Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Kwa kweli inatia huzuni sana.kama kweli hayo mahela ya epa yamerudishwa nashauri wawalipe hawa wazee wetu.
 
UPDATE:
Wazee kadhaa wamefikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa makosa kadhaa ikiwamo kufanya maandamano bila kibali, kusababisha fujo na kuzuia kufanyika kwa shughuli za kiuchumi.
Lakini wote wameachiwa kwa dhamana
 
UPDATE:
Wazee kadhaa wamefikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa makosa kadhaa ikiwamo kufanya maandamano bila kibali, kusababisha fujo na kuzuia kufanyika kwa shughuli za kiuchumi.
Lakini wote wameachiwa kwa dhamana

mambo mengine hayahitaji utawala wa sheria, kinachotakiwa ni kuwalipa pesa zao tu kwani ni shilingi ngapi?
 
Hivi kwa uzembe huu wa UWT(TISS) kushindwa kuliona hili mapema kuna mtu atawajibika?
 
Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.

Kauli yako ya "Huu ni uchoyo wa watu weusi.." inakasoro kubwa Mkuu. Sijui kwanini tunadhani mtu mweusi ndie mwenye makosa tu. Inaweza kuwa kauli hizi zinatokana na kujidharau kabla ya kudharauliwa, na ndio chimbuko la kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu na watu wasio weusi. Naomba tuachane na kauli za namna hii. Mimi ninajua watu weupe wengi wasio na uwezo ambao sisi weusi tunao. Maandamano yapo dunia nzima, sidhani kuwa tumeyaanzisha sisi. Ulaya, Asia, na mabara mengine hufanya maandamano (Demonstrations) kila wanapoona inafaa. Tena hufanya hivyo kwa kuzuia shughuli nyingi zaidi kuliko hata wazee hawa walivyofanya leo.

LA msingi ni kwa wote wanaohusika na kusababisha wazee hawa kufikia uamuzi huu wajiulize wanachofanya kina mslahi gani. Wajiulize kama ni haki kuwanyima wazee hawa haki yao (kama kweli wanayo haki katika madai yao). Wazee hawa mpaka kufika umri walionao, ni dhahiri wamevumilia mengi sana (katika nchii hii yenye maumivu makali). Kwa maana hiyo, nina amini kuwa kama kuna ushughulikiaji wowote unaoeleweka unaofanywa na serikali ungeeleweka tu kwa wazee hawa. Kufikia uamuzi huu, ina maana wameshindwa kuvumilia kabisa, na wanaona wanachezewa shere tu.
 
Taarifa zilizofika hivi punde ni kuwa wale wazee wetu wa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekuja na style mpya ya kushinikiza madai yao baada ya kuamua kufunga barabara ya Ali Hasan Mwinyi karibia na Salender ili kuonyesha ni jinsi gani wamechoshwa na usanii na uonevu huu wa serikali yetu.
Hii ni hatua mpya binafsi nimependa style yao LAKINI JE SERIKALI YETU ITAWASIKILIZA au ndo yale yale ya kuziba masikio?

Taarifa zinasema kuwa kikosi cha askari kimetumwa kikiambatana na gari la maji ya kuwasha kwenda kuwaondoa bara barani.
Habari ndio hiyo,
KWELI TUMECHOKA NA MFUMO HUU WA LICHAMA HILI LA JEMBE NA NYUNDO huku kiukweli NI UFISADI NA UBINAFSI

Nimekumbuka usemi usemao UKITAKA UGOMVI DAI CHAKO
Bongo haki haipatikani bila mshikemshike. Wazee (wastaafu) hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.


Mkuu, heshima mbele. unafanya kosa lile lile ambalo unawalaumu nalo wenzako. "kutazama kila mtu masilahi yake"! wewe kwa vile leo umechelewa kwenye kubangaiza kwako basi njia waliyotumia wazee imesababisha usumbufu!!
Walichoamua kufanya wazee wetu ni kufanya kitu ambacho kitaifanya serikali "ku-sit up na ku-take note!"(Mwalimu Nyerere!) na too bad for all those who will be inconvenienced,kama wewe!
Binafsi, nawaunga mkono wazee wetu katika hili kwa asilimia 110! Hamkani si shwari tena!
 
Halafu unaweza kukuta wazee kama hawa ndio makada wakubwa wa CCM na wakati wa uchaguzi wako mstari wa mbele kukipigia debe Chama Cha Mafisadi (CCM).

Hili tatizo limeanza toka wakati wa Nyerere, akaja Mwinyi akaja Mkapa na sasa Kikwete lakini bado halijapatiwa ufumbuzi. Wakati MAFISADI wanatanua na kujitajirisha na rasilimali za nchi bila ya kubughudhiwa, hawa wazee wanateseka na umasikini wa hali ya juu huku wakinyimwa haki zao kwa vipigo.

Wengine mnadai sijui angekuwa Mwalimu Nyerere ndio rais basi hawa wazee wangekuwa treated with dignity and respect, lakini kumbukeni Nyerere ndio alikuwa rais wakati Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ilipokufa. Tukubaliane kabisa kuwa Mwalimu Nyerere nae ni mhusika moja kwa moja katika kuwanyima haki hawa wazee na wala msitake kumtetea hapa.
 
Wazee hawa masikini wanatia huruma. 8 wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa kosa la kusababisha uvunjifu wa amani. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 6 mwaka huu baada ya wazee hawa kukanusha.

Serikali inadai mpaka sasa imeshalipa Tshs 114,229,588,396.63/= na inadaiwa kuwa waliotakiwa kulipwa ni wastaafu 21 tu na wengine walikuwa vibarua hivyo hawastahili kulipwa lolote.

Inasikitisha...
 
Wazee hawa masikini wanatia huruma. 8 wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa kosa la kusababisha uvunjifu wa amani. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 6 mwaka huu baada ya wazee hawa kukanusha.

Serikali inadai mpaka sasa imeshalipa Tshs 114,229,588,396.63/= na inadaiwa kuwa waliotakiwa kulipwa ni wastaafu 21 tu na wengine walikuwa vibarua hivyo hawastahili kulipwa lolote.

Inasikitisha...


wait a minute.... kwa hiyo kiasi hicho kimelipwa kwa watu 21 tu?
 
Kutokana na kutokuwa na Social Security system inayoeleweka, mimi nasema hivi Serikali iwalipe tu hawa wazee, hata kama walikuwa vibarua who cares, walipwe kwa sababu pesa wanazodai sio nyingi hivyo.

Wawalipe kama fadhila wakishindwa sababu zote.

Right or wrong wazee hawa wameteseka na ENOUGH is ENOUGH.

Mbona serikali hawakosi hela za kufanya safari za kifahari za Vasco Da Gama wetu???
 
Kabla hujaenda kuangalia picha kwenye blog ya Mjengwa, soma kwanza comments za hawa jamaa.



Anonymous
Mi ushauri wangu kwa serikali ni huu, bora watume magari ya petrol wawachome moto hao wazee woooooote, tena hapo walipo ingekuwa rahisi kuwamalizia mbali kabisaaaaaa. Mara kwenye mlango wa Ikulu mara barabarani, hao wastaafu wamedharilika vya kutosha. Kama hamtaki kuwalipa...kuliko kuwadharirisha basi wauweni tujue dhamira yenu


Anonymous
AAah Hapana Ukichukua petroli na kuwachoma wengine watakimbilia baharini na kujitumbukiza hivyo watapona wengine. Kwanza serikali iwachukue na kuwapakiza kwenye mabasi kama ya magereza yale yenye nondo kisha iwapeleke msitu wa pande kupitia njia ya masaki waone majumba yaliyojengwa kwa pesa zao HALAFU moja kwa moja msituni anashushwa mmoja mmoja na kuchapwa viboko kisha ZOMBE ANAKUJA NA KUWATWANGA RISASI hapo kwishili karibu hawawasumbui tena.SIE mafisadi tuendelee kula BATA tu mtaani.tehe.....tehe....tehe.....tehe....tehe.....DUU MAFISADI BWANA MPETO TU NYIE MLIE TU NA VIMAFAO VENU HUKO.


SteveD, please, tell me you don't have anything to do with this!




.
 
moelex23,

Mimi imefikia hatua nikafikiria hadi kina mama wamefikia kuvua nguo vile wakilia na kugalagala, serikali inabidi ifumbe macho iepushe laana hizi. Wanafanyiwa wao hivi, kesho ni sisi!
 
Wazee hawa masikini wanatia huruma. 8 wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa kosa la kusababisha uvunjifu wa amani. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 6 mwaka huu baada ya wazee hawa kukanusha.

Serikali inadai mpaka sasa imeshalipa Tshs 114,229,588,396.63/= na inadaiwa kuwa waliotakiwa kulipwa ni wastaafu 21 tu na wengine walikuwa vibarua hivyo hawastahili kulipwa lolote.
Inasikitisha...

Serikali inauhakika na inaloongea au ni bla bla tu. Kisheria kibarua ana muda maalumu wa kufanya kazi ukishapita zaidi ya hapo anakuwa na haki kama mfanyakazi mwingine. Sasa kama serikali(au iliyokuwa Jumuia) iliteleza kwenye hili wakapitisha muda wa kuwatumia hawa wazee kama vibarua kisheria inabidi tu wawalipe stahili zao. Kifupi inabidi wabebe msalaba wa uzembe uliofanyika.

Inawezekana vile vile serikali yetu ina-suffer kwa sababu ya 'poor record keeping' hawana uhakika so they play defence. Wazee watapukutika kwa umri with time then mambo yatasahauliwa. Kama ni suala la poor record keeping still wa kubeba msalaba ni serikali.

Nadhani nakumbuka wakati fulani hawa wazee walienda mahakamani kudai haki yao na wakapewa ushindi, ina maana mahakama haikuona kuwa kuna baadhi walikuwa vibarua kwa hiyo hawastahili hayo malipo? Serikali yenyewe baada ya kupewa hati ya hukumu kama ilijua wengine (wengi wao ni vibarua) kwa nini wasikate rufaa kwa hiyo hukumu ili hao vibarua waondolowe kwenye kulipwa?
 
Back
Top Bottom