uhuru tech
Member
- Apr 16, 2017
- 48
- 52
Ila kumrecod mwenzako na kutuma kwenye mtandao si vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nchi kumbe humu wengi maofisini wa hovyo tu kaahhh....mnamtetea rose kabisa?kosa la James ni lipi?
Tuwe wazalendo bwana
Mkuu inshu ya James haikuwa ya udume zima kama ulivyomuelewa. Inshu yake ilikuwa ni afya za watz, alituonyesha in backyard ambako hatuna access nako pakoje. Yule Rose anawakilisha wahudum wengi sana ambao wanatuhudumia kwenye ofisi za umma, hawana utu wala ubinadam. Wamejaa visilani na hawajali afya zetu. Kwenye clip Rose alisisitiza wagonjwa wachomwe hivyo hivyo hatakama zimexpai. Utetezi wa FIFO na FEFO ni sawa na TRUB na TRAT.My Take
Nilijua tu yule jamaa ni mzushi, dume zima unakaa kurekodi watu. Kama mwanaume si upeleke kwenye vikao?
Swali hili hata Mimi nilijiuliza maana camera imemlenga dada sawia lakini dada haioni Wala hashtuki kuwa anarekodiwa.Ni kamera ya kifaa kipi iliyotumika kumrekodi?, kama ni sim ya mkononi si angeona kuwa jamaa anamrekodi. Wataalam mnisaidie
Hili nilitabiri mwanzo kabisa mwa sakata baada ya mkuu wa hospitali kutoa maelezo kama alivyoeleza mtoa mada.James akiambiwa atoe ushahidi atabaki kubabaika kuwa niliona, niliona!
Angetakiwa awe mjanja, awe na Akili, Akili yake, iende mbali.
Kama aliamua kufanya kitu angefanya kweli.
Angerekodi kwanza hivyo vifaa vilivyo-expire kisha ndio akamrekodi huyo Bidada.
Lakini Kwa vile anaakili ndogo, akashindwa kuona kitakachomtokea.
Ingawaje hata angerekodi hivyo vifaa bado isingemsaidia kutopewa adhabu Kali.
Ila ingemsaidia kutufanya Sisi tusiopenda maneno matupu kuuelewa ukweli.
Vinginevyo ameifanya kesi yake kuwa na maswali mengi.
Wapo watakaoona anaugomvi na Yule Rose.
Wapo watakaomuona mkweli lakini ushahidi WA maneno yake kuthibitisha ukweli haupo.
Mwisho ameichafua serikali. Na ukiwa Mtumishi WA serikali ukiichafua serikali matokeo yake yanajulikana