Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea


Mkuu Masatu,
Mpaka wanaleta ombi la kununua mitambo ya Dowans, hakuna aliyekosa. Hayo yalikuwa maoni yao. Ila ilipokataliwa wakabweteka. Hapa WAKOSAJI ni wote. Idis kwa kutokutafuta PLAN B. Wabunge kwa kutokutafuta jinsi ya kurahisisha ununuzi wa mitambo mipya, Rais kwa kutoinglia kati swala linaloweza kuharibu uchumi wa taifa, Waziri kwa kutokumshauri Rais ........ Tanesco kama Tanesco hawana ubavu. Wamebanwa kama mjusi kwenye mlango na macho yamewatoka. Wanaangalia tu jinsi Mafahali wawili wanavyogombania KULA na mmoja akitaka kuzuia na mwisho inakuja kukomoana. Kama ingelikuwa wakati wa uchaguzi, ingelikuwa safi sana. Mwendo huu huu hadi mwakani..... watu waje wabebe misalaba yao wenyewe.
 
If Tanzania cannot get out of power problems then we shouldnt even exist as a state because to be honest its ridiculous! We are surrounded by more water than any other country on the continent and in addition to this we have massive gas deposits. This problem is easily resolvable (in the long term of course) that it is should not be a problem in the true sense of the word. The only thing of course is to behave in a more resposible way like NOT putting people like ngeleja in these positions. The man is a stooge and the country's energy sector is not VODACOM. This is the main problem with us. We are led by imbeciles.
 

Hapana mkuu, kununua mitambo ya Dowans sio muarobaini wa tatizo la umeme. Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco mitambo ya Dowans ni suluhisho la muda mfupi tu wakati mikakati ya muda mrefu kinafanywa.

Tusidhani kununua mitambo ya kuzalisha umeme ni sawa na kununua standby gen set unanunua na kufunga siku hiyo hiyo. Suala lina mapana marefu na ukijumlisha na hiyo sheria ya PPRA ndio linakuwa gumu zaidi.

Ufupi ni tumewapiga kumbo wataalamu wetu tunaona haya kukubali ukweli huu
 


Mkuu Plan B ipo underway itachukua more than a year kupata mitambo ya kudumu kutokana na sheria ya PPRA. Hilo la Dowans was not even plan A lilikuwa ni emergency Plan
 
Nyie wote mnaofikiri kununua mitambo ya DOWANS ni kumaliza tatizo la umeme Tanzania, nasema hivi:

"Nyie ni sawa na Mwanamke/Gigolo au SHOGA anayefuatwa na mteja ili atoe huduma ya mapenzi bila Condom huku akijua kabisa jamaa ana UKIMWI".
Ukiulizwa unasema "heri nife kesho kutwa na ukimwi, kuliko kufa kesho na njaa".

Kibaya zaidi ni kuwa, ulifahamu kuwa pesa na unga ndani vinaisha na wewe ukakaa bwerere kwa kisingizio kuwa "ilikuwa uende kwa jirani kumtoa mwali" na hivyo ukawa umechoka kwenda kazini.......
 


JF Home Of Great Thinkers!
 


Ha ha ha ha! wewe naona sasa umeshakuwa ni kichekesho. Unajitahidi kadri ya uwezo wako kutaka kumtetea huyu fisadi Idrissa Rashid ambaye alistahili kufukuzwa kazi siku nyingi zlizopita kwa kushindwa kazi pale TANESCO na pia kustahili kuchunguzwa kwa kuhusika kwake na ufisadi wa rada, lakini badi umekazana tu na juhudi zako sijui umeahidiwa nini na papa fisadi Rostam ikiwa mitambo yake ya kifisadi ya Richmond itanunuliwa na TANESCO. Juhudi zako haziwezi kufika mahali popote huyu fisadi Idissa Rashid na yeyote yule anayetetea ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya RA wamechemsha sana na Watanzania tumeshaamka kutoruhusu manununuzi yoyote yale ambayo yana harufu kali ya kifisadi. Endelea na juhudi zako za kumtetea fisadi Idrissa Rashid, lakini ujue kamwe hazitafanikiwa.
 

.....wewe bado unaishi kwenye ujima,nenda kawadanganye wale mnaowahonga pilau na madebe ya pombe na usisahau kwa sababu zisizozuilika na kwa usalama wa Taifa!
 
Mkuu Plan B ipo underway itachukua more than a year kupata mitambo ya kudumu kutokana na sheria ya PPRA. Hilo la Dowans was not even plan A lilikuwa ni emergency Plan

Kwa nini emergency plan isiwe kwenye kununua mitambo HARAKA kwa kuruka hizo sheria za PRRA? Si wangeliambiwa Wabunge, Rais na PM kuwa inabidi TUVUNJE sheria kwa serikali YENYEWE kwenda kununua mitambo na wenye mitambo kutoa guarantee na si kusubiri TENDA? Tenda ingelikuwa ni kwa wenye mitambo moja kwa moja na kazi ifanywe na watengeneza mitambo na wahandisi wa Tanesco. Kuna mtu angelalamika kuvunja sheria? Kama wangelitaka, amini sasa hivi mitambo mipya ingelikuwepo.
 
JF Home Of Great Thinkers!

Habari ndiyo hiyo. Dowans ni kama bwana/bibi mwenye ukimwi. Halafu mtu anakuja anasema nenda kampakate/kapakatwe na huyo jamaa mwenye ukimwi na tena pekupeku. Hii Raha ya siku moja, itatupa matatizo mengine mengi zaidi mbele. Mwanakijiji alishatuandikia hapa kuwa hiyo mitambo ilinunua na pesa za Bank. Sasa wenye bank wakija kudai mitambo yao na wakati huo sisi tumenunua, MTASEMA nini?
 

Totally nonsense, rubbish... wewe unawatetea mafisadi tu,,, huna lolote
 
Hata watu wale majani, ndege ya rais itanunuliwa!

Hata watu wale mchanga, rada mpya itanunuliwa!

Leo inakuaje watu wanakubali kuwasha vibatari ili mitambo mipya inunuliwe lakini serikali haiko tayari kununua mitambo mipya ila ya DOWANS ndio ya kununua?

Nani ni mtendaji mkuu wa Tanesco? Naona kila mtu anashauri tu!

Dr. Iddrissa anashauri, Kamati ya bunge wanashauri, sasa nani ni mtendaji hapa Tanesco? Kuna haja gani ya kuwa na DG kama hawezi kuwajibika?

Kama wizara ndio wanawajibika, Ondoa cheo cha DG acha wataalamu wamshauri waziri na katibu mkuu.

Kuwa gizani sio sababu ya kununua Dowans. NO WAY!
 

Hicho unachoshauri hapo juu ndicho kilichofanyika kwenye Richmond matokeo yake ni history....

Bado nasisitiza kununua mitambo hii si sawa na kununua standy gen set la nyumbani kwako. Kutokana na ukubwa wa gharama zake huwezi ukakurupuka tu
 
.....wewe bado unaishi kwenye ujima,nenda kawadanganye wale mnaowahonga pilau na madebe ya pombe na usisahau kwa sababu zisizozuilika na kwa usalama wa Taifa!

Umesikika mkuu, hukuwa na haja ya kutoa mipovu yote hiyo hata hivyo
 

Is that all?
 
Masatu,
Mkuu nilishasema kama mnataka generator semeni na sisi tuifanye kazi... Nimetoka kuzungumza na mtu wa kampuni hii sasa hivi na kanambia mzigo upo tayari kinachotakiwa ni ndululu tu...Haya maswala ya gari sijui baiskeli yametoka wapi?.. si maneno yenu ya kutunga kuwazuga wadanganyika! generator ya Mw 100 wanayo pia..
Sasa ikiwa mtambo wa Richmond ulikwisha fungwa na kutayarishiwa sehemu iweje kazi hii iwe kubwa..Mkitaka isafirishwe kwa ndege inawezekana, kazi kwenu..
Haya jaribu wewe site yao ni hii hapa. Bofya
 
Hicho unachoshauri hapo juu ndicho kilichofanyika kwenye Richmond matokeo yake ni history....

Bado nasisitiza kununua mitambo hii si sawa na kununua standy gen set la nyumbani kwako. Kutokana na ukubwa wa gharama zake huwezi ukakurupuka tu

No Mkuu,
Richmonduli sheria zilipindwa na kila sehemu. Kama ingelikuwa imefanywa kwa uwazi ili kuleta hiyo mitambo na hilo lifanywe moja kwa moja sidhani kama lingelikuwa na ubaya. Usalama wa taifa, Wazuia Rushwa, Upinzani, Bunge, Tanesco, Rais, Waandishi wa habari kama wangelijulishwa na kuonyeshwa mpango mzima wa kununua mitambo kutoka kwa watengenezaji moja kwa moja na mwenye UBISHI basi aende KIWANDANI kuhakikisha, sidhani kama hili swala lingelileta ubishi.

Sasa unataka kusema Richmonduli lilifanywa kwa faida ya Mtanzania, basi naona tunaongelea kwenye ANGA mbili tofauti na NINANAWA mikono.
 

Bora Mkuu Sikonge umeamua kunawa mikono, Nakuunga mkono katika uamuzi huo.
 
Mnapoteza muda na huyu kada na shati zake za njano na kijani,yeye mwenyewe usikute anaishi gizani lakini haoni!
 
Kisha jamani sii hawa Dowans waliuweka huo mtambo kuuza huko Kijiji.com kama miezi sita iliyopita?.. kama haukununuliwa huko kwa walalahoi bado tunapigishana kelele hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…