Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Nasikia baada ya kuondolewa pale darajani, sasa wamevamia central Police. kazi yaendelea
 
Dawa wasiwachague CCM. Ila huo ni mwanzo mzuri, walale hapo mpaka malipo yao yatolewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama wamefuata taratibu zote na bado wanapigwa dana dana wafanyaje?
Si bora kujichukulia sheria mkononi baada watavamia magogoni mpaka waingie ndani tena bila hodi.
 
Mods, hii si iunganishwe na ileliyoko kwenye habari mchanganyiko
 
Sitashangaa hawa wazee wakifikia hatua ya kugoma kula. Hiyo itakuwa funga kazi

.
 
Wengine huwa hawaendi kwenye migomo kwa sababu strategies zitumiwazo hazijatulia, cheki mavitu ya wazee. Huyo strategist wao bab-kubwa!

.

Nilikuwa siamini kama JK anaweza kuwa raisi wa kipindi kimoja!!! Hizi laana za wazee zitamweka pabaya, jamaa amekalia kuti kavu....na serikali yao. Cha muhimu ni kuugana na hawa watu waliokata tamaa na sisi tunapigana nyuma ya PC zetu, udhalimu wa sisiem unaelekea mwisho!

Ushi
 
Kikwete alidai fedha za epa hazina mwenyewe. basi akate fungu hapo awalipe wazee wetu. Hii ni shame kabisa. Watoto wa shule wamegoma, wakafuata walimu wao, watu wa benki na sasa wazee wanazua janga... hii inanikumbushe hadithi ya yule mfalme mjinga ambaye alifuga paka... paka akaanza kula kuku, wakamfuata wakamwambia akajibu... paka wangu kuku wangu, asichukue hatua. akala bata, asichukue hatua.. paka akazidi kuwa mkubwa, akaanza kula mbuzi... akasema mbuzi wangu, paka wangu... akala mbwa, ng'ombe jamaa hachukui hatua. mwisho akaanza kula binadamu... wakamwambia mkuu, paka wako anakula watu.. kwanini tusimwue? akajibu watu wangu, paka wangu... paka akawa nunda kwelikweli... akaendelea kutafuna watu... akalamba mtoto wa mfalme... wakamwambia paka kala mwanao... asishtuke akajibu paka wangu, mtoto wangu...watu wakaisha... akabaki uso kwa uso na Paka.

haya yatatokea hapa Tanzania.
 
Sina ndugu huko but I feel like I should join them!

wazeebc.jpg

Picha na Father Kidevu.

Ok.. somebody explain this (Picha)

.
 
Wana JF...

Wazee wetu wamekuwa wakitamka kwamba, Wazee wenzao wa Kenya na Uganda walokuwa wakifanya kazi kwenye "EAC" walikwishalipwa mafao yao. Ningependa kujua kama kuna mjumbe yoyote anayeweza kupata usahihi wa taarifa hii kutoka nchi hizo, ili kwa namna moja au ingine, jamii pia isaidie kutoa msukumo ili awa Wazee wapatiwe wanachodai...

Ni ushauri...
 
I hope haya matukio yatamfanya muungwana, aanze kutulia ofisini na kuchapa kazi.

Inaonyesha kuna mambo mengi ya msingi ambayo hana details nazo za kutosha kuweza
kutolea maamuzi.

Kutegemea briefings za 1 hr, zinazojumuisha mambo yoooote ya taifa, hazimsaidii.

Akae ofisini apitie mafile, hasa yale ya msingi. folio 1 mpaka folio 1000.
 
Leo tumejionea mengi kwa kweli...Kandoro, Kova na Kimbisa wakiongoza magari. Tusubiri tamko la serikali kuhusiana na hali hii...hasa hasa Rais Kikwete atakapoongea na taifa mwisho wa mwezi kama ilivyo ada.

Rais hana mpango wa kuongea na taifa..... yuko busy anahudhuria vikao vya Bunge la Afrika, SADC, etc!!!

Expect nothing new from him.
Pantoni leo limeleta gumzo, wazee wa ex-EAC nao wamefunga barabara lakini no one is reading the signs!!!.....too bad!
 
Sina ndugu huko but I feel like I should join them!

wazeebc.jpg

Picha na Father Kidevu.

Ok.. somebody explain this (Picha)

.

Ni ishara ya upendo, umoja, amani, ujirani, mshikamano, ushirikiano, masikilizano waliokuwa nayo wazee hawa tangu mwanzo wa maisha yao, na mengine mengi ya aina hiyo. Ndio hii TANZANIA Mwalimu aliyotaka iwe. Lakini wendawazimu fulani wakapindisha maana. Achilia mbali Ukweli kwamba "UVUTAJI SIGARA NI HATARI KWA AFYA ZAO."
 
Sitashangaa hawa wazee wakifikia hatua ya kugoma kula. Hiyo itakuwa funga kazi

.

Unadhani huu uongozi wa CCM utawajali.... mi siwashuri wagome kula.... wafanye mavitu yanayo fanana na hii ya leo mpaka wasikilizwe.... tuwapeni msaada wa mawazo na mengineyo yaliyo ndani ya uwezo wetu
 
Nimesoma threads zooooote mpaka najisikia kulia. Kweli hii siyo Tanzania ambayo Mwl. alitaka kuijenga. Imekuwa nchi inayoongozwa na WAHUNI. Lakini siku ipo!

Walinunua rada mbovu kwa bei kubwa tukawavumilia, Wakanunua ndege mbovu ya Rais kwa bei kubwa tukanyamaza, Wakasaini mikataba feki ya madini tukakaa kimya, Wamefanya usanii kwenye RICHMOND tukanyamaza, Wakajenga majengo ya BOT kwa gharama kubwa tukatulia, Wamekula hela zetu za EPA bado tumenyamaza, wametafuna hela za walimu waliowafundisha hata kuandika bado tumenyamaza tu, SASA WANAWADHALILISHA WAZEE WETU, JE TUTAENDELEA KUKAA KIMYA? eti kisa ni kulinda amani? Potelea mbali kama ni amani na itoweke tugawane wote hicho kilichopo. Amani wakati mwenzio ameshiba wewe una njaa????????????? Nani kasema!!!!
 
pics za wazee hizo ...

i4_DSC001121.JPG
.
i5_DSC001132.JPG

Nimeipenda hii picha, wazee walivyokaa walipatia sana maaana kuna Bango hapo Nyuma nadhani ni la DHL linasema MORE POWER na Kuna Polisi na kalandinga lao, Nadhani hii picha inahabari zaidi ya habari
 
Kikwete alidai fedha za epa hazina mwenyewe. basi akate fungu hapo awalipe wazee wetu. Hii ni shame kabisa. Watoto wa shule wamegoma, wakafuata walimu wao, watu wa benki na sasa wazee wanazua janga... hii inanikumbushe hadithi ya yule mfalme mjinga ambaye alifuga paka... paka akaanza kula kuku, wakamfuata wakamwambia akajibu... paka wangu kuku wangu, asichukue hatua. akala bata, asichukue hatua.. paka akazidi kuwa mkubwa, akaanza kula mbuzi... akasema mbuzi wangu, paka wangu... akala mbwa, ng'ombe jamaa hachukui hatua. mwisho akaanza kula binadamu... wakamwambia mkuu, paka wako anakula watu.. kwanini tusimwue? akajibu watu wangu, paka wangu... paka akawa nunda kwelikweli... akaendelea kutafuna watu... akalamba mtoto wa mfalme... wakamwambia paka kala mwanao... asishtuke akajibu paka wangu, mtoto wangu...watu wakaisha... akabaki uso kwa uso na Paka.

haya yatatokea hapa Tanzania.

Aloo umenikumbusha mbali, paka mla watu!
Wazee bravo, I love you oooh!
 
Back
Top Bottom