Bajeti ya taifa ni nyenzo muhimu inayolenga kuhakikisha serikali inatoa huduma kwa wananchi na kuendeleza taifa. Ni hati ya fedha inayotoa dira ya mapato na matumizi ya taifa. Hata hivyo, bajeti ya mwaka 2025/2026 imeonyesha mazingira ya kipekee ambapo mjadala wa kitaifa juu ya bajeti uligubikwa na mvutano mkali kati ya vilabu vya soka vya Yanga na Simba. Je, hili lilikuwa tukio la bahati mbaya au mkakati wa makusudi wa kufubaza ajenda muhimu?.Timeline ifuatayo inaonyesha namna mfululizo wa matukio ya sakata hili lilivyoshabihiana kwa karibu na ratiba ya kisiasa na kiuchumi ya taifa, hususan bajeti kuu ya serikali.
Timeline ya Matukio Muhimu
6 Mei 2025: Bodi ya Ligi yafanya marekebisho ya ratiba, ikiweka mechi ya Yanga vs Simba (namba 184) kufanyika tarehe 15 Juni 2025.
9 Juni 2025: Saa 10:30 jioni, Yanga watangaza kutoshiriki mchezo huo hadi madai yao ya fedha yatimizwe. Saa 11:00, msemaji Ali Kamwe asema hawatacheza fainali ya Kombe la CRDB wala mechi ya Zanzibar.
10 Juni 2025: Saa 6:49 mchana, CRDB yajibu kwamba ilishalipa fedha kwa TFF. Saa 7:40, Yanga wajibu TFF kwamba hawajalipwa kwa misimu mitatu na hawawezi kucheza bila kulipwa.
12 Juni 2025 (siku ya bajeti): Saa 10:00 jioni, Simba watangaza mechi itaendelea kama kawaida. Wakati huo huo, Waziri wa Mipango Prof. Kitila Mkumbo atangaza kuwa deni la taifa limepanda hadi dola milioni 26,670.32 (sawa na takribani Tsh trilioni 107), ongezeko la asilimia 12.4.
12 Juni 2025: Prof. Anna Tibaijuka na Zitto Kabwe watoa kauli kali kuhusu ongezeko la deni la taifa, wakisisitiza uzito wa tatizo hili kwa wananchi. Hata hivyo, mjadala huo haupati mvumo mkubwa wa kitaifa.
Wakati huo huo: Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba atumia fursa hiyo kumpongeza mfadhili wa Yanga GSM ndani ya hotuba ya bajeti. Pongezi hizo zasambazwa na kurasa za mitandao ya kijamii za Yanga.
13 Juni 2025: Simba watangaza kupata ruhusa kufanya mazoezi. Viongozi wa Yanga na Simba wakutana na Rais Ikulu, jambo linalopokelewa kwa hisia tofauti. Bodi ya Ligi yatangaza kuahirisha mechi hadi 25 Juni. Yanga wachapisha bango la "Kariakoo Derby 25.06.2025 - HAINA KIPENGELE."
Katika sayansi ya jamii, usanifu wa kijamii mbinu za makusudi za kuelekeza mitazamo ya jamii au kuunda ukweli mpya wa kijamii kwa kutumia taasisi au mawakala wenye ushawishi mkubwa ni jambo la kawaida. Katika tukio hili, vilabu vya mpira vya Yanga na Simba viligeuka kuwa mawakala wa kuficha ajenda kuu ya kitaifa kwa kutumia mvutano wa burudani.
Timu kama Vyombo vya Nguvu ya Umma: Simba na Yanga zina jumla ya zaidi ya wafuasi milioni 15 mitandaoni. Uwezo wa kushawishi mawazo ya jamii ni mkubwa zaidi ya taasisi nyingi za serikali. Migogoro yao inaathiri mjadala wa taifa.
Mkakati wa "Distraction by Substitution": Siku ya bajeti, umma ukazama katika mijadala ya nani mwenye haki, Yanga au TFF? Mechi itachezwa au la? Bajeti ikasahaulika. Hisia zikatawala hoja.
Uingiliaji wa Kisiasa Katika Burudani: Pongezi kwa GSM ndani ya hotuba ya bajeti, viongozi wa timu kwenda Ikulu, ni mifano ya mbinu ya “symbolic resolution” , kutumia taswira za upatanisho kutuliza hisia badala ya hoja za msingi.
Kifo cha Mjadala wa Bajeti: Kauli kali za wachambuzi kama Prof. Tibaijuka kuhusu deni la taifa, matumizi ya fedha na kodi hazikupewa nafasi ya kutosha. Umma ulibeba bango la "25 Juni Kariakoo Derby" badala ya kuuliza trilioni 107 zimeenda wapi.
Timeline hii inaonyesha jinsi mfumo wa burudani, haswa soka, unavotumika kama zana ya kisiasa ya kufunika hoja muhimu. Iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, mjadala wa bajeti ulimezwa na sakata la Simba na Yanga. Hii inaacha maswali muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na uwajibikaji nchini.
Je, ni halali kwa ajenda ya taifa kupewa nafasi ya pili nyuma ya burudani?.Ni nani anafaidika pale wananchi wanaposhindwa kufuatilia bajeti yao?.Je, tunahitaji mfumo wa kusimamia ajenda za kitaifa zisifunikwe na kelele za kihisia?.Majibu ya maswali haya hayawezi kupatikana kwa kushabikia timu, bali kwa kuamsha fikra za wananchi na kuwajibisha mamlaka.