.
“Karibu sana Mr Mafupa” alimkaribisha mgeni wake huku akiwa ananyanyuka kwenye kiti chake na kumpa mtu huyo mkono na ilionekana kwamba walikuwa wakijuana sana.
“Nadhani sio waafrika wote ambao hawajastaarabika, kuna watu mpo safi sana na huo ndio utamaduni wetu waafrika bwana lazima tusalimiane kwanza hata kama hatupo sawa” Mr Mafupa alijibu naye huku akiwa anaukutanisha mkono wake na mheshimiwa Apson Limo.
“Ujinga wa mtu mmoja usiujumlishe kwa waafrika wote, sio kawaida sana wewe kuja hapa, nilivyo ipata taarifa kwamba unahitaji kuniona nilishtuka kidogo kwamba kwanini usingesubiri sehemu nyingine nje na hapa tukakutana ila nikaamua kukubali kwa sababu nilijua huenda una shida ya mhimu sana” mr Apson aliongea akiwa anaketi baada ya kuhakikisha pia mgeni wake ameketi chini kwa ajili ya mazungumzo.
“Mhhhh sehemu yoyote ile inafaa kwa mazungumzo hususani kwa wanasiasa na wafanya biashara kama mimi na wewe, vipi mwanao alisharudi kutoka masomoni? Maana ni muda sana naskia yupo nje ya nchi”
“Sio muda anarudi nadhani kwa sasa amemaliza masomo yake”
“Kwahiyo anakuja kumsaidia baba yake kwenye mambo ya kampeni? Maana ndiye mtoto wa pekee wa kiume uliye naye”
“Ni vizuri kama ungeenda moja kwa moja kwenye maada ambayo imekuleta hapa sidhani kama mambo ya familia yangu yanakuhusu sana au yana umuhimu kwa hapa tulipo”
“Sawa ila yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana kwa hapo baadae ndiyo maana nakuuliza usidharau sana. Lengo la mimi kuja mpaka hapa kwenye ofisi yako kuna makubaliano ambayo nahitaji tuyafanye mimi na wewe. Ni makubaliano ya mhimu sana ambayo yanakubidi wewe ufanye maamuzi ya kiume, narudia tena ni ya mhimu sana mr Apson”
“Nenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi acha kuzunguka mr Mafupa”
“Nahitaji ujitoe kwenye mbio za kugombea uraisi”
“Hahahaha Mr Mafupa nadhani uliko toka umelewa sio? Hivi unajua hata kuja hapa nimekukubalia tu kwa sababu nakuheshimu sana, huu muda mimi na wewe ni wapinzani sidhani kama ni sahihi kukutana kutana kirahisi sana namna hii maana wananchi wakijua wanaweza kuanza kuwaza mambo mabaya, nadhani kama hauna jambo la mhimu la kuongea na mimi ni vizuri zaidi kama utanyanyuka na kutoka nje ya ofisi yangu kisha usije ukarudi tena hapa maana nitafanya kama sijawahi kukufahamu”
“Najua mr Apson, najua kwamba ndani yako kuna moto unawaka sana hususani pale ambapo unakuwa unaiwaza ile Ikulu, unawaza namna watu wanavyo yasimulia maisha ya pale ukiwa kama ndiye kiongozi mkuu maana hata baadhi ya vikao vingi na mialiko mikubwa ulikuwa unaipata ila nimekuja kukuomba kistaarabu sana achia hiyo nafasi na awekwe mtu ambaye ni dhaifu na hawezi kuniyumbisha kwa sababu mimi nahitaji kuingia pale Ikulu kisha kuna makubaliano ambayo mimi na wewe tutaingia hata nikiingia Ikulu utakuwa kama mkono wangu wa kulia”
“Makubaliano yapi hayo Mr Mafupa ambayo unahisi yatanishawishi mimi kukubali kuwasaliti wananchi wangu ambao wameniamini na kuniruhusu mimi kuingia Ikulu na kuahidi kunipa kura zao za ndiyo na kwa sababu ipi hasa?”
“Kuna mpango ambao nimeuandaa, sababu tutatengeneza ugonjwa feki na kudai kwamba utakuwa nje ya nchi hospitali kwa mwaka mzima ambapo uchaguzi utakuwa umekamilika na hauwezi kuchaguliwa mtu ambaye upo hospitali hivyo watatakiwa kusubiri mpaka upone. Mwaka ukiisha mimi nitakuwa tayari Ikulu na wewe nitakuteua uwe makamu wangu kwa kuwaahidi wananchi kwamba utaingia Ikulu kama wanavyo hitaji kwenye uchaguzi ambao unafuata huku wakihisi kwamba hakuna tatizo baina yetu ni upendo tu umetawala ndiyo maana nimekupa nafasi kubwa ya umakamu wa raisi na hayo mambo inabidi uyathibitishe wewe mwenyewe kwenye vyombo vya habari. Ukikubali tu kutoka kwenye hiyo nafasi, utaingiziwa bilioni mia moja kwenye akaunti yako maana mimi najua namna ya kuzirudisha nikiingia Ikulu kisha tutaingia mikataba ya kibiashara mimi na wewe ambayo itatusaidia kutengeneza pesa kadri tutakavyo na kutufanya kuwa miongoni mwa watu matajiri sana hapa Afrika”
“Kwahiyo unahisi bilioni mia moja na hiyo mikataba ndiyo itanifanya mimi niuze uzalendo wangu na kuwasaliti wananchi wangu na kuuza utu wangu? Mr Mafupa tangu unatoka kwako ulitakiwa kuwaza kwa umakini aina ya mtu ambaye unaenda kuongea nae. Kwahiyo umeona kwamba mimi nina njaa sana na unaweza kuninunua kwa hiyo pesa? Umekosea sana, nitafanya kama hili hujaliongea naomba utoke kwenye ofisi yangu”
“Koh, koh, Mr Apson mimi huwa ni mara chache sana kumuomba mtu jambo ambalo naweza kulifanya hata kwa lazima bila mapenzi yake, mpaka nakuja kukuomba hapa ni kwa sababu nimeamua kukuheshimu kama rafiki tu japo hatujawahi kuwa karibu. Mimi Ikulu naingia kwa gharama yoyote ile na haujui kwanini naihitaji sana ile Ikulu. Hivi umewaza labda kwamba kwanini nimekubali kuingia kwenye kinyang’anyiro na mheshimiwa raisi ambaye yupo madarakani wakati nipo naye chama kimoja? Ungejua hayo basi hiyo nafasi ungeiachia mwenyewe bila kulazimishwa. Unaongelea uzalendo kwenye nchi hii ambayo wananchi wakipewa hata noti moja tu wanauza utu wao? Uzalendo upi labda ambao unakufanya ujione wewe ndiye ulizaliwa kwa ajili ya hii nchi? Jambo la msingi zaidi ambalo wewe unapaswa kuliwaza sana kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale ni familia ndugu yangu. Nitajisikia vibaya sana kama itafikia hatua ya kunilazimu niingie mpaka upande wa familia wakati una nafasi ya kufanya maamuzi sahihi, una wanao ambao ni waz…….”
“Stooop! mjinga wewe, una jeuri gani ya kuiongelea familia yangu mbele yangu kirahisi sana namna hiyo? Nitakupiga risasi nikuzike humu humu ndani kwangu. Nisije nikakusikia tena ukiwa unaitaja familia yangu kirahisi sana namna hiyo, mimi siyo kama wewe ambaye unashinda na hao wanawake ambao unawabadilisha kila siku kama nguo kwenye makasino. Tena ukija kutaja neno familia kwangu basi nitakuua hapo hapo” alikuwa amesimama mr Apson akiwa ameitoa bastola yake amemnyooshea mwanaume mwenzake huyo ambaye alionekana kwamba alikuwa ni mgombea mwenzake kwenye nafasi ya uraisi wa nchi ya Tanzania. Mwenzake huyo baada ya kushindwa kumshawishi aliamua kuitumia familia kama ngao ya kumdhoofisha na ndiyo sababu ya mr Apson kumnyooshea bastola mr Mafupa kwani kwake familia ndilo lilikuwa jicho lake aliipenda mno. Mr Mafupa alijikohoza kidogo na kumfungukia;
“Huo uwezo wa wewe kunipiga risasi mimi hauna kwa sababu watu wameniona naingia hapa hivyo nisipo toka lazima wewe ndiye utakuwa mhusika namba moja na kesho tu asubuhi magazeti na vyombo vya habari vitaandika kwamba umemuua mgombea mwenzako ili uingie Ikulu, unadhani nani atakuamini tena? Nani atatamani kukupigia kura tena wakati wewe ni muuaji na una tamaa ya madaraka? Hahahaha utakuwa unaisubiria jela wakati huo na familia yako haitakuwa na msaada wowote ule hivyo huo ubavu hauna wa kuiacha familia yako maana unaipenda mno, mpaka hapo nipo salama na hauwezi kunifanya lolote” alitulia kidogo kuacha maneno yamuingie vyema mr Apson kisha akaendelea.
“Mimi nimekuomba kistaarabu lakini umeishia kunidharau, unajua kuna maongezi ya wanaume yanatakiwa kufanywa kiume hata maamuzi yake yanatakiwa kwenda kiume pia na hivyo ndivyo siasa inavyotakiwa kuwa lakini kwa sababu hautaki kwenda kistaarabu basi mimi nitakuonyesha namna sahihi ya kuweza kuyafanya maamuzi magumu ukiwa hauna namna na huenda kwa wakati huo hautakuwa na namna zaidi ya kutoa kilio. Likumbuke neno familia kwenye kichwa chako mr Apson na ujue tu kwamba nitarudi na kwa sasa sitarudi kukubembeleza bali nitarudi na kukufanya ulie huku ukija mwenyewe mbele yangu kunipigia magoti na kuniomba kwamba umekubali masharti yangu ila huenda utakuwa umechelewa tayari”
“Out” aliongea kwa sauti kali yenye uchungu sana baada ya mr Mafupa kumaliza kujigamba mbele yake na kuitishia familia yake huku akiwa anaikoki bastola yake, mr Mafupa alitabasamu na kutoka humo ndani kwa dharau kubwa mno.
Mr Apson alipigiza bastola yake chini kwa hasira sana huku akiwa anahema kwa nguvu mno, aligeukia ukutani na kuangalia picha ya familia yake ambayo ilikuwa kwenye tabasamu zuri sana, moyo wake ulizidi kumuenda mbio isivyo kawaida. Alikusanya begi lake na kutoka haraka sana humo ndani, alitaka kuwahi nyumbani kwanza aione familia yake maana vile vitisho ambavyo alipewa pale alihisi huenda familia yake ilikuwa kwenye matatizo huku akiwa anaendelea kumpigia simu mkewe ambaye naye hakuwa akipokea basi alizidisha wasiwasi sana kwenye nafsi yake, siasa ilianza kumtokea puani mapema sana.
Ukurasa wa kwanza naweka nukta hapa. Niseme tu karibu sana tuweza kujumuika kwa pamoja ndani ya simulizi hii ili tuweze kujua kwamba imetuandalia nimi haswa ndani yake. Unataka kujua hilo salata la uchaguzi linahusiana vipi na hizo pesa kwenye damu? Basi usibanduke twende sawa.
Kwenye kalamu nipo mwenyewe, mwapenda kuniita Bux the storyteller lakini jina langu waweza kuniita;
FEBIANI BABUYA.
Wasalaam.View attachment 2818483
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
MaliziaSIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA TANO
“Unajua wewe ndiye mtu namba moja ndani ya nchi hii, wewe ndiye mtu mwenye nguvu zaidi ndani ya taifa hili lakini pia wewe ndiye mtu ambaye kauli yako ina nguvu na maamuzi ya mwisho ndani ya hii nchi. Lakini ukiacha hayo yote jambo la hatari zaidi kwako ni uwepo wa watu wenye nguvu zaidi ndani ya nchi yako nadhani hiyo ndiyo inaweza kuwa hatari kubwa zaidi kwako” Mzee huyo alitamka sentensi fupi ambayo ilikuwa na maana kubwa sana na alikuwa na uhakika kwamba mheshimiwa lazima angeielewa vizuri tu.
“Una maanisha nini kusema hivyo?”
“Mheshimiwa kitu ambacho kinampa jeuri mtu yeyote yule ni nguvu, mtu anapokuwa na nguvu kubwa sana anakuwa anajihisi kwamba yeye anaweza kufanya jambo lolote lile na hakuna mtu yeyote yule wa kuweza kumzuia wala kitu chochote kile cha kutokea kati kati na kuweza kumuyumbisha hivyo anaanza kujikuta hata mamlaka haziheshimu kwani anaamini hata hao ambao wapo kwenye mamlaka anaweza kuwaendesha atakavyo yeye na mgawanyiko huwa unaanzia hapo” aliongea na kuhitaji kuendelea lakini alitulia baada ya kuona kama mheshimiwa anahitaji kuongea, hakuwa tayari kumzuia bosi wake
“Unataka kusema kwamba?”
“Mheshimiwa nadhani unamkumbuka vizuri Mr Pandei Santo”
“Ndiyo namkumbuka vizuri sana, anahusikaje na swali langu?”
“Yule bwana ni wewe mwenyewe ndiye uliuondoa utawala wake kwa ushauri wangu mimi hapa, nadhani unakumbuka baada ya kuwa na pesa nyingi sana alianza kuleta jeuri hadharani kwa kuhisi kwamba mamlaka zote zipo chini yake na anaweza kuyafanya yale ambayo anajisikia yeye mwisho wa siku akaanza kukukosea heshima mpaka wewe tena hadharani lakini kwa kile ambacho ulimfanyia kilitosha kurudisha heshima yako na kuitoa hatari ambayo alikuwa anaitengeneza kwako. Sasa kwenye nchi wakiwepo watu kama wale tena wakiwa wengi linakuwa sio jambo zuri kwani muda wowote wanaweza kufanya jambo lolote kwa sababu wanakuwa na pesa na pesa inaweza kuinunua nafsi ya mtu yeyote yule”
“Mbali na hilo jambo ambalo ni hatari zaidi kwa nafasi yako ni pale ambapo wanakuwepo watu wenye uwezo mkubwa zaidi kichwani kukuzidi wewe halafu hawapo upande wako. Ni vyema kama kuna watu wana kuzidi uwezo wewe hakikisha wanakuwa upande wako na wanakuwa chini yako hivyo wewe unazitumia akili zao kuweza kukamilisha mambo yako. Akili ndiyo inaweza kumuendesha mtu, akili ndiyo inaweza ikakuweka kwenye hicho kiti chako na akili ndiyo inaweza kukufanya ukatolewa kwenye hiyo nafasi yako. Sasa ukikutana na mtu ambaye ana nguvu kubwa ya pesa na akili tena wengine wanakuwa wanabarikiwa unakuta pia ana nguvu kubwa ya ushawishi kwa watu wanao mzunguka na wananchi kwa ujumla, kukutoa kwenye nafasi yako au kukutawala linakuwa ni suala la muda tu mheshimiwa”
“Mhhhhh, mhhhhhhh umenipa jambo kubwa sana ambalo sikulifikiria kwa wakati huu, unahisi ni kitu gani unatakiwa kukifanya unapo fanikiwa kuwapata au kuwajua watu wa namna hiyo?”
“Hapo ndipo unatakiwa kuyafanya maamuzi kama uliyo yachukua kwa Pandei Santo mheshimiwa”
“Hahahahah hahahaha hahaha naomba ukapumzike, kwa leo inatosha. Kuna namna unanifanya nijivunie sana kuwa na mshauri kama wewe hakika sikufanya makosa kukuweka karibu yangu, kwa sasa hili jambo niachie mimi wewe waweza kwenda ila kabla ya kufanya hivyo peleka taarifa kwa watu wangu wawasiliane na mkurugenzi wa usalama wa taifa apewe maagizo kwamba nahitaji kuonana naye ndani ya masaa mawili yajayo. Unaweza kwenda, asante sana kwa ushauri wako” mheshimiwa raisi alicheka sana kwani alikuwa amefunguliwa akili kwa jambo ambalo alihisi lilikuwa linamuumiza kichwa wakati alikuwa na uwezo wa kulimaliza kwa njia rahisi sana.
Mzee huyo ambaye alikuwa mshauri wake, alitoka mpaka nje ya ofisi hiyo, aligeuka na kuangalia mlango wa kuingilia ndani kabisa ya ofisi hiyo kisha akatingisha kichwa kwa masikitiko sana, baada ya hapo aliondoka kwenda kuyafanyia kazi maagizo ya bosi wake na kisha arudi nyumbani kwake ambako alitoka kwa muda mfupi ambao ulikuwa umepita.
Ilikuwa ni usiku sana tayari lakini hiyo haikuwa sababu ya kumfanya aukatae wito wa bosi wake Ikulu, Mr Lingson Mfwomi ambaye ndiye alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa wa nchi ya Tanzania aliweza kufika Ikulu kama alivyo agizwa, hakuelewa majira ya usiku wote huo kiongozi wake alikuwa anahitaji nini ambacho alishindwa kumwambia kwenye simu au kuhitaji kuongea naye hata siku ya kesho yake? Hakujua ila huenda uwepo wake hapo kwa wakati huo ungemfanya aelewe vizuri sana. Alinyoosha moja kwa moja kuelekea kwenye ofisi kiuu ya raisi ambapo aliongozana na walinzi wa raisi walio mpa maelekezo juu ya kusubiriwa kwake na bosi wake.
“Heshima yako kiongozi wangu” alimpa heshima yake mheshimiwa raisi huku akiwa anaketi kwenye kiti chake ambacho mgeni yeyote angekikalia anapo ingia humo ndani.
“Lingson nyumbani kwema?”
“Kwema kiongozi japo wasiwasi wangu mkubwa ni juu yako tu maana sio kawaida sana kuniita ghafla hivi bila taarifa ya awali na leo nimeshangaa natafutwa na watu wengine wakati huwa unanipigia wewe mwenyewe moja kwa moja pale unapokuwa unauhitaji uwepo wangu hapa!”
“Ni kweli kabisa, mpaka nawaagiza watu wengine basi ujue kwamba mimi sipo sawa na ndiyo maana nikakuhitaji uje hapa wakati huu ili tujue tunafanya nini maana wewe ndiye kiongozi wa usalama namba moja ndani ya nchi hii” mheshimiwa aliongea akiwa anaifungua droo yake na kuitoa bahasha moja ambayo aliifungua na kumrushia mkurugenzi huyo. Bahasha hiyo ilikuwa inaonyesha kama mfumo wa uongozi kwenye taasisi fulani lakini uliandikwa kwa code maalumu ambao ilikuwa ni ngumu sana kuutafsiri kiwepesi mpaka mtu akupe maelekezo yake.
“Mheshimiwa unajaribu kumaanisha nini kunipatia hii?”
“Huo ni mfumo mzima wa namna Ikulu ilivyo, nina uhakika unaujua vyema. Baada ya ofisi yangu ofisi ambayo ipo karibu hapo kwenye huo mchoro ni ya makamu wa raisi kisha ni ofisi yako. Unajua maana yake?”
“Ndiyo mheshimiwa”
“Inamaanisha nini?”
“Ina maanisha kwamba mimi ni mtu wa karibu zaidi ambaye natakiwa kuhakikisha kwamba ofisi yako, Ikulu pamoja na nchi kwa ujumla ipo salalama wakati wote”
“Safi sana, watu wangu mnanifurahisha sana kwa sababu nimewaweka watu ambao mna uwezo mkubwa sana wa kuweza kufikiria na kuweza kuyachanganua mambo” aliongea mheshimiwa kisha akaendelea;
“Unajua kwenye mifumo ya ulinzi wa nchi, kuna mambo mengi sana ambayo yanawekwa ili mfumo mmoja unapo shindwa kufanya kazi vizuri basi mfumo mwingine unasaidia kuweza kuziba hilo kosa, hapo ndipo unapata jeshi la polisi, unalipata jeshi la nchi la kujenga taifa, utakutana na jeshi la majini, na mengine lakini hayo yote yanategemea zaidi idara yako ya usalama wa taifa. Ni rahisi sana kwa wewe hapo kwenda jeshini kumchukua mtu ambaye unahisi anafaa na kumleta kwenye ofisi yako ila huwezi ukakuta mtu anatoka kwako anaenda sehemu nyingine ya ulinzi kama jeshi la kujenga taifa, jeshi la wananchi au hata jeshi la polisi isipokuwa kama kuna kazi maalumu ambayo inampeleka kule kwa wakati huo”
“Hiyo inamaanisha idara ya usalama wa taifa ndiyo taasisi nyeti zaidi kuhakikisha nchi inakuwa salama, ndiyo taasisi ambayo inaendesha nchi na ndiyo taasisi ambayo nchi inaitegemea zaidi kwenye kila sekta kuanzia kwenye uchumi, kisiasa, kidiplomasia lakini hata kiteknolojia pia kwani tunategemea taarifa zenu ambazo mtazikusanya ndani na nje ya nchi ndizo tuzitumie kuweza kuijenga nchi yetu”
“Wakati mimi nasoma pale Tabora boys, kuna waalimu pale sikuwahi kujua kama ni majasusi na walishafanya kazi nyingi sana za nje ya nchi ambazo zingine zilikuwa ni hatari sana ila siku ambayo nilikuja kujua hilo jambo nilivutiwa sana na hii idara baada ya kugundua kumbe huwa wapo pale ili kuwatafuta wanafunzi ambao wanafaa kabisa kuingia kwenye idara ya usalama wa taifa na kuja kulikomboa taifa baadae na ndio wengine mpo huko pamoja na vijana wako”
“Umenielewa Mr Lingson?” mheshimiwa raisi aliyatoa maelezo mengi sana lakini akakatisha na kuuliza swali ambalo bila shaka hata mkurugenzi lilimuacha kinywa wazi
“Yote uliyo yaongea ni sahihi sana mheshimiwa lakini sijajua pointi yako ni ipi hasa mpaka uyaongee yote hayo?”
“Maana yangu ni kwamba wewe ni moja kati ya watu wa mhimu sana ambao mimi nawategemea kwenye taifa hili kwa sababu wewe ndiye ambaye una mamlaka makubwa zaidi ya ulinzi ambayo nimekupa. Kuna watu huwa wanahisi mkuu wa majeshi pamoja na kapteni wa jeshi ndiyo ambao wana nguvu sana kwenye nchi kuhusu ulinzi ila sio kweli, huyo hata akihitaji kuipindua nchi kama hana mawasiliano mazuri na wewe hapo basi hana uwezo wa kufanya hivyo. Kwahiyo nahitaji sana uujue umuhimu wako kwanza kwenye hiyo nafasi ambayo nimekuweka japo ipo chini ya ofisi yangu ila wewe ni mtu mhimu sana kwangu”
“Kuna hili sakata la uchaguzi ambalo linaenda kutokea siku za usoni hapa kwanza nahitaji ule kiapo mbele yangu kwamba hautafanya jambo lolote lile la kijinga na utakuwa makini sana kuhakikisha mambo yangu yanaenda kama nilivyo panga mimi na utafuata yale yote ambayo mimi nayasema” mheshimiwa alimeza mate na kuendelea akiwa amemkazia macho mkurugenzi.
“Nahisi kuna mambo ambayo yanaendelea chini chini kuhusu hili sakata sasa nahitaji nizipate taarifa zote na kila hatua ambayo inapigwa hususani na washindani wangu na kila siku niwe naipata ripoti ya mambo yao yote, ratiba zao zote pamoja na mambo yote ambayo yanaendelea kwenye familia zao” alitulia baada ya kuongea hayo.
“Mheshimiwa mimi nilisha apa kufanya yale ambayo unayahitaji, wewe ndiye ambaye uliniweka mimi kwenye hii nafasi na wewe ndiye ambaye una uwezo wa kunitoa hivyo nitayatoa hata maisha yangu kukusaidia wewe kwa kila hali. Muda wowote nipo kwa ajili yako hivyo unaweza ukanituma lolote lile na nikalitekeleza kwa namna unavyo hitaji wewe. Kama hilo ndilo linakutatiza basi limeisha kiongozi wangu, kesho tu asubuhi naamka nalo ofisini kwangu linaanza kufanyiwa kazi” maelezo ya mkurugenzi yalimfanya atabasamu na kumimina pombe kwenye bilauri mbili ambapo moja alimpa kiongozi huyo.
“Sisi tuna historia kubwa sana ndugu yangu, historia ya baba zetu. Nakumbuka historia ya baba yangu kumsaidia baba yako wakiwa jeshini ambapo bila baba yangu huenda baba yako angekufa na wewe usinge zaliwa kabisa hivyo najisikia fahari sana na mimi pia kuja kukusaidia kwa baadae kisha na wewe unaenda kuwa msaada mkubwa kwangu. Haujawahi kuniangusha kwenye majukumu ambayo nakutuma na ndiyo sababu ambayo inanifanya niendelee kukuamini zaidi na kukupa hiyo nafasi hivyo nitafurahi kama msaada wa baba yangu kwa familia yako na msaada wangu kwako ukaulipa kwa moyo wote. Nahitaji ufanye kazi yangu kama ninavyokutuma ili tubakie Ikulu kwani hatujui mtu mwingine ambaye ataingia atakuwa na upepo gani, kama tukicheza vibaya hata wewe unaweza ukaipoteza hiyo nafasi yako na ukaishia kupewa hata kesi ambazo haukuhusika nazo ukaishia jela. Unaweza kwenda mr Lingson” kiongozi huyo aliongea kwa msisitizo sana kisha akamruhusu mwanaume huyo aondoke bila kutoa jibu la mwisho.
Mr Lingson Mfwomi aliinama kutoa heshima kabla ya kutoka humo ndani, baada ya hapo alitoka na kubaki kwenye mshangao mkubwa sana maana ilikuwa ni ghafla sana kuambiwa maneno mazito kama hayo na kiongozi wake, alijua kabisa kulikuwa na mambo ambayo hayakuwa sawa hata bosi wake hakuonekana kabisa kuwa sawa hivyo aliondoka kichwa chake kikiwa na mashaka mengi sana. Kwanini raisi alikuwa anasisitiza sana kulindwa yeye na sio nchi au ofisi yake? Maana yake alikuwa anajijali yeye zaidi kuliko maslahi ya nchi? Alisikitika na kutoweka hilo eneo haraka sana.
Ukurasa wa tano unafika mwisho.
Febiani Babuya.View attachment 2863215
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu unataka iishe leo leo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Malizia
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA SITA
Asubuhi kulikuwa kumekucha salama kabisa na shughuli za kila siku zilikuwa zikiendelea kama ilivyokuwa kwa watafutaji na wasaka tonge ambao hawajawahi kuamini kufanikiwa kwa miujiza zaidi ya kuzitumia nguvu zao vizuri ili kuyafikia malengo yao. Ndani ya jiji la Dar es salaam, asubuhi hiyo watu walikuwa na pilika pilika zao lakini usingekosa kuwakuta watu kadhaa wakiwa wamekaa sehemu wakiteta jambo kuhusu siasa kwa sababu maandaliza ya uchaguzi mpya yalikuwa yanaanza taratibu.
Kuna watu ambao muda wao mwingi waliutumia kwenye kusoma magazeti ambayo yalikuwa na zile habari moto moto zilizokuwa zinasubiriwa kwa hamu na wengi hivyo ilipelekea watu kuwa na mengi sana ya kuyazungumza kuhusu siasa.
Maeneo ya mabibo sokoni, wengi huwa wanapaita mahakama ya ndizi. Ni eneo ambalo linayabeba maisha ya sehemu kubwa sana ya jiji la Dar es salaam kama sio lote kwa ujumla kwani sehemu hiyo vinapatikana vyakula kwa bei rahisi sana ambavyo vinatoka moja kwa moja mashambani na kuletwa mjini kwa ajili ya wananchi kunufaika na moja kati ya uwekezaji bora ambao unafanywa kwenye kilimo. Watu wengi sana huvutiwa kufika ndani ya soko hilo kwa sababu mahitaji yanapatikana kwa bei rahisi sana basi huwa inapelekea kuwa na msongamano mkubwa sana wa magari pamoja na watu kiujumla bila kusahau wale wanachuo ambao wanasoma ndani ya chuo cha taifa cha usafirishaji ambacho kipo jirani sana na eneo hilo.
Asubuhi hiyo wakati hizo pilika pilika zikiwa zinaendelea ndani ya eneo hilo, walikuwa wamekati watu wakiwa wanabishana sana kuhusu siasa ya nchi yao yaani ungehisi kwamba wao ndio ambao walikuwa wanaiendesha nchi kwa namna walivyokuwa wanajinasibu huku kila mtu akijinadi kwamba yeye ndiye ambaye alikuwa na taarifa za kweli kabisa kuhusu uhalisia wa nchi ya Tanzania kwani hata babu yake alikuwa akimsimulia sana.
“Nisikilize Chande wewe umekuja juzi tu hapa kutoka huko kwenu Mtwara kulima korosho, hakuna jambo ambalo unalijua kuhusu nchi hii zaidi ya majirani zako wa Msumbiji huko. Tumekupokea wenyewe ndani ya jiji hili utatuambia nini kuhusu siasa ya hapa wewe? Tukikwambia hata utupe historia ya mwenge wa uhuru ya Forojo Ganze unaijua wewe? Tukikwambia kwamba utume tafsiri ya ile namba miamoja kumi na tano (115) ambayo kwa baadae ilikuja kutafsiriwa na shekhe Yahya kwa mwalimu Nyerere unaijua wewe? Hahahaha sasa utatuambia nini kuhusu nchi hii wewe na siasa zake? Acha kutupigishia kelele sisi wakubwa tunapokuwa tunaongea wewe unatulia na kula somo”
“Na wewe Ismail acha kumtisha mwenzako kwa historia ambayo imeandikwa na unaweza hata kwenda kuisoma, wewe mwenyewe mweupe tu basi uliibahatisha hiyo ukaanza kutupigia makelele hapa. Hata wewe nikikuuliza unipe historia ya TAA na TANU hauzijui, hata tu vyama vya sasa na sera zake huzijui, unapata wapi nguvu ya kumtishia mwenzako na kumwambia anyamaze? Vijana wa siku hizi mnatanguliza majigambo kuliko uhalisia wa mambo yalivyo” ni mzee mmoja mwenye busara alimjibu kijana ambaye aliitwa Ismail aliyekuwa anamkosoa na kumsema vibaya mwenzake kwa kudai kwamba hajui lolote. Aliambiwa ukweli basi naye akajikuta anakuwa mpole maana angedhalilika kama angeendelea kubishania kitu ambacho hakukijua.
Kijana Chande baada ya kuona hata mtesi wake naye pia alipewa vidonge vyake, alitabasamu sana na kumgeukia mzee huyo.
“Mzee wangu asante sana kwa busara zako, naomba kukuuliza hivi kwa sasa unahisi ni kiongozi gani anaweza kuingia madarakani na kwa sababu zipi ambazo unahisi zitamfanya apate hicho kiti?” aliuliza na kukohoa kidogo na kutega sikio ili kumpa nafasi mzee huyo kuweza kujibu.
“Kwa bahati mbaya sana nchi haiongozwi kama unavyo hisi wewe au kama unavyotaka wewe iwe. Hii nchi kuna watu ambao wanaamua kipi kiwe kipi au nani awe nani hivyo kukujibu swali lako ni kwamba wataamua wao kwamba ni nani ambaye anafaa kuwa Ikulu na sio mimi kukueleza maana hata nikikupa sababu za mtu kuingia huko haitakuwa na maana yoyote ile” mzee huyo aliongea kwa ufupi sana huku akiwa analikunjua gazeti lake ili aweze kuzipata habari
“Mzee sijakuelewa unamaanisha nini, unasema wao ndio wanaamua nani awe nani! Kwani unawazungumzia akina nani hao?” mzee huyo alimwangalia sana Chande
“Wewe bado ni mdogo sana kuna mambo hautakiwi kuyajua kwenye maisha yako kwa sababu yanaweza kuwa hatari sana kwako. Mimi nimeishi miaka mingi sana kwenye nchi hii na niliwahi kuwa pia ndani ya jeshi hivyo kuna baadhi ya mambo nayajua vizuri sana japo siwezi kukueleza. Kitu ambacho unatakiwa kuwa nacho kichwani mwako ni kwamba duniani hakuna demokrasia na haitakuja kuwepo kama ambavyo wewe huwa unaambiwa kwamba demokrasia ipo, hivyo ambao wanaamua nani awe pale ni wenye mamlaka na sio wewe hapo. Vijana mimi nawahi nyumbani muwe na asubuhi njema” mzee huyo aliongea jambo ambalo wote liliwaacha njiapanda wasielewe anamaanisha nini na mzee huyo baada ya kuona kwamba vijana hao wanaanza kumchimba sana aliamua kuondoka tu kwani yangekuwa mengine hapo mwisho wa siku waanze kuongelea habari ambazo huenda zingewaingiza kwenye matatizo.
Hayo yalikuwa maisha ya kawaida tu mtaani hapo watu wakiwa wanaendelea na maisha yao ya kila siku na vijana hao wa vijiweni wakiwa wanaendelea kupiga hadithi ambazo hawakuwa hata na uhakika nazo. Pembeni mwa hicho kijiwe cha hao vijana ambao walikuwa wanapiga hizo stori na mzee huyo palikuwa na mwanaume mmoja ambaye kwa mavazi yake tu ambayo yalikuwa mwilini, ungegundua kwamba alikuwa ni mbeba mizigo wa hapo sokoni.
Alikuwa makini sana isivyo kawaida kusikiliza hayo majibizano ya watu hao hapo japo alijfanya kama mtu mwenye mawazo mengi sana kwenye kichwa chake. Baada ya mzee huyo kuondoka naye alizuga zuga na kuanza kutoka hiyo sehemu huku akiwa anasogelea taratibu karibu na eneo la kuchezea michezo ya kubashiri ambalo lipo karibu sana na eneo hilo.
Alisimama hapo na kuangalia namna vijana walivyokuwa wanapishana wakiingia na kutoka ndani ya jumba hilo la michezo ya kubashiri na kusikitika namna vijana walivyokuwa wanautumia muda wao kuamini kwamba wanaweza kuchota pesa kwa zile namba ambazo zilikuwa zinabandikwa kwenye makaratasi huku wao wakiwa wanatoa vile vidogo ambavyo walikuwa wanavisaka kwa jasho sana.
“Naona unajaribu kuangalia namna namba za kusadikika zinavyo wapumbaza wenzako mpaka wanakuwa kama wajinga wa kushindwa kupambana huku wakiamini kwamba wanaweza kupata utajiri bila kufanya kazi” ilikuwa ni sauti ya mzee mmoja ambayo ilimshtua kutoka kwenye hiyo tafakuri yake.
“Ndiyo mzee, hawa watu wa nje wamefanikiwa sana kwenye suala la kuwageuza vijana wengi kuwa wajinga. Yaani mtu anaamka kwake anakuja hapa akiwa ana amini kwamba anaweza kuchota hizi pesa kirahisi sana namna hii kwa sababu anaona namba zimebandikwa ukutani. Matokeo yake unaweza ukaondoka miaka kumi, ukarudi na bado utamkuta anazunguka hapo hapo na makaratasi mkononi akiamini miujiza. Nadhani nchi ina hasara kubwa sana kuwa na idadi kubwa ya vijana ambao wana akili za kijinga sana namna hii”
“Shida ya vijana wa siku hizi wanaamini kwamba wao ndio wajanja sana, wanaamini kwamba wao ndio wanayajua mambo mengi sana zaidi yetu. Ukiwashauri wanakwambia umepitwa na wakati hivyo unawaacha tu umri na muda utakuja kuwahukumu vibaya sana na ndo hapo wanaanza kuwachukia watu wenye mafanikio na kuwasingizia kwamba wao wana pesa mara za manyoka, utasikia za mashetani, hayo ndiyo mawazo pekee ambayo watu maskini huwa wanahisi yanawafariji bila kujua kwamba wanaudumaza uwezo wao wa akili kufikiria mambo makubwa. Kwa umri wako wewe bado ni kijana sana, jitahidi upambane mno, jitahidi uwekeze sana kwani kuna muda utafika utakuwa hauna uwezo wa kupambana tena, kuna wakati utafika mwili hautakuwa na uwezo wa kunyanyua hata mfuko wa unga sasa hapo kama ulijiwekeza vizuri basi hautapata shida yoyote ile ila kama ulicheza vibaya utaanza kuwachukia watu na kulia lia kwamba hawakusaidii. Nawahi nyumbani kijaja wangu, nilikuwa kuhemea kidogo sokoni hapo Mungu akubariki sana kwa kujielewa na kujua kwamba hivyo vitu ni jela kubwa sana” mzee huyo baada ya kumaliza mawaidha yake kwa mwanaume huyo alimuaga na kuondoka, aligeuka na kumwangalia sana mzee huyo akaishia kutabasamu tu kwani aliongea mambo ya maana sana japo hawakuwa wakifahamiana ila alimuelewa sana.
Mwanaume huyo aliangalia saa yake kisha akajichanganya ndani ya soko ambako alitumia dakika ishirini tu pekee akatoka tena mpaka barabarani. Alisogea pembeni kabisa akaruka mtaro na kwenda kukaa katikati ya uwanja ambao unatenganisha kati ya soko hilo na chuo cha taifa cha usafirishaji, aliitoa simu yake ndogo sana ambayo ilikuwa imechoka mfukoni na kuipiga mahali ambapo iliita kwa sekunde kumi na tano tu kisha ikapokelewa.
“Mkuu nimemaliza kutega kamera kila sehemu ya mhimu ya soko hivyo tutakuwa tunaona na kupata kila habari mpya ambayo inaendelea lakini pia hata sehemu za mhimu kama sehemu zenye majumba ya michezo ya kubashiri pia nimeweka ili tuwe tunajua mitazamo ya wananchi juu ya jambo hili na kila kitakachokuwa kinaendelea, nadhani hiyo itaturahishia sana kuchukua hatua za haraka pale itakapo bidi”
“Safi sana, kwa sasa una kazi moja kubwa sana, hakikisha unaifuatilia familia ya Mr Apson Limo. Kuanzia asubuhi wanapo amka mpaka usiku wanapo enda kulala na kama kuna mtu atakushtukia kwenye hayo mambo yako basi haraka sana hakikisha unampoteza ili kutoacha ushahidi eneo lolote lile”
“Sawa mkuu” kisha simu ikakatwa. Mwanaume huyo alisonya kwa hasira baada ya simu hiyo kukatwa kwani kwa wakati huo alikuwa anaongea na kiongozi wake ambaye ndiye alikuwa amempa hiyo kazi. Mwanaume alikuwa ni shushushu aliyekuwa akizikusanya taarifa mbali mbali ndani ya nchi lakini pia alikuwa ni jasusi mbobevu sana ambaye alikuwa amefanya kazi nyingi sana za nje.
“Ndiyo maana siipendi kabisa siasa mimi, yaani juzi tu nimetoka kufanya kazi ngumu huko Kongo hata sijapumzika napewa kazi nyingine tena halafu wenyewe wapo na wake zao ndani wamelala tu wanasubiri ukosee waje kukulaumu na vitambi vyao, pumbavu sana. Wana siasa ni watu wa hovyo sana muda mwingine” aliongea kwa kulalamika sana kwa sababu hakupewa muda wa kupumzika, kupewa kazi hiyo ya kumfuatilia mwana siasa huyo kwake hakuona kama ni sawa kwa sababu yalikuwa ni maslahi binafsi na sio nchi ila hakuwa na namna kwa sababu ni kazi ambayo alipewa na kiongozi wake hivyo hakuwa hata na nguvu ya kuhoji au kukataa.
Alikuwa anaitwa Matiasi Ndugu mwanaume wa shoka huyo. Alikuwa amepewa kazi ambayo aliijua moja kwa moja kwamba ilikuwa ni ngumu na ni hatari sana endapo kama ingetokea siku akaweza kukamatwa. Aliondoka hilo eneo kishingo upande baada ya kumaliza kutega vifaa vyake hayo maeneo ambavyo vingempa urahisi sana wa kupata taarifa ambazo wangezihitaji wakubwa wake kuhusu yale yanayo endelea mtaani. Sasa kazi iliyokuwa mbele yake ilikuwa ni kuzikusanya taarifa zote za Apson Limo pamoja na familia yake kuanzia asubuhi mpaka usiku.
Ukurasa wa sita naweka nukta hapa. Tukutane tena wakati ujao.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app