Sakata la Warere Beach hotel kwa mtalii mgeni, Serikali ichunguze, wahusika wachukuliwe hatua, wametia doa sekta ya utalii nchini

Sakata la Warere Beach hotel kwa mtalii mgeni, Serikali ichunguze, wahusika wachukuliwe hatua, wametia doa sekta ya utalii nchini

Ndugu zangu watz someni uzi wa tukio tusikimbilie kukomenti ili tuwe wa kwanza.

Huyo ni binti wa Nigeria alikuja kula sikukuu yake ya kuzaliwa akiwa mwenyewe ndiposa kuna jibaba lilijitosa usiku kumbaka.

Ila mpaka muda huu, waniger wameshachafua sana huko tweeter na hiyo hoteli inapigwa misumari ya kufa mtu, muda huu nilipokuwa naandika kwenye vile viwango vya hotel bora google best hotel review kutoka 5.0 mpaka 1.8 ...
View attachment 2190293
Na waniger wameambizana kuireport kule booking.com ambao ni mtandao unaotoa taarifa mbalimbali za hotel duniani ikiwa ni huduma, usalama, chakula nk, ambapo mwishoni upigiwa kura na hotel kupewa cheti.

Yaani pasipo serikali kuingilia kati basi kuna hatari utalii znz kupungua sana.


Kutokana na kisa hiki nashauri mambo kadhaa kwa hasa hasa kwa serikali ya zanzibar, na huu ni ukweli japo haupendwi hapa visiwani, asilimia kubwa ya vijana wazawa wa visiwani si waaminifu, wajuzi na wabunifu kwenye tasnia ya utalii mpaka mahotelini.

Yaani ni vile serikali ya Zanzibar inawabeba, mfano, unakuta kijana yupo na mtalii (anamuongoza) huko mbele anaanza kuongea deal na rafiki zake kwa hao watalii vile hawasikii kiswahili au hotelini, hii si sawa, nimeshuhudia haya.

Tofauti na guide wa bara kama Arusha, Iringa, Kilimanjaro wale ni kazi kazi mambo mengine ni baada ya kazi, yaani zanzibar undugu ndiyo tatizo na isingekuwa serikali kuwalinda basi upande huo utalii ungekimbia sana.


Wasafari na watalii wengi wanadhurika sana mjini Zanzibar sema baadhi yao wanapotezea tu, sasa akipatikana kama huyu ndiposa utajua ukweli.


UPDATE HII HAPA 👇🏾...

Kiukweli kuna mambo ya ovyo sana kwenye sekta nzima ya masuala ya utalii yanafanyika. Na yote tatizo kuu si Serekali ambayo haipo serious kabisa kwenye mambo ya msingi.
 
Mimi nmeona wamejibu hii japo sina hakika.

View attachment 2190619
Haya ndio majibu, huyo dada anataka pesa kutoka kwenye hiyo hotel.

Pesa amekosa, sasa anatafuta umaarufu. Watu wajifunze, wanaigeria sio watu wazuri. Hata ukifanya nao kazi kua makini, ni wezi walioshindikana.

Sasa anaichafua hotel na Zanzibar nzima.

Ningekua sehem ya Management ya hiyo hotel ningetangaza kufilisika then nikawapa likizo watumishi baadae nikafungua kwa Jina tofaut kabisa kwa maana reputation imeshuka tayar.

Story yake ina mashaka mengi, umeona wapi mbakaji akaahirisha kwenda kutafuta Kondom? Kweli mbakaji asimamishe halafu aahirishe?
 
Kuna mtu kasema ukienda kwenye insta ya huyo mdada anaonekana alijiwish birthday tarehe tofauti na aliyosema kwenye thread ya insta....mambo ni mengi but all in all Serikali iingilie kati Kwa kufatilia Cha kweli ni kipi na kama ni kweli wamuombe msamaha public na kuhakikisha watalii kwamba ni salama Kuja znz
Achana na huyo mtu wa insta hilo tukio limetokea mwaka jana na dada kaweka ushaidi tunahitaji wahusika na serikali ndio waseme
We hujanielewa..nimesema Ivi kwamba Kuna mtu kaconfirm page ya Zainab ya Instagram birthday yake ni tofauti ya aliyoiandika kwenye thread kule Twitter
 
Hii story ya huyu dada sijui kama ina ukweli lakini polisi na sekta nzima ya utalii ijirekebishe. Tunafanya mambo kienyeji sana mradi siku iende. Kuna uozo mwingi sana huko Zanzibar labda watajirekebisha baada ya kuabishwa dunia nzima.

Polisi wa Tanzania nzima ni uozo. Ukiwa nashida hawawezi kukusaidia tena watakuzidishia tatizo. Labda kwa kuabishwa huku watajirekebisha.
 
Katika pitapita zangu za leo nimekutana na tweet hii ya binti kutoka Nigeria,aliyekuja Tanzania kwenye matembezi na kusherekea sikukuu yake ya kuzaliwa .



Ameeleza namna ambavyo alikuwa amelala Warere beach hotel na usiku wa manane akashangaa kuna mwanaume kitandani anampapasa papasa na kutaka kumbaka.
Kwa namna alivyoandika habari hii naona kuna shida kubwa sana katika hiyo hotel..kuna shida namna polisi aliporipoti walivyolichukulia na kushughulikia jambo lake.

Lakini pia to me namuona kama binti ambaye ni very strong,kama asingekuwa na hizo evidence huenda angeambiwa kapika hili jambo.Pamoja na kwamba kalitoa wakati huu ambao tuna issue ya uzinduzi wa royal tour ni vyema serikali yetu ilifuatilia kwa karibu na kutoa majibu ya sakata hili.

Nimeangalia hiyo tweeter namna inakuwa retweeted na baadhi ya comments za watu kucancel Plans zao za kuja Tanzania baada ya hiyo habari...ni aibu kwa kweli..wahusika wawajibishwe na binti huyo arudishiwe fedha zake. Kama kuna hotel zingine wenye tabia kama hii zikomeshwe pia mara moja ili kuendelea kulinda na kukuza sekta yetu ya utalii.Raisi wetu anajitahidi sana lakini unakuta tuna watu wenye akili mgando kama hao wa hiyo hotel.Kama room ilifungwa,namna ya mtu mwingine kuingia ni kwa master key ambayo hotel inayo..ili jambo linakasirisha sanaa.
UPDATEShttps://www.jamiiforums.com/threads/warere-beach-resort-wamiliki-wajibu-kwa-barua-nzito-wanasema-yule-binti-alimpapatikia-mlinzi.1974708/
UPDATES
Tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia commision ya utalii imetoa statement na kwamba uchunguzi umeanza mara moja






View attachment 2190393

Swali, huyo mlinzi aliingiaje chumbani kwa huyo demu?

Naona kuna uongo mwingi hapa, hata kama kweli, usalama wa chumba chake ni wajibu wake kwanza kabla ya Menejimenti ya Hotel, ndo maana kila room ina funguo zake na kila mteja ana room yake, AACHE UJINGA NA UZANDIKI
 
Swali, huyo mlinzi aliingiaje chumbani kwa huyo demu?

Naona kuna uongo mwingi hapa, hata kama kweli, usalama wa chumba chake ni wajibu wake kwanza kabla ya Menejimenti ya Hotel, ndo maana kila room ina funguo zake na kila mteja ana room yake, AACHE UJINGA NA UZANDIKI
Alialikwa kula keki ya Birthday chumbani akaenda matokeo yake mlinzi akawa anataka kubakwa na huyo Mnigeria akatimua mbio

Screenshot_20220417-144025_Instagram.jpg


Screenshot_20220417-144211_Instagram.jpg
 
Huyo mtu mwenye harufu mbaya si ndio huyo masai wamepiga selfie
sina uhakika kama ndio uyo ila iyo picha ilipostiwa baada ya tukio, kiujumla stori ya huyu dada ina maswali mengi kuliko majibu maana inaonekana ishu ilifika mpaka kwa mkuu wa wilaya bidada akataka alipwe $10000 walivyokataa akasema ataichafua hotel
 
Lakini umesoma tweets zake uko twitter na clips alizoziweka?

Instagram Account ya hiyo hotel imeblock hasiweze kuendelea kutoa lawama, sababu ya kublock ni nini?

Kama ni uongo si wangejibu alafu wamchukulie hatua za kisheria, kwa kublock watu wasitoe mawazo yao kunaonyesha kuna tatizo kwenye hiyo hoteli.


View attachment 2190501

View attachment 2190502
Nadhani majibu mmeshaanza kuyapata sasa na huo utapeli anaoufanya
 
sina uhakika kama ndio uyo ila iyo picha ilipostiwa baada ya tukio, kiujumla stori ya huyu dada ina maswali mengi kuliko majibu maana inaonekana ishu ilifika mpaka kwa mkuu wa wilaya bidada akataka alipwe $10000 walivyokataa akasema ataichafua hotel
Ni maajabu hapo mtu mwenye trauma ya kutaka kubakwa kwa maelezo yake. Imemchukua mwaka mzima mpaka kukaa sawa aandike mlolongo mrefu mtandaoni. Akaendelea kula maraha huko zenji halafu depression ikaja baadae au.

Kweli hapa kuna harufu ya utapeli nawashangaa ambao wamefumba macho. Alikua amesha andaa movie yake ya kujiingizia pesa huyu.
 
Back
Top Bottom