Gaga rhino
Senior Member
- Aug 15, 2023
- 196
- 252
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja sana mkuuMzee nimeipiga mwanzo mwisho aisee huyu Tommy na Rais walawala af na harakat za Mafupa na Mpango makakati wa Oscar na vp Kirusi???? Daaah hongera Kaka nasubiri Mzigoo
Mkuu kwema? Weka hata vipande 10 pls umeniacha na arosto Kali sanaSIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA HAMSINI NA NNE
Hakuwa tayari kuweza kuitaja siri ambayo ilikuwepo hivyo mwanaume huyo alimteka mke na watoto mapacha wa Boniphace Walawala huku akimtaka aongee ukweli vinginevyo angeshuhudia mambo ya kutisha sana ambayo huenda asingeweza kuyaamini kwenye maisha yake au asingetamani yaje kumtokea lakini bado alikula msimamo na kugoma tena kusema basi mwanaume hakuwa na namna zaidi ya kumbaka mke wa kiongozi huyo huku naye akiwa anaona kwa macho yake na wanae wawili mapacha ambao walikuwa ni wadogo wakishuhudia.
Baada ya Grant kutekeleza ukatili huo kama njia ya kuilipa nchi kwa usaliti mkubwa ambao walifanyiwa pamoja na kuwapoteza wenzake watano alitaka kuua familia hiyo mbele ya Boniphace ndipo alipokubali kuongea ukweli kwamba watu hao walikuwa wanayahitaji yale madini ambayo waliyapata huko na walikuwa hawana namna nyingine ya kuyapata hivyo wao ndio ambao walicheza lile dini la kuwakamatisha watu wao huko wakijua kwamba makomando hao wakienda lazima watafanikisha zoezi hilo na kutoshtukiwa kwa sababu ingeonekana kwamba madini yalipotea kwenye oparesheni ya uokoaji ambapo hakuna mhusika ambaye angekuwa na nguvu ya kuanza kuhoji.
Baada ya zoezi hilo kuweza kukamilika waliamini kwamba makomando hao wanaweza wakaja kuanza kuhoji baadae na ikawa ni hatari kwa upande wa viongozi hao hivyo wakaamua kabisa kuwaua ili kuwapoteza jumla moja kwa moja kufanya jambo libakie kwenye mikono yao tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kuweza kuuliwa na wenzake ambapo kama bahati tu yeye pekee ndiye ambaye alifanikiwa kuishi kwenye tukio hilo.
Alilazimika pia kuwataja wenzake ambao walihusika akiwepo mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mheshimiwa raisi mwenyewe ambaye ndiye alikuwa anatoka madarakani wakati huo ambao Boniphace Walawala alikuwa anaingia madarakani. Hilo jambo lilimsikitisha sana Grant, alijua kama hadi raisi anahusika basi hilo ni tukio la nchi nzima ambalo lilikuwa limewahusisha watu wengi sana chini chini kwani raisi alikuwa anasimama kama taasisi.
Baada ya kuujua ukweli huo ndio alipo anza kujitokeza hadharani kufanya hizo interview kwamba yeye ni Boniphace Walawala na alikuwa imara japo watu walihitaji kuweza kumdondosha. Hata ile ambayo aliifanya baada ya mkewe kufariki na watoto alikuwa ni Grant mwenyewe na kwa wakati huo alijikuta anakuwa na hamu kubwa sana ya kuweza kuingia Ikulu. Jambo moja ambalo lilikuwa linamfanya asigundulike kama sio mhusika mwenyewe ni kwa sababu alikuwa anavaa manguo makubwa sana ya hospitalini kwa wakati huo hivyo mwili haukuwa unaonekana jinsi ulivyo.
Alimtesa sana kiongozi huyo lakini hakuwahi kumuua bali alimhifadhi sehemu ili ashuhudie kile ambacho angewafanyia wenzake kisha yeye angekuwa wa mwisho kutekelezewa hilo. Baada ya siku tatu matokeo yalitangazwa na Boniphace Walawala alikuwa ameshinda kwa kishindo kikubwa sana ambapo alikuwa amebakiza kiapo tu pekee aweze kuapishwa Ikulu huku akitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa akiwashukuru sana watanzania wote kwa kuweza kumuamini na kwa wakati huo hakuwa akiruhusu mtu yeyote kuweza kukutana naye bali alisema wataonana kuanzia siku ya kuapishwa kwake ambapo angeanza kuvaa mavazi makubwa mpaka pale afya yake itakapo tengamaa ndipo angerejea kwenye mavazi ya kawaida ikiwa kama ushauri kwa madaktari wake ambao walimwambia kwamba mwili unatakiwa upate hewa ya kutosha.
Hilo halikuwa jambo la ajabu kwa wananchi kwani walikuwa walishamkubali mtu wao na hivyo ndivyo mwanaume alivyo ishinda karata na kuingia Ikulu bila kutumia nguvu kwa kutumia jina la mwenzake huku mhusika akiwa amefichwa. Baada ya kuapishwa mwanaume huyo alianza kuwaua mmoja mmoja kwenye ile orodha ndefu ya wale ambao ndio waliwasaliti ambapo baadae alikuja kumalizana na yule aliyekuwa raisi ambaye alimuachia kijiti kwa kuhakikisha anachomwa na sindano ya sumu ambayo ilipelekea moyo kuacha kabisa kufanya kazi na mwisho hali hiyo ikapelekea mauti yake.
Aliendelea kuua kimya kimya watu wote ambao walionekana kuhusika kwenye lile tukio mpaka alipohakikisha amewamaliza wote. Lengo lake lilikuwa ni kufanya kisasi tu kisha apotee lakini baada ya kulionja lile joto la Ikulu hakutamani kuweza kuiachia nafasi hiyo kirahisi hivyo akaamua kuichukua nafasi hiyo mazima na kuahidi kuilipa nchi hii kadri ilivyo mletea madhara ya kuwapoteza wenzake na ndipo hapo ambapo rasmi alianza kuishi kama Boniphace Walawala kwa kisingizio kwamba ameanza mazoezi ya siri sana ili kujiweka sawa kama ushauri wa madaktari ulivyokuwa unasema na baada ya mwaka alikuwa ameanza kuvaa mavazi ya kawaida ambayo yalionyesha mabadiliko makubwa sana ya mwili wake ambao haukuonyesha mashaka yoyote yale kwenye macho ya wengi” Harper alionekana kuijua kwa undani sana simulizi ya maisha ya mwanaume huyo ambaye alidaiwa kuwa na kisasi kizito sana na nchi ambayo alizaliwa. Alipumzika kidogo Tommy akiwa ametulia kwa umakini sana kusikiliza bila kutia neno lolote lile. Harper alijiweka sawa kisha akaendelea tena.
“Kwenye harakati zake zake alikutana na mzee mmoja ambaye alionekana kumfuatilia kwa muda mrefu sana kwenye huo utafutaji wake na mzee huyo alionekaa kwamba alikuwa amemshtukia mtu huyo kwa muda mrefu sana kwa sababu Grant alimkuta mzee huyo akiwa anafanya kazi hapo Ikulu hata kabla ya ule ujio wake. Mzee huyo alimuweka wazi kwamba yeye alijua kwamba huyo mtu hakuwa mwenyewe lakini alikuwa tayari kufanya naye kazi kwa sababu hayo ambayo yalitokea hayakuwa yakimhusu kabisa yeye alikuwa anaangalia maslahi yake tu.
Grant alishtuka sana baada ya kujua kwamba ameshtukiwa lakini mzee huyo alimtoa wasiwasi na mpaka sasa mzee huyo ndiye ambaye ni mkono wake wa kulia. Mwanaume huyo anamsikiliza huyo mzee na kumwamini kuliko binadamu yeyote yule na ndiye ambaye amemsaidia kuiongoza nchi kwa miaka hii yote kumi bila wasiwasi maana yeye Ikulu anapajua vyema kuliko Grant ambaye wananchi wanamjua kama Boniphace Walawala na mzee huyo ndiye ambaye pia alimsaidia kumuua mpinzani wake mmoja ambaye alikuwa anaitwa Pandei Santo ambaye ilibakia kidogo asababishe Grant atolewe Ikulu kwa jeuri ya utajiri wa Pandei Santo lakini majivuno yake yalimfanya komando huyo amuwahishe kaburini.
Grant hakuna anachojali tena kuhusu nchi hii, hakuna kitu ambacho anaogopa kukipoteza zaidi ya kuangalia maslahi yake binafsi. Kisasi chake na wale watu kilisha isha lakini kwa sasa anaikomoa nchi ambapo amejilimbikizia mabilioni ya fedha, ana shehena kubwa sana ya dhahabu na madini mbali mbali pamoja na ardhi nyingi sana na hakuna anaye jua hili kwa upande wa viongozi wengine. Mtu huyu anamiliki watu wengi sana wa hatari, ana magenge mengi sana ya wauzaji wa madawa ya kulevya, ana watu wengi sana ambao anawaendesha na wanamtii na ndiyo maana ana jeuri ya kufanya chochote anacho kihitaji lakini kubwa zaidi ni kwamba yeye mwenyewe ni miongoni mwa wanadamu hatari sana tena zaidi ya sana kwa sababu alikuwa komando wa daraja la juu sana.
Hii ndiyo sababu ilikuwa rahisi sana yeye kuweza kufanya makubaliano na gaidi kuhusu kirusi ambacho kinaweza kuleta madhara sana kama kikiachiwa kwahiyo wao wanaamini kwamba watakitumia kuishi maisha ambayo wayataka wao japo inasemekana kwamba anaweza kumuua yule gaidi muda wowote ule ili abaki nacho pekeyake kwani kwenye moja kati ya sifa zake kubwa ni kwamba huwa hamuamini mtu yeyote yule. Huyo ndiye Boniphace Walawala ambaye huwa unamuona kama ni raisi wa nchi ya Tanzania” Harper alikamilisha maelezo ambayo yalimfanya atumie muda mrefu sana kuweza kuyaelezea na baada ya maelezo hayo kukamilika alihema kwa nguvu na kusogea kwenye friji dogo ambalo lilikuwa ndani ya chumba hicho, aliyatoa maji ya baridi na kuyanywa kisha akasogea kando na alipokuwa amekaa Tommy naye akikaa hapo akiwa amevaa bikini tu kwenye mwili wake.
Mwanamke huyo hakuonekana kuwa anabahatisha kwenye kazi yake kwani kuwa kwenye shirika kubwa la kijasusi namna hiyo kulimfanya kupata taarifa nyingi sana kwa sababu walifanikiwa kupenyeza wajasusi wao wengi sana kwenye taasisi zingine ikiwemo ya nchi ya Tanzania ambayo kwa wakati huo ilikuwa ni mhimu sana kwa sababu walikuwa wanakitafuta kirusi hicho ambacho kilitengenezwa na Tommy ndiyo maana walikuwa makini sana kuchimba kila taarifa ambayo ingeonekana kuwa mhimu kwao kwa wakati huo.
“Kuna muda unanitisha sana, najaribu kuwaza mpaka inafika sehemu nahisi kuna mambo mengi sana ambayo huenda mimi siyajui kabisa kuhusu wewe, nashindwa kuelewa kwamba hizi taarifa huwa unazipata wapi H2 kwa sababu haya mambo ambayo umeniambia licha ya kuwa ya mhimu sana lakini ni taarifa za siri sana ambazo haziwezi kupatikana kirahisi na sio taarifa ambazo kila mtu anaweza kuzipata”
“Kama nilivyokwambia mwanzo, sisi ni moja kati ya mataifa makubwa ambayo yamepiga hatua kubwa sana kwenye kazi za kiitelijensia hivyo tangu muda mrefu sana tulisha wapenyeza watu wetu huko ndiyo maana kuna taarifa tunakuwa nazo ambazo unakuta hata mashirika ya kijasusi ya nchi husika yanakuwa hayana”
“Nimekuelewa vyema sana lakini sijajua sababu ya wewe kuniambia habari hizi ambazo hakukuwa na ulazima kwani sikuwa nimeomba uniambie haya. Sasa ni kitu gani ambacho unahisi kinakufanya uone mimi nastahili kupewa taarifa za ndani sana kama hizi ambazo huenda kama viongozi wako wakijua kwamba umenipa zinaweza kukuletea matatizo?”
“Kwa sababu nakupenda T1, mimi nipo tayari kukutwa na jambo lolote lile kwa ajili yako, nipo tayari hata kuachana na kila kitu kwenye maisha yangu kwa ajili yako. Najua ipo siku utakuja kunielewa na kunisamahe moja kwa moja kwenye moyo wako na ndio huo muda ambao mimi nausubiri sana kwenye maisha yangu hata ukichelewa”
“Tuachane na hayo kwanza, kwa mtazamo wako unahisi kwamba ni kwanini ameamua kuweza kukiachia kiti cha uraisi kirahisi sana namna hiyo wakati ndiyo sehemu ambayo angeweza kuendelea kuitekeleza hiyo adhma yake ya kuweza kuendelea kuilipizia nchi?”
“Kama nilivyokwambia kwamba huyu mtu ana mtu wake wa pembeni ambaye ndiye mkono wake wa kulia yaani kiufupi ni kwamba huyo mtu akili yake ndiyo ambayo Grant anaitumia ili kuweza kutekeleza yale ambayo anahisi kwamba yanamfaa na yana manufaa makubwa kwake. Inasemekana japo bado haijathibitishwa kwamba kuna mtu miongoni mwa wale ambao walimletea maafa kwenye maisha yake ana kisasi naye binafsi yeye kama yeye achana na kile ambacho kilitokea kwa wenzake”
“Umeniacha kidogo hapo sijakuelewa unamaanisha nini?”
“Upo sahihi. Kwenye simulizi ya maisha yake kuna sehemu sijaigusia nimeiruka, mwanaume huyo kwenye harakati zake za kulitumikia taifa ambazo zilimfanya kuwa mtu wa kutembea tembea sehemu nyingi sana alifanikiwa kukutana na mwanamke mmoja mrembo sana ambaye alikuwa na asili ya nchi ya Rwanda. Watu hao walipendana sana tena zaidi ya sana, wakafanikiwa kupata na mtoto kabisa hivyo kiufupi naweza kusema kwamba mwanamke huyo alikuwa mkewe japo jambo hilo hakuwahi kuliweka wazi”
Ukurasa wa 54 naweka kalamu chini.
Wasalaam,
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Watanzania tunafeli wapi mkuu?[emoji848] Yaani huwezi kuwaza kwamba atleast nimuunge mkono mwandishi kwa muda wake ila unawaza tu ufutwe.