Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
View: https://x.com/lifeofmshaba/status/1840444113025400944?t=HQa05gIZAhN0Xht5BZzddQ&s=09
Tamasha la mziki la Wasafi Festival lililoandaliwa kwa gharama kubwa limeingia dosari mkoani Mbeya baada ya nsanii wake Zuchu kurushiwa chupa za maji stejini pale alipoanza tu kutumbuiza hali iliyomfanya asiendelee
Ni utamaduni wa kiafrika na mwafika kushirikiana kila jambo kwenye jamii
Kiafrika wanasema tulie wote tucheke wote.. Ukienda tofauti na hii kanuni.. Wanakubiri pa kukupata!
Taifa liko kwenye mtanziko mkubwa wa watu kudhulumiwa uhai wao
Watu kutekwa na kuteswa mateso mabaya kabisa
Watu kutekwa na kupotezwa
Ilitarajiwa hata litoke tamko la kinafiki kutoa pole na walau kulaani haya matukio lakini ndio kwanza wako wanasema mitano tena kwa mama!
Walipaswa kujua ya kwamba mashabiki wanaowategemea kuwachangia na kuhudhuria matamasha yao ni wa
Itikadi zote
Vyama vyote
Jinsia zote nknk
Na ndio hawa wanaotekwa kuteswa na kupotezwa kila siku.. Ndio hawa hawa ambao ndugu jamaa na Watanyika wenzao wamefanyiwa yote haya.. Unategemea nini kuwaendea watu kama hawa ambao tayari umeshaonesha upande wako?
Kamati ya Wasafi Festival ina nafasi bado ya kujirudi na kuweka mambo sawa.. Mashabiki ndio kila kitu.. Wakipuuzia hili mwaka huu tamasha linaweza kuvunja rekodi ya kufanya vibaya.. Jambo ambalo ni baya sana kwa brand kubwa kama Wasafi kibiashara na kijamii
Sakata la Diddy ni kichocheo tuu cha kulipua yaliyojaa vifuani mwa watu