Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA MOJA
Aliinyanyua simu yake ya mkononi na kuipiga mahali. Simu hiyo ilienda moja kwa moja mpaka kwa kijana wake wa kazi ambaye alikuwa akijulikana kama Pablo Mkinga, simu hiyo ilikuwa imemkutia juu ya kiuno cha Sasha ambaye kwa mara ya kwanza alijulikana kama Noelia. Mwanaume huyo aliipokea na kuiweka sikioni kwake.
“Unajua kinacho endelea?”
“Hapana bosi”
“Kwahiyo haujui kama mwanangu amekufa sio?”
“Bosi unamaanisha nini kusema kwamba mwanao amekufa?”
“Hivi wewe mpuuzi mimi nakulipa shingapi mpaka unakuwa haujui hata kinacho endelea? Kulikuwa na sababu zipi za mimi kukutoa gerezani wewe kama sio kukuacha kule kule uendelee kutumikia adhabu yako?”

“Mheshimiwa mimi tangu siku ile nipo naifanya kazi, nilikutana na binti akawa amenipa taarifa zote kuhusu kila ambacho kilitokea hivyo nikawa nimeanza kufanya msako mtaani ambapo nilifanikiwa kuwaua vijana kumi ambao niliona moja kwa moja wanahusiana na hilo tukio ambalo lilikuwa limetokea na kwa wakati huu nipo kumtafauta mhusika mwenyewe wa jambo hili moja kwa moja. Hivyo nina siku kadhaa tu za kuweza kumpata mhusika wa tukio hili na baada ya hapo nitamleta mkononi mwako kisha wewe ujue nini unakifanya kwake. Na pole sana kwa huo msiba mzito bosi” mwanaume huyo aliongea kwa msisitizo kiasi kwamba ungehisi alikuwa anamaanisha sana kile ambacho alikuwa anakiongea lakini kiuhalisia hakuwa akimaanisha hicho kitu kwani wakati huo alikuwa juu ya kiuno cha mwanamke.

“Ni vyema hilo jambo ulitekeleze kwa huo muda kama ulivyosema kwa sababu vinginevyo nitakuua kwa mkono wangu mwenyewe” alitamka mzee huyo na kuikata simu yake ili aendeelee kuugulia maumivu yake mwenyewe ndani kwa ndani. Lakini ilikuwa ni tofauti kwa Pablo kwani wakati huo walionekana kuanza kupongezana na Sasha baada ya kusikia taarifa hiyo kwani ingewafanya wabaki wakiyafurahia mapenzi yao kwa amani bila kuingiliwa na R ambaye alikuwa kama anammiliki Malaya huyo.


Tommy alishtuka kutoka kwenye usingizi ambao ni wazi ulikuwa wa kifo, alikuwa kitandani amelala. Mazingira ya hicho chumba yalikuwa tofauti sana na ambayo huenda yeye alikuwa ameyazoea kulala siku nyingi za maisha yake hususani pale anapokuwa ndani ya ardhi ya nchi ya Tanzania. Alitaka kuinuka kwa nguvu lakini alihisi kama kifua chake hakipo sawa sana hivyo akajilaza tena ili kuweza kurudisha kumbukumbu zake juu ya jambo ambalo lilikuwa limemtokea mpaka akaishia kuwa kwenye hali kama hiyo ambayo alikuwepo kwa wakati huo.

Ndipo matukio ya mambo ambayo yalitokea yalianza kupita kwenye kichwa chake ambapo alifanikiwa kuweza kukumbuka kila ambacho kilikuwa kimetokea kwa usahihi sana. Alisikitika sana baada ya kila kitu kuweza kurudi vyema kwenye kichwa chake.
“Nimefanya uzembe ambao ungenifanya nife kijinga sana kwa mara ya kwanza kabisa kwenye maisha yangu” aliongea akiwa ananyanyuka na kujikuta akiwa na suruali tu pekee kwenye mwili wake. Alisogea mbele kidogo sehemu ambayo ilikuwa na kioo ili aweze kujitazama vyema, ndipo alipoona alama kifuani kwake ya kushonwa, aliinama na kujiangalia tena eneo hilo na kujionea huruma.

“Yule mjinga kama angekuwa makini angenipiga kwenye moyo na habari yangu ingeishia pale pale. Hata hivi niko wapi hapa na nani huyu ambaye ameonekana kuyasaidia maisha yangu?” alijiuliza mwenyewe maswali ambayo hakuwa na uwezo hata wa kuyajibu. Akiwa kwenye hiyo tafakuri alihisi kama mlango wa ndani ya chumba hicho ulikuwa unafunguliwa na hapo ndipo alipo pigwa na mshangao ambao hakutaka kuuamini kama ni kweli.

Aliingia mwanamke ambaye kwenye mwili wake alikuwa na nguo nyepesi sana kiasi kwamba kila kitu kilikuwa kinaonekana ndani yake. Alikuwa ni Harper Campbell, mwanaume alimwangalia sana mwanamke huyo.
“Imekuwaje nimefika hapa?”
“Hiyo ndiyo salamu T1?”
“Sipo hapa kwa ajili ya kusaliminana na wewe, nimekuuliza imekuwaje nimefika hapa?”
“Najua mpaka sasa bado unanichukia sana na huenda jambo hili litaishi kwenye maisha yako kwa muda mrefu sana ila angalau kuna muda ungekuwa unaruhusu hata najielezea basi” mwanamke huyo aliongea kinyonge sana huku akiwa anaifungua dawa ambayo bila shaka alikuwa amemletea mgonjwa huyo ambaye hakuwa na namna zaidi ya kuipokea na kuinywa na maji.
“Nakusikiliza”
“Ni kama bahati nimewahi eneo la tukio kwani kama ningechelewa kidogo tu yule jamaa alikuwa anakuua”
“Wewe ulijuaje kama mimi nipo pale?”
“T1 kumbuka mimi nakupenda na siku ambayo tuliingia kwenye ugomvi mkubwa nilisema nitajitahidi kukulinda kwa namna yoyote ile ambayo mimi ningeiweza na ndiyo kama hivi ninavyo fanya kwa sasa”
“Hilo siyo jibu la nilichokuuliza H2, acha kuzunguka nenda kwenye hoja ya msingi”
“Siku ile ulivyokuja hapa nilijua kabisa umeondoka kwa hasira na ungeenda kufanya mambo ya hovyo huko ambayo yangekuja kukuletea athari sana kwa hapo baadae hivyo kwenye simu yako hapo kwa pembeni kuna kisticker kidogo sana nilikibandika na nilijua kwa haraka zako usingeweza kukishtukia. Hicho ni kifaa cha mawasiliano ambacho kingekuwa kinanisaidia kujua wewe uko wapi kwa muda wote ule kikubwa tu kama usinge kitoa.

“Siku zingine huwa nahitaji kukufuatilia lakini huwa naachana kabisa na hayo mawazo ila kwa leo kila nilipotaka kupotezea nafsi yangu ilikuwa inauma sana hivyo nikawa sina namna zaidi ya kufanya hivyo na hapo ndipo nikaamua kuangalia kilipo kifaa hicho, nimeshtuka baada ya kuona unaelekea Kigamboni nikajua kabisa huko hakuna usalama hivyo na mimi nikaamua kukufuatilia mpaka nilipokukuta kwenye hiyo hali, nikaamua kufanya hivyo na kuondoka na wewe maana muda mchache tu polisi wangefika pale”

“Asante sana kwa kuyaokoa maisha yangu”
“Ni jukumu langu kufanya hivyo”
“Jukumu lako kivipi?”
“Kwa sababu yale hayakuwa maigizo T1, licha ya mimi kuifanya kazi yangu ambayo sikuwa na namna kwa sababu ya taifa langu lakini mimi nilikupenda kweli na mpaka kesho sijawahi kuwaza kuja kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako na ndiyo sababu wewe ndiye ulikuwa wa kwanza kuitoa bikra yangu licha ya watu wengi ambao nimewahi kuwatega kwa kutumia uzuri wangu ila hakuna ambaye alifanikiwa kunivua chupi yangu zaidi yako” mwanmke huyo alikuwa anaongea huku akiwa anamsogelea mwanaume huyo ambapo hatua zao zilikuwa zinazidi kupungua na hatimaye vinywa vyao vikawa vinafanya mawasiliano kwa vitendo na sio maneno tena wakajikuta wanaingia kwenye sayari nyingine kabisa ambayo ingezifanya nafsi zao zikiri wazi kwamba wao bado walikuwa wanahitajiana sana. Kazi zao hazikutakiwa kabisa kuwa sehemu ya kuweza kuwagombanisha watu hao wawili na wakati mgumu kama huo walipaswa kuwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Walipiga show moja nzito sana kwa muda wa saa moja ndipo walipokuja kuachiana wote wakiwa hoi sana. Lakini wakati Tommy akiwa anafanya mapenzi na mwanamke huyo aligundua kwamba alikuwa na jeraha la risasi kwenye huo mwili wake jambo ambalo mwanaume huyo lilionekana kushangaza kidogo kwamba ni kivipi mwanamke huyo alilipata jeraha hilo?
“Imekuwaje tena?”
“Mimi nilifanikiwa kukutana na yule gaidi”
“Unamaanisha ulimteka?”
“Hapana, alitoweka na mtu wake kwani mimi ndiye ningekufa siku ile, siyo mtu wa kawaida kama ambavyo nilikuwa namfikiria?”
“Ilikuwaje wewe ukampata kirahisi namna ile?”
“Nilikuwa namfuatilia kwa ukaribu sana na ni mapema sana nilikuwa nimejua kwamba alikuwa ameenda pale kama mwanamke hivyo hata kama kuna mtu angefika pale ambapo walikuwa wanafanyia mkutano basi moja kwa moja angejua kwamba mheshimiwa alikuwa na mchepuko na sio mfanya biashara mwenzake ambaye ni gaidi”
“Hili ni jambo la hatari sana ambalo linakupasa wewe kuwa makini sana”
“Hilo nalitambua usijali nipo makini sana”
“Baba yangu pale hospitali umemhamisha kama nilivyo kwambia?”
“Ndiyo mzee yupo salama”
“Asante sana kwa hilo. Najua kwa wakati huu wamesha anza kuhisi kwamba mauaji haya yote ni mimi ambaye nahusika hivyo wanaweza wakataka kuitumia familia yangu kwa ajili ya kuweza kunidhoofisha na kama wakitaka kuitumia hiyo njia basi watakuwa wamefeli sana maana familia yangu kwa sasa inaishi mafichoni mpaka pale ambapo nitakuwa naimaliza kazi hii” mwanaume aliongea akiwa anaamka na kuanza kuvaa nguo maana mechi ambayo ilipigwa hapo ilikuwa ni ya kibabe sana.

“Leo ndiyo kwa mara ya kwanza nimeona ukiwa kwenye hali mbaya kama ile kwene maisha yangu, kiukweli nimeogopa sana T1” aliongea Harper akiwa anamkumbatia mwanaume huyo kwa nyuma.
“Unajua mwisho wa siku hata mimi ni binadamu wa kawaida tu kama walivyo wengine na kuna siku na mimi pia nitakufa kama wengine hivyo hautakiwi kushtuka kwa kunikuta kwenye hali kama ile japo huenda ni mara chache sana inatokea ila ukweli unabaki pale pale kwamba hata mimi ni mwanadamu mwenye nyama, damu na mifupa na nina moyo unaokufa kama wengine”
“Hivi kuna mtu alishawahi kusimama na wewe kwenye mapigano na akakupiga mpaka ukapoteza fahamu kama ilivyokutokea leo?”

“Ndiyo, ndiyo imewahi kunitokea. Unajua ngumi ni kama sanaa na kuna watu ni wasanii, hii dunia ukiizungukia maeneo mengi ndipo utajua kwamba kuna vitu vingi hauvijui kuhusu maisha yako mwenyewe. Wakati tukiwa Tirana Albania baada ya kutoka China, sikuwahi kabisa kuamini kwamba kuna mtu alikuwa anaweza kusimama na mimi kwenye ngumi wakati ule hapa duniani ila niligundua kwamba sikuwa sahihi kwenye mawazo yangu baada ya kukutana na bwana mdogo mmoja ambaye nilimuacha kama miaka miwili hivi”

“Yule bwand mdogo alinipa elimu kubwa sana kwani alinipiga na kunifanya nizimie kwa siku mbili. Nilipokuja kuzinduka aliniambia kwamba mimi ni fundi sana kwenye ngumi lakini kitu pekee ambacho nimekikosa ni ule ubora wa mud mrefu. Alinihakikishia kwamba kama mimi ningefundihswa nikiwa bado mdogo basi huenda nisingekuwa mwanadamu wa kawaida huenda ningekuwa kiumbe kibaya sana, yeye alisema kwamba ngumi amefundishwa tangu anaanza kusimama akiwa bado mdogo hivyo alikuwa na aina zaidi ya kumi za mapigano ya hatari kwenye mwili wake na baada ya pale nilimuoamba anifundishe ambapo tulitumia mwezi mmoja ulio niivisha sana”

Ukurasa wa 51 naweka nukta hapa.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA MBILI
“Kitu cha ajabu ambacho kilinishangaza baada ya huo mwezi kuisha alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha sana huku akiniachia barua na kudai kwamba yeye alitumwa na Mungu kusaidia watu hivyo anaizungukia dunia ili sehemu ambapo unahitajika msaada wake kutuliza amani basi anaifanya hiyo kazi na mpaka leo sijawahi kupata taarifa zake wala kusikia kwamba anapatikana popote pale maana ni mwanadamu ambaye hata picha yake huwezi kuipata mahali popote pale duniani. Hivyo naweza kukwambia kwamba watu ambao wanaweza kunipiga mimi vizuri wapo japo ni wachache na kuwapata watu hao huwezi kuwapata ukiwa umekaa ndani kwako, ni mpaka uweze kuizungukia dunia hii” mwanaume alimpa shule mwanamke huyo ili kubadili mawazo yake kuamini kwamba Tommy asingeweza kupigika kitu ambacho yeye mwenyewe alikikataa kwani alikuwa anaamini kwamba siku zote huwa yupo ambaye ni zaidi yako kwa namna yoyote ile hata uwe na uwezo vipi.

Tommy baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa alihitaji kuondoka hilo eneo hivyo wakati anamaliza kutoa maelezo yake alikuwa yupo mlangoni tayari ndani ya chumba hicho cha kifahari sana.
“Kuna ile siku nilikwambia kuna mambo mazito sana ya kumhusu raisi wako na kisasi kizito ambacho yupo nacho dhidi ya nchi yake, je upo tayari kukisikia?” kitu ambacho Harper alikiongea kilimfanya Tommy atulie kwanza maana lilionekana kuwa ni jambo kubwa isivyo kawaida na alitamani sana kuweza kulijua. Alirudi na kukaa kitandani akiwa yupo tayari kumsikiliza mwanamke huyo ampe kinaga ubaga juu ya nani ambaye alimvesha paka kengele.

“Miaka ya zamani sana huko wilayani Makete ndani ya mkoa wa Njombe ndiko ambako alizaliwa mwanaume mmoja ambaye alitabiriwa kuja kuwa moja kati ya watu wakubwa sana kuwahi kutokea ndani ya taifa hili. Alizaliwa mtoto wa kiume ambaye nyota yake ilionekana tangu mapema sana baada ya kuzaliwa kwake”

“Ilikuwa ni kama neema kubwa sana kutokea kwake kwani alionekana kuwa mtoto mwenye uwezo mkubwa sana tangu alipo anza kugusa vitu mbali mbali akiwa bado mtoto mdogo sana. Siku alipo anza kuongea ndipo uwezo wake ambao ulikuwa ndani yake ulipo anza kuonekana hadharani na kujidhihirisha waziwazi bila kificho tena. Mtoto huyo alionekana kuwa na haiba ya uongozi hivyo ukafanyika mpango wa kumpeleka shule akiwa bado mdogo sana na huko shule alianza kuonyesha uwezo wa uongozi akiwa bado kijana mdogo tu”

“Kuna aina mbili za viongozi duniani. Kuna wale viongozi wa kuzaliwa lakini kuna wale viongozi ambao wanapatikana kwa njia ya kutengenezwa, itifaki za uongozi zinasema kwamba kiongozi bora ni yule ambaye anazaliwa japo kulingana na mabadiliko ya ulimwengu na namna teknolojia inavyo sogea pia unaweza ukabahatika kupata kiongozi bora ambaye anakuwa ametengenezwa japo hawa ni wachache sana na wengi ambao wanatokea siku hizi ndio ambao wanakuwa mafisadi wa kutupwa na kuwaweka watu wenye uwezo mdogo kwenye madaraka”

“Kijana huyo wa kiume alikuwa anaweza kuwaongoza wenzake kwa ustadi mkubwa sana na kuweza kutengeneza hoja fikirishi ambazo zilifanya hadi watu wazima wawe na udadisi kuhusu mtoto huyo na uwezo wake wa akili ambao alikuwa nao kwenye ubongo wake. Sifa zake zilianza kusambaa kila sehemu kuhusu uwezo wa mtoto huyo hivyo akiwa kijana mdogo tu akawa anawaongoza wenzake kwenye shughuli mbali mbali za shule lakini pia hata namna ya kuweza kufaulu aliwasaidia watoto wengi sana”

“Hicho kitu kilifanya aanze kupendwa sana mtaani na kila sehemu huku watu wengi wakimtabiria kwamba huyo alikuwa anaonekana kabisa kuja kuwa kiongozi mkubwa sana hapo baadae ambaye huenda alistahili kuingia hata Ikulu kwa mawazo mapana ambayo alikuwa nayo. Kijana huyo aliendelea na masomo yake mpaka alipohitimu na kufaulu kwa alama za juu sana kitu ambacho kilisababisha yeye kupelekwa kwenye shule za vipaji kwa ajili ya kuendelezwa. Nako huko alifanya hivyo hivyo kama huko mwanzo na kumfanya kuzidi kujulikana kwenye kila ardhi ambayo alikuwa anaikanyaga”

“Mpaka anafika chuo hakuna sehemu ambayo hakuacha alama kubwa hivyo baada tu ya kuhitimu elimu hiyo ya juu moja kwa moja aliteuliwa na kupewa kazi serikalini ambapo aliifanya kwa weledi mkubwa sana na kadri muda ulivyozidi kwenda alizidi kujulikana kila sehemu mpaka pale alipo amua kurudi nyumbani kwao na kuweza kugombea ubunge ambao alipita bila kipingamizi kwa kura zote na hakuna mtu hata mmoja ambaye alithubutu kumpigia kura mpinzani wake zaidi ya familia tu ya mpinzani wake huyo. Kwa mara ya kwanza kabisa alifanikiwa kuingia bungeni kwa ajili ya kuwapigania wananchi wake”

“Moja kati ya sifa yake kubwa ambayo illifanya apendwe sana ulikuwa ni uwazi na ukweli. Alikuwa mtu ambaye aliwasisitiza sana wananchi wake kwamba maendeleo hayawezi kuletwa kwa muda mfupi hivyo walitakiwa kushikamana pamoja ili kuweza kuibadilisha sehemu hiyo ya kwao na kuwasaidia wenye uhitaji. Alifanikiwa kuwasaidia vijana wengi sana kuweza kujiajiri na kujiendeleza kimasomo kutoka huko kwao mpaka baadhi ya watu wakawa wanatamani kwamba mtu huyo angezaliwa kwenye majimbo yao”

“Ujengaji wake wa hoja na upana wa mawazo yake makubwa ambayo yalikuwa yanaonyesha mwelekeo bora wa hapo mbeleni ulifanya ale kitengo na kuwa naibu waziri wa ujenzi, huko hakukaa sana hatimaye akawa waziri wa mali asili na utalii lakini mwisho wa siku waliamua kumpeleka wizara ya mambo ya ndani baada ya kuona sehemu hiyo imepwaya sana. Baadae mwanaume huyo alikaa kwenye wizara ya mambo ya nje na alipo hakikisha kwamba hata huko amepaweka sawa, raisi wa wakati ule aliamua kumhamisha na kumteua kuwa kama waziri wa ulinzi”

“Na huko ndiko aliko anzia harakati zake za kutaka kuingia Ikulu kama ilivyokuwa ndoto yake na kwa watu wote ambao walikuwa wanamfahamu kwani waliona kwamba alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa sana hivyo hilo kwake lisingekuwa tatizo kabisa kufanya kitu hicho. Kwenye hizo harakati akawa amepokelewa kwa ukubwa sana na kila mtu akawa ameonyesha shauku yake kuweza kumpatia nafasi hiyo kwani waliamini kupitia yeye basi nchi ingeweza kupata mabadiliko makubwa sana ambayo yangewafikisha kwenye nchi ya ahadi”

“Huyo ndiye Boniphace Walawala ambaye kwa sasa ndiye raisi ambaye yupo madarakani kama wewe na watanzania wote mnavyojua japo kuna siri kubwa sana ambayo ilijificha nyuma ya jambo hili na wengi kama sio watanzania wote hawaijui kabisa ila kwa leo wewe utaifahamu kuhusu uhalisia wa mtu huyu” Harper alikuwa ndani ya chumba hicho ambacho walikuwa na Tommy akiwa ameamua kumpasulia ukweli juu ya uhalisia wa maisha ya raisi wa nchi yake ambaye yeye alihisi kwamba anamjua ila mwanamke huyo alimwambia kwamba alitakiwa kutulia ili ampe sababu kwamba ni kwanini alimwambia kwamba raisi huyo ana kisasi.


“Wakati mambo yote hayo yanatokea, miaka ya baadae kidogo mwanaume huyo akiwa anaendelea kuwa na ushawishi na kula vitengo tofauti tofauti serikalini. Kuna vijana wadogo sana ambao walikuwa wamefuzu kwenye mafunzo ya jeshi hivyo kwa wakati huo walikuwa wapo kwenye majaribio ya mwisho ambayo yangewafanya kuchaguliwa kwenda kupata mafunzo ya kikomando. Wanaume hao ambao walikuwa wanayachukua mafunzo hayo walikuwa jumla ishirini lakini walikuwa wamejigawa kwenye vikundi vikundi kulingana na jinsi walivyokuwa wakijuana na kufanya kazi kwa pamoja.

Kwenye moja kati ya kundi la vijana hao walikuwa wamejigawa saba ambao walijuana huko huko jeshini na kutengeneza umoja wao ambao waliuita the SEVEN ikiwa ni idadi yao. Vijana hao walikuwa na bidi kubwa sana huko kwenye mafunzo yao wakiwa na imani kwamba siku moja wangeweza kufaulu wote kwa pamoja na kuanza kulitumikia taifa kwa moyo mkunjufu kwa pamoja. Kwa bahati mbaya sana wakiwa wanapata mafunzo hayo mmoja kati yao alikufa mazoezini baada ya kudondoka umbali mrefu sana na kufikia shingo chini”

“Kufa kwake kulileta majonzi kwenye umoja huo lakini haikuwa sababu ya umoja huo kufa bali ulizidi kuwa imara kila siku iliyokuwa inakuja mbele yao. Waliamua kubadilisha jina na kuamua kujiita SIX POINT ZERO SOLDIERS (6.0). Hiyo namba sita pointi sifuri ndio ulikuwa utambulisho wao huku kwenye namba hizo wakikoleza rangi nyeusi na nyekundu. Rangi nyeusi ilikuwa ni kwa ajili ya watu wasio julikana ambao mambo yao wangeyafanyia gizani lakini hiyo rangi nyekundu ilikuwa ni kwa ajili ya heshima ya damu ya mwenzao ambayo ilikuwa imemwagika”

“Baada ya kumaliza mafunzo yao serikali ilikubali kuwapa kibali cha kufanya kazi pamoja wote sita hivyo ikawa ni timu moja kama ombi lao lilivyokuwa. Wanadaiwa kwamba walikuwa ni watu ambao walikuwa wakipendana sana na kulindana kwa kila hali yaani kama ungegombana na mmoja basi ulikuwa umegombana na wote na wangekushughulikia kwa pamoja hivyo likawa ni moja ya makundi yaliyo ogopeka sana kulingana na kazi ngumu ambazo walipewa na wakafanikiwa kuzifanya kwa ufanisi mkubwa mno kiasi kwamba likawa ndilo kundi ambalo serikali ilianza kulitegemea kwa siri kwa wakati ule”

Wakati huo lilitokea jambo moja la ajabu sana huko ndani ya nchi ya Kongo ambalo lilikuwa linaihusu nchi ya Tanzania moja kwa moja. Machafuko ya huko yalisababisha raia hamsini ambao walikuwa na asili ya kitanzania kutekwa na magaidi ambao walikuwa wafanya mauaji kikatili sana huko na taarifa hizo Tanzania walipenyezewa na jasusi mmoja ambaye walikuwa wamefanikiwa kumuingiza huko kwenye hayo makundi ya magaidi na baada ya kufanikiwa kupenyeza taarifa hizo anadaiwa kwamba aliuawa.

Taarifa hiyo ilikuwa mbaya sana lakini kama taifa ilikuwa ni lazima kufanya jambo ili kuwaokoa raia wake hivyo wakawa wametuma wanajeshi kwenda kuifanya kazi ya kuwakomboa hao raia. Wanajeshi waliotumwa walikuwa ishirini lakini kwa bahati mbaya sana baada ya kwenda huko wanajeshi kumi na watano waliuawa hapo hapo kwenye shambulizi na wanajeshi watano wakawa wamekamatwa. Baada ya magaidi hao kugundua kwamba wanajeshi hao walikuwa watanzania walitishia kuingia kwenye vita na Tanzania au vinginevyo Tanzania ilipaswa kuwapelekea shehena kubwa ya madini ili mateka wote waachiwe lakini pia waweze kumalizana nao kwa amani.

Hiyo kazi ilitua kwenye mikono ya Boniphace Walawala ambaye kwa wakati huo ndiye alikuwa waziri wa ulinzi wa nchi ta Tanzania. Mwanaume huyo alikutana na mkuu wa majeshi na kumpa taarifa kwamba inatakiwa awatumie watu hao kwa sababu kutuma wanajeshi wa kawaida ilikuwa ni kesi nyingine ambayo ingepelekea kazi kuharibika ndipo ikaamuliwa kwamba hao 6.0 ndio waende huko. Waliamua kujiita 6.0 kwa sababu mmoja wao alikuwa amekufa hivyo hiyo sifuri waliamini kwamba iliwahi kuwa namba yenye thamani ila kwa wakati huo ilikuwa mbele ya pointi hivyo haikuwa na thamani ila ilikuwa na maana kubwa sana kwao.

Wnaume hao hawakuwa na shida kwa sababu walichokuwa wanakisubiri ilikuwa ni amri tu pekee ya kwenda huko. Baada ya kwenda huko Congo wanaume hao waliifanya kazi yao kwa weledi mkubwa na kuakikisha wanawapata watu ambao walikuwa wamewafuata huko ambapo walitumia masaa nane tu pekee kuweza kuimaliza kazi hiyo ambayo iliwapeleka huko.

Ukurasa wa 52 unafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mzee nimeipiga mwanzo mwisho aisee huyu Tommy na Rais walawala af na harakat za Mafupa na Mpango makakati wa Oscar na vp Kirusi???? Daaah hongera Kaka nasubiri Mzigoo
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA TATU
Jambo la kwanza la kushangaza ambalo walikutana nalo huko kwanza ni mzigo ambao walitakiwa kurudi nao kwa sababu wao hawakuwa wakikaguliwa lakini mzigo huo hawakuruhusiwa kabisa kuukagua ila kwa bahati mbaya sana mmoja wao aliufungua na kugundua kwamba yalikuwa mabox ya dhahabu, walishangaa sana lakini wakati huo huo ambao walikuwa pembezoni mwa ziwa Tanganyika kusubiria usafiri wa majini ambao ulikuwa unawafuata hapo walibaki wanajiuliza maswali ambayo hata hawakuelewa yalikuwa yanahusu nini.

Wakiwa wanaendelea kujiuliza hayo maswali watu ambao walikuwa wameenda kuwachukua walifika lile eneo na kuanza kuwamiminia risasi nyingi sana ambazo ziliwatoboa vibaya sana kisha watu hao ambao walikuwa kwenye hiyo eneo wakatoweka kwa kasi sana na kupotea na hiyo dhahabu ambayo walikuwa nayo wanaume hao.

Miili yao ilibakia pembezoni mwa hayo maji mpaka pale ambapo binti wa tajiri mmoja alipokuwa anapita kando kando ya ziwa hilo akiwa anafanya utalii na wafanyakazi wake alipokuja kukuta kuna mtu anaelea kwenye maji akiwa kama amekufa. Aliamuru walinzi wake waweze kumtoa mwanaume huyo na baada ya kumkagua waligundua kwamba hakuwa amekufa, bado alikuwa mzima.

Mwanamke huyo aliondoka naye na kwenda kumsaidia ambapo ilichukua miaka miwili mwanaume huyo kuweza kuamka alipokuwa amelala na kuweza kuyafumbua macho yake kwa mara nyingine tena. Alikumbuka vyema kuhusu tukio ambalo lilikuwa limetokea, aliishia kulia sana kwa sababu aliwapoteza watu ambao kwake walikuwa zaidi ya familia na ni yeye pekee ambaye alifanikiwa kuishi tena baada ya lile sakata ambalo liliweza kutokea.

Kilicho muuma ni baada ya kugundua kwamba wale viongozi ambao walikuwa wamewatuma kwenye ile kazi walikuwa na mipango yao kwani ni kama walikuwa wamewatuma wanaume wale wakafanikishe zoezi lile la kuweza kuziiba dhahabu kwani kama lengo lilikuwa ni kuwasaidia wale mateka na wanajeshi basi wangefika salama nyumbani lakini magazeti ambayo aliyakuta ya wakati huo yalikuwa yameandika habari mbaya sana kwamba mateka wote ambao waliokolewa na makomando wa Tanzania walitunguliwa wakiwa kwenye ndege kuweza kurudishwa nyumbani huku makomando hao wakituhumiwa kufanya tukio hilo kwa sababu ya tamaa ya mali na kwamba kuna kiasi cha dhahabu ambacho walipotea nacho na walitakiwa kutafutwa kwa nguvu yoyote ile na kwa mtu ambaye angefanikisha kupatikana kwao basi angelipwa pesa nyingi sana.

Mwanaume huyo alisikitika sana kwa mambo ambayo alikuwa anayaona, yaani nchi ambayo yeye alikuwa amejitolea kwa maisha yake yote kwa wakati huo ilikuwa imewapa kesi nzito sana namna hiyo ambayo hawakuhusika hata kidogo zaidi ya kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kuwalinda wananchi wao ila siasa iliamua kuwalipa kwa namna hiyo.

Mwanaume huyo alijaribu kufuatilia habari zingine na kugundua kwamba kwa wakati huo Boniphace Walawala ambaye ndiye alikuwa amewatuma kufanya kazi hiyo alikuwa amechukua fomu ya kuweza kugombea nafasi ya uraisi ndani ya taifa la Tanzania. Mwanaume alijikuta anatukana kwa sauti kali sana yenye hasira na maumivu ndani yake kwa sababu mwanaume huyo ndiye ambaye alikuwa amesababisha yote hayo ambayo yalikuwa yakiendelea.

Mwanamke ambaye alikuwa amemsaidia mwanaume huyo alikuwa ni mzungu ambaye alikuwa ameenda Congo kwa ajili ya utalii na ndege yake binafsi ambayo ilikuwa moja kati sehemu za utajiri mkubwa sana ambao alikuwa nao baba yake. Kwa wakati huo alikuwa amesafiri na mwanume huyo mpaka Ugiriki na ndiko aliko itumia miaka hiyo miwili yote akiwa anaipambania afya yake kitandani.

Mwanamke huyo alijaribu sana kumhoji mwanaume huyo ili kuweza kujua kwamba yeye alikuwa ni nani hasa kwenye maisha yake kwani alimkuta akiwa ziwani amepigwa risasi huku mwilini akiwa uchi kabisa. Mwanamke huyo alishindwa kumtambua mwanaume huyo kwa sababu hata taarifa ya makomando ambayo iliongelewa huko Congo haikuhusisha kabisa picha zao ndiyo maana alishindwa kabisa kumjua na kingine isingekuwa rahisi kuamini kwamba watu hao walipigwa risasi kwa sababu kwa taarifa ya serikali ambayo ilitoka ni kwamba wao walipotea na madini wakiwa wazima kwa maana hiyo kwa lugha rahisi mwanamke huyo asingeweza kumhisi kwa lolote mwanaume huyo ambaye alikuwa mbele yake kwa wakati huo.

Licha ya kuweza kushawishiwa sana ili aweze kulielezea jambo hilo mwanaume huyo alisema kwamba hakuwa akikumbuka jambo lolote lile kwenye maisha yake zaidi ya muda huo tu ambao alikuwepo kwenye ile sehemu akidai kwamba anacho kumbuka ni kwamba alikuwa amewahi kuishi ndani ya nchi ya Tanzania. Jambo hilo halikumpa maswali mengi sana mwanamke huyo bali kwake alichukulia kama jambo la faraja baada ya kuamini mwanaume huyo shababi angekuwa ni wake na akamuomba kama yupo tayari amuoe ili waanze maisha mapya kama mume na mke.

Mwanaume huyo kwa wakati huo hakuwa na mwelekeo wa maisha hivyo akakubali kuishi na mwanamke huyo ambaye aliamini kapata mume bila kujua kwamba kapatikana japo alipewa sharti la kwamba waishi kama wachumba kwamza ndani ya mwaka kisha ndipo wafunge ndoa. Mwanamke huyo alijikuta anakubali kirahisi kwani alikuwa anazidi kumpenda mwanaume huyo kila dakika.

Mwanaume huyo ambaye jina lake halisi alikuwa anaitwa Grant Mshani alikuwa anafuatilia kwa umakini sana siasa ya Tanzania na namna wananchi walivyokuwa wanadanganywa, mwanaume huyo aliamini kwamba serikali kwa ujumla ilikuwa imehusika na hilo jambo kwa sababu kama kungekuwa na viongozi ambao hawakutaka kuwa sehemu ya hilo jambo au hawakuhusika kwenye kuutekeleza mpango huo basi lazima wangehoji kuhusu kupotea kwa makomando hao lakini tangu kauli hiyo itoke hakukuwa na mkazo wowote wa kuwafuatilia na wala hakuna ambaye alionekana kujali hivyo mwanaume akaamini kwamba basi huo ulikuwa ni mpango wa watu wengi sana ambao walihusika moja kwa moja kuhakikisha kwamba wao wanapotezwa kwenye ulimwengu.

Taratibu akawa anaipata imani ya yule mwanamke ambapo kutokana na mapenzi ambayo alikuwa nayo kwake alifanikiwa kumshawishi mrembo yule ambaye alikuwa ni daktari mkubwa sana kumbadilishia sura. Mwanaume huyo aliichora kwa ustadi sana sura ya Boniphace Walawala na kutaka kutengenezwa kwenye sura kama hiyo ambayo alihitaji ifanane kila kitu na hiyo ambayo alielekeza wamfanyie hivyo. Mwanamke huyo alipo jaribu kuhoji kwamba kwanini anataka kuishi kwenye sura nyingine, mwanaume alimjibu kwamba ile sura yake ya mwanzo ilikuwa inamfanya anaota mavitu ya ajabu hivyo alitaka kuwa mtu mwingine kabisa ndiyo maana aliihitaji sura nyingine tofauti na ile ambayo alikuwa ameizoea mwanzo.

Kwa sababu mrembo huyo hakuwa mtu wa siasa hakuweza kujua kwamba sura hiyo ilikuwa ni ya moja kati ya wanasiasa wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya taifa la Tanzania. Akaamua kumfanyia upasuaji mwanaume huyo kwa makubaliano ya kuilinda na kuitunza siri yao hiyo wao wawili tu pekee kama wapendanao ikiwa ni kama moja kati ya njia ya kuongeza upendo baina yao ili wayaanze maisha mapya ya mapenzi.

Mrembo mapenzi yalimchanganya sana sehemu ya kutumia akili kuweza kuchanganua mambo akajikuta anatumia hisia na kama ilivyo kwa wazungu, huwa ni rahisi sana kuamini kirahisi bila kujua kwamba kuna muda imani ikizidi sana inaweza kuwa na madhara makubwa. Baada ya jambo lile kukamilika mwanaume yule aliyejulikana kama Grant aliweza kumnyonga mwanamke yule na kupotea kusiko julikana na kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho kilikuwa kinamilikiwa na daktari huyo.

Familia yake ilijaribu kufuatilia kwa umakini sana juu ya jambo hilo ila kwa bahati mbaya hawakubahatika kupata chochote kile kwani uchumba wa watu hao wawili ulikuwa ni siri kubwa sana hivyo hawakumjua mtu ambaye alihusika na mauaji ya binti yao na kuwaachia majonzi makubwa sana kwenye maisha yao lakini mwanaume huyo hiyo ilikuwa ni safari yake ya moja kwa moja kurudi kwenye ardhi aliyo zaliwa, ardhi ya nchi ya Tanzania kwa mara nyingine akiwa anarudi kwa hasira sana ya kuweza kulipa yote ambayo yalimkuta yeye na ndugu zake ambao waliuawa na kutelekezwa huko Congo huku waliofanya hayo matukio wakishindwa kuelewa kwamba kuna uzembe ulifanyika na kuna binadamu aliweza kuishi.

Wakati Grant anafika ndani ya nchi hakuna mtu ambaye alijua uwepo wa mtu huyo, alikuwa akiishi kwa siri sana huku akiwa anazisoma nyendo zote za mheshimiwa Boniphace Walawala na namna alivyokuwa akiishi na maisha ambayo aliyaishi kwa muda ambao mwanaume huyo hakuwepo nchini kwani maisha ya huko nyuma ya kiongozi huyo alikuwa anayajua yote.

Zikiwa zimebakia siku kadhaa tu uchaguzi kuweza kufanyika msafara wa kiongozi huyo ukiwa unatokea kwenye majukumu ya kupiga kampeni za mwisho ulivamiwa ambapo walinzi wake wote waliuawa isipokuwa mlinzi wake mkuu ambaye hakuonekana eneo la tukio na kiongozi huyo hakuonekana kabisa eneo hilo kitu ambacho kilileta taharuki kubwa sana kwa wananchi wakiwa wanaamini kwamba huyo ndiye ambaye alikuwa mtu ambaye alifaa sana kuingia Ikulu.

Baada ya masaa ishirini kiongozi huyo aliongea mbele ya vyombo vya habari na kuweka uwazi kwamba alikuwa amevamiwa na watu ambao bila shaka walikuwa wamedhamiria kuweza kumuua lakini Mungu bado alikuwa upande wake kwani aliweza kumlinda na kumuepusha na kikombe hicho ambacho alitakiwa kukinywa. Alidai kwamba mlinzi wake aliweza kupigwa risasi lakini alifanikiwa kumtorosha kiongozi huyo na kuhakikisha yupo salama kabisa kitu ambacho kilimtia simanzi sana kuweza kumpoteza mlinzi wake huyo na kuamua kumzika kimya kimya kama heshima kubwa ya kuendelea kumuenzi.

Aliwashukuru sana wananchi kwa kuwa naye pamoja kwa wakati huo ambao alikuwa anapitia mambo magumu. Taarifa yake hiyo ndiyo ambayo ilihitimisha safari yake ya kwenda Ikulu na kumpa pointi zote kwani wananchi walihisi kwamba ni mpinzani wake ndiye ambaye alifanya hilo tukio hivyo hakuwa akifaa kuwa kiongozi wao wote wakawa wamepania kabisa kumpigia kura mtu huyo. Hata siku ya kupiga kura asubuhi yake wakati watu wakiwa wanajiandaa kuelekea kwenye vituo vya kupigia kura kilitangazwa kifo cha mke na watoto wa mwanaume huyo ikiwa ni kama njia nyingine ya kuendelea kumdhoofisha lakini bado alitoa lai kwa wananchi kwamba licha ya hayo yote ambayo yamemtokea lakini ilikuwa ni lazima aingie Ikulu ili aweze kuyamaliza kabisa hivyo kwa wale ambao walikuwa wanamfanyia hayo, hawakuwa wakimvunja moyo bali walikuwa wakimpa nguvu ya kuendelea kupambana zaidi na zaidi mpaka pale ambapo angefanikiwa kuingia madarakani angehakikisha wote anawakomesha kwa hiyo tabia ya kishenzi ambayo ilikuwa imeanza kuota mizizi kwenye nchi yake.

Kama ambavyo wananchi huwa wanapenda maneno matamu kutoka kwa wanasiasa wanapokuwa wanawadanganya ndivyo ilivyokuwa kwa watanzania, wote walienda kumpigia kura mwanaume huyo ambaye aliingia madarakani kilaini sana kwa akili za mtu ambaye alikuwa ametulia kando akiwa anawaangalia walivyokuwa wakihangaika. Hayo yote yalifanywa na Grant Mshani, mwanaume huyo ndiye ambaye aliuvamia msafara wa kiongozi huyo na kuweza kumteka ambapo aliondoka naye pamoja na mlinzi wake ili ionekane kama mlinzi huyo alifanikiwa kuokoka na baada ya hapo alienda kumuulia mlinzi huyo eneo la mbali na hapo.

Walawala alishangazwa sana kumuona mtu ambaye alikuwa anafanana naye kwa kila kitu mbele yake kitu ambacho walikuwa wametofautiana kilikuwa kimoja tu, miili yao. Mwanaume huyo alikuwa na mwili wa mazoeazi sana huku yeye akiwa na mwili ambao uliridhika kwa maisha mazuri ambayo alikuwa nayo. Hakuwa na haraka sana ilibidi amkumbushe lile tukio la miaka miwili ambayo ilikuwa imepita na namna walivyoweza kutelekezwa na makomando wenzake hivyo alimtaka kiongozi huyo aseme kila kitu na idadi ya watu ambao walikuwa kwenye huo mpango mpaka amri ikatolewa kwamba watu hao waweze kuuawa.

Ukurasa wa 53 niseme basi.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA NNE
Hakuwa tayari kuweza kuitaja siri ambayo ilikuwepo hivyo mwanaume huyo alimteka mke na watoto mapacha wa Boniphace Walawala huku akimtaka aongee ukweli vinginevyo angeshuhudia mambo ya kutisha sana ambayo huenda asingeweza kuyaamini kwenye maisha yake au asingetamani yaje kumtokea lakini bado alikula msimamo na kugoma tena kusema basi mwanaume hakuwa na namna zaidi ya kumbaka mke wa kiongozi huyo huku naye akiwa anaona kwa macho yake na wanae wawili mapacha ambao walikuwa ni wadogo wakishuhudia.

Baada ya Grant kutekeleza ukatili huo kama njia ya kuilipa nchi kwa usaliti mkubwa ambao walifanyiwa pamoja na kuwapoteza wenzake watano alitaka kuua familia hiyo mbele ya Boniphace ndipo alipokubali kuongea ukweli kwamba watu hao walikuwa wanayahitaji yale madini ambayo waliyapata huko na walikuwa hawana namna nyingine ya kuyapata hivyo wao ndio ambao walicheza lile dini la kuwakamatisha watu wao huko wakijua kwamba makomando hao wakienda lazima watafanikisha zoezi hilo na kutoshtukiwa kwa sababu ingeonekana kwamba madini yalipotea kwenye oparesheni ya uokoaji ambapo hakuna mhusika ambaye angekuwa na nguvu ya kuanza kuhoji.

Baada ya zoezi hilo kuweza kukamilika waliamini kwamba makomando hao wanaweza wakaja kuanza kuhoji baadae na ikawa ni hatari kwa upande wa viongozi hao hivyo wakaamua kabisa kuwaua ili kuwapoteza jumla moja kwa moja kufanya jambo libakie kwenye mikono yao tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kuweza kuuliwa na wenzake ambapo kama bahati tu yeye pekee ndiye ambaye alifanikiwa kuishi kwenye tukio hilo.

Alilazimika pia kuwataja wenzake ambao walihusika akiwepo mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mheshimiwa raisi mwenyewe ambaye ndiye alikuwa anatoka madarakani wakati huo ambao Boniphace Walawala alikuwa anaingia madarakani. Hilo jambo lilimsikitisha sana Grant, alijua kama hadi raisi anahusika basi hilo ni tukio la nchi nzima ambalo lilikuwa limewahusisha watu wengi sana chini chini kwani raisi alikuwa anasimama kama taasisi.

Baada ya kuujua ukweli huo ndio alipo anza kujitokeza hadharani kufanya hizo interview kwamba yeye ni Boniphace Walawala na alikuwa imara japo watu walihitaji kuweza kumdondosha. Hata ile ambayo aliifanya baada ya mkewe kufariki na watoto alikuwa ni Grant mwenyewe na kwa wakati huo alijikuta anakuwa na hamu kubwa sana ya kuweza kuingia Ikulu. Jambo moja ambalo lilikuwa linamfanya asigundulike kama sio mhusika mwenyewe ni kwa sababu alikuwa anavaa manguo makubwa sana ya hospitalini kwa wakati huo hivyo mwili haukuwa unaonekana jinsi ulivyo.

Alimtesa sana kiongozi huyo lakini hakuwahi kumuua bali alimhifadhi sehemu ili ashuhudie kile ambacho angewafanyia wenzake kisha yeye angekuwa wa mwisho kutekelezewa hilo. Baada ya siku tatu matokeo yalitangazwa na Boniphace Walawala alikuwa ameshinda kwa kishindo kikubwa sana ambapo alikuwa amebakiza kiapo tu pekee aweze kuapishwa Ikulu huku akitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa akiwashukuru sana watanzania wote kwa kuweza kumuamini na kwa wakati huo hakuwa akiruhusu mtu yeyote kuweza kukutana naye bali alisema wataonana kuanzia siku ya kuapishwa kwake ambapo angeanza kuvaa mavazi makubwa mpaka pale afya yake itakapo tengamaa ndipo angerejea kwenye mavazi ya kawaida ikiwa kama ushauri kwa madaktari wake ambao walimwambia kwamba mwili unatakiwa upate hewa ya kutosha.

Hilo halikuwa jambo la ajabu kwa wananchi kwani walikuwa walishamkubali mtu wao na hivyo ndivyo mwanaume alivyo ishinda karata na kuingia Ikulu bila kutumia nguvu kwa kutumia jina la mwenzake huku mhusika akiwa amefichwa. Baada ya kuapishwa mwanaume huyo alianza kuwaua mmoja mmoja kwenye ile orodha ndefu ya wale ambao ndio waliwasaliti ambapo baadae alikuja kumalizana na yule aliyekuwa raisi ambaye alimuachia kijiti kwa kuhakikisha anachomwa na sindano ya sumu ambayo ilipelekea moyo kuacha kabisa kufanya kazi na mwisho hali hiyo ikapelekea mauti yake.

Aliendelea kuua kimya kimya watu wote ambao walionekana kuhusika kwenye lile tukio mpaka alipohakikisha amewamaliza wote. Lengo lake lilikuwa ni kufanya kisasi tu kisha apotee lakini baada ya kulionja lile joto la Ikulu hakutamani kuweza kuiachia nafasi hiyo kirahisi hivyo akaamua kuichukua nafasi hiyo mazima na kuahidi kuilipa nchi hii kadri ilivyo mletea madhara ya kuwapoteza wenzake na ndipo hapo ambapo rasmi alianza kuishi kama Boniphace Walawala kwa kisingizio kwamba ameanza mazoezi ya siri sana ili kujiweka sawa kama ushauri wa madaktari ulivyokuwa unasema na baada ya mwaka alikuwa ameanza kuvaa mavazi ya kawaida ambayo yalionyesha mabadiliko makubwa sana ya mwili wake ambao haukuonyesha mashaka yoyote yale kwenye macho ya wengi” Harper alionekana kuijua kwa undani sana simulizi ya maisha ya mwanaume huyo ambaye alidaiwa kuwa na kisasi kizito sana na nchi ambayo alizaliwa. Alipumzika kidogo Tommy akiwa ametulia kwa umakini sana kusikiliza bila kutia neno lolote lile. Harper alijiweka sawa kisha akaendelea tena.

“Kwenye harakati zake zake alikutana na mzee mmoja ambaye alionekana kumfuatilia kwa muda mrefu sana kwenye huo utafutaji wake na mzee huyo alionekaa kwamba alikuwa amemshtukia mtu huyo kwa muda mrefu sana kwa sababu Grant alimkuta mzee huyo akiwa anafanya kazi hapo Ikulu hata kabla ya ule ujio wake. Mzee huyo alimuweka wazi kwamba yeye alijua kwamba huyo mtu hakuwa mwenyewe lakini alikuwa tayari kufanya naye kazi kwa sababu hayo ambayo yalitokea hayakuwa yakimhusu kabisa yeye alikuwa anaangalia maslahi yake tu.

Grant alishtuka sana baada ya kujua kwamba ameshtukiwa lakini mzee huyo alimtoa wasiwasi na mpaka sasa mzee huyo ndiye ambaye ni mkono wake wa kulia. Mwanaume huyo anamsikiliza huyo mzee na kumwamini kuliko binadamu yeyote yule na ndiye ambaye amemsaidia kuiongoza nchi kwa miaka hii yote kumi bila wasiwasi maana yeye Ikulu anapajua vyema kuliko Grant ambaye wananchi wanamjua kama Boniphace Walawala na mzee huyo ndiye ambaye pia alimsaidia kumuua mpinzani wake mmoja ambaye alikuwa anaitwa Pandei Santo ambaye ilibakia kidogo asababishe Grant atolewe Ikulu kwa jeuri ya utajiri wa Pandei Santo lakini majivuno yake yalimfanya komando huyo amuwahishe kaburini.

Grant hakuna anachojali tena kuhusu nchi hii, hakuna kitu ambacho anaogopa kukipoteza zaidi ya kuangalia maslahi yake binafsi. Kisasi chake na wale watu kilisha isha lakini kwa sasa anaikomoa nchi ambapo amejilimbikizia mabilioni ya fedha, ana shehena kubwa sana ya dhahabu na madini mbali mbali pamoja na ardhi nyingi sana na hakuna anaye jua hili kwa upande wa viongozi wengine. Mtu huyu anamiliki watu wengi sana wa hatari, ana magenge mengi sana ya wauzaji wa madawa ya kulevya, ana watu wengi sana ambao anawaendesha na wanamtii na ndiyo maana ana jeuri ya kufanya chochote anacho kihitaji lakini kubwa zaidi ni kwamba yeye mwenyewe ni miongoni mwa wanadamu hatari sana tena zaidi ya sana kwa sababu alikuwa komando wa daraja la juu sana.

Hii ndiyo sababu ilikuwa rahisi sana yeye kuweza kufanya makubaliano na gaidi kuhusu kirusi ambacho kinaweza kuleta madhara sana kama kikiachiwa kwahiyo wao wanaamini kwamba watakitumia kuishi maisha ambayo wayataka wao japo inasemekana kwamba anaweza kumuua yule gaidi muda wowote ule ili abaki nacho pekeyake kwani kwenye moja kati ya sifa zake kubwa ni kwamba huwa hamuamini mtu yeyote yule. Huyo ndiye Boniphace Walawala ambaye huwa unamuona kama ni raisi wa nchi ya Tanzania” Harper alikamilisha maelezo ambayo yalimfanya atumie muda mrefu sana kuweza kuyaelezea na baada ya maelezo hayo kukamilika alihema kwa nguvu na kusogea kwenye friji dogo ambalo lilikuwa ndani ya chumba hicho, aliyatoa maji ya baridi na kuyanywa kisha akasogea kando na alipokuwa amekaa Tommy naye akikaa hapo akiwa amevaa bikini tu kwenye mwili wake.

Mwanamke huyo hakuonekana kuwa anabahatisha kwenye kazi yake kwani kuwa kwenye shirika kubwa la kijasusi namna hiyo kulimfanya kupata taarifa nyingi sana kwa sababu walifanikiwa kupenyeza wajasusi wao wengi sana kwenye taasisi zingine ikiwemo ya nchi ya Tanzania ambayo kwa wakati huo ilikuwa ni mhimu sana kwa sababu walikuwa wanakitafuta kirusi hicho ambacho kilitengenezwa na Tommy ndiyo maana walikuwa makini sana kuchimba kila taarifa ambayo ingeonekana kuwa mhimu kwao kwa wakati huo.

“Kuna muda unanitisha sana, najaribu kuwaza mpaka inafika sehemu nahisi kuna mambo mengi sana ambayo huenda mimi siyajui kabisa kuhusu wewe, nashindwa kuelewa kwamba hizi taarifa huwa unazipata wapi H2 kwa sababu haya mambo ambayo umeniambia licha ya kuwa ya mhimu sana lakini ni taarifa za siri sana ambazo haziwezi kupatikana kirahisi na sio taarifa ambazo kila mtu anaweza kuzipata”

“Kama nilivyokwambia mwanzo, sisi ni moja kati ya mataifa makubwa ambayo yamepiga hatua kubwa sana kwenye kazi za kiitelijensia hivyo tangu muda mrefu sana tulisha wapenyeza watu wetu huko ndiyo maana kuna taarifa tunakuwa nazo ambazo unakuta hata mashirika ya kijasusi ya nchi husika yanakuwa hayana”

“Nimekuelewa vyema sana lakini sijajua sababu ya wewe kuniambia habari hizi ambazo hakukuwa na ulazima kwani sikuwa nimeomba uniambie haya. Sasa ni kitu gani ambacho unahisi kinakufanya uone mimi nastahili kupewa taarifa za ndani sana kama hizi ambazo huenda kama viongozi wako wakijua kwamba umenipa zinaweza kukuletea matatizo?”

“Kwa sababu nakupenda T1, mimi nipo tayari kukutwa na jambo lolote lile kwa ajili yako, nipo tayari hata kuachana na kila kitu kwenye maisha yangu kwa ajili yako. Najua ipo siku utakuja kunielewa na kunisamahe moja kwa moja kwenye moyo wako na ndio huo muda ambao mimi nausubiri sana kwenye maisha yangu hata ukichelewa”

“Tuachane na hayo kwanza, kwa mtazamo wako unahisi kwamba ni kwanini ameamua kuweza kukiachia kiti cha uraisi kirahisi sana namna hiyo wakati ndiyo sehemu ambayo angeweza kuendelea kuitekeleza hiyo adhma yake ya kuweza kuendelea kuilipizia nchi?”

“Kama nilivyokwambia kwamba huyu mtu ana mtu wake wa pembeni ambaye ndiye mkono wake wa kulia yaani kiufupi ni kwamba huyo mtu akili yake ndiyo ambayo Grant anaitumia ili kuweza kutekeleza yale ambayo anahisi kwamba yanamfaa na yana manufaa makubwa kwake. Inasemekana japo bado haijathibitishwa kwamba kuna mtu miongoni mwa wale ambao walimletea maafa kwenye maisha yake ana kisasi naye binafsi yeye kama yeye achana na kile ambacho kilitokea kwa wenzake”

“Umeniacha kidogo hapo sijakuelewa unamaanisha nini?”
“Upo sahihi. Kwenye simulizi ya maisha yake kuna sehemu sijaigusia nimeiruka, mwanaume huyo kwenye harakati zake za kulitumikia taifa ambazo zilimfanya kuwa mtu wa kutembea tembea sehemu nyingi sana alifanikiwa kukutana na mwanamke mmoja mrembo sana ambaye alikuwa na asili ya nchi ya Rwanda. Watu hao walipendana sana tena zaidi ya sana, wakafanikiwa kupata na mtoto kabisa hivyo kiufupi naweza kusema kwamba mwanamke huyo alikuwa mkewe japo jambo hilo hakuwahi kuliweka wazi”

Ukurasa wa 54 naweka kalamu chini.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA NNE
Hakuwa tayari kuweza kuitaja siri ambayo ilikuwepo hivyo mwanaume huyo alimteka mke na watoto mapacha wa Boniphace Walawala huku akimtaka aongee ukweli vinginevyo angeshuhudia mambo ya kutisha sana ambayo huenda asingeweza kuyaamini kwenye maisha yake au asingetamani yaje kumtokea lakini bado alikula msimamo na kugoma tena kusema basi mwanaume hakuwa na namna zaidi ya kumbaka mke wa kiongozi huyo huku naye akiwa anaona kwa macho yake na wanae wawili mapacha ambao walikuwa ni wadogo wakishuhudia.

Baada ya Grant kutekeleza ukatili huo kama njia ya kuilipa nchi kwa usaliti mkubwa ambao walifanyiwa pamoja na kuwapoteza wenzake watano alitaka kuua familia hiyo mbele ya Boniphace ndipo alipokubali kuongea ukweli kwamba watu hao walikuwa wanayahitaji yale madini ambayo waliyapata huko na walikuwa hawana namna nyingine ya kuyapata hivyo wao ndio ambao walicheza lile dini la kuwakamatisha watu wao huko wakijua kwamba makomando hao wakienda lazima watafanikisha zoezi hilo na kutoshtukiwa kwa sababu ingeonekana kwamba madini yalipotea kwenye oparesheni ya uokoaji ambapo hakuna mhusika ambaye angekuwa na nguvu ya kuanza kuhoji.

Baada ya zoezi hilo kuweza kukamilika waliamini kwamba makomando hao wanaweza wakaja kuanza kuhoji baadae na ikawa ni hatari kwa upande wa viongozi hao hivyo wakaamua kabisa kuwaua ili kuwapoteza jumla moja kwa moja kufanya jambo libakie kwenye mikono yao tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kuweza kuuliwa na wenzake ambapo kama bahati tu yeye pekee ndiye ambaye alifanikiwa kuishi kwenye tukio hilo.

Alilazimika pia kuwataja wenzake ambao walihusika akiwepo mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mheshimiwa raisi mwenyewe ambaye ndiye alikuwa anatoka madarakani wakati huo ambao Boniphace Walawala alikuwa anaingia madarakani. Hilo jambo lilimsikitisha sana Grant, alijua kama hadi raisi anahusika basi hilo ni tukio la nchi nzima ambalo lilikuwa limewahusisha watu wengi sana chini chini kwani raisi alikuwa anasimama kama taasisi.

Baada ya kuujua ukweli huo ndio alipo anza kujitokeza hadharani kufanya hizo interview kwamba yeye ni Boniphace Walawala na alikuwa imara japo watu walihitaji kuweza kumdondosha. Hata ile ambayo aliifanya baada ya mkewe kufariki na watoto alikuwa ni Grant mwenyewe na kwa wakati huo alijikuta anakuwa na hamu kubwa sana ya kuweza kuingia Ikulu. Jambo moja ambalo lilikuwa linamfanya asigundulike kama sio mhusika mwenyewe ni kwa sababu alikuwa anavaa manguo makubwa sana ya hospitalini kwa wakati huo hivyo mwili haukuwa unaonekana jinsi ulivyo.

Alimtesa sana kiongozi huyo lakini hakuwahi kumuua bali alimhifadhi sehemu ili ashuhudie kile ambacho angewafanyia wenzake kisha yeye angekuwa wa mwisho kutekelezewa hilo. Baada ya siku tatu matokeo yalitangazwa na Boniphace Walawala alikuwa ameshinda kwa kishindo kikubwa sana ambapo alikuwa amebakiza kiapo tu pekee aweze kuapishwa Ikulu huku akitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa akiwashukuru sana watanzania wote kwa kuweza kumuamini na kwa wakati huo hakuwa akiruhusu mtu yeyote kuweza kukutana naye bali alisema wataonana kuanzia siku ya kuapishwa kwake ambapo angeanza kuvaa mavazi makubwa mpaka pale afya yake itakapo tengamaa ndipo angerejea kwenye mavazi ya kawaida ikiwa kama ushauri kwa madaktari wake ambao walimwambia kwamba mwili unatakiwa upate hewa ya kutosha.

Hilo halikuwa jambo la ajabu kwa wananchi kwani walikuwa walishamkubali mtu wao na hivyo ndivyo mwanaume alivyo ishinda karata na kuingia Ikulu bila kutumia nguvu kwa kutumia jina la mwenzake huku mhusika akiwa amefichwa. Baada ya kuapishwa mwanaume huyo alianza kuwaua mmoja mmoja kwenye ile orodha ndefu ya wale ambao ndio waliwasaliti ambapo baadae alikuja kumalizana na yule aliyekuwa raisi ambaye alimuachia kijiti kwa kuhakikisha anachomwa na sindano ya sumu ambayo ilipelekea moyo kuacha kabisa kufanya kazi na mwisho hali hiyo ikapelekea mauti yake.

Aliendelea kuua kimya kimya watu wote ambao walionekana kuhusika kwenye lile tukio mpaka alipohakikisha amewamaliza wote. Lengo lake lilikuwa ni kufanya kisasi tu kisha apotee lakini baada ya kulionja lile joto la Ikulu hakutamani kuweza kuiachia nafasi hiyo kirahisi hivyo akaamua kuichukua nafasi hiyo mazima na kuahidi kuilipa nchi hii kadri ilivyo mletea madhara ya kuwapoteza wenzake na ndipo hapo ambapo rasmi alianza kuishi kama Boniphace Walawala kwa kisingizio kwamba ameanza mazoezi ya siri sana ili kujiweka sawa kama ushauri wa madaktari ulivyokuwa unasema na baada ya mwaka alikuwa ameanza kuvaa mavazi ya kawaida ambayo yalionyesha mabadiliko makubwa sana ya mwili wake ambao haukuonyesha mashaka yoyote yale kwenye macho ya wengi” Harper alionekana kuijua kwa undani sana simulizi ya maisha ya mwanaume huyo ambaye alidaiwa kuwa na kisasi kizito sana na nchi ambayo alizaliwa. Alipumzika kidogo Tommy akiwa ametulia kwa umakini sana kusikiliza bila kutia neno lolote lile. Harper alijiweka sawa kisha akaendelea tena.

“Kwenye harakati zake zake alikutana na mzee mmoja ambaye alionekana kumfuatilia kwa muda mrefu sana kwenye huo utafutaji wake na mzee huyo alionekaa kwamba alikuwa amemshtukia mtu huyo kwa muda mrefu sana kwa sababu Grant alimkuta mzee huyo akiwa anafanya kazi hapo Ikulu hata kabla ya ule ujio wake. Mzee huyo alimuweka wazi kwamba yeye alijua kwamba huyo mtu hakuwa mwenyewe lakini alikuwa tayari kufanya naye kazi kwa sababu hayo ambayo yalitokea hayakuwa yakimhusu kabisa yeye alikuwa anaangalia maslahi yake tu.

Grant alishtuka sana baada ya kujua kwamba ameshtukiwa lakini mzee huyo alimtoa wasiwasi na mpaka sasa mzee huyo ndiye ambaye ni mkono wake wa kulia. Mwanaume huyo anamsikiliza huyo mzee na kumwamini kuliko binadamu yeyote yule na ndiye ambaye amemsaidia kuiongoza nchi kwa miaka hii yote kumi bila wasiwasi maana yeye Ikulu anapajua vyema kuliko Grant ambaye wananchi wanamjua kama Boniphace Walawala na mzee huyo ndiye ambaye pia alimsaidia kumuua mpinzani wake mmoja ambaye alikuwa anaitwa Pandei Santo ambaye ilibakia kidogo asababishe Grant atolewe Ikulu kwa jeuri ya utajiri wa Pandei Santo lakini majivuno yake yalimfanya komando huyo amuwahishe kaburini.

Grant hakuna anachojali tena kuhusu nchi hii, hakuna kitu ambacho anaogopa kukipoteza zaidi ya kuangalia maslahi yake binafsi. Kisasi chake na wale watu kilisha isha lakini kwa sasa anaikomoa nchi ambapo amejilimbikizia mabilioni ya fedha, ana shehena kubwa sana ya dhahabu na madini mbali mbali pamoja na ardhi nyingi sana na hakuna anaye jua hili kwa upande wa viongozi wengine. Mtu huyu anamiliki watu wengi sana wa hatari, ana magenge mengi sana ya wauzaji wa madawa ya kulevya, ana watu wengi sana ambao anawaendesha na wanamtii na ndiyo maana ana jeuri ya kufanya chochote anacho kihitaji lakini kubwa zaidi ni kwamba yeye mwenyewe ni miongoni mwa wanadamu hatari sana tena zaidi ya sana kwa sababu alikuwa komando wa daraja la juu sana.

Hii ndiyo sababu ilikuwa rahisi sana yeye kuweza kufanya makubaliano na gaidi kuhusu kirusi ambacho kinaweza kuleta madhara sana kama kikiachiwa kwahiyo wao wanaamini kwamba watakitumia kuishi maisha ambayo wayataka wao japo inasemekana kwamba anaweza kumuua yule gaidi muda wowote ule ili abaki nacho pekeyake kwani kwenye moja kati ya sifa zake kubwa ni kwamba huwa hamuamini mtu yeyote yule. Huyo ndiye Boniphace Walawala ambaye huwa unamuona kama ni raisi wa nchi ya Tanzania” Harper alikamilisha maelezo ambayo yalimfanya atumie muda mrefu sana kuweza kuyaelezea na baada ya maelezo hayo kukamilika alihema kwa nguvu na kusogea kwenye friji dogo ambalo lilikuwa ndani ya chumba hicho, aliyatoa maji ya baridi na kuyanywa kisha akasogea kando na alipokuwa amekaa Tommy naye akikaa hapo akiwa amevaa bikini tu kwenye mwili wake.

Mwanamke huyo hakuonekana kuwa anabahatisha kwenye kazi yake kwani kuwa kwenye shirika kubwa la kijasusi namna hiyo kulimfanya kupata taarifa nyingi sana kwa sababu walifanikiwa kupenyeza wajasusi wao wengi sana kwenye taasisi zingine ikiwemo ya nchi ya Tanzania ambayo kwa wakati huo ilikuwa ni mhimu sana kwa sababu walikuwa wanakitafuta kirusi hicho ambacho kilitengenezwa na Tommy ndiyo maana walikuwa makini sana kuchimba kila taarifa ambayo ingeonekana kuwa mhimu kwao kwa wakati huo.

“Kuna muda unanitisha sana, najaribu kuwaza mpaka inafika sehemu nahisi kuna mambo mengi sana ambayo huenda mimi siyajui kabisa kuhusu wewe, nashindwa kuelewa kwamba hizi taarifa huwa unazipata wapi H2 kwa sababu haya mambo ambayo umeniambia licha ya kuwa ya mhimu sana lakini ni taarifa za siri sana ambazo haziwezi kupatikana kirahisi na sio taarifa ambazo kila mtu anaweza kuzipata”

“Kama nilivyokwambia mwanzo, sisi ni moja kati ya mataifa makubwa ambayo yamepiga hatua kubwa sana kwenye kazi za kiitelijensia hivyo tangu muda mrefu sana tulisha wapenyeza watu wetu huko ndiyo maana kuna taarifa tunakuwa nazo ambazo unakuta hata mashirika ya kijasusi ya nchi husika yanakuwa hayana”

“Nimekuelewa vyema sana lakini sijajua sababu ya wewe kuniambia habari hizi ambazo hakukuwa na ulazima kwani sikuwa nimeomba uniambie haya. Sasa ni kitu gani ambacho unahisi kinakufanya uone mimi nastahili kupewa taarifa za ndani sana kama hizi ambazo huenda kama viongozi wako wakijua kwamba umenipa zinaweza kukuletea matatizo?”

“Kwa sababu nakupenda T1, mimi nipo tayari kukutwa na jambo lolote lile kwa ajili yako, nipo tayari hata kuachana na kila kitu kwenye maisha yangu kwa ajili yako. Najua ipo siku utakuja kunielewa na kunisamahe moja kwa moja kwenye moyo wako na ndio huo muda ambao mimi nausubiri sana kwenye maisha yangu hata ukichelewa”

“Tuachane na hayo kwanza, kwa mtazamo wako unahisi kwamba ni kwanini ameamua kuweza kukiachia kiti cha uraisi kirahisi sana namna hiyo wakati ndiyo sehemu ambayo angeweza kuendelea kuitekeleza hiyo adhma yake ya kuweza kuendelea kuilipizia nchi?”

“Kama nilivyokwambia kwamba huyu mtu ana mtu wake wa pembeni ambaye ndiye mkono wake wa kulia yaani kiufupi ni kwamba huyo mtu akili yake ndiyo ambayo Grant anaitumia ili kuweza kutekeleza yale ambayo anahisi kwamba yanamfaa na yana manufaa makubwa kwake. Inasemekana japo bado haijathibitishwa kwamba kuna mtu miongoni mwa wale ambao walimletea maafa kwenye maisha yake ana kisasi naye binafsi yeye kama yeye achana na kile ambacho kilitokea kwa wenzake”

“Umeniacha kidogo hapo sijakuelewa unamaanisha nini?”
“Upo sahihi. Kwenye simulizi ya maisha yake kuna sehemu sijaigusia nimeiruka, mwanaume huyo kwenye harakati zake za kulitumikia taifa ambazo zilimfanya kuwa mtu wa kutembea tembea sehemu nyingi sana alifanikiwa kukutana na mwanamke mmoja mrembo sana ambaye alikuwa na asili ya nchi ya Rwanda. Watu hao walipendana sana tena zaidi ya sana, wakafanikiwa kupata na mtoto kabisa hivyo kiufupi naweza kusema kwamba mwanamke huyo alikuwa mkewe japo jambo hilo hakuwahi kuliweka wazi”

Ukurasa wa 54 naweka kalamu chini.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu kwema? Weka hata vipande 10 pls umeniacha na arosto Kali sana
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA TANO
“Sasa inasemekana hiyo miaka ambayo alipotea pia kuna kiongozi mmoja mkubwa ambaye naye alihusika kwenye ule mpango lakini aliona haitoshi akaenda kumbaka mkewe na kumuulia mtoto wake. Sasa kwenye kuwatafuta inasemekaana kwamba mtu huyo yeye alisahaulika kabisa ila amekuja kujua ni baadae sana kwamba kuna mwanadamu hakugundulika miongoni mwa wale viongozi ambao waliwatuma Kongo ambapo alitumia nguvu kubwa sana kuweza kumpata. Mtu huyo haijulikani ila kwa sasa inadaiwa kwamba atakuwa anamfahamu mwanaume huyo ambaye alihusika hivyo kuna kitu ambacho anataka kukifanya ndiyo maana inahisiwa kwamba ndiyo sababu iliyomfanya akakubali kuweza kutoka kwenye hiyo nafasi yake ghafla sana namna hiyo”

“f***k kwahiyo anataka kukifanya kama kile ambacho alikifanya kwa Boniphace Walawala?”
“Yes, inadaiwa kwamba ni hivyo kwahiyo muda wowote anaweza kupotea na usije ukaiona ile sura tena kwenye maisha yako akaishia kutengeneza mtego ambao utawaaminisha watanzania kwamba yeye amekufa na kila mtu ataamini kama alivyo wadanganya watanzania kwa miaka yote hii akiishi kwenye sura ambayo haikuwa yake”
“Mshenzi ana akili sijapata kuona, kwahiyo natakiwa kumpata haraka sana maana kama tukichelewa tunaweza kukikosa hata kirusi chenyewe”
“No, kama tukienda haraka tutakosa kila kitu, huyu mtu huwa anapiga hatua nne mbele ndipo anaanza kufanya maamuzi kwahiyo ukitaka kushindana naye unaweza ukafanya akajua kwamba ameshtukiwa akafanya tukio lingine ambalo likatuacha midomo wazi tu”
“Kwahiyo unahisi ipi njia bora zaidi?”
“Jambo la msingi ni moja tu, tunatakiwa kujua kwamba anahitaji kuitumia sura ya nani kwa sasa ambapo anaenda kutoka kwenye siasa na tujue sababu kubwa nyuma yake ni nini hasa maana hawezi kuondoka pale hivi hivi lazima kutakuwa kuna jambo kubwa sana nyuma yake yule ni mtu ambaye anaangalia sana upande wenye faida tu.
“Yeah kuna watu wanaweza wasiwe wamesoma ila wana akili za mtaani nadhani ukiwa na watu kama hawa kumi halafu wakaamua kuwa kinyume na taifa basi taifa hilo muda wowote ule linaangamia maana ni jambo la hatari huenda kuliko hatari yenyewe inavyoweza kutajwa. Unavyohisi ni mtu gani ambaye anaweza kuwa target ya kwanza?” swali la Tommy lilimfanya binti huyo atabasamu kwa sababu wakati huo walikuwa wanaongea vizuri sana na usingeweza kuamini kwamba watu hao walikuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu kwa sababu ya mambo ambayo walifanyiana huko nyuma.

Mwanamke huyo aliiwasha komputa yake ya bei ghali ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa sana kisha akaingia kwenye mtandao kutafuta picha ambazo mheshimiwa huyo alikuwa amezisasisha kwa siku kadhaa ambazo alikuwa zimepita ndipo walipo ipata moja ambayo alikuwa anampigia chapuo mr Mafupa kwamba ndiye binadamu ambaye anafaa kuingia Ikulu na kuiongoza nchi, wote wawili waliishia kuangaliana kama wanaulizana kwamba hivi haya ni ya kweli au kuna mchezo hapa.

“No haiwezekani” Tommy aliongea akiwa anasimama na kuanza kuzunguka humo ndani.
“Kwanini?”
“Kwa mambo ambayo umenisimulia kwamba ameyafanya huko nyuma sidhani kama huyu ndiye tageti yake kubwa kwa sababu kama huyu angekuwa kwenye mahesabu yake maana yake yeye mwenyewe angeendelea kubaki Ikulu hakuwa na haja ya kumtumia mr Mafupa sehemu ambayo yeye mwenyewe alikuwa na uwezo wa kusimama na kuendelea kula mema ya nchi. Hii inamaanisha kwamba kuna samaki mkubwa ambaye anautawala mto na kuna samaki mdogo ambaye anamtii na samaki mwenyewe mdogo ni mr Mafupa hivyo nyuma yam r Mafupa kuna kiumbe kingine ambacho ndiye samaki mkubwa na huyo huenda ndiye target yake kubwa”

“That’s why you are a genius” aliongea mwanamke huyo akionyesha alama ya Ok kwamba mwanaume huyo alikuwa amewaza mbali sana na mawazo yake yalionekana kuwa sahihi. Tommy alikumbuka alifanya mazungumzo na mkurugenzi wa usalama wa Taifa akamwelekeza kwamba nyuma ya huyo mtu amekaa mr Oscar ndo anampa jeuri hivyo huenda ndiye alikuwa samaki mkubwa ambaye ndiye alikuwa kwenye mahesabu ya huyo Grant ambaye wengi walimjua kama Boniphace Walawala.

“Yes, mr Oscar”
“Ndo nani?”
“Huyu ni waziri mkuu wa zamani wa nchi hii, inamaanisha moja kwa moja kwamba yeye ndiye ambaye yupo nyuma ya mr Mafupa na Grant anahitaji kuwa huyu mtu ili aweze kumuendesha mr Mafupa akiwa madarakani. Inamaanisha kwamba anataka jambo huyu nadhani itakuwa kuna mambo ambayo anataka kuyafanya na yatakapo kamilika basi ajiweke nje ya hatia na lawama zote zitamwangukia mr Mafupa. Huyu mjinga hata wakati akiwa komando kama angekuwa anatumia akili sana namna hii alikuwa ana uwezo wa kuipindua hii ndani ya usiku mmoja tu pekee na kila mtu akaweza kumtii vizuri kabisa bila wasiwasi wowote” iliwalazimu kuanza kuitafuta miaka ambayo mheshimiwa huyo alikuwa waziri mkuu na ilienda kuonyesha kwamba ni wakati ule ule ambao yale matukio yalitokea. Sasa walikuwa na uhakika kwamba huyo mtu anataka kuitumia sura ya Mr Oscar, ilikuwa kazi kwao kuona kama wanaweza kumzua binadamu ambaye alidaiwa kumiliki watu wa hatari sana.

“Nionyeshe picha zake halisi huyo Grant” Tommy aliongeza macho yake yakiwa bado kwenye komputa hiyo ambapo haikuchukua hata muda mwanamke huyo aliikuza picha ambayo ilikuwa mbele ya skrini ikimuonyesha mwanaume mmoja mwenye upara uliokuwa unang’aa haswa huku sura yake ikiwa inaonekana kabisa kwamba ilikuwa ni sura ya kazi.


Siku hiyo hiyo na usiku huo huo ambao matukio hayo yalikuwa yanafuatana kuweza kutokea CDF alimfuata mr Oscar na kumpa masaa kadhaa ahakikishe kwamba familia ya Zola ameirejesha maana kijana huyo alichokuwa amekubaliana naye alikuwa amekitekeleza hivyo ilikuwa imebakia zamu yake yeye kuweza kutimiza kile ambacho walikuwa wameahidiana mwanzo. Licha ya kwanza ulitokea mzozo mkali sana baina yao ila mzee huyo alikubali kuweza kuirejesha familia hiyo ambayo kuanzia wakati huo ingekuwa kwenye mikono ya CDF.

Wakati CDF anatoka kwa mheshimiwa huyo alipishana na msafara wa gari kadhaa ambao nao ulikuwa unaelekea kule kule ambako alikuwa ametokea naye akiwa na msafara wake, alitamani sana kumjua mtu ambaye alikuwa anaenda kumuona mr Oscar wakati huo lakini hakuwa na namna ya kufanya na gari hizo zilikuwa na vioo vyeusi hali ambayo ilimfanya kushindwa kumuona mwanaume ambaye aliingia mle ndani.

Aliingia mr Mafupa akiwa na macho mekundu sana, huo ni wakati ambao alienda eneo hilo bila hata taarifa lakini hata mwenyeji wake haikumshangaza kwani alielewa kabisa kwamba mtu huyo hakuwa kwenye hali yake ya kawaida kwa wakati huo ilikuwa ni lazima kufanya hivyo hakukuwa na namna ya kufanya.
“Unajua kilicho tokea?”
“Yeah najua”
“Ni mwanangu yule ambaye ameuliwa unajua hilo?”
“Hapana sijui kwa sababu hukuwahi kunipa taarifa zaidi kuhusu yeye japo uliniambia kwamba unaye mtoto wa kiume”
“Yes, ameuawa na huyo huyo muuaji ambaye anajiona kwamba yeye ni maarufu sana”
“Naweza kusema pole sana ndugu yangu kwa sababu najua namna inavyo uma kumpoteza mtoto hususani ambaye anakuwa mmoja tu. Niliwahi kuwa na familia kubwa tu huko nyuma lakini ajali iliichukua nikiwa bado naihitaji sana hivyo najua uchungu wake”

“Huwezi kuuelewa utamu wa ngoma mpaka uingia na wewe kuicheza hapo unaweza ukawa hata na uwezo wa kuielezea kuliko mtu yeyote yule na ndicho ambacho mimi nakipitia kwa wakati huu”
“Unaenda kufanya nini kwa sasa?”
“Namhitaji huyo bwana mdogo kwenye mkono wangu, nimemuingiza kijana wangu ambaye namuamini sana mtaani kwamba ahakikishe ananiletea mtu huyo akiwa mzima wa afya kabisa, nahitaji apitie kila hatua ya maumivu makali ambayo mwanangu ameyapitia kabla ya kuweza kupoteza maisha”

“Unahisi itakuwa rahisi sana namna hiyo?”
“Sijali, kwa gharama yoyote ile siwezi kuruhusu hilo jambo liende bure ni lazima ambaye amehusika naye alipe kwa gharama kubwa sana”
“Kwa sasa ungetulia kwanza hii kazi nitaifanya kwa ajili yako hivyo wewe waza kuihusu uchaguzi tu kwa sasa usije ukaharibu mambo yakiwa mwishoni”
“Unataka niwaze uchaguzi na mwanangu yupo mochwari? Unahisi ni rahisi sana namna hiyo mr Oscar?”

“Kwenye maisha ni ngumu sana kuwa na vitu vyote kati ya nguvu kubwa na familia hivyo ni lazima uchague kimoja na kimoja ukikose ndiyo maana hata mimi hapa licha ya kuwa na kila kitu kwenye maisha yangu ila sina familia na hivyo ndivyo haya maisha yetu yanavyo endeshwa”

“Nisikilize kwa umakini mr Oscar waingize vijana wako kila sehemu wamtafute huyu bwana mdogo na nahitaji hadi wanafamilia wake walipe kwa hili lakini kwa sasa sitakuacha ulifanye hili pekeyako bali na mimi nitaingiza vijana wangu kazini”
“Sawa ila kuwa makini sana”
“Na mwanangu kuhusu mwili wake inakuwaje maana hakuna anayejua mama mimi ndiye baba yake”
“Unatakiwa uache azikwe na mamlaka za jiji tu na wewe usije ukaonyesha kuhusika kwa namna yoyote ile”
“Whaaat?”
“Yes, kama ukijionyesha basi biashara yako inakuwa imeishia hapo kwani utazua taharuki kubwa sana ambayo itafanya watu waanze kukufikiria kwa jicho lingine na huenda mamlaka za usalama zitaanza pia kukufuatilia jambo ambalo litaibua mambo mengi sana mabaya kwa kipindi kama hiki ambacho utulivu ndiyo silaha kubwa sana ambayo unatakiwa kuwa nayo kwenye mkono wako”

“Hahahahaha hahaha hahaha yaani mwanangu amekufa na sitakiwi hata kumzika?” alicheka na kuongea kwa sauti kali sana mwanaume, sauti ambayo ilikuwa na uchungu sana ndani yake huku mwenzake ambaye alikuwa mbele yake akiwa amemkazia macho tu bila wasiwasi, watu walikuwa wanawaza kuhusu maslahi tu hayo ya familia angejua mwenyewe. Alitoka humo ndani kwa masikitiko makubwa sana baada ya kuona kwamba hakuna msaada wowote ambao angeweza akaupata kwa mtu huyo zaidi ya kupoteza muda wake tu.

Ukurasa wa 55 naweka nanga.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA SITA
Usiku wa siku hiyo ambayo mauaji hayo yalitokea, mheshimiwa raisi baada ya kunusa usaliti mkubwa sana kutoka kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, alichukua msafara wake na watu wake wa kazi haswa na kuelekea Magomeni, sehemu ambayo yalikuwepo makazi ya kiongozi huyo wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania ambapo wananchi wengi hawakuwa wakitambua kabisa wala kumjua kwani maisha yake yalikuwa ya usiri mkubwa mno mheshimiwa huyo.

Walitumia dakika thelathini tu kabla magari hayo hayajafika ndani ya eneo ambalo alikuwa anaishi. Ilitolewa amri kwamba umeme ukatwe ndani ya Magomeni kila kona na kila mtaa usiku huo kasoro tu kwenye jumba la kiongozi huyo ambalo kiuhalisia umeme haukuwa ukikatika hata mara moja kwa sababu ya nafasi kubwa ambayo alikuwa nayo nchini.

Umeme ulizimika ghafla sana hiyo mitaa, wakati umeme huo unazimika, Nickson alikuwa anaingia ndani ya mitaa hiyo ya Magomeni kwa sababu muda mchache tu uliokuwa umepita alikuwa amepewa maagizo na mkurugenzi kwamba afike nyumbani kwake kwa sababu kuna kazi kubwa sana ambayo alikuwa anahitaji kumpatia. Alimsisitiza sana alikuwa amenusa mambo ya hatari sana kuhusu raisi hivyo bwana mdogo huyo kuna kazi ambazo alitakiwa kuzitekeleza kabla raisi mwingine hajaingia madarakani kwani huenda naye angekuja kuwaweka watu wake kwenye hizo nafasi ambazo walikuwepo.

Kukatika kwa umeme huko kulimpa shaka sana hivyo ikabidi awahi haraka sana nyumbani kwa kiongozi wake huyo, licha ya kujua kwamba nyumbani kwa mzee huyo kulikuwa na ulinzi mkali ila aliamini kwamba huenda kuna watu walikuwa wanatumika na watu wengine au na viongozi fulani kwa ajili ya maslahi yao wenyewe na matumbo yao hivyo alipaswa kuwahi maana yalikuwa ni matukio ya ghafla sana.

Wakati Nick anawahi eneo hilo kwa mkubwa wake wa kazi, msafara wa mheshimiwa raisi ulikuwa unaingia ndani ya eneo hilo ambapo baada ya kugundulika kwamba ni mheshimiwa alikuwa hapo, geti lilifunguliwa haraka sana walinzi wakibakia wanatoa heshima tu kwa mtu huyo. Mheshimiwa raisi alitoa amri walinzi wote ambao walikuwa ndani ya jumba hilo wakusanyike sehemu moja kisha mkurugenzi naye na familia yake watoke nje usiku huo huo.

“Mheshimiwa mbona na usiku nyumbani kuna tatizo gani?” mkurugenzi baada ya kutoka nje aliweza kuuliza swali hilo ambalo lilipuuziwa kabisa na mwisho wa siku lilitokea jambo ambalo halikutegemewa kabisa baada ya mheshimiwa raisi kutoa amri walinzi wote wa mzee huyo wapigwe risasi jambo ambalo lilitekelezeka kwa haraka mno na kuacha kilio na mshangao kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa.

“Lingson kitu kimoja ambacho unajisahau sana ni kwamba kwenye hiyo nafasi ni mimi nilikuweka, nilikuweka kwa sababu jina lako lilipendekezwa mezani kwangu na baada ya kuichimbua historia yako niliona kabisa kwamba unanifaa na unafaa kuwa kijana wangu ambapo nilikusisitiza sana uweze kufanya kazi kwa moyo wote na kwa kujituma wakati wote kwa ajili yangu lakini wewe ukaamua kuanza kunizunguka mwisho wa siku imefikia hatua unaanza kunikatia hadi simu mimi?”

“Unafanya kosa kubwa sana kiongozi endapo kama hizi taarifa zikijulikana, umewaua malinzi kumi na watano ambao serikali imetumia gharama kubwa sana kuweza kuwapatia mafunzo nje ya nchi, hivi unahisi utakuwa sehemu gani kama haya mambo yakija kujulikana kwamba wewe ndiye umeyafanya haya?”

“Hahahaha hahahaha Lingson acha kunichekesha na usiku wote huu ndugu yangu, yaani unaongelea kuhusu gharama ambazo mimi ndiye nilikuwa nazipitisha? Unaongelea gharama ambazo mimi ndiye nilikuwa nazisaini ili ziweze kugawanywa kwenye makundi mbali mbali ya nchi? Na kuhusu wananchi kama ambavyo hawakujui wewe kwa sababu unaishi kwenye kificho basi kamwe hakuna mtu hata mmoja ambaye atakuja kujua kwamba uliwahi kuwepo au ulipotelea wapi na kama kuna mtu atahitaji kuweza kulitambua hili basi moja kwa moja naye nitamtafutia sehemu nzuri ya kwenda kupumzika”

“Kwani wewe unahitaji nini mheshimiwa?”
“Mimi nahitaji mambo madogo tu, mimi nahitaji kujua siri ambazo wewe unanificha, mimi nahitaji kujua aliye sababisha mauaji ya leo huko Kigamboni kwa kutumia kamera za siri za usalama maana najua hamuwezi kukosa hata sura yake, mimi nataka kujua kwamba wewe kuna kitu gani ambacho unanificha mimi na una mpango gani haswa juu yangu na serikali hii, nataka kujua kwamba kwanini umeamua kuikata simu yangu jambo ambalo ni kosa kubwa sana lakini nataka kujua kwamba labda wewe ni nani kwa upande mwingine maana naona kama unaanza kupishana na mimi?”

“Mimi hakuna jambo ambalo nalijua, mimi ni huyu huyu unaye mfahamu, mimi ni mzalendo wa nchi hii ambaye sitaki kuruhusu nchi iharibikie mikononi mwangu lakini mimi ni mtu ambaye sitaki kuendelea kuuona ushenzi ambao unaufanya kwa kudanganya watu na kujifanya kwamba wewe ni kiongozi bora au ni mtu mwema sana wakati kiuhalisia wewe ndiye chanzo cha matatizo mengi sana nchini” mkurugenzi aliongea kwa hasira sana mbele ya mheshimiwa raisi huyo ambaye siku chache zijazo angeitwa raisi msataafu.

“Mimi nawapenda watu kama wewe, mimi napenda watu ambao wanaishi kwenye ukweli wao kuliko kuigiza, mimi napenda sana wewe umeniambia ukweli kuhusu jambo ambalo lipo kwenye moyo wako. Leo nimejua kwamba haukuwahi kuwa kwenye upande wangu hata siku moja hivyo sidhani kama kutakuwa na umuhimu wa wewe kuendelea kuishi tena Lingson, unatakaiwa ukapumzike ili wapewe nafasi wengine ambao wana uwezo wa kuzitumia vizuri zile nafasi ambazo wanakuwa wanapewa na sio kuanza kushindana na watu ambao wanawahakikishia mlo wao hapa mjini”

“Nakuahidi utakuwa na mwisho mbaya sana mheshimiwa, mwisho wako unakaribia mimi nakusihi badilika bado unao muda kwani kama mambo haya yakikufikia huenda hautakuwa na hiyo nafasi ya kutamba tena. Kumbuka hivi vyeo vipo tu kwa muda fulani na vitapotea na hapo ndipo utagundua kwamba unawahitaji watu kwenye maisha yako, hapo ndipo utagundua kwamba ulitakiwa kuwa mtu mwema na sio kuishi kwa kujipakulia huo ujiko ambao unajisifia nao” maelezo ya Lingson yalimfanya mwanaume huyo amsogelee kwa umakini.

“Umesema mwisho wangu unakuja ina maana unajua kinacho endelea sio? Unaweza ukaniambia kwamba kuna nini kinafanyika chini chini ambacho mimi sikijui?”
“Hilo sahau siwezi kukwambia mheshimiwa, utanisamehe sana”
“Leo unaongea kirahisi sana namna hiyo mbele ya raisi wako kwamba hauwezi ukaniambia?”
“Nipo tayari kufa lakini sio kukwambia mheshimiwa kwa sababu jambo hili linaenda kuutoa uongozi wa udhalimu ambao umeamua kuuanzisha kwa ajili maslahi yako binafsi”

“Sawa” mzee huyo alijibu huku akiwa anaisogelea familia ya kiongozi huyo wa usalama ambaye alikuwa na watoto watatu na mke mzuri sana. Boniphace Walawala aliwaangalia sana watoto hao, kitu alicho kifanya kilikuwa ni cha ghafla sana na cha kutisha mno, ni baada ya kuichomoa bastola moja na kumtandika nayo binti wa mkurugenzi kwa risasi nyingi sana kifuani ambazo ziliyapoteza maisha yake hapo hapo.

“Noooooooooo” aliongea kwa sauti sana lakini hakuna ambacho alikuwa anaweza kukibadilisha hapo kwani ukweli ulibaki kwamba mwanae huyo alikuwa amekufa tayari kitu ambacho kilileta simanzi kubwa sana ndani ya eneo hilo.
“Umemponza na mwenzako DCI kwa sababu naye kujifanya mjuaji kumemfanya afe akiwa bado anayahitaji sana maisha yake hata wewe naona umeamua kulifanya kosa lile lile bila hata kufikiria madhara yake. Wewe ulizaliwa kunitumikia mimi na si vinginevyo hivyo unapotaka kunizunguka kuhusu jambo fulani unakuwa unajitengenezea mazingira mabaya sana hususani baina yako na familia yako. Uamuzi unao kwenye mkono wako wewe kama uniambie ukweli au wewe na familia yako hadithi yenu iweze kuishia hapa hapa na isije kujulikana mahali popote pale kwamba iliwahi kuwepo familia kama hii kwenye haya maisha” mwanaume huyo hakuwa hata na tone la huruma kwenye macho yake wala hakuwaza madhara ambayo yangetokea baada ya hapo kwa sababu alijiamini sana.

“Siku zako zinahesabika bepari mkubwa sana wewe, nashangaa sana ulifanikiwaje kupewa nafasi na kuwa raisi wa nchi hii. Unahisi ukiniua mimi ndo utakuwa umebadilisha kila kitu kwenye maisha haya? Nakuhakikishia kwamba muda mfupi tu ujao utakufa vibaya sana na utaishia sehemu mbaya kuliko hata unavyo fikiria wewe”

“Mhhhhh kuna kitu unakikosea Lingson, unahisi unanijua sana mimi, hapo ndipo unakosea. Unataka kujua labda kwamba mimi nilifanikiwaje kuingia madarakani? Unahitaji kujua kwamba labda hii nafasi nilifanikiwa vipi kuweza kuipata? Unataka kujua kwamba mimi nilifanikiwaje kwenye maisha yangu na kuwa mtu mkubwa zaidi ndani ya nchi hii? Kila unapo ona kuna mambo yanapendeza basi ujue kwamba nyuma yake kuna wanaume waliumiza vichwa vyao, ujue kwamba nyuma yake kuna watu waliwahi kipitia mateso makali sana Lingson tofauti na wewe ambaye hapo umeitwa tu ukae ukawa unavaa suti tu usielewe hizi nafasi uchungu wake upoje”

“Upo sahihi kusema huenda sikustahili kuwepo hapa nilipo kwa sababu mimi siye Boniphace Walawala, yule mjinga mimi nilimpoteza kwenye mfumo kwa mkono wangu ndipo nikaingia kwenye hii sehemu ambayo unaniona nipo na naendelea kuyafaidi mema ya nchi bila wasiwasi. Mimi na wenzangu tulisalitiwa tukiwa tumeenda kwenye misheni ya kazi huko nchini Kongo. Mimi nilisalitiwa na nchi na viongozi wote lakini hata wananchi maana tulisingiziwa kesi mimi na wenzangu na hakuna mwananchi hata mmoja ambaye alitaka kujua kwamba tulionewa au ilikuwa ni kweli ambacho serikali iliamua kutuhukumu nacho. Kuanzia siku ile ndipo niligundua kwamba kwenye maisha hakuna anayekujali zaidi ya wewe mwenyewe hivyo nilivyorudi nilikuja kuchukua kila ambacho niliona kinanifaa, sasa wewe nimekuweka hapo unaanza kunikoromea? Mimi ni komando wa daraja la juu sana ambaye nimefanya kila kazi ngumu na ya hatari unayo ijua wewe sasa utanifunza nini mimi kuhusu nchi hii? Jeuri yako leo inakuponza” alimpa historia fupi ambayo ilimuacaha kinywa wazi kiongozi huiyo asiamini kwama anayo yaongea mtu huyo yalikuwa ya kweli au alikuwa anatania tu.

Lakini akiwa kwenye huo mshangao mtoto wake mwingine alidondoka chini kwa kupigwa risasi ya kichwa huku mke wa mkurugenzi huyo akidondoka chini na kuzimia.
“Usiwaue tafadhali nakuomba sana” jeuri ilikuwa imemuishia, alitakiwa kuwa mpole huenda mwanaume huyo angemuonea huruma labda.
“Umechelewa sana Lingson kwa sababu majivuno yako yamekufanya uiue familia yako kwa mikono yako mwenyewe kwani kama ungeamua kutoa ushirikiano ambao unahitajika familia yako ingekuwa salama mpaka hivi tunavyo ongea. Jeuri ni moja kati ya vitu vibaya sana kwenye haya maisha”
“Huyo mtu ambaye anakutafuta wewe anajua kwamba una kirusi hatari zaidi duniani” aliamua kufunguka baada ya kuona kwamba mtu huyo angeimaliza familia yake yote.
“Whaaaaat?”
“Alijuaje?”
“Kwa sababu yeye ndiye ambaye alikitengeneza”
“Unamzungumzia nani labda?”

Ukurasa wa 56 sina la nyongeza.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA SABA
“Mtu ambaye anayatafuta sana maisha yako”
“Nimekuuliza nahitaji jina lake na nataka uniambie kajuaje kwamba mimi ndiye ninacho hicho kirusi kwenye mkono wangu?”
“Kumbe hata wewe unaogopa eeh?”
“Unahisi namuogopa mbwa yoyote ndani ya nchi hii labda?”
“Anaitwa Tommy” mkurugenzi aliongea kwa masikitiko sana kwa sababu alikuwa amemchomea bwana mkubwa ili apate huruma ya familia yake kuweza kuachwa hai.
“Tommy yupi?”
“Mtoto wa Apson Limo”
“Una maanisha kwamba ndiye ambaye yupo nyuma ya haya mauaji ambayo yanaendelea?”
“Ndo huyo huyo”
“Hili linawezekanaje?”
“Na huyo ndiye ambaye anajua kwamba wewe una hicho kirusi kwenye mkono wako na hata ule mkutano wako na gaidi mwenzako ambaye mlipanga kukiuza kwa bei ghali sana huko uarabuni yeye ndiye ambaye amenipa hiyo taarifa ndiyo maana nilitokea lile eneo”
“Ooooh shiit! Amewezaje kujua haya mambo yote?” aliuliza kwa ukali akiwa anamsogelea mkurugenzi huyo kwa hasira.
“Hata mimi sijui amejuaje ila anajua kila hatua yako ambayo unaipiga hivyo jiandae muda wowote kuanzia sasa anaweza kukutafuta”
“Hawezi, hawezi, mimi ndiye mtu mkubwa zaidi ndani ya taifa hili, unahisi kuna binadamu anaweza kunigusa mimi? Nataka kujua kwamba umesemaje yeye ndiye emekitengeneza?”
“Yule alikitengeneza akiwa huko nchini Uingereza”
“Ebu nipe maelezo ya kutosha, yule gaidi aliniambia kwamba kiliibiwa kutoka kwenye mikono ya MI6 sasa unaniambiaje kwamba huyo mtoto ndiye ambaye alikitenegeneza?”
“Nikikwambia hili jambo naomba umuache mwanangu aliyebaki na mke wangu tafadhali”
“Yes, natafanya hivyo”
“Tommy ni moja kati ya majasusi kutoka ndani ya shirika hilo la MI6” Hilo ni jambo ambalo lilimfanya Boniphace Walawala abaki ameachana mdomo wake tu asiamini kwamba hicho kilichokuwa kinaongelewa kilikuwa ni cha kweli maana ni kama taarifa zilikuja kipindi ambacho hakuwa amezitegemea.

“No, no, haiwezekani kuhusu hili jambo”
“Hata mimi nilipigwa na mshangao zaidi yako lakini haikubadili ukweli kwamba inabakia kuwa hivyo”
“Wewe hizi taarifa ulizijulia wapi?”
“Kwake mwenyewe”
“Anawezaje kukupa taarifa zake kiwepesi sana namna hii?”
“Tulikuwa na makubaliano ya kazi hivyo tukaamua kuelezana uhalisia wa mambo ulivyo ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja”
“Huyo bwana mdogo amefanya kosa kubwa sana, naenda kuua familia yake yote kisha nitamaliza na yeye mwenyewe”
“Usifanye hilo kosa kwa sababu kama ukikurupuka kidogo tu ana ushahidi wako mwingi sana wa mambo ambayo unayafanya hivyo inaweza kukufanya ukajulikana na dunia nzima kwamba unataka kuiingiza dunia kwenye matatizo kwahiyo unahisi ni nchi gani itakubali hilo jambo litokee? Utaanza kusakwa sana na umoja wa mataifa, kama una shida ya kumaliziana naye mtafute yeye kama yeye na sio kugusa familia yake tena kwa sababu hata sasa anajua kwamba na wewe pia umehusika kwenye yale matatizo ambayo yameikumba familia yake hivyo anakuhesabia ni siku zako tu”

“Hawezi kunisogelea mimi kwa sababu huo utakuwa mwishio wake, naenda kumtafuta kila kona ya jiji hili, naenda kumsaka kila sehemu ambayo mwanadamu anaweza kujificha na kama nikimpata basi atajuta kuzaliwa kwenye dunia hii”
“Usihangaike sana hata kumtafuta kwa sababu muda ukifika atakujia yeye mwenyewe hata hivi kama sio mimi kumuomba muda kwanza huenda mpaka sasa angekuwa amesha wafikia. Najua unajiamini sana kwa sababu humjui wala hujawahi kumuona gizani na mambo ambayo anayafanya” aliongea kiongozi huyo wa usalama huku akimrushia mheshimiwa simu aweze kuangalia baadhi ya video za marejeo ambazo zilikuwa zinamuonyesha mwanaume huyo akiufanya mauaji, alikuwa anaua kikatili sana mpaka hata kiongozi huyo alijikuta anasisimka sana.

Alitoa ishara kwa walinzi wake ambao walimshambulia mtoto wa mkurugenzi aliyekuwa amebaki kwa risasi nyingi sana hata mkewe akiwa amezimia alipigwa risasi pale pale. Lingson alishikwa na uchungu sana kwani kama kumpa taarifa alizo zihitaji alikuwa amempatia lakini bado mtu huyo akaamua kuiua familia yake yote. Hali hiyo ilimfanya ashikwe na hasira sana kitu ambacho kilimfanya awasogelee watu hao akihitaji kuwavaa lakini kabla hata hajamfikia kiongozi huyo alipigwa risasi nyingi sana kichwani.

“Nooooooo” ni sauti ambayo ilisikika juu ya fensi ya jumba hilo ikiita kwa uchungu huku mtu huyo akiwa anarusha risasi kwa nguvu, risasi ambazo ziliondoka na walinzi wa raisi watatu baada ya kupigwa kweye vichwa. Mwanaume ambaye alikuwa anapiga makelele alikuwa ni Nick, wakati anafika ndani ya eneo hilo ndio wakati ambao kiongozi wake huyo alikuwa anapigwa risasi huku akishuhudia hivyo hakuweza kuvumilia, alipiga makelele huku naye akiwa anashambulia.

Kelele zile ndizo ziliwashtua watu hao lakini walikuwa wamechelewa kwani wenzao watatu walikuwa wamepoteza misha tayari hivyo wengi walimzingira mheshimiwa huku wengine wakiendelea kumrushia risasi kwa wingi sana Nick ambazo zilimfanya arukie upande wa pili na kutoweka hilo eneo.

“Amekimbia mheshimiwa ila haweza kufanikiwa kutoka nje ya jiji hili tutamtafuta kila kona” aliongea mlinzi ambaye alikuwa ametoka mpaka nje kwenda kumsaka mwanaume huyo.
‘Ni nani huyo?”
“Ni jasusi kutoka ndani ya idara ya usalama anaitwa Matiasi ndugu. Huyu ndiye ambaye mr Lingson alikuwa akimwamini sana ndiyo maana baada ya kufika tu hapa na kuona kiongozi wake anapigwa risasi ameanza kushambulia na huyu ndiye ambaye anazijua siri nyingi sana za huyu mzee kwani ni kama mkono wake wa kulia”
“Nahitaji atafutwe kila sehemu, atafutwe kwenye kila kichochoro ndani ya jiji hili na namtaka akiwa hai huyu anaweza kunisaidia kwenye mambo mengi sana”
“Sawa mheshimiwa”
“Na kwenye hii nyumba safisheni kila kitu kiasi kwamba pabakie kama hakuna ambacho kimetokea hapa na hii nyumba kuanzia kesho awekwe mtu hapa aanze kukaa ili mtu yeyote asije akahisi jambo lolote lile”
“Nimekuelewa bosi” mheshimiwa alimaliza kazi ambayo ilikuwa imempeleka huko huku akiwa amefanikiwa kuzijua na siri kadhaa ambazo zingeenda kuwa msaada mkubwa sana kwake.

Yalikuwa ni mazoea sasa ndani ya jiji la Dar es salaam kwamba usiku hauwezi kuisha bila mauaji kuweza kufanyika. Hata siku hiyo ndani ya jiji la Dar asubuhi na mapema sana wakati wavuvi wanaelekea baharini kuweza kuifanya kazi yao, waliukuta mwili wa kiongozi mkuu ambaye alikuwa anadili na makosa ya jinai nchini ukiwa umetupwa huko na mtu huyo amepigwa risasi za kutosha. Hawakuwa na namna zaidi ya kuliripoti jambo hilo polisi na habari hizo zikaanza kusambazwa kila sehemu na kila kona ya jiji.

Kuna watu ambao walijiita kwamba wao ni wajuvi wa mambo na walikuwa na habari nyingi za nchi pia walithibitisha kwamba hata mkurugenzi wa usalama wa taifa alikuwa ameuliwa usiku huo huo. Hizo ni habari ambazo zilibakia kuwa kama tetesi tu kwenye masikio ya watu wengi kwani hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaweza kuzithibitisha moja kwa moja mbele za watu wengi. Jiji lilikuwa linaendelea kutisha kila siku ilivyokuwa inazidi kupungua na kuwafanya hata wananchi waache kabisa kujiamini huku wale waoga sana wakianza kulikimbia taratibu maana ilionekana kuwa sehemu ya watu ambao walikuwa na mabavu na uwezo mkubwa wa kuyafanya makubwa ambayo wengi hawakuwa na uwezo wa kuyafanya.

“Hivi kwa haya ambayo yanatokea nchini alaumiwe nani?”
“Ni ngumu sana kumpata mtu sahihi wa kuweza kumlaumu moja kwa moja nadhani labda ulaumiwe mfumo”
“Unahisi ni kwanini labda?”
“Kwa sababu kuna sehemu unataka kumlaumu raisi lakini unagundua kwamba hata viongozi wa huku chini wameamua kujigeuza vibaraka. Ngoja nikupe mfano, mimi niliwahi kubahatika siku moja kupata mwaliko bungeni kwenda kusikiliza, mategemeo yangu niliwahi kufikiria kwamba wale jamaa ile nafasi wanaitumia kueleza matatizo ambayo majimbo yao yanapitia, nilijua wabunge wapo pale kwa ajili ya kutoa kero za wananchi, niliamini kwamba wapo pale ili kuzipigania sehemu ambazo wanaziendesha lakini pia kutoa hoja zenye mashiko kuhusu mwelekeo wa taifa kwa ujumla ila nilichokishuhudia mle ndani ndicho kilinimaliza nguvu sana nikaamini kwamba kwenye taifa hili ili tuje kufanikiwa basi huenda kuna miaka hata mia tano mbele huko kama miaka ya hapa katikati tutakuwa tunapata viongozi wa aina hii hii”

“Kitu gani hicho ulikishuhudia huko bungeni?”
“Wabunge ni watumwa kifikra, wabunge ni watu wasio jiamini, wabunge ni vibaraka wa viongozi wakubwa lakini wabunge wengi wana uwezo mdogo sana kichwani kiasi kwamba ukimpa maiki azungumze, kwenye dakika tatu mpaka tano ambazo atatumia, dakika mbili na nusu mpaka nne na nusu anazitumia kumsifia raisi wa nchi jambo ambalo lilinishangaza mno zaidi ya sana. Kila mbunge lazima aanze kwanza namshukuru mheshimiwa raisi mara ikawa hivi ikawa vile kitu ambacho kinafanya hata hizo kero za wananchi wao zisizungumzwe tena na zinakuwa kama zinafukiwa jumla na wananchi wanasahaulika. Hapo ndipo nikataka kujua kwamba ni kwanini watu hao wanachagua kuwa watumwa kwa raisi?”

“Enhe uligundua kitu gani hapo”
“Kumbe wengi wanakuwa wanafanya hivyo ili waweze kupata nafasi mbali mbali kama uwaziri na maeneo mengine ya muhimu”
“Hilo ni jambo la hatari sana”
“Yeah ni jambo la hatari sana kwa sababu hata raisi mwenyewe anakuwa hawezi kusikia kero za wananchi kwani watu ambao wamepewa dhamana ya kuwawakilisha wananchi hao wanaitumia kumsifia yeye huku wananchi wakiwa hawana hata umeme wa uhakika, hawana huduma za maji ya uhakika, hawana huduma za barabara lakini hata mahospitali hakuna na ndio hao watu wao wanatumia muda mwingi kumsifia raisi bungeni hapo unategemea nini ndugu yangu?”
“Hapo kweli tunaingia pabaya sana”
“Hapawezi kuwa pazuri, mimi kama ningepewa nafasi ya kuishauri serikali moja kati ya jambo ambalo ningewashauri ni kwamba watoe kigezo cha mtu akitaka kuwa waziri lazima awe mbunge kwanza kwa sababu inawafanya wabunge waishie kuwasifia tu wakubwa hususani raisi ili tu awateue wale ambao anahisi kwamba wanamfaa yeye kwa sababu wanamsifia kila wakati kwahiyo anaamini kwamba wale wanao msifia watamlindia maslahi yake na atawatumikisha kadri anavyo hitaji yeye kwa sababu wanakuwa hawana kauli mbele yake”

57 niseme basi.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
Back
Top Bottom