Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA TATU
“Ni vizuri kama ukinipa taarifa zote ambazo zinahitajika ili niweze kuifanya kazi yangu” ilimlazimu kuutumia uanaume wake ili kuweza kukamilisha kilicho mpeleka maana kama angelegea huenda wangefika mpaka asubuhi akiwa hajapewa hayo maelekezo. Sasha hakuwa na namna ilimlazimu kumuelezea kila kitu kuanzia mchezo ulipokuwa umeanzia mpaka siku hiyo ambayo mauaji yalitokea kwa vijana wa mr Mafupa ambaye alikuwa na wasiwasi kwamba huenda watu hao walikuwa wanahitaji kumharibia kwenye mbio zake za kukiwania kiti cha uraisi.

Baada ya kuzipata taarifa hizo alitoweka hilo eneo huku akiwa anajua wazi kwamba mtu wa kwanza kumpata ni Tommy maana angetaja kwamba ni nani ambaye yupo nyuma yake na alihusikaje na yale mambo ambayo alikuwa akiyafanya kwa sababu hawakuwa na imani kabisa kwamba yeye anaweza kuyafanya yale yote.

Saa kumi usiku ni nyakati ambazo harakati zilikuwa zimeanza kama kawaida ndani ya jiji la Dar es salaam watu wakiwa wanaipokeea siku mpya na kuianza kwa amani lakini ilikuwa ni tofauti kidogo kwa baadhi ya watu kwani usiku huo haukuonekana kuwa mwema sana kwa upande wao. Mwanaume ambaye alikuwa anajulikana kama Jabeli, alikuwa ni moja kati ya walinzi wa kuaminika sana kwenye kampuni ya R ambaye ndiye alikuwa bosi wake.

Mwanaume huyo alikuwa anayaficha mambo yake kupitia duka lake kubwa la vifaa vya pikipiki maeneo ya Riverside hivyo hata kufanya kwake shughuli haramu mjini hakuna mtu ambaye alikuwa anamshtukia kwani waliamini kwamba alikuwa anapatia pesa ndani ya duka lake. Wakati huo kunakaribia kukucha ndio muda ambao yeye alikuwa anarudi nyumbani kwake Kimara akiwa na gari ya bei kubwa sana.

Baada ya kufika Kimara mwisho aliikata kona ya kushoto na kuanza kuelekea sehemu ambayo inajulikana kama Vinane, hapo ndipo alipokuwa amejenga jumba lake la kifahari huku mtaani akiwa mtu ambaye hakuwa akionekana kabisa kwani hata majirani zake hawakuwahi kumfahamu zaidi ya kuona gari ikiingia tu mida ya usiku na hata kama ingefanikiwa kuondoka mapema basi wasingefanikiwa kumuona kabisa kwani vioo vilikuwa vinafungwa vyote.

Aliendesha kwa kasi sana akionekana kwamba ni mtu ambaye alikuwa anawahi hilo eneo ambalo lilikuwa ni kwake. Alifika saa kumi na moja kasoro kwa sababu kulikuwa kumetulia sana mida hiyo na hakukuwa na foleni, baada ya kufika hapo nyumbani kwake alishtuka baada ya kuona kuna gari ilikuwa imepaki maeneo ya jirani na lilipo jumba lake. Alilitilia mashaka lakini hakuwa na la kufanya maana huenda ni mtu tu aliamua kuiweka hiyo gari mahali hapo.

Baada ya kufungua geti lake kwa rimoti na kufanikiwa kuingia ndani kisha akaifunga geti tena, alishtuka na kuitoa bastola yake na kuinyoosha kuelekea kwa mtu ambaye alimuona amekaa humo ndani karibu na karo la kuhifadhia vyombo wakati wa kuosha akiwa ameinama kwa wasiwasi sana. Alimwangalia kwa umakini kisha akairudisha bastola yake kiunoni kwa sababu alionekana kumjua vyema mtu huyo ambaye alikuwa mbele yake.
“Steve vipi na usiku bila taarifa?” huyo alikuwa ni mfanyakazi wa dukani kwake, alishangaa sana kumkuta ndani ya hilo eneo wakati kama huo tena bila taarifa.

“I’m sorry boss” mwanaume huyo alitamka akionekana kuwa na wasiwasi sana kitu ambacho kilimshtua tena Jabeli hivyo akahitaji kuitoa bastola yake kwa mara nyingine maana hakuamini kama kulikuwa na usalama hilo eneo lakini kabla hajafanya hivyo alihisi kwamba kulikuwa na sauti ya mtu akionekana kuikoki silaha yake vizuri ni jambo la ghafla sana lilikuwa.

“Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kutikisika tu hauna kichwa” ni sauti nzito ya mwanaume ambaye alijitokeza mbele yake akiwa na bastola mkononi. Hakuwa mwingine bali Tommy, alikuwa amemfuata mwanaume huyo kama alivyokuwa amepewa maelekezo na Nick kwamba kama anautaka ukweli basi mwanaume huyo ni chaguo sahihi kwani alikuwa ni mlinzi mkuu ndani ya ile kampuni. Sasa hapo ndipo Jabeli alielewa kwamba ni kwanini alimkuta kijana wake huyo akiwa mnyonge hilo eneo kumbe kulikuwa na mtu ambaye alijibanza konani. Alimgeukia kijana wake na kumwangalia kwa hasira sana lakini hakuwa na la kufanya kwa wakati huo kwani kama angefanya jambo lolote baya basi angekuwa anacheza kamali moja mbaya sana ya maisha.

“Nipatie hiyo bastola na usijaribu kufanya ujinga wowote nitakufanyia kitu kibaya sana” aliogea kwa sauti nzito ambayo ilimfanya Jabeli asiwe na namna zaidi ya kuitoa bastola hiyo kiunoni na kuirushia alipokuwa Tommy ambaye aliiokota kisha akaiweka na yake kiunoni bila wasiwasi na hicho kilimpa tabasamu Jabeli kuona mwanaume huyo ameiweka bastola kiunoni, kwake huo ndio ulikuwa wakati wake bora zaidi wa kuweza kujilinda ndani ya hilo eneo.

Aliwahi kwa kukimbia mithili ya mtu anaye upiga mpira danadana, alijivuta kuelekea kwa Tommy na kurusha mateke sita mfululizo, mateke ambayo yaliishia kuubumoa ukuta kwa pembeni kidogo. Mwanaume huyo alijigeuza tena kwa sarakasi nzito sana ambayo ilidakwa begani na Tommy kisha akamshindilia ngumi nzito sana ya kifua iliyo mrudisha Jabeli nyuma, akatua chini kwa goti moja huku akiwa anakichomoa kisu kiunoni kwake. Hakuwa na silaha moja tu pekee ya kuitegemea kwake aliamini kwamba linaweza kutokea jambo lolote lile.

Alikuja kwa staili ya nge akiwa bado yupo chini, alikiachia kisu chake kwa nguvu kuelekea kifuani kwa Tommy akiwa anakuja kwa kasi sana na mateke ya mzungusho makali mno. Kisu hicho Tommy alikikwepea pembeni akakiacha kipite kisha akakidaka kwenye mkono wake kikiwa kinamvuka tayari lakini wakati anakidaka kisu hicho mateke yalikuwa yamemfikia kifuani, alipigwa mateke mawili mazito sana ambayo yalimrudisha nyuma hatua kadhaa kutoka pale alipokuwa amesimama.

Kufanikiwa kumpiga yale mateke Jabeli aliona ushindi wa mezani upo upande wake hivyo akawa anamuendelea Tommy kwa kasi sana ambapo alishangaa baada ya kumfikia mwanaume huyo aliachiwa apige anavyo jisikia yeye. Alirusha ngumi nyingi sana za tumbo kupiga tumbo ambalo lilikuwa limekomaa mno kwa namna lilivyokuwa limekazwa, aliachia ngumi mbili za mbavu ambazo kwa mbali Tommy alionekana kuzisikilizia kisha mwanaume huyo alijibinua sarakasi ya mbele kwa buti kali ambalo lilitua kwenye kifua cha Tommy. Buti hilo lilikuwa zito mithili ya kufanikiwa kumnyanyua Tommy mpaka ukutani ambapo hakujibamiza bali alitua kwa miguu yake na kujirusha mithili ya spring na kutua alipokuwa amesimama mwanzo huku kisu kikiwa kwenye mkono wake.

Jabeli alikuwa anahitaji kuimaliza kazi haraka haraka kisha amalizane na mfanyakazi wake kwa kumletea mgeni ndani ya hilo eneo hivyo alikuwa anataka mambo yaende haraka haraka sana. Spidi yake ya uendaji eneo ambalo alikuwepo Tommy ilimponza baada ya mguu wake kudakwa na kuzamishwa kisu upande wa mshipa wake wa nyuma kwenye ugoko wa mguu kisha mshipa huo ukakatwa pamoja na soli ya kiatu. Alipiga makelele japo hakuweza kwenda mbali kwani alihitaji kuutumia mguu wake mwingine ambao ulikuwa imara, hivyo aliurusha kwa nguvu lakini ulipiga hewa hivyo akaitanguliza mikono wake.

Alipigwa ngumi nzito za mbavu huku mkono wake mmoja ukiwa unadakwa, kisu kilizamishwa kwenye kiganja chake na kukichana chana vibaya sana. Maumivu ambayo aliyapata ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuyahimili, alipiga makelele sana lakini ni kama alikuwa anafanya makosa kwani alifunikwa na buti la shingo, wakati anataka kudondoka chini alipigwa mtama wa juu kwa juu hivyo nafasi ya kutua chini hakuipata vyema kwani wakati anashuka alipigwa na teke kali la tumbo kama mchezaji anaye upiga mpira wa volley ambao unakuwa umetoka juu huku yeye akiwa ameutega mguu wake.

Alijibamiza vibaya sana kwenye ukuta maana mgongo ulitua vibaya sana. Alikuwa anasimama kwa kujikakamua sana kwa kutumia ukuta huo ila hali yake haikuwa kwenye ubora kwani mguu mmoja ulikuwa hauwezi kusimama vyema na mkono mmoja haukuwa na kazi kiganja kilikuwa kimeharibiwa vibaya sana. Hakutaka kuwa mzembe hivyo alirukia lile aneo ambalo Tommy alikuwepo ili amzoe wadondoke wote lakini mahesabu yake na kasi yake havikuweza kwenda sawa kwani wakati huo anajirusha mwenzake alifanikiwa kumkwepa na kumfanya adondokee tumbo.

Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana kwake kwani kudondokea tumbo kulipelekea yeye kupokea buti la mgongo ambalo lilimfanya aheme na kuliangalia zege ambalo lilikuwa chini hapo kwenye mjengo wake mwenyewe. Aliburuzwa vibaya sana kwa kutumia uso wake hali ambayo ilimfanya apige makelele ya kuhitaji msaada baada ya uso wake kuharibiwa na zege hilo ambalo lilikuwa chini. Alipiga kelele kuhitaji msaada kwa majirani lakini ni nani ambaye angeweza kumsaidia wakati hakuwa akijulikana kwa watu wala kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii? Hiyo pati alitakiwa kuicheza mwenyewe.

Aligeuka na kukutana na sura ya mwanaume huyo ambayo haikueleweka kwamba ni lini ilikuwa mara ya mwisho kucheka. Hakuwa akiongea kabisa Tommy bali alikizamisha kisu hicho kwenye paja la mwanaume huyo kisha kisu kikiwa ndani, akaanza kukivuta kwa nguvu kurudi kwenye goti hali iliyo pelekea eneo hilo kuchanika vibaya sana.

“Unataka nini? Nitasema tafadhali naomba uniachie maisha yangu” alishindwa kuvumilia kwa sababu hakuelewa mwanaume huyo alikuwa anahitaji nini hasa maana alikuwa anamtesa tu huku akiwa kimya kabisa haongei jambo lolote lile hali ambayo hata yeye ilimtisha sana basi ikabidi aulize mwenyewe. Aliuliza akiwa anatokwa machozi ya kira rangi na mdomoni kwake alikwa anatokwa na udenda mwingi sana ambao ulikuwa umeambatana na damu nyingi.

“Unaniuliza nataka nini?” mwanaume huyo hakujibu hilo swali kitu ambacho kilionekana kuwa dharau kubwa, alitoa mguno baada ya kisu kuzamishwa kwenye mabavu kwa nguvu na kutolewa kwa kasi ya ajabu. Alikuwa anahisi alikutana na shetani kwa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa mkatili asiye na moyo wa kibinadamu kabisa.
“Ndiyo, ndiyo” alijibu kwa pupa sana.
“Kichwa cha mdogo wangu kiko wapi na dada yangu amehifadhiwa wapi?”
“Mimi sijui utakuwa unanionea tu” kauli yake ilikuwa inaashiria kwamba alitoa jibu la kijinga sana mbele ya huyo mwanaume. Kilicho mkuta alikijutia sana kwani kisu hicho kilizamishwa kwenye jicho lake moja ambalo lilitobolewa bila huruma hali hiyo ilimfanya aruke ruke kama mtoto mdogo kwani alipitia maumivu makali sana ambayo hayakuwa ya kawaida hata kidogo kwenye maisha yake.

“Nasema, nasema, nasema, nasema usiniue tafadhali” alikuwa anaongea huku akiwa analia kwa uchungu mithili ya mtoto mchanga ambaye anakuwa amezaliwa siku hiyo hiyo akilia kwa mara ya kwanza kutoa sitofahamu ya utoaji wa sauti. Mwanaume huyo alikuwa anamwangalia tu usoni huku yule mfanyakazi wa Jabeli ambaye alijulikana kama Steve akiwa anatetemeka kwa wasiwasi sana maana alionekana kabisa kutoyazoea hayo mambo ambayo alikuwa anayaona mbele yake.

“Kurasini, kurasini. Ukitoka chuo cha TIA wakati unaelekea darajani njia ya Kigamboni unakunja mkono wa kulia. Ukikaribia relini kuna ghorofa la zamani pale ambapo wanaishi wapangaji ndiyo sehemu ambayo dada yako amehifadhiwa na kichwa cha mdogo wako kipo pale” aliongea akiwa anatetemeka sana hakuelewa aguse wapi na aache wapi maana kila sehemu ilikuwa inamuua isivyo kawaida.

Ukurasa wa thelathini na tatu sina la ziada mpaka wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA NNE
“Nielezee kwa kirefu mdogo wangu aliuwawaje labda?” hasira zilikuwa zinaongezeka baada ya kuyasikia maneno hayo kutoka kwa huyo mwanaume.
“Alitekwa wakati anatoka shule”
“Najua alitekwa ndiyo sasa nataka kujua alitekwaje na nani ambaye aliitoa hiyo amri ya kufanya kitu kama kile?”
“Amri aliitoa bosi”
“Remsi sio”
“Ndiyo, ndiyo”
“Endelea”
“Kiufupi ni kwamba lile eneo la shule ambayo alikuwa anasoma mdogo wako kuna mwalimu ambaye alikuwa anafanya kazi chini ya bosi hivyo alikuwa akitoa taarifa zote juu ya yule mtoto kuanzia ratiba yake ya kwenda shule, muda ambao angetoka na muda ambao angeingia. ikawa rahisi sana sisi kuitekeleza ile kazi ambayo tulitumwa kuifanya ambapo tulisubiri wakati anahitaji kutoka lile eneo tukawaua walinzi wake wote na kwenda kuwatelekeza na gari kule baharini kisha mtoto tukaenda naye kwa bosi” maelezo ambayo alikuwa anayatoa yalizidi kumfanya mwanaume huyo Tommy macho yake kuwa mekundu zaidi maana mtu huyo alikuwa anaelekea sehemu mbaya sana kwenye maelezo yake.
“Huyo mwalimu yuko wapi kwa sasa?”
“Aliuawa baada ya kazi ile kukamilika ili asije akawa shahidi kwa baadae kitu ambacho kingepelekea kazi kuharibika”
“Dada yangu mmekuwa mkimfanya nini huko aliko?”
“Bosi tu ndiye ambaye huwa anaenda kufanya naye mapenzi sisi wengine haturuhusiwi kufanya lolote lile”
“Ok, kuna mtu mwingine ambaye yupo nyuma ya bosi wako labda?”
“Hapana sijui”
“Haujui kivipi wakati inasemekana wewe ndiye mlinzi mkuu wa ile kampuni?”
“Ndiyo lakini sina nafasi kubwa sana hivyo kwa sababu pale huwa naona wanaume wengine wakija na mimi huwa naambiwa nitoke nje nisisikilize kile ambacho kinakuwa kinaongelewa”
“Unatakiwa kuripoti kazini saa ngapi?”
“Usiku ndipo nitaenda tena kwa sababu nina siku kama mbili sijarudi kutokana na majukumu kuwa mengi sana”
“Hivyo hawawezi kukutafuta mpaka usiku sio?”
“Ndiyo”
“Vizuri sana, ni nani ambaye alipitisha upanga wake kwenye shingo ya mdogo wangu?” swali la Tommy lilimfanya mwanaume huyo ameze mate kwa shida sana na kuongezeka kwa wasiwasi kwenye uso wake. Tommy hakutaka kuendelea kumbembeleza, alitoa bastola moja akaikoki na kuachia risasi zote sita kwenye goti la mwanaume huyo bila huruma. Jabeli hakuna lugha aliacha kuiongea hapo akihitaji kuonewa huruma, alilia kwa uchungu sana na nguo zake zilionekana kulowa vyema.

Tommy aliichukua na ile bastola ambayo ilikuwa ya Jabeli pia nayo akaikoki vyema
“Ni……mimi” wakati anamalizia neno mimi paja lake lilikuwa limetawanyishwa vibaya sana na risasi zingine sita hivyo mwili wake ulikuwa umemeza risasi kumi na mbili ambazo zilifanya goti na paja kubakia kama nyama zilizo pondwa pondwa buchani. Jabeli alikuwa anahema kwa nguvu kubwa sana akiwa anaishiwa pumzi taratibu.
“Kumuua mdogo wangu kwa maumivu hilo ni kosa kubwa sana ambalo litafanya kila ambaye ameugusisha mkono wake kwenye hili afe kwa maumivu makali sana” macho yake yalikuwa mekundu mithili ya nyanya wakati huo alikuwa anakishika kisu ambacho alikizamisha kwenye shingo ya mwanaume huyo taratibu akiwa anakizungusha ambapo Jabeli alipitia maumivu ambayo hata angesema amwelezee mtu basi ingekuwa ni ngumu sana kueleweka mpaka pale ambapo naye mtu husika angeweza kuyapitia moja kwa moja. Steve yale ambayo aliyashuhudia yalimfanya aweze kuzimia pale pale.

Tommy alimuua Jabeli kikatili sana na kuhakikisha amekitoa kichwa cha mwanaume huyo kama ambavyo mdogo wake alifanyiwa kisha akachukua silaha zote na kwenda kumshikisha vizuri sana Steve akiwa amezimia. Kijana huyo alikuwa anauziwa kesi ya mauaji kwa sababu hata vingechukuliwa vipimo ingegundulika kwamba muuaji ni yeye kwa sababu kwa sababu yeye ndiye ambaye angekutwa eneo la tukio.

Wananchi kwa kuogopa usalama wao licha ya kuwa saa kumi na moja kila ambaye aliisikia milio hiyo ya risasi alijibanza nyumbani kwake hata na wale ambao walikuwa wameamka kuendelea na shughuli zao walizikimbia kwanza mpaka pale ambapo wangesikia habari ya utulivu. Tommy alitoka nje ya geti hilo kwa kupitia ukutani maana geti lilikuwa limefungwa kwa rimoti wakati Jabeli anaingia humo ndani. Mwanaume aliingia kwenye gari yake na kutoweka hilo eneo ambapo baada ya kutoka alisikia ving’ora vya polisi vikija kwa kasi sana ila kwa bahati mbaya walikuwa wamechelewa mno.

Ndani ya muda mfupi baada ya tukio hilo kuweza kutokea, polisi kutoka kituo cha polisi cha Kimara waliingia hilo eneo kwa msaada mkubwa wa simu za majirani. Polisi hao walikuwa wakiongozwa na inspekta Kaoneka, mwanaume ambaye alipenda sana majivuno na ujiko hususani kwa watu ambao alikuwa ana imani kwamba anawamudu kwa kila kitu. Kupenda sana sifa ndiyo ilikuwa sehemu kubwa sana ya maisha yake huku akiwa anaamini kwamba alikuwa anaweza kufanya jambo lolote lile, kwa mtu yeyote yule na kwa wakati ambao angeutaka yeye bila kuingiliwa na mtu yeyote yule.

Hayo mauaji ambayo walikuta yamefanyika hapo yulikuwa yanatisha sana kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa mtu mwenye nafsi ya kawaida yenye uoga mkubwa ndani yake kuweza kuangalia mara mbili mbili kile ambacho kilitokea. Afande mmoja alikuwa amechuchumaa karibu na alipokuwa amelala Steve huku mkononi akiwa na bastola mbili kwenye kila mkono wake na bastola moja na kisu kilichokuwa kimejaa damu kikiwa pembezoni kidogo na mwili wake.

Alimwagiwa maji ya baridi baada ya kuonekana kwamba yeye alizimia tu na hakuwa ameathirika kwa lolote lile, hivyo alikurupuka kutoka kwenye huo usingizi wa kifo kitu ambacho kilipelekea yeye kuanza kuvuja jasho kwa wingi sana.
“Usiniue tafadhali, usiniue mimi sijui lolote lile” aliongea kwa hofu sana baada ya kumuona mtu amechuchumaa mbele yake nadhani yeye bado alihisi kwamba alikuwa ni Tommy akihitaji kumuua. Alituluia akiwa anahema kwa nguvu baada ya kujua kwamba mtu ambaye alikuwa hapo alikuwa ni polisi tena akiwa ameongozana na wenzake hivyo hakuwa pekeyake.

“Wewe ni nani?” liklikuwa swali la askari huyo akiwa na pingu zake mkononi ishara ambayo ilionyesha wazi zilikuwa kwa ajili ya Steve.
“Naitwa Steve”
“Hapa unafanya nini?” Steve alishindwa kuongea aliishia kuigeuza shingo yake na kuangalia pembeni ambako aliona kichwa cha bosi wake Jabeli kikiwa kimetenganishwa na kiwili wili chake, alipiga sana makelele lakini alitulia akibaki anahema tu baada ya kupokea kibao kizito sana kutoka kwa huyo afadne ambaye alikuwa mbele yake.
“Hapa ni kwa bosi wangu” alijibu bila kupenda.
“Vipi upo tayari kuhukumiwa kuyongwa au upo tayari kuongea ukweli uendelee kubakia hai?”
“Nitasema nitasema kila kitu”
“Nakusikiliza”
“Mimi naitwa Steva Mrisho. Nimezaliwa Kilimanjaro na huku Dar es salaam nimekuja kutafuta maisha. Kwenye kuhangaika kwangu nilikuja kukutana na Jabeli ambaye ndiye alikuwa bosi wangu, wakati anajenga duka lake kule Riverside mimi ndiye ambaye nilikuwa napeleka maji kwenye ujenzi hivyo ikafanya tuwe tunakutana mara kwa mara. Kukutana kwetu kulitufanya tuongee mambo mengi sana ya biashara kwani tulizoeana na baadae akaja kuniambia kwamba anataka kufungua duka la vifaa lakini hakuwa na mtu wa kumuweka pale hivyo kama sitajali ile sehemu niingie mimi yeye angenilipa mimi pesa nzuri sana”

“Kutokana na maisha yangu kuwa magumu sikuwa na namna nikaamua kukubali na kuanza rasmi kazi nikiwa chini yake. Alinifanya kuwa kama ndugu kwake na kufikia hatua ya kuniamini sana kiasi cha kuja kunileta hadi kwake kwa sababu nilikuwa nafanya kazi kwa bidi sana, kwa muda mfupi tu nilifanya lile duka likawa kubwa sana na wateja wakawa wengi mno kwahiyo ilipelekea baadhi ya muda mimi kuja huku kwake kukutana naye moja kwa moja ili kuongea ni namna gani tunaweza kuifanya bishara ikawa kubwa zaidi”

“Maisha yaliendelea kama kawaida mpaka usiku wa jana ambapo nimepigiwa simu na mtu ambaye sikuwa namjua kwa sababu namba zangu nimeandika pale dukani hivyo mtu mwenye shida ya kibiashara na mimi anaweza kunipata muda wowote ule. Mtu huyo ameniambia kwamba ana shida ya kununua vifaa vingi sana kwa sababu kesho yake asubuhi alikuwa na kazi kubwa sana ya kufanya kwenye gereji yake hivyo nikampatie vifaa hivyo”

“Kwa pesa ambayo alikuwa ameitaja nimeshindwa kabisa kukataa ikanibidi niende nikamuuzie hivyo vitu lakini kitu ambacho nimekutana nacho ni tofauti na matarajio yalivyokuwa kwani mwanaume huyo amenitishia kuniua kama nikikataa kufanya anacho kihitaji huku akiniwekea bastola kichwani akasema kwamba nimlete mahali ambapo anapatikana bosi wangu na kwa mazingira yalivyokuwa sikuwa na namna zaidi ya kumleta hapa ambapo bosi alikuwa hajafika bado”

“Baada ya bosi kuweza kufika ndipo wakaanza kupigana, nimeogopa sana baada ya kuona bosi anapigwa risasi nyingi sana kwenye miguu yake kisha akawa anazamisha kisu kwenye shingo yake. Baada ya hapo sijaelewa kilichokuwa kinaendelea maana nilizimia” Steve alielezea ukweli wake huku akiwa analia, alitamani ni bora angebakia kwenye biashara yake ya kuuza maji kama ilivyokuwa zamani kuliko mambo kama hayo ambayo yalianza kuyatia dosari maisha yake mapema sana. Askari huyo hakuonekana kuliridhika na maneno ya mwanaume huyo hivyo akaendelea kumhoji kwa undani zaidi wakati askari wengine wakiwa wanafanya taratibu za kuupima mwili.

“Umesema amemshambulia bosi wako? Kwamba amemuua bila sababu za kufanya hivyo?”
“Nilisikia akimuuliza bosi kwamba kichwa cha mdogo wake kiko wapi na dada yake yuko wapi?”
“Whaaaat?”
“Ndiyo mkuu”
“Na bosi wako anasemaje?”
“Kwakweli sijajua maongezi yao yameishaje mimi nilizimia”
“Unataka kuniambia kwamba huyo bosi wako alimuua mdogo wake na huyo mtu kisha akamteka dada yake?”
“Sijui ila nahisi hivyo” Askari huyo hiyo taarifa ilimshtua sana kiasi kwamba hakuendelea kumhoji mtuhumiwa wake bali alimfunga pingu haraka sana kwani ilionekana kuwepo kesi nyingine tena nzito ndani yake.

Naam ukurasa wa thelathini na nne unafika tamati, panapo majaaliwa tukutane tena ukurasa unao fuata.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA TANO
Wakati hayo yote yanaendelea inspekta Kaoneka alikuwa makini sana kwenye kuangaza kila eneo kuona hali ilivyokuwa. Akiwa anangaza aligundua kwamba taa moja ambayo ilikuwa karibu na hilo eneo ambalo tukio hilo lilifanyika ilikuwa na kamera ndani yake, aliangalia kama kuna mtu alikuwa anamuona, baada ya kuona kwamba hakukuwa na macho ambayo yalikuwa upande wake aliihifadhi kwenye mfuko wa koti lake kisha akasogea mpaka ulipo mlango mkubwa wa nyumba hiyo ambapo alivunja kitasa na kuingia ndani akionekana kuwa mtu mwenye haraka sana.

Kwenye kuzunguka kwake humo ndani aliishia kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa cha kuongozea kamera ndani ya jengo hilo. Alizima kila kitu ambacho kilikuwa nje na kuufunga mlango kisha akaanza kuangalia matukio ya muda mfupi ambao ulikuwa umepita nyuma. Mambo ambayo alifanikiwa kuyaona hapo yalimfanya kufumba macho kwani ulikuwa ni ukatili ambao ulikuwa umezidi mipaka sana.

“Mhhhhhh hii nchi tunaishi na mijitu ya namna hii na ndo wanataka sisi polisi tuitafute kweli? Huku si kutafuta kifo kabisa” mwili wake ulikuwa ukimsisimka sana akiwa anayatamka hayo maneno kwa namna alivyo shuhudia mwenzake akiwa anauliwa kikatili. Aliichukua video hiyo ya hilo tukio na kuihifadhi kwenye simu yake na kufuta kila kitu hata ile taa ambayo ilikuwa kwenye mkono wake aliivunja kabisa na mabaki yote akayatupia chooni.

Wakati anahitaji kutoka ndani ya chumba hicho ni kama kuna kitu alikikumbuka kuhusu ile video ambayo alikuwa ameiona, alishtuka sana basi ikamlazimu kuweza kuirudia tena kwenye simu na kuikuza ile sura ambayo alikuwa ameishtukia. Baada ya kuiona sura hiyo hakuamini kile ambacho alikuwa anakiona ikambidi kuitoa simu nyingine na kuipekua picha moja ambayo ilikuwa inafanana na yule mtu ambaye alikuwa anaonekana kwenye video. Mawazo yake yalikuwa sawa maana ile picha ya yule mwanaume alikuwa nayo na alikuwa ni mtoto wa damu na wa kiume pekee kwenye familia ya Apson Limo.

Hilo ni jambo ambalo lilimshtua sana hivyo ikamlazimu kuitafuta namba moja kwenye simu haraka sana na kuipiga akiwa anahema kwa wasiwasi isivyo kawaida.
“Hello, nahitaji kuongea na bosi” aliongea kwa pupa sana baada ya simu hiyo kuweza kupokelewa.
“Utaongea naye baadae yuko busy sana kwa sasa”
“Ni jambo la mhimu sana”
“Njoo usiku ukutane naye nitampa taarifa na eneo la kukutania ni lile lile kwa leo” sauti nzito ilisikika upande wa pili.
“Hey, nisikilize ni jambo la mhimu sana kuliko unavyo fikiria wewe. Niunganishe naye haraka sana” aliongea kwa hasira lakini kwa sauti ambayo hakutaka mtu yeyote amskie mbali na pale ila aligundua kwamba simu hiyo ilikuwa imekatwa muda mrefu sana upande wa pili.

“F*****k” alijikuta anatukana sana baada ya kugundua hilo. Alijaribu kupiga tena kwenda kwenye namba hiyo lakini namba hiyo ilikuwa inatumika kila wakati akagundua mtu huyo alikuwa ameizuia simu hiyo baada ya mhusika kuonekana kwamba alikuwa msumbufu sana. Aliishia kutukana tena na kutoka humo ndani ambapo alitoa taarifa kwamba taarifa juu ya mtu huyo aliyekuwa ameuliwa isitolewe sehemu yoyote ile kwani ingeleta mkanganyiko mkubwa sana kwa watu na jamii hususani ukizingatia kuna mambo ambayo yalikuwa yametokea tayari hivyo akaahidi kulishughulikia hilo jambo mweyewe akiamini kwamba atapata mwafaka mzuri zaidi akikutana na bosi wake huo usiku huku ikiwa haijulikani kwamba huyo bosi wake alikuwa ni nani hasa.

Inspekta Kaoneka aliusogelea ule mwili wa Jabeli ambao ulikuwa umefanywa kitu kibaya sana na kuutoa kwenye hali ya ubinadamu kabisa. Mwili wake ulisisimka sana baada ya kushudia moja kati ya matukio ya kutisha zaidi kwenye maisha yake, aliwasha gari yake na kutokomea kusiko julikana asubuhi ya mapema hiyo.

Asubuhi hiyo haikuwa njema sana kwenye masikio ya watu wengi na kwenye maisha ya watanzania kwa ujumla kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje kabisa ya uwezo wao lakini ilikuwa ni tofauti sana kwa baadhi ya watu ambao kwao hali hiyo ilikuwa inaendelea kuwapa upepo safi wa kuhakikisha kwamba maisha yanakuwa safi na wanaishi kwa namna wanavyotaka wao.

Majira hayo ya asubuhi aliyekuwa raisi wa nchi na kwa wakati huo alikuwa amekubali kuachia madaraka na kuamua kumpa sapoti kubwa mr Mafupa alikuwa ndani ya ofisi yake akionekana kuzichambua taarifa fulani kwa umakini mkubwa sana. Alitumia zaidi ya dakika ishirini akiwa amekaa na kuinamia kwenye komputa mpakato yake na baada ya kumaliza hapo alinyanyuka na kutoka hilo eneo kisha akafungua chumba ambacho kilikuwa mita kadhaa kutokea hilo eneo ambalo yeye alikuwepo.

Ndani ya chumba hicho kulikuwa na mlango mwingine ambao ulitengenezwa kwa shaba, aliweka mkono wake kama finger print kisha akajaza namba kadhaa kwenye kibox ambacho kilijitokeza mbele yake na baada ya kukamulisha jambo hilo, mlango wa hiyo sehemu ulifunguka wenyewe akaingia ndani kisha ukajifunga tena.

Hicho kilikuwa ni chumba chake ambacho alikuwa anakitumia kutunzia kumbukumbu zake na taarifa zake za mhimu za siri sana ambazo hazikutakiwa kupatikana na mtu mwingine yeyote yule kwa sababu uhalisia wa maisha yake ulikuwa ndani ya hicho chumba. Kwenye moja ya kona ya chumba hicho kulikuwa na safe moja kubwa sana ambayo ilitengenezwa kwa madini ya shaba hivyo aliisogelea na kuchuchumaa hapo. Aliingiza namba nyingi sana kwa kuzichanganya ndipo sehemu hiyo ikafunguka.

Ilikuwa kama droo kubwa ambayo kuna baadhi ya sehemu ilijaa pesa za kimarekani na uingereza na bastola. Droo nyingine ilikuwa na madini mengi sana ambayo yalionekana kuwa ya pesa nyingi isivyo kawaida, hata hivyo nayo hiyo hakuijali kabisa mpaka alipofika sehemu ambayo ilikuwa na kichupa kimoja chembamba ambacho kilihifadhiwa kwenye plastic moja ngumu sana kutokana na unyeti wake. Pembezoni mwa kichupa hicho pia kulikuwa na kichupa kingine ambacho kilikuwa kimeandikwa antidote na chini kabisa mwa droo hiyo kukiwa na bahasha.

“Kirusi hatari zaidi duniani kipo kwenye mkono wangu, hiyo inamaanisha kwamba naweza kufanya lolote nilalo litaka mimi hapa duniani na ulimwengu mzima ukanisikiliza mimi kwa lolote ambalo nalihitaji hivyo wakinipinga tu inakula kwao. Hahahaha mimi ndiye mtu pekee ambaye naenda kuutawala ulimwengu bila shaka na mtu yeyote ambaye atahitaji kujitokeza mbele yangu basi nitamfanyia kitu kibaya sana ambacho hatakisahau kamwe kwenye maisha yake yote” aliongea kwa kujiamini sana kwani aliamini kila kitu kilikuwa kwenye mkono wake na lilikuwa ni jukumu lake yeye kuchagua kwamba alikuwa anahitaji kufanya nini na kirusi hicho.

Chini kabisa kwenye kona ya droo hiyo kulikuwa na simu ndogo ambayo baada ya kuiwasha ndani yake ilikuwa na namba moja tu pekee. Aliipiga bila wasiwasi ambapo iliita kwa sekunde sita tu.
“Tukutane leo usiku saa saba kamili” ilikuwa ni sauti ya msisitizo ambayo aliitamka kisha akaikata simu hiyo na kutoka humo ndani huku akipaweka sawa kama palivyokuwa mwanzo kabla ya kuingia. Aliichukua simu ya mezani kwake kwenye ofisi yake na kuiipiga mahali tena.
“Nakuhitaji ofisini haraka sana” ilikuwa ni amri hivyo ndani ya muda mfupi tu vilisikika viatu nje ya ofisi hiyo mtu ambaye alikuwa amepigiwa hiyo simu alikuwa amefika ndani ya hilo eneo.

“Leo usiku nataka kukutana na mshirika wangu ili tuweze kufanya makubaliano kujua mzigo tutamuuzia nani hivyo inatakiwa ulinzi mkubwa sana kwake kama unavyo jua yule anaishi kama kivuli hatakiwi kabisa kujulikana lakini hili jambo halitakiwi kuvuja kwa mtu yeyote yule kwani mhusika utakuwa ni wewe kwa vile ndiye ambaye pekee unalijua hili jambo na sio mtu mwingine yeyote yule” raisi aliongea kwa msisitizo huku akiwa anampa ishara ya kuketi huyo mzee ambaye alikuwa ameingia hapo, hakuwa mwingine bali mshauri wake ambaye alikuwa naye karibu muda mwingi.

“Nimekuelewa kiongozi, siwezi kukuangusha juu ya hilo. Mapema sana kila kitu nitakiweka sawa na hakuna tatizo lolote ambalo litaweza kutokea”
“Mpango ambao uliuwa umeuchora ni kwamba mr Oscar afe lini?”
“Nadhani kwa sababu siku chache mbele kampeni zinaanza tunatakiwa kusubiri siku moja baada ya uchaguzi ndipo tufanye hivyo kwa sababu yule kijana atakuwa amekabidhiwa Ikulu nawe ndiye ambaye utamkabidhi hivyo wakati huo ndio utakuwa muda sahihi wa kumuua mr Oscar na wewe utakuwa yeye”
“Nimewaza sana juu ya hilo jambo, itakuwaje pale watakapo nihitaji kuja kuwa mshauri kwa upande wa raisi ambaye atakuwa madarakani na itawezekana vipi mimi kujigawa kila upande?”
“Mheshimiwa mbona hilo jepesi sana. Siku zote unapokuwa unapanga mipango mikubwa sana lazima uwe na plan B”
“Ipi hiyo?”
“Wewe utatakiwa kufa kabisa kwenye macho ya watanzania”
“Whaaaaat?”
“Ndiyo wewe hautakiwi kuwepo tena”
“Umeniacha njiani kidogo, unamaanisha kwamba?”
“Siku ambayo tutamuua mr Oscar ndiyo siku ambayo wewe pia watu watajua kwamba umekufa”
“Kivipi?”
“Itatengenezwa ajali mbaya sana ambayo itawahusisha watu kadhaa na gari kadhaa zitahusishwa. Kwenye moja kati ya miili ambayo itakuwepo, tutamtafuta mtu ambaye atakuwa anaendana mwili na wewe. Kwa sababu gari hizo zitatakiwa zilipuke na kuungua vibaya sana basi hakuna ambaye ataweza kujua kwamba sio wewe kwani hata kama vikosi vya wokozi vitafika hilo eneo kuweza kuleta msaada kuna watu ambao tutakuwa tumewaweka hivyo watawapotezea muda mpaka tukio litakapo kamilika”
“Enhe!”

“Hapo kitakacho fuata ni uchunguzi mkali sana pamoja na msako mali kujua aliye husika na mauaji yako. Kwenye msako mkali hapo kuna vijana ambao tutawatoa sadaka kwa kuwakamatisha ambao watasaidia kuvipotezea muda vyombo vya usalama lakini kwnye uchunguzi tutafanya kila namna ili vipimo vionekane ni vya kwako na madaktari watathibitisha kwamba wewe umekufa kweli na hiyo ndiyo itakuwa nafasi ya kumuua mr Oscar na kuishi kwenye nafasi yake kwa namna utakavyo hitaji mwenyewe”
“Mhhhhhh mpango wako ni mzuri sana ila inawezekanaje niishi kwenye sura ya mtu yule mpaka nakufa aisee mbona aibu sana hii?”
“Kiongozi kwani hiyo sura ya sasa ni yako?” raisi huyo alitabasamu sana,alionekana kwamba aliambiwa ukweli ambao ulimgusa.
“Na vipi kama sitaki kumuua mr Oscar?”
“Basi itatakiwa umhifadhi eneo ambalo hakuna mtu atakuja kujua kuhusu uwepo wake”
“Yes, hilo ndilo bora zaidi”
“Unataka kumuacha hai?”
“Ndiyo”
“Kwanini kiongozi?”
“Yule nina historia naye nzito sana, ni mwanadamu ambaye nahitaji atoe machozi ya damu huku akiwa ananipigia magoti”
“Kwahiyo utafanyaje?”
“Sitamuua bali nitamuacha hai ila atatamani kwamba ni bora ningemuua kwa mambo ambayo nitamfanyia, na huu unaenda kuwa muda sahihi sana wa mimi kulipa kisasi kwa kila aliye husika kunipa maumivu nikiwa sijulikani kama nipo hai. Hakuna familia hata moja ambayo nitaacha hata mtu mmoja kwa wale wote ambao walitia mkono kunipa maumivu ya maisha na kuipoteza familia yangu ambayo niliipenda sana. Nitawafanyia mambo mabaya sana” raisi huyo aliongea kwa msisitizo sana akionyesha wazi kwamba alikuwa na kisasi kizito sana kwenye moyo wake. Mshauri wake hakuwa na cha kuongea kwani yalikuwa ni mambo binafsi sana.

“Unaweza kwenda ila nahitaji kuipata taarifa yote ya familia ya Apson Limo kabla ya kukutana na mkurugezi wa idara ya usalama wa taifa” alimpa maagizo hayo mshauri wake na kuruhusu aweze kuondoka ndani ya hilo eneo.


Rasmi ukurasa wa thelathini na tano sina kingine cha kuweza kuongeza, nafika tamati.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA PILI
Mr Apson baada ya safari yake ya muda mfupi ambao aliutumia kuendesha gari yake kwa kasi isiyo ya kawaida alifanikiwa kufika nyumbani akiwa anahema kwa nguvu mno, walinzi wake walibaki wanamshangaa kiongozi huyo maana hakuwahi kuwa kwenye hali kama hiyo siku zote za maisha yake hata ule msafara wake ambao ulikuwa unamlinda ulikuwa unamshangaa kiongozi huyo kwani hakuwa akiendesha gari bali alikuwa akiendeshwa siku zote lakini siku hiyo alitoka ofisini na kuingia kwenye gari akaitoa kwa kasi bila taarifa hali ambayo ilipelekea walinzi wake kumfuata nyuma na magari mengine.

Alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana mheshimiwa Apson kwani hata jumba lake tu lilielezea namna alivyokuwa na maisha mazuri. Aliwapita walinzi wake kama vile hakuwa akiwaona huku gari akiwa ameiacha nje. Alikimbilia mpaka ndani lakini hakukuta mtu ila alisikia kelele upende wa pili ambako aliwaona watoto wake wakiwa wanacheza na mkewe, alijikuta anatabasamu na kukaa kwenye korido ya kushukia eneo hilo ambalo lilikuwa na bustani nzuri na bwana la kuogelea akiwa anaiangalia familia yake.

Kwake familia ilikuwa kila kitu, hakuwa na kitu ambacho angeweza kukiweka sawa na hiyo familia akakilinganisha kwenye mzani mmoja. Mkewe alikuwa ni rafiki mkubwa sana kwa wanae hususani yule mtoto wa mwisho ambaye ndiye alionekana kupendwa kuliko wengine wote. Baada ya kuona watu hao hawana muda naye kabisa ikabidi ajikohoze kidogo ili kuwashtua na ndipo hapo walipo tulia kwanza na kugeukia upande ambao yeye alikuwepo.

Mtu wa kwanza kumkimbilia alikuwa ni mwanae wa mwisho wa kike ambaye ndiye alikuwa kipenzi chake, alimkumbatia baba yake huku akidai zawadi zake lakini tajiri huyo hakuwa na zawadi kwa muda huo kwani aliondoka kwa kasi tu kuweza kuwahi nyumbani hakuwa hata na muda wa kubeba zawadi yoyote ile hivyo akamuahidi mwanae kwamba angemletea baadae maana ameagiza tayari.

Watoto wote walimkumbatia kwa mapenzi mazito mno kuonyesha ni familia ambayo ilikuwa na raha mstarehe isivyo kawaida, mtu wa mwisho kabisa alikuwa mkewe ambaye alimkumbatia baada ya watoto kuondoka na kwenda ndani. Akiwa kwenye kifua cha mmewe aliinua uso wake na kumtazama mwanaume huyo kwenye uso wake

“Una hofu sana, nini shida baba?” kitu ambacho hakuwa na uwezo wa kukificha ni uhalisia wake kwa mwanamke huyo ambaye alikuwa anamjua vizuri sana, kumkumbatia tu kidogo aligundua kwamba mumewe alikuwa na wasiwasi isiyo ya kawaida.

“Nawaza sana kuhusu mustakabali wa maisha yangu kuhusu siasa, siasa naiona kabisa kama sio sehemu salama kwangu, nadhani ile siku ambayo nilikubali kuwa mwanasiasa ndiyo siku ambayo niliamua kuitoa sadaka familia yangu. Naomba unisamehe mke wangu, naogopa sana” aliongea huku akiwa anaketi chini kwenye hizo korido lakini mkewe alimkumbatia na kukilaza kichwa cha mumewe kwenye mapaja yake.

“Hili unalo lifanya ndilo limeifanya familia hii kuwa yenye furaha kubwa sana, watoto huwa wanajivunia sana kuwa na baba kama wewe hususani unapokuwa mbele ya vyombo vya habari ukiwa unaongea, namna unavyo tengeneza hoja fikirishi, namna ulivyokuwa mtu wa kuwaza mambo makubwa na mambo ambayo yanajenga fikra za mtu yeyote hivyo hauna haja ya kutuomba sisi msamaha bali unatufanya tujivunie kuwa na wewe. Najua siasa ina mambo mengi sana na sio hapa tu bali duniani kote kwani unakuwa na maadui wengi sana na ndiyo maana wewe hapo una mke ili pale unapokuwa kwenye hali kama hii mimi nipo kukuweka sawa. Kitu ambacho unatakiwa kukifanya popote ulipo kifanye kwa ukubwa hata kama utakutana na changamoto gani kwa sababu unatakiwa kujua kwamba mkeo ndiyo mshabiki wako namba moja ambaye anakupenda sana kama kiongozi wake lakini pia anakupenda na kukuheshimu kama mumewe” alitabasamu mr Apson na hiyo ndiyo sababu ambayo mara nyingi sana ilikuwa ikimfanya amuwaze mkewe kila anapokuwa mbali naye. Huyo mwanamke alikuwa chanzo kikubwa sana cha furaha kwake, ambapo angehisi kuchanganyikiwa basi akiwa mbele ya mwanamke huyo alikuwa anakuwa sawa. Mawazo yake yote yaliisha ndani ya dakika moja wakajikuta wote wanacheka sana huku wakitaniana na mkewe alimtaka mwanaume huyo akaoge kisha wakapate chakula pamoja.

“Dady nataka kumuona kaka, nimemmiss” ilikuwa ni sauti ya Latifa ambaye alikuwa ndiye mtoto wa mwisho kabisa wa mr Apson, aliongea wakati wakiwa wanaendelea kupata chakula. Kauli yake aliiongea kwa masikitiko sana, alikuwa ni mtoto wa mwisho ambaye alipendwa sana hivyo wazazi walikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake yeye. Ndani ya familia hiyo kulikuwa na mtoto wa kiume mmoja tu ambaye alikuwa anaelewana sana na Latifa na ndiyo sababu alikuwa akimkumbuka sana kaka yake kwani ndiye aliyekuwa akimpenda sana kuliko ndugu zake wengine wote.

Mr Apson aligeukia upande wa ukutani akiwa kwenye tabasamu zito, ukutani palikuwa na picha kubwa sana ya wanaume wawili wakiwa ndani ya suti za blue ambazo zilikuwa zinafanana kwa kila kitu. Wanaume hao walikuwa wanafanana mno ila kilichokuwa kinawatofautisha ni umri, upara na kitambi. Mr Apson kwenye hiyo picha ndiye alikuwa na umri mkubwa zaidi, na ndiye ambaye alikuwa na kitambi pamoja na upara ila ilikuwa ni tofauti kwa huyo mwanaume mwingine ambaye bila shaka alikuwa ni mwanae wa damu kwani alikuwa anafanana naye utadhani alijitoa kopi yake.

Huyo ndiye alikuwa mwanae pekee wa kiume ambaye ndiye alikuwa mrithi wake kwa kila kitu hivyo mwanae huyo wa kike kudai anataka kumuona kaka yake, alitabasamu sana baada ya kuiona ile picha kisha akatamka

“That’s my boy” aliongea akiwa na cheko la furaha kisha akaitoa simu yake na kupiga video call kwa mtu huyo ambaye alionekana kuwa nje ya nchi ili mdogo wake huyo aweze kumuona. Kweli simu iliita kwa muda mfupi kisha ikapokelea na mtu ambaye ungehisi ni yeye mwenyewe kwa namna walivyokuwa wanafanana. Hawakuongea lolote zaidi ya kumpa simu kwanza Latifa maana angeanza kusalimiana na wengine hapo ingekuwa kesi nyingine hiyo. Alifurahi sana kumuona kaka yake ambaye alimpenda mno kisha kijana huyo akawasalimia na wengine kisha akakata simu yake huku akiahidi kwamba muda mfupi ambao ulikuwa unakuja angeweza kurudi nchini maana amemaliza masomo na kwa wakati huo alikuwa anatalii kabla ya kuianza safari.

“Mwanangu arudi tu nimemkumbuka sana, ni muda sana sijampikia chakula change, watakuwa wanamlisha mavyakula ya hovyo ya dukani huko maana naona amepungua sana” aliongea mama yake akiwa amemkazia macho mumewe kama kumwambia hakikisha mtoto anarudi haraka namtaka nyumbani hapa. Mzee Apson ilibidi ajikohoze maana mkewe alimpiga jicho kali mpaka yeye mwenyewe ikabidi azuge kwa kubadilisha maada ya hapo.

“Linda yuko wapi?” aliuliza swali kuhusu uwepo wa binti yake mkubwa ambaye ndiye alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia.

“Atakuwa kwenye biashara zake huko maana alisema kwamba amepata watu wa nje wa kufanya nao kazi nadhani atakuwa anamalizana nao kwenye masuala mazima ya mikataba” mkewe alimjibu kwa ufupi ili kumridhisha maana mzee huyo kwa namna alivyokuwa anawapenda wanae kama asingepewa taarifa ya maana angeacha hata kula hapo akamtafute mwanae.

“Hahahaha my princess, anapambana sana ndiyo maana najivunia yeye kuwa wa kwanza kuzaliwa kwani anakuwa mfano kwa wenzake kila inapo itwa leo. Nataka nimfungulie kampuni kubwa zaidi ya mitindo maana ile aliyo nayo kwa sasa ana uwezo wa kuisimamia vizuri hahahaha nataka mwanangu awe malkia wa mitindo kwenye hili bara zima la Afrika” aliongea kwa kutamba mzee huyo akiwa ananyanyuka na kucheza kidogo kitu kilicho pelekea wote kulipuka kwa kicheko maana mzee huyo alikuwa mwenye furaha sana na alipenda wakati wote familia yake iwe ina furaha.

“Na mimi sasa unitafutie biashara kubwa nyingine sio unawawaza wanao tu unamsahau mkeo aliyekuletea hao watoto, yaani nyie wanaume mkiwa na watoto tu hata mke unamsahau sijui mlirogwa na nani” mkewe aliongea huku akiwa anacheka kitu kilichofanya watoto wote wamzunguke kumcheka.

“Mama unawaonea wivu hadi wanao hahahahaha” wanae walikuwa wanamcheka huku wakiwa wanamtekenya, walianza kukimbizana humo ndani huku mumewe akikimbilia bwawani kuogelea. Ilikuwa ni moja ya familia ambazo zilikuwa kwenye furaha kubwa sana.


Ndani ya jengo lingine kubwa la kifahari majira ya usiku, alionekana mr Mafupa akiwa anavuta sigara yake ya bei ghali akiwa ametulia sehemu ambayo bila shaka ilikuwa ni mapokezi akiwa anasubiria kukutana na mwenyeji wake. Baada ya dakika tano za kusubiri akiwa anaivuta sigara yake, alikuja mwanaume mmoja ambaye alikuwa amejaa sana kwenye mwili wake na kumtaka asimame. Hakuwa na usumbufu wowote kwani alisimama na kuikabidhi sigara hiyo kwa kijana wake ambaye alikuwa amemshikia mkoba wake kisha akasimama na kuanza kusachiwa kama ana silaha yoyote kwenye mwili wake na baada ya kuonekana kwamba hana shida, mwanaume huyo alimpa ishara ya kumfuata ili akakutane na mtu ambaye alikuja kumuona huku mlinzi wake akibakia nje sehemu ya mapokezi.

Baada ya kuingia ndani alikutana na mtu mmoja ambaye alikuwa amesimama kageukia ukutani akiwa anaangalia picha kubwa nzuri za gharama ambazo zilikuwa zimepambwa ukutani mwili wake ukiwa ndani ya kanzu ndefu sana nyeupa na kichwa chake kikiwa wazi kabisa.

“Samahani sana kwa kukuingilia kiongozi, naona unajikumbushia mbali sana kwa kuangalia picha nzuri za kihistoria” Mr Mafupa aliongea huku akiwa anautua mkoba wake chini na kubaki amesimama kama alivyo ingia maana hakuona kama ni sahihi kukaa kabla ya kukaribishwa ingali mwenyeji wake naye bado amesimama.

“Unajua watu wengi mpaka leo bado hawajui kwamba hii ni moja ya nchi zilizo barikiwa kila kitu. Huwezi kuamini kwamba haya mazingira yapo hapa hapa Tanzania na hata mchoraji ni mtanzania, hizi ni miongoni mwa picha adimu sana kupatikana duniani hata nikiamua kusema nazipeleka kwenye minada huko kwa wenzetu naweza kutengeneza pesa ambayo nitakula mpaka nakufa na bado nitaiacha”

“Mhhhhh sasa kwanini hauziuzi?”

“Kuna muda kwenye maisha yako hakikisha kwenye mkono wako una vitu vya thamani ambavyo ni adimu kupatikana hiyo itakufanya upate heshima kubwa sana kwenye maisha yako yote na ndiyo maana hizi huwezi kuzikuta popote pale zaidi ya kwangu tu kwani hata mchoraji alikufa miaka mingi sana iliyo pita. Wamekuja wachoraji wengi sana wamejitahidi ila bado hakuna ambaye anaweza kuingia ligi moja na aliye zichora picha hizi na ndiyo maana zinabaki kuwa picha bora sana kuwahi kuchorwa ndani ya nchi ya Tanzania” mzee huyo aliongea akiwa anampa ishara mgeni wake aweze kuketi chini, haikuwa sawa kufanya mazungumzo wakiwa wamesimama wakati walitakiwa kupata vinywaji kidogo.

“Mr Oscar, kila nikiyaona matendo yako, nikisikia maneno yako kama hayo lakini pia nikitulia na kuisoma akili yako pamoja na misimamoyako basi naishia kumkumbuka sana wajina wako na nawaza sana kwamba kwanini uliishia tu kuwa waziri mkuu wakati kwa uwezo wako ulikuwa unaweza kuingia mpaka Ikulu kabisa?”

“Mhhhh usiniambie kwamba unamzungumzia Oscar ambaye ni miongoni mwa waasisi wa TANU?”

“Ndiyo mheshimiwa”

“Maisha hayakupi unacho kitaka wewe na kuna muda akili ikizidi sana matatizo makubwa yanaweza kutokea na ndiyo sababu hakuwa na mwisho mzuri sana. Tuachane na hayo unaweza ukaniambia sababu ya msingi ya mimi kukutana na wewe?”

“Nahitaji kuingia Ikulu”

“Sasa mimi nahusikaje hapo wakati ni suala la wewe kuwa na ushawishi mkubwa tu ili uchaguliwe na kuungwa mkono na wananchi pamoja na watu wa chama chako?”

“Mpaka nakuja kwako nina uhakika unaelewa vyema namna siasa ilivyo, unaelewa vizuri kwamba ninashindana na raisi wangu lakini pia nina uhakika wewe unaelewa namna siasa inavyo fanya kazi, kuna muda Ikulu sio wananchi wanao kuweka bali watu kama wewe hapo ndio ambao wana uwezo wa kumuweka mtu Ikulu au kumtoa Ikulu kwani hii nchi nyie mnaijua kuliko mtu mwingine yeyote yule”

“Mhhhhh unahisi ni sababu gani labda ambayo itanishawishi mimi kukusaidia wewe uingie Ikulu kama unavyo hitaji?”

Naam ukurasa wa pili nafika mwisho, ungana na mimi kwenye ukurasa wa tatu ambao unafuatia.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Well
 
BADO NINAISHI.

Je umeisoma dunia ya kutisha ya REMY CLAUDE? Kama jibu ni hapana basi leo nakusogezea ofa ya mwisho ya mwezi ambapo unaisoma kwa 4000 tu badala ya 5000.

4000 yako tu leo inakufanya unalisoma moja kati ya andiko bora sana la kijasusi kuwahi kuandikwa.

Muda ni wako sasa, lipia 4000 kwa hizi namba

0621567672 .....HALO-PESA

0745982347...... M-PESA

0714581046..... TIGO-PESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.


ASHRAFU NDILO JINA LANGU..... usilikose hili andiko kwa namna yoyote ile.
FB_IMG_1709203161279.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA SITA
Mr Oscar naye upande wake hakuwa na papara wala wasiwasi na maisha kwani alijua kila kitu kilikuwa kipo upande wake, alikuwa anahesabu wiki kadhaa tu kuweza kuitia nchi kwenye mkono wake kupitia Mr Mafupa. Asubuhi hiyo alikuwa ametulia kwake akiwa anapitia habari mbali mbali ambazo zilikuwa zimejitokeza ndani ya nchi huku akiwa mwingi wa tabasamu.

Mambo ambayo yalikuwa yanaendelea yalikuwa ni mengi sana lakini hayakuwa yakimhusu, kikubwa zaidi ambacho alivutiwa nacho sana ni kelele za wananchi kuhusu hali ya mtu ambaye walikuwa wanamtumainia sana Apson Limo. Walikuwa wakidai kwamba serikali haikuwa imetoa tamko tena kuhusu hali yake au ile sitofahamu ambayo ilitengenezwa kutoka kwenye ofisi ya DCI kwamba mzee huyo ana makosa ya jinai mengi sana hivyo mahakama ingechukua hatua yake.
“Hivi unahisi kwamba hili wazo lilikuwa la nani kuamua kumchafua huyu mzee?” mr Oscar alimuuliza kijana wake akiwa anapekua pekua kuona undani wa taarifa hiyo.
“Huenda ni mamlaka za juu zaidi kwani kumtuhumu mtu mkubwa kama huyo sio rahisi sana inabidi uwe umejipanga kwani ukishindwa kuthibitisha madai yako kumhusu inaweza kula kwako baadae”
“Sitaki kuamini kwamba hata raisi anahusika na jambo hili ambalo linaendelea!”
“Inawezekana bosi wanadamu sio wa kuwaamini sana”
“Mhhh unamaanisha hata wewe sipaswi kukuamini sana?”
“Sina maana hiyo kiongozi”
“Vijana wapo tayari?”
“Ndiyo kiongozi”
“Waruhusu waingie ndani niweze kuongea nao” kijana huyo ambaye ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa mr Oscar alitoka na kwenda kuwachukua watu hao ambao aliwataka waingie hapo ndani. Waliingia wanaume wa kazi wanne ambao miili yao tu ilikuwa inaonyesha namna walivyokuwa watu wa kazi huku wawili wakiwa na asili ya nchi ya Japan.
“Nadhani mnajua kilicho waleta hapa?”
“Yes, ni kazi”
“Sawa, kijana wangu atawapa maelekezo, nahitaji muingie mtaani muue kila mtu ambaye anahusiana na mr Mafupa ambaye muda sio mrefu anaingia Ikulu. Sitaki awe na mtu yeyote yule ambaye anaweza kumfanya kwa baadae aanze kunikimbia au kunisaliti maana simuamini sana. Mkishamaliza kazi yenu malipo yenu yapo tayari” hawakuwa watu wa kubonga sana, baada ya kuyapata tu hayo maelezo wanaume hao walitoka humo ndani na kumuacha mzee huyo akiwa anazama kwenye fikra ndefu sana.

Siku hiyo ilienda vibaya kwani iliisha isha tu ila ndiyo hivyo hakukuwa na namna wala uwezo wa kuanza kuyarudisha masaa nyuma tena. Usiku wa siku hiyo inspekta wa polisi ambaye alijulikana kama Kaoneka alikuwa kwenye mwendo mkali sana ndani ya gari yake ya polisi akionekana kuwahi sehemu ambako angekutana na mtu wa mhimu sana kwake.

Baada ya mwendo wa muda mrefu hatimaye alisimamisha gari yake maeneo ya Kawe karibu kabisa na viwanja vya Tanganyika Parkers. Alishuka na kuanza kutembea taratibu mpaka alipofika karibu na majengo makubwa sana ambayo kwa sasa yanatumika kama sehemu ya ibada, karibu na hilo eneo alionekana mwanaume ambaye alikuwa ndani ya suti akiwa amezungukwa na walinzi huku amempa mgongo Kaoneka.
“Heshima yako kiongozi”
“Umeniweka kama dakika tano hapa, unaweza ukanipa sababu ya msingi?”
“Foleni ilikuwa kali sana kiongozi”
“Sawa nambie kilichokufanya ukahitaji kuniona moja kwa moja na kudai una shida kubwa sana” mtu huyo baada ya kutamka hilo neno aligeuka na kumwangalia Kaoneka. Sura yake haikuwa ngeni sana alikuwa ni mr Mafupa mwanaume ambaye ilidaiwa kwamba baada ya siku kadhaa angefanikiwa kuingia Ikulu kuweza kuliongoza taifa la Tanzania.

Kaoneka hakuongea jambo lolote mbele ya bosi wake zaidi ya kumpatia simu na kuiruhusu video ambayo ilikuwa kwenye kioo ianze. Mheshimiwa aliitazama video hiyo kwa umakini sana mpaka ilipofika mwisho.
“Sijakuelewa umenionyesha hii movie watu wanauana una maana ipi labda?”
“Hiyo siyo movie mzee, hata mimi mwanzo nilikuwa nafikiria hivyo hivyo ila hilo ni tukio la kweli”
“Una maanisha nini?”
“Hilo jambo limetokea leo hii”
“Sasa mimi linanihusu nini”
“Irudie tena video hiyo kisha uiangalie vizuri sura ya huyo muuaji nahisi utakuwa unamfahamu vizuri sana”
“Whaaaat?”
“Tumia dakika yako moja tu mkuu ni mhimu sana” mr Mafupa hakuwa na namna basi ilimlazimu kuizoom sura ya mtu huyo, alishtuka sana hata mikono yake ilionekana kuanza kutetemeka kwani hakuwa akiamimi kile ambacho alikuwa anakiona. Aliitoa simu yake mfukoni pia na kuitafuta picha moja ambayo ilikuwa inamuonyesha Apson Limo akiwa na mwanae wa kiume, yule ambaye alikuwa anamuona na kwenye video ilikuwa ni sura moja.
“Hapana, hili haliwezekani”
“Hata mimi nilishindwa kuamini kwa mara ya kwanza kama wewe hivyo hivyo mpaka baadae sana ndipo nimekuja kujua kwamba kumbe hili jambo ni kweli”
“Unataka kuniambia kwamba huyu ni mtoto wa kiume wa Apson Limo?”
“Ndiyo kiongozi, ni yeye mwenyewe huyu”
“Ooooh f********! Hili linawezekanaje?” aliongea akiwa anairudia hiyo video kwa umakini sana, alijikuta anaanza kutetemeka kiasi kwamba alitaka mpaka kudondoka chini ikabidi vijana wake waweze kumdaka kiongozi wao ili asije akapata tatizo. Kitu ambacho alikishuhudia kwenye video hiyo mara ya kwanza alihisi anaonyeshwa ni movie za kuigiza lakini aliambiwa kwamba haikuwa movie bali ulikuwa ni ukweli hilo tukio lilitokea.

Kitu ambacho kilimtisha zaidi huenda halikuwa tukio lenyewe tu bali mtu ambaye alikuwa analifanya tukio hilo ndiye ambaye alimtisha sana. Aliwahi kupewa onyo na mr Oscar kwamba asipende kujihakikishia mambo mengine ambayo anakuwa hayajui na asije akamdharau mtoto huyo kwani hawakuwa wakijua kwamba huko nje miaka yote hiyo alikuwa anafanya nini lakini yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kabisa kutetea kwamba mtoto huyo hakuwa na changamoto yoyote ile kwa sababu alikuwa akimjua vyema.
“Hili tukio la mwaka gani?”
“Leo kiongozi”
“Unanitania sio?”
“Hapana hilo tukio limetokea leo na huyo ambaye ameuawa ni mlinzi wa kampuni ya mwanao”
“Whaaaaaat?”
“Ndiyo mkuu” kauli hiyo ilimlazimu tena Mr Mafupa kuweza kuirudia video hiyo maana hakuwa ameitilia maanani sana. Baada ya kuikuza kwa ukubwa zaidi ni kweli aliiona sura ya Jabeli ambaye alikuwa moja kati ya walinzi wa kutumainiwa sana na Remsi. Alipigwa na butwaa mno na kushindwa kuamini hilo tukio kwani kama mlinzi huyo alikuwa amefikiwa basi lilikuwa ni suala la muda tu mwanae kuweza kufikiwa na mtu huyo.
“Kipi kimeendelea mbona hakuna taarifa yoyote ile kuhusu hili tukio sehemu yoyote ile?”

“Hiyo ndiyo sababu nilipiga simu asubuhi ile nikihitaji kuonana na wewe mkuu kwani nilitaka tuongee hili jambo ili tujue tunafanyaje. Hili jambo sijataka lijulikane na kuamua kulimaliza kimya kimya kwa sababu kama lingejulikana basi mambo yangeharibika sana kwani moja kwa moja ingejulikana kwamba yule alikuwa ni mlinzi wa Remsi na huenda watu wangeanza kuchimbua kuhusu hilo hivyo ungekuja kujulikana kwamba wewe ndiye baba yake na jambo hilo lingekuharibia sana jina ukizingatia kwa wakati ambao unao huu wa uchaguzi”

“Safi sana kijana wangu, umefanya kazi nzuri sana. Nitakupa nafasi kubwa sana kwenye utawala wangu” mzee huyo aliongea akiwa anaitoa simu yake mfukoni na kupiga kwa mwanae ili ampe taarifa kwamba mambo yameanza kuharibika lakini kwa bahati mbaya sana simu hiyo haikuwa ikipokelewa kwa wakati huo. Aliwataka watu hao waweze kuondoka eneo hilo kwa haraka sana ili waweze kumuwahi Remsi ili abadili mipango ikiwemo ya kumhamisha dada yake na Tommy maana huenda walikuwa wamejulikana tayari.

Lakini wakati watu hao wakiwa na mipango hiyo ya kuweza kuwahi kwa Remsi ikiwezekana aweze kumhamisha mwanamke huyo ni kama walikuwa wamechelewa kidogo kwenye suala zima la muda. Maeneo ya Kurasini wakati huo gari safi sana ilikuwa inapaki maeneo ya barabarani huku akishuka mwanaume Tommy akiwa kwenye mavazi yake ambayo hayakuwa na utani kabisa na mtu, yalikuwa ya kazi haswa. Kwenye kiuno chake alikuwa na bastola mbili lakini upande wa pembeni mwa kiuno alikuwa amechomeka bisu kubwa sana ambalo lilikuwa limefungwa vizuri.

Alikuwa na ramani ya nyumba na namba ya nyumba sehemu ambayo alikuwa anelekea hivyo hakuwa na wasiwasi alianza kutembea taratibu huku akiwa amevaa hood ambayo ilimfunika uso wake na kufanya asiweze kutambulika hata kama mtu angekutana naye basi hakuna mtu ambaye angeweza kumjua kwamba ni yeye. Mwanaume alitembea kwa dakika tatu tu akaiona reli mbele yake, aligeuza macho upande wake wa kulia ni kweli kulikuwa na lango la kuingilia kwenye uwanja wa ghorofa moja ambalo lilionekana kuwa la muda mrefu sana ila palionekana kwamba kuna watu walikuwa wanaishi humo ndani.

Alisogea taratibu na kwenda kusimama kwenye gari moja ya zamani sana ambayo ilikuwa imetelekezwa hilo eneo. Akiwa amesimama hapo aliona kuna mwanaume anapita kwa mbele kidogo akiwa anaangaza kila sehemu kana kwamba kuna kitu alikuwa anakitafuta lakini ilikuwa ni kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Aliguna kidogo na kumfanya mtu huyo ashtuke na kugeuka kwa kasi ili kujua ni kipi kilimshtua, lakini kugeuka kwake ndio ulikuwa mwisho wake kwani alipigwa na kiganja cha shingo ambacho kiliitegua shingo yake vibaya sana hakufanikiwa kutamka hata neno moja habari yake ikawa imeisha.

Alimvuta na kumhifadhi upande wa pili wa gari hiyo mbovu, hazikupita hata sekunde hamsini alisikia kuna mtu anaita kwa sauti ikionyesha wazi alikuwa anamuita mwenzake ambaye alikuwa amepotea ghafla tu. Aliangaza kila sehemu hakuona chochote kile akaamua kugeuka ili arudi kwenye floor ya chini ya ghorofa hiyo lakini wakati anageuka tu alikutana na mtu akiwa karibu yake sana, alihitaji kupiga kelele kisu kilizamishwa kwenye shingo yake na kutolewa akasukumiwa chini akibaki anahangaika huku ameiweka mikono yake shingoni kuzuia damu ambayo ilikuwa inatoka kwa wingi sana, hakuchukua muda habari yake ikawa imeishia hapo.

Ukurasa wa thelathini na sita unafika tamati.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA SABA
Tommy aliangalia saa yake alihisi kama anapoteza sana muda, alitembea kwa haraka na kuingia kwenye hiyo floor ya chini kabisa ya eneo hilo ambapo aliona kuna mwanaume mmoja akiwa kwenye gwanda ambalo lilionekana kuwa la jeshi akiwa anamenya chungwa bila wasiwasi. Alikirusha kisu chake kwa nguvu ila ni kama mtu huyo alikuwa amekiona kwani aliinama chini kikaenda kukita kwenye tairi ambayo ilikuwa imesimamishwa ukutani. Aligeuka haraka ili kujua ni mgeni yupi alikuwa ameingia hapo akiwa na kisu chake mkononi lakini muda ulikuwa umemuishia kwani alikuwa amewekewa bastola kichwani kwake huku ikiwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti kiasi kwamba kama angefanya kosa dogo tu basi mtu ambaye alikuwa mbele yake angeondoka na kichwa chake.
“Wamemhifadhi sehemu gani?”
“Wewe ni nani na unamuulizia nani?”
“Jibu nilicho kuuliza”
“Huwezi kutoka ukiwa ha……” hakumalizia sentensi yake risasi iliachiwa na kuzama kwenye goti lake, alitaka kupiga makelele alipigwa na buti la kichwa ambalo lilimfanya ajibamize kwenye kile kisu chake ambacho alikishika mwenyewe kikawa kimemchana vibaya sana usoni.
“Shiiiiiiiiiii, nijibu kwa upole na taratibu, huwa simpendi mtu jeuri ambaye baadae anaanza kutia huruma”
“Ukipandisha ghorofa ya juu kabisa mkono wa kulia kuna mlango una rangi nyeusi humo ndimo ambayo amehifadhiwa”
“Kuna watu wangapi humu ndani”
“Mpaka unafika huko kuna walinzi wanne njiani ila nje ya chumba hicho kuna wanaume watatu ambao ndio wanakilinda hicho chumba. Unaweza ukafika pale usiwaone lakini wanakuwa muda wote wapo jirani na hilo eneo” alijibu huku akiwa anayasikilizia maumivu makali na huenda alihisi kwamba baada ya kuongea angeweza kuachwa hai lakini mwanaume aliizamisha risasi kwenye shingo ya mwanaume huyo akawa amepoteza maisha, mwanaume alikichomoa kisu chake na kutoweka hapo.

Kama alivyokuwa ameelekezwa kwamba njiani angekutana na walinzi hao wanne, alikutana nao na hakutaka kupoteza muda aliwapiga wote risasi za vichwa. Akiwa anakaribia hilo eneo kuna korido ambayo aliona ina kiza kinene sana halafu mita tatu kutoka hapo ndipo kulikuwa na hicho chumba ambacho alikuwa ameambiwa kwamba dada yake alihifadhiwa. Akiwa amejibanza aliangalia kwa umakini sana eneo hilo maana lilikuwa limetulia sana, alikirusha kisu ambacho alikuwa nacho kikawa kinazunguka kwa nguvu sana kuelekea sehemu ile ambayo ilikuwa na kiza, kilisikika kilio kikali sana kwa mtu ambaye bila shaka alipata maumivu makali mno.

Kile kilio ndicho ambacho kiliwatoa wanaume wawili wakiwa wazima lakini huyo mmoja alikuwa amechanwa vibaya mguu wake ambao ulibakia kidogo tu kuweza kukatika huku kisu hicho kikiwa kimenasa hapo mguuni. Mwenzake mmoja alikuwa amemshikilia baada ya kuiwasha taa ya eneo hilo ambalo walikuwa wamejificha huku mwingine akiwa ameishikilia bastola yake mkononi.

“Nina uhakika ninaweza kuiachia risasi hii kwa haraka zaidi yako hivyo usifanye ujinga wowote ule ukahatarisha maisha ya wenzako?” Tommy hakutaka kufanya ujinga wowote ilikuwa ni lazima kwanza ahakikishe kwamba dada yake yupo salama na yupo ndani ya hilo eneo ndipo afanye maamuzi ya kuwaua watu hao. Alikuwa anaongea huku akijitokeza hadharani ambapo alikuwa na bastola mbili kwenye mkono wake moja akiwa amewalenga wote ikiwemo yule ambaye alimshika mwenzake mmoja akiwa na jeraha kubwa mguuni lakini moja alikuwa amemuelekezea mwanaume huyo ambaye ndiye alikuwa naye ameishika bastola mkononi mwake.

Risasi moja iliachiwa na kwenda kutua kwenye kichwa cha yuke ambaye alikuwa amechanwa vibaya na kisu huku bastola nyingine akiwa amemuelekezea mtu wake kama kawaida hivyo yule mwanaume mmoja akawa amebaki bila silaha maana yeye alikuwa amemnyanyua mwenzake hivyo walikuwa wanamtegemea yule mmoja ambaye ndiye alikuwa amenyoosheana na Tommy pia.
“Nitamuua mwenzako pia hivyo achia bastola yako ili tuongee kiume kwa sababu kama ninmgetaka kuwaua ningewapiga risasi muda tu ndiyo maana nimefanikiwa hata kujua kwamba mmejificha hapo.”

Yule mwenzake alimpa ishara ya kutii maagizo maana ni kweli kama angekuwa anahitaji kuwaua basi huenda angesha waua muda mrefu sana. Aliirushia hiyo bastola katikati, Tommy akamtaka hata yule mwingine pia aweze kuitoa yake kiunoni na kuirushia chini, hakuwa na namna naye pia akawa amefanya hivyo. Baada ya kuhakikisha wote wamefanya hivyo naye pia aliirudisha bastola yake kiunoni ambapo wanaume hao waliona hiyo ndiyo nafasi yao kuweza kumalizana naye haraka sana.

Tommy ni kama alikuwa amelitarajia hilo jambo kwani aliwapokea kama walivyokuwa wamekuja kwa kasi, wanaume hao walikuwa na mafunzo ya kutosha hivyo hawakuwa na wasiwasi na uwezo wao kabisa. Walikuwa wanakuja kwa mateke makali mno wote wawili ambayo yaliishia kwenye mikono ya Tommy, mwanaume alikuwa anayapangua mateke hayo huku miguu yake ikiwa inatembea ukutani akafanikiwa kudondokea upande wa pili.

Wanaume wale walisimama na kuangaliana kisha wakawa wanaiangalia ile sehemu ambayo walikuwa wamerushia bastola zao ni kama walikuwa wanapiga mahesabu kamili ya namna ya kuweza kuziwahi. Tommy aliliona hilo hivyo ikawa ni kufanya mtihani wa kuziwahi bastola hizo ambazo zilikuwa katikati yao. Wakati wale wanaume wakiwa wanashuka kuinama kwa sarakasi kuzifikia zile bastola mwanaume mabuti yake mawili yalikuwa yanakuja kwa kasi ya ajabu mno. Mmoja alifanikiwa kugusisha mkono wake kwenye bastola lakini mkono huo haukufanikiwa kuweza kutoka salama kwani buti lilitua kwenye kifundo cha mkono hatimaye ukavunjika vibaya sana.

Lakini yule wa pili yeye alikwepa buti hili na kurukia mbele zaidi kitu ambacho kilimfanya Tommy aziwahi zile bastola, aliziokota na kuzirusha kwa nguvu kuelekea kwao ambazo ziliishia kuwapiga vibaya sana usoni. Yule ambaye alikuwa amevunjwa mkono alindondoka vibaya sana chini ikawa bahati mbaya sana kwake maana mwanaume ambaye alikuwa mbele yake hakuwa na huruma naye kabisa ni baada ya kuzunguka juu hewani kisha akatua na buti lake kwenye shingo ya mwanaume huyo na kuivunja kikatili mno hivyo akawa amebakia mmoja ambaye alipaswa kuyapigania maisha yake kwa mwanadamu ambaye hakujua ametokea wapi zaidi ya kuwaua kikatili sana.

Aliiangalia bastola yake ilikuwa imedondokea mbali sana hivyo hata angesema kwamba anataka kuikota kwa wakati huo angechelewa ikawa inambidi apambane kwanza kwa mkono ili kutetea maisha yake. Alikuja kwa pupa akihisi huenda itamsaidia Tommy, alimtisha mtu huyo akapoteza mwelekeo na kumfanya asite kurusha ngumi zake lakini hilo ndilo kosa ambalo lilimponza kwani Tommy alitua na buti lake kwenye paja ambalo bila shaka liliteguka vibaya sana, mwanaume huyo akiwa amekosa balansi ya kusimama alipokea ngumi tano za mbavu ambazo zilivunja mbavu zake na kumfanya atoe sauti ya miguno huku akiwa anahema kwa nguvu sana.

Hakua na la kufanya zaidi ya kuanza kutambaa kuelekea ilipokuwepo ile bastola yake na wakati huo mwanaume alikuwa anasogea taratibu kilipokuwa kisu chake, alikiokota na kumsogelea mwanaume yule ambaye alibakisha sentimita chache sana kuweza kuipata bastola. Alichanwa kwenye kiganja ambacho kilionekana kuwa na haraka sana ya kuiwahi bastola hiyo akaishia kupiga makelele kwa uchungu mkubwa mno.

“Dada yangu emehifadhiwa wapi?” kamanda hakuweza kujibu bali alikuwa anaendelea kugugumia kwa maumivu ambayo alikuwa anayapitia hali ambayo ilipelekea yeye kuweza kuzamishiwa kisu kingine kifuani kwake kisha kikachomolewa kwa nguvu sana.
“Huwa napenda kuuliza mara moja tu kwenye maisha yangu, watu ambao naruhusiwa kuwauliza mara nyingi ni wazazi wangu. Utanijibu au bado uko busy sana?” swali ambalo jibu lake lilikuwa ni rahisi sana.
“Yupo mle ndani”
“Na kichwa cha mdogo wangu?”
“Nacho kimehifadhiwa mle ndani kwenye jokofu dogo” mwanaume alichoka aisee kwani alikuwa anaogopa sana kukiona kichwa cha mdogo wake.
“Luck unamjua?”
“Aliyekuwa mlinzi wa baba yako”
“Ndiyo”
“Yuko wapi?”
“Tabata”
“Nyumba gani” mwanaume huyo hakuwa na namna zaidi ya kutaja kila kitu ambacho alikuwa anaulizwa hapo kwani ndiyo ilikuwa njie pakee ya yeye kuweza kubaki hai lakini hakuwa anajua kile ambacho kilikuwa kinakuja kwa upande wake kwani baada ya kutamka tu jambo hilo kisu kilizama vibaya sana kwenye hiyo shingo.
Akiwa anataka kuondoka hapo simu ya mwanaume huyo ambaye alikuwa amemuua ilianza kuita kwa fujo sana kutoka kwenye mfuko wake. Aliitoa simu hiyo ambayo ilitoka kwa mtu aliyeseviwa bosi, aliipokea na kuiweka kwenye sikio lake.
“Kuna mtu anakuja kuvamia hapo ondokeni sasa hivi mimi nipo njiani nakuja na walinzi wengine”
“Too late”
“Whaaaa? Nani wewe?”
“Nakupa masaa ishirini na manne, kama utafanikiwa kubakia hai ndani ya hayo masaa basi mimi sitakuja kukutafuta tena kwenye maisha yangu nitakuacha uishi kwa namna unayoona inakufaa wewe na nitayaacha maisha yako” alijibu kisha akaivunja simu hiyo huku akimuacha mtu huyo wa upande wa pili akiendelea kupiga kelele.
“Hello, hello nani wewe, mpuuzi mkubwa sana nitakufanyia kitu kibaya sana” kelele zake hazikusaidia kitu chochote kile kwani ni kama alikuwa amechelewa, ilikuwa ni lazima aweze kujuta sana.

Tommy baada ya kumalizana na mwanaume huyo alipiga buti kali sana kwenye mlango huo ambao ulikuwa mbele yake ambao ulifunguka kwa lazima. Baada ya kuingia ndani mazingira yalikuwa masafi sana lakini mtu ambaye alikuwa akiishi ndani alikuwa amepoteza kabisa matumaini ya maisha.

Hakuamini alichokuwa anakiona. Mbele ya kitanda ambacho kilikuwa ndani ya chumba hicho alikuwa amelala dada yake kipenzi, mwanamke ambaye alimuachia ziwa wakati anazaliwa. Hakuwa kwenye hali ya kujitambua huku akiwa ndani ya bikini tu pekee, mwanaume alitafuta shuka moja na kumfunika mwanamke huyo ambaye alikuwa amepoteza fahamu bila shaka. Aliipiga risasi pingu ambayo alikuwa amefungwa nayo kisha akamkagua kuanzia mapigo ya moyo na puani na baada ya kuona kila kitu ipo sawa alianza kuangaza angaza humo ndani.

Juu ya kabati moja kubwa aliona kuna kijokofu kimoja kidogo ambacho alikuwa anaogopa sana kukikagua, alijikaza na kukishusha, baada ya kukifungua alikifunga kwa kasi sana kwani hakuwa tayari kabisa kuweza kushuhudia kile ambacho kilikuwa ndani humo. Kilikuwa ni kichwa tu pekee ndiyo maana hakuhitaji hata kuendelea kukiangalia, alibeba kila kitu mpaka kwenye gari yake ambapo alitoweka kwa kasi sana kuweza kuwahi eneo ambalo alikuwa analijua yeye mwenyewe.

Ukurasa wa thelathini na saba sina la kuongezea.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom