Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea

Naona swala la kwanza la Tanesco wamechukua hatua gani limeshajibiwa. Sasa swali langu la pili la serikali imechukua hatua gani linahitaji kujibiwa maana niliuliza maswali matatu huko siku za nyuma.

Jibu la swali lako ni kuwa kamati ya Bunge iliridhika na namna serikali ilivyotumia fedha katika kufuatilia suala hilo.
 


Te he he! Waambie!
 
Ngekewa,
Mkuu kazi yote hii tunayoifanya hapa ni kuunyesha Umma kwamba tuna viongozi wabovu.. bahati mbaya wapo watu wanaofikiria tofauti na kibaya zaidi ni pale baadhi ya wajumbe wetu kwa upande wa Upinzani tuna kina Zitto na Lipumba wanaafiki upumbavu huu ati kwa maslahi ya Taifa.. sijui kama wanaelewa haswa maana ya maslahi!
 

Wakulaumiwa ni wanasiasa "maslahi" kina Sitta na kundi lake.
Hivyo vitisho vyote vilivyotolewa na wababe hao hukuvishuhudia hata kuwapaka lawama Serikali na Tanesco?
Hivyo kwa akili yako hiyo mitambo iliyokwishakula fedha za Watanzania ni haki ya nani kama si Watanzania waliotowa Fedha zao?
Tulikuwa na haki ya kuitumia mitambo hiyo hata kama kwa kuitaifisha, sasa wapi hao wababe wwako walitowa ushauri utakaowezesha Watanzania wafaidi kile ambacho walitapeliwa? Au hadi sasa wanasemaje ? Tunachotaka ni umeme na wala sio siasa kwani hata wao tuliwachaguwa ili watuletee maendeleo na sio kuturudisha nyuma kiasi hiki. Wababe hawa wanastahilki kuwajibishwa kama walivyofanywa walwe wa Richmond.
 

Hivi kweli Babu unataka kunieleza kuwa huoni seriousness ys hili tatizo kwa nchi na mawazo yako yote yameishia kwa Rostam? Huyu Rostam atawalipa watu wangapi? Loo kazi bado ipo kwa wa TZ na Iddi Simba yuko right.
 
Wanacho taka mafisadi ni kuinunua hiyo mitambo na sio kuitaifisha kama wewe unavyosema, ukitaka suala la kutaifisha, huna budi ufuate mchachato wa akina Sitta yaani wafuate maazimio ya Bunge waliofanya makosa wadhibiwe, watoe report ya kweli ya kiasi nchi ilizopoteza kwenye huu mkataba, aliyekuwa anachukua pesa tanesco ajulikane, ndio litafuata suala la kutaifisha kinyume cha hapo itakuwa hadithi za abunuwasi.
 
Totally nonsense, rubbish... wewe unawatetea mafisadi tu,,, huna lolote

Labda mwenzangu huelewi maana ya extract. Hayo maneno si yangu ni ya wale waliyoyasema wakiwemo hao hao unao watetea. Lete hoja ndugu.
 


Sawa iwapo unataka lazima tukubali kuwa Kikwete mwenyewe anahusika na hili tatizo la umeme lakini ningeomba nizungumzie mambo machache ambayo hukuyatilia maanani wakati ukilenga hizo lawama zako.
Kwanza hili tatizo la umeme kwa Tanzania halikuanza katika kipindi cha Kikwete bali limekuwepo kwa muda mrefu lakini kwa wakati huo hatukuwa na uhuru wa kusema kama wakati huu wa Kikwete. Msingi wa umeme wa Tanzania ni maji ambayo ni matokeo ya maumbile yaliyo nje ya Kikwete au mwengine yeyote. Ni miaka minne tu tangu Kikwete achukuwe madaraka na ilichukua chini ya mwaka mmoja kukabiliwa na tatizo la umeme, suala jee ni mchakato gani endelevu uliowekwa na hao waliomtangulia Kikwete?
Pili, si tulikwishajuwa kuwa mitambo ya Dowans ililetwa kitapeli, sasa wasiwasi wwetu ulikuwa wapi iwapo tulikwishadanganywa huko nyuma lakini sasa tungeingia katika mchakato wa kuangalia faida ya mitambo hiyo huku tukijiepusha na kudanganywa tena? Labda lengo letu lilikuwa kuona kuwa ile mitambo haitunufaishi sisi na badala yake kumtia adamu mmiliki wake? Nafikiri wakati wa kujitowa muhanga kijingajinga kama huku umeshapitwa kwani ile mitambo tulikwishaigharamia na ingekuwa jambo la busara kuitumia baada ya kuhakikisha kuwa hakuna udanganyifu mwengine.
Tatu nafikiri umeshafika wakati kwa Watanzania kupokea maonyo na ushauri kutoka kwa anaeonya kwani Wabunge wetu walikuwaq wakali kuonya lakini wakakaidi hata shauri za wataalamu na wala hawakutoa mapendekezo ya kuepusha hali hii na badala yake sasa ni kutafutana uchawi.
 


Waswahili husema 'mnyoge mnyongeni na haki yake mpeni' Hivyo Bunge tukufu lina watu wangapi? wanapi maprofesa? na wangapi wataalamu wa fani mbali mbali? Hivyo huyu Rashidi mmoja baada ya Watanzania kungamuwa kuwa kawekwa na mafisadi ameweza kuwashinda akili wabunge wote kwa kutowa pendekezo ambalo kutotekelezwa kwake kumetokea yale aliyoyatabiri?
Ni ufinyu wa akili zetu zilizolemazwa na masilaha ya kisiasa uliotufikisha hapa na kumlaumu Rashid ni kupungukiwa na hoja. Kwani si alikwishatuonya iwapo ni fisadi au ni shujaa si issue, issue ni jitihada na mawazo gani yalifanywa kucounter huo ufisadi wa Rashid.

Nionavyo mimi kilichokuwa muhimu kwa Wakubwa wetu wakiwemo wabunge walikichukulia hatuwa muafaka kukipata, si hatuoni maboresho ya maslahi yao?
 

Nafikiri una bifu hapo! Kwanini hatuzungumzii giza tulilonalo na tunarukia mengine? Kila jambo kina wakati wake la tutatengeneza mseto usoeleweka.
 

Hatujanunua hiyo mitambo kama unavyoshauri wewe mwenye akili timilifu, jee huo mgao haupo?
Pengine ungenunuliwa huo mgao usingekuwepo.
Halafu siasi tulionafikira unazozibeza hizo ndio fikira zetu sasa zenu na kina shelukindo ni zipi ilikututowa kwenye tatizo?
 
Bob,
Yaani inashangaza sana mkuu.............watu hawaoni wala hawakumbuki............. Hii kitu Dowans naona watu wamelogwa nayo.................tulishasema hapa Mafisadi walifanya na wataendelea kushirikiana kwa makusudi ili tuingie gizani................

.........kuna mtu eti kasema Richmond ni ilikuja kwa sababu ya ubovu wa procurement procedures zetu............sijui huyu mtu kama alisoma maelezo ya kamati ya Bunge kuhusu mchakato ulivyokuwa..........yaani watu wankumbatia ufisadi hivi hivi unaona...............inaudhi sana kwa kweli
 

Wewe unaefikiria kuwa utapata umeme kwa maneno matupu ni sawa sawa na mwanamume goigoi usieamuwa kuowa ati utatekegemea kutoka kwa wa wenzako utakufa na haja zako. Ujanadume ni kujitowa muhanga na kukabili vikwazo.

Eti tusinunue mitambo na huku hatuna uwezo wala utaalamu wa kupata mitambo mengine na bado tunawategemea wale wale tukiowakatalia ushauri wao ni kichekesho cha mwaka. Tanesco na Rashid kama tuliwaona kuwa wanatupeleka siko basi tunge kuwa agressive katika ktutowa ushauri na mapendekezo na sio kupogozwa shuka na kungojea mke wa jirani apite.
 

Mkuu mbona unashuka hadhi kiasi hiki? Hivyo hoja hapa ni Rashid peke yake? Kwa hadhi yako sikutegemea kuwa utakuwa rahisi hivi. Kama Rashidi alikuwa ana tuhuma au la haitusaidii sana kwa hili tatizo kwani Rashidi ni mtu mmoja na kutowa nguvu zako zote kumlega yeye bila kutupa ushauri wa kutoka katika janga hili utakuwa hutusaidii kitu.
Unataka tuamini kuwa hili suala ni la one man show/ Mkuu tunategemea busara zako katika kututowa katika kiza na sio chuki binafsi.
 
.....wewe bado unaishi kwenye ujima,nenda kawadanganye wale mnaowahonga pilau na madebe ya pombe na usisahau kwa sababu zisizozuilika na kwa usalama wa Taifa!

Haya tumeyazowea! Pasipo hoja basi huko ndiko mnakotupeleka. Aibu lakini.
 

Haya ni matokeo ya LAITI!
 

Naona sababu zinapunguwa kutoka ufisadi na kuwa ukimwi na mali ya Benki , sijui hiyo Benki ni ya Obama?
 

Angalau una msimamo iwapo si mtumiaji wa koroboi kama mimi.
 

Sasa iwapo nyie mnachukuwa wajibu wa kuelimisha wananchi waingie kizani na mnahisi mna haki kwanini mnawaona kina Zitto hawana haki ya kuwatakia wananchi umeme? Lengo langu ni kuwa tuwe na hoja katika mawanzo yetu na sio kushabikia eti jambo limefanywa na watu fulani tunaowapenda au kuwachukia.
 

Na hilo linashindikana vipi wakati"mna" ushahidi wa hayo mnayoyaeleza?
Iko wapi hiyo good will ya kina Sitta iwapo wana ushahidi lakini wananyamaza na kuipeleka nchi kwenye kiza?
Uambiwapo lazima nawe ujiambie au utawala bora uko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…