Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea


Mkuu wangu nakuomba unisome vizuri na pengine wote ambao mnakubaliana na hoja hii au kupinga ni muhimu sana kusoma maeleoz yangu yafuatayo kwani inaonyesha wazi tunabishana tuuu pasipo kuelewa taratibu za kiuchumi na maendeleo.
Mkuu nitarudia tena kusema kwamba mimi sii msomi kuliko viongozi wetu tena naweza sema ni mbumbumbu ktk taaluma ya Umeme na uongozi, lakini hoja kubwa ya mjadala huu haihusiani na Utaalam isipokuwa ku Solve TATIZO la Umeme.
Hapo nyuma nimekwambia kuhusu MAHITAJI yetu ya Umeme ambayo mikakati imekwisha jengwa na serikali yetu (serikali ya Kikwete) ilipoingia Ikulu. Na katika mikakati hiyo ya MAHITAJI yetu, ambayo ipo ya muda mfupi namuda mrefu (short term/long term), huo umeme wa Richmond/ Dowans haupo ktk mipango hiyo (strategically). Nakuomba elewa hilo kwanza.
Mtambo wa Richmond/Dowans ulikubaliwa au kuletwa nchini kama mtambo wa dharura kutokana na upungufu wa umeme nchini kutokana na mabwawa yetu kutotoa umeme jambo ambalo lilisababishwa na miradi hiyo kutegemea mvua..Sawa na wewe leo hii ukanunue kibatari sokoni kutokana na umeme kukatika mara kwa mara au wananchi na wafanya biashara wanapo nunua generator zao binafsi.

Kwa hiyo basi ndio kusema kwamba mipango ya serikali kuboresha mahitaji ya umeme nchini haijapatiwa ufumbuzi hadi leo kwa muda wa miaka minne na ahadi zote alizotoa rais wetu Kikwete alipoingia madarakani ni ahadi hewa iwe kwa short term au long term isipokuwa leo hii kumewekwa ktk wakati mgumu wa kutegemea kuendesha uchumi wa nchi yetu kwa kutatua TATIZO tukitumia vibatari au generator as a short term strategy..Yaani umeme wa dharura unageuzwa kuwa ni mpoango wa muda mfupi ktk maendeleo ya mahitaji yetu ya umeme.

Ndipo napokuja na hoja yangu kubwa na ya msingi kiutalaam ktk Mahitaji.. Richmond/ Dowans wameingizwa nchini kuondoa tatizo la umemem uliopungua kutokana na mvua chache zilizonyesha wakati wa Utawala wa Mkapa, Tukaweza ku identify PROBLEM hiyo na kwa haraka tulitoa tender ili kukabiri tatizo hilo la muda..Tatizo ambalo ni nje ya hesabu ya MAHITAJIi yetu ya Umeme.
Meaning kama (mathlan) MAHITAJI yetu ya Umeme ni Mw 1500, vyanzo vyetu vya umeme vulikuwa vikifua umeme wa Mw 900 hivyo hesabu pungufu ni Mw 600 ambazo mikakati ya serikali ilikuwa imejengwa kukidhi mahitaji hayo na ya ziada kulingana na ongezeko la watu na matumizi kila mwaka.

Nitarudia kusema Dowans haikuwepo ktk hesabu hii ya upungufu wa megaWatts 600 za mahitaji yetu, isipokuwa inalenga kutatua tatizo la ambalo vyanzo vyetu vilishindwa kuzalisha zile Mw 900 kutokana na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mvua kutonyesha. Tuseme tena mathlan vyanzo vyetu vilizalisha Mw 700 hivyo tulipatwa na tatizo pungufu la Mw 200 na ufumbuzi wa haraka ili tupate kufidia pengo hilo la Mw 200 ndipo mashirika haya yalishinikizwa kuingia mkataba kuziba pengo hilo la Mw 200.

Lakini kwa bahati nzuri mvua zilirudi kunyesha na mabwawa yetu yakajaa maji hivyo kibatari hiki cha Dowans hatukukihitaji tena..case closed...hatukihitaji tena kibatari kulingana na mipango ya serikali ya muda mfupi na mrefu KAMA ingeanza mara moja kufanya kazi..
Lakini serikali kwa Ufisadi wake wamegeuza mradi wa Dowans na mashirika mengine yaliyoingia nchini kama suluhisho la TATIZO la umeme kuwa ndio mpango wa muda mfupi ktk MAHITAJI yetu ya Umeme. Mtu kama Dr. Rashid anaelewa ukiritimba na pengine ubovu wa serikali yetu ktk kupanga na kutambua mahitaji ya nchi yetu ambayo leo hii kwa mfano wa hapo juu umefkia pengine Mw 2000 na haoni kabisa mpango wowote wa kutuwezesha kufua Mw 2000 au hata robo tatu ya mahitaji hayo. Ndipo naye anacheza na mzee kuturudishia Kibatari kwani sii kazi yake kuhakikisha nchi ina umeme ila ni kazi yake kusambaza umeme ulkiopo.

Kwa kumalizia mkuu wangu nakuomba sana fikiria kwa makini kuhusiana na hiki kibatari cha Dowans, tulikihitaji tu ikiwa umeme utakatika lakini yaonyesha wazi mwenye nyumba Kikwete na serikali yake hawana mpango wa kutuwekea Umeme ktk nyumba yetu.. na The only solution kwetu sisi kama watoto wa mzee Kikwete hatutaki kutumia kibatari, acha iwe kiza nyumba nzima hadi mzee wetu atakapo tambua kwmba Umemem ni ktk MAHITAJI ya nchi yetu ili tupate kuendelea lakini sio kutumia kibatari au mchumaa.. na kwa sababu ya Ufisadi unaoendelea. viongozi wetu watakuja fikiria kwamba sisi tumesha zoea vibatari na mishumaa, kupika kwa jiko la mkaa na kadhalika. Umeme hautawekwa na ndiyo yatakuwa maisha yetu (kimaendeleo).
Sijui kama umenipata mkuu wangu!
 
Eti

  • Hatuna umeme kwa sababu hatukununua mitambo ya Dowans !
  • Tunaendelea kukaa gizani kwa sababu tuliikataa mitambo ya wizi !
  • Tunateseka kwa sababu tuliwatolea nje matapeli na mafisadi !
Halafu eti

  • Tulikataa ushauri wa jizi lililobobea kwa jina likiitwa Rashidi !
  • Na sasa tunakula matunda ya jeuri yetu ya kususia mali ya wizi !
  • Na humu JF sasa mafisadi na maswahiba wao wanasherehekea hali hii !
Hakika inatisha eti

  • Tanzania sasa itabidi tule matapishi yetu kwa kununua hiyo mitambo !
  • Na tuwasulubu wote waliotetea maslahi na heshima ya taifa !
  • Na Jf itumiwe kupigilia misumari kwenye jeneza la wazalendo hawa !
Mwisho nakata tamaa eti

  • Nchi yangu kipenzi imewekwa rehani na wezi na wahujumu !
  • Wanatuibia usiku na mchana wanaendelea kutamba mitaani !
  • Huku viongozi tuliowachagua wakiendelea kuwalamba miguu !
Inasikitisha ! Dowans - who is Dowans !

 


"ACHA NCHI IINGI GIZANI NA LIWALO NA LIWE"-HARISSON MWAKYEMBE

Hivi jamaa (Dr. Mwak) kajichimbia wapi? Mbona siku hizi hasikiki? Kama position ingekuwa reversed yaani Zitto akawa ndiye aliyepinga mapendekezo ya Tanesco na Mwakyembe akawa ndiye aliyeunga mkono, hivi hali ingekuwaje?

Nionavyo mimi na jinsi ninavyowafahamu wote wawili, Zitto angejitokeza kuomba radhi umma na Mwakyembe angejitokeza kujigamba na kutamba saaana.
 
naona suala la umeme wanasubiria yule owner wa chelsea au mwekezaji yoyote yule wa nje akishirikiana na wandani sasa taratibu za kuwaweka sawa ndio tatizo mpaka mradi uanze, maana kwa akili nzuri tu, hakuna sababu ya kutoanza kutekeleza miradi hiyo ya umeme iwe muda mfupi na ya muda mrefu.
 
MKuu hapo nadhani umemaliza yote, maana haingii kichwani eti leo hii tuseme Dr Rashid alikuwa right wakati tunajua kuwa ni fisadi namba moja na amwezesha dili chafu ikiwa ni pamoja na dili lile la rada, mpaka ametajwa kwa jina katika ripoti ya SFO ya Uingereza. Sasa kama tunajua ni fisadi tujue hatuwezi kuamini chochote anachokisema.
Alafu Mzee Mkandara umeongea kitu cha maana sana, hicho kibatari cha Dowans ni short term solution, sasa tunaigeuza kuwa ndi long term investment alafu Zitto na Rashid wanataka tuliamini hilo. Inasikitisha kutaja jina la Zitto in the same breath as Rashid.... ni aibu kwa Chadema!
 
mashirika ambayo ubinafsishaji wake ulitakiwa au unatakiwa kuangaliwa kwa makini na ikiwezekana kubaki mikononi mwa serikali ni umeme, reli maji, na mafuta na kama yakibinafsishwa sio kwenye eneo ambalo linaweza kuangamiza nchi, yaani tunakuwa mateka wa wawekezaji?
 
Susuviri,
Mkuu afadhali hata ingekuwa short term strategy ktk MAHITAJI yetu ya Umeme. Kibatari cha Dowans kilikuwa ni mpango wa DHARURA kifidia upungufu wa Umeme ulotokana na mabwawa kukosa maji ya kutosha..
Ushauri wa baraza la mawaziri ulikuwa mzuri, ushauri unatazama mahitaji yetu na kuunganisha na tatizo la umeme pungufu, hivyo tungeweza kuua ndege wawili kwa mara moja lakini Lowassa na wahusika wake walichagua njia ya mkato, njia ambayo ingewaingizia fedha kinyume cha matakwa ya bunge na baraza..Ndio tunapowakuta hawa Dowans, watu wasiojulikana wala kutambulika wameingia kihuni kihuni na kibatari chao. Licha ya hivyo serikali na wabunge wetu wamekwisha ona hasara kubwa zinazotokana na vyanzo hivi nya kina IPTL, Songos, na hata Watsila. Hivyo kuimarisha Tanesco kuwa chombo cha ufuaji umeme kuwa ndio solution. halafu basi badala ya kuanza vizuri tunaanza na kununua kibatari!. megawatts 100 kwa shirika la Taifa kama Tanesco ni matusi makubwa hata kujadili.
 
idrisaa hawezi kuwa sawa au sahihi na kamati kuwa walikosea kwa sababu mtoa hoja na idrissa wameshindwa kuelewa jambo moja katika sheria, ya jambo kuwa kamilifu kisheria basi mlolongo wake wote unatakiwa uwe na uhalali kisheria, ama sivyo jambo hilo linakuwa void ab initio
<LI class=g>Void (law) - Wikipedia, the free encyclopedia

The term void ab initio, which means "to be treated as invalid from the outset," ... Void ab initio. A contract is null from the beginning if it seriously ...
en.wikipedia.org/wiki/Void_(law) - Cached - [ame="http://www.google.co.ug/search?hl=en&ie=UTF-8&q=related:en.wikipedia.org/wiki/Void_(law)"]Similar[/ame]
<LI class=g>Legal Definition of Void or Void Ab Initio

intio<LI class=g>sasa idrissa na u'dokta wake pamoja na kegal team ya nchi yetu yote hili hatulioni?/?/
 

Mkuu Joka.....heshima mbele
tuko ukurasa mmoja mkuu..........watu wanafikiri wengine tukiwa nje ya nchi ya kwamba hili jambo halitugusi............shame on them
 

well said mkuu.............kuna watu wameziba masikio...........too bad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…