Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
​

Mhe. Rais Magufuli afanya ziara ya ghafla bandari ya Dar es salaam muda huu. Anakagua matanki ya mafuta ya kula. Fuatilia matangazo TBC1 muda huu.

Atembelea kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam na kupewa maelezo kuhusu Mafuta kukwama bandarini.

Rais Magufuli amesema...

Baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa kwenye matanki hayo kuna ambayo yalikuwa na 'crude oil', na mengine yalikuwa na 'refined oil' ambayo yalifichwa kwa makusudi.

Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei. Nawaomba tuwe wazalendo. 'Crude Oil' ichajiwe bei ya juu ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Haiwezekani 'crude oil' ukachaji sawa na 'semi refined', na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo. Wabunge walipitisha kitu kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupitishwa kuwa sheria kimebadilishwa kuwa kingine.

Hii 'crude oil' ichajiwe bei ya juu ili watu wengi wajenge viwanda hapa, tujenge nchi yetu.

Jiwe.jpg

​
====

UPDATES:

Rais Magufuli anasema;


=> Nlituma wachunguzi wangu waje kufanya analysis ya haya mafuta. Wote wameleta majibu sawa. MAfuta yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Nmesoma ripoti yote.

=> Ukitaka kutengeneza mafuta yoyote, kwanza mafuta yote yanatokea kwenye crude Oil, yakishatoka kwenye crude Oil..unafanya Neutralization na kwenda semi-refined oils au bridging kuchange colour of oil. Viwanda vingi vya tanzania ni semi refined Oil. Double refined.

=> Tatizo tulilonalo;

*Crude inachajiwa 10%

*Semi refined inachargiwa kwa 10%

Sasa unakuta vyote vinachajiwa sawa.

=> Haya mafuta yaliyoleta hapa ukiuliza yametoka wapi hutopata document, haya ni yale mafuta yanayonunuliwa baharini, waliombwa na TRA leteni document zinazoonesha mafuta haya yametoa Malesia au wapi, Hawana. Baada ya kukosa document tukapata mashaka. ndo wakaanza kuzunguka wanasema kwenye tv na radio kwamba mafuta yameisha yamepanda bei, tukachukua wataalam wakakusanya sample hizi na kuangalia kama yamafaa kwa matumizi.

=> Wamechunguza yale yote yanatotakiwa kujua. Bahati nzuri tukakuta hayana tatizo. Tukaamua tujue kama ni cude au semi refined au double refined. Na wao karibu yote walisema ni Crude. Kwahiyo watapigwa faini ya kufanya udanganyifu. Yaliyobaki mtank manane wala sio mafuta, ni material ya kutengenezea sabuni. Hayafai kuliwa. tumeyawekea alama.

=> Nchi yetu tulifanya makosa ndani ya Serikali katika kutunga Sheria ya Mafuta ya kuliwa. Nawaagiza Wizara ya fedha na viwanda wakafanye marekebisho bungeni kuhusu hii sheria ya mafuta

Nmeagiza mafuta yaanze kutoka leo


Nlituma watu waje kufanya uchunguzi wa kitaalam. wakafanya analysis. Wameleta matokeo;

=> Vegetable oil, katika sample 13, matanki mawili (namba 4 na namba 12), haya yana double refined oil wanatakiwa kulipa 25 % ya charge

=> Kuna matenki 4 yana materials ya sabuni yalipiwe 10% na Mengine yote yalipiwe 10%

=> Tanzania liquid storage tank namba 3 ina double refined litalipiwa 25% Mengine yote yachagiwe 10%

=> Kuna mafuta East Coast Oils, imegundulika mafuta yote ni semi refined 10% na Matenki manne (ecb 1, 2, 9, na 3) yatalipiwa 25%

=> Katika Sample 13, matanki 7 yote yana content ya double refine, yanatakiwa yachagiwe 25%, na yaliyobaki yanachajiwa 10%

=> Natoa wito, kwenye mafuta hapa, haya nmeruhusu yatoke kutokana na condition. Lakini kama watadanganya tena wapigwe fine

=> Nawaagiza Mpeleke amendment bungeni ili mtu akileta crude semi refined au double refined chages zitolewe kutokana na mafuta aliyoyaleta.

=> Crude manaake haijafanyiziwa process yoyote. Hakuna mfanyabiashsara anayeweza kwenda ulaya kuleta crued

=> Hii sheria ya mafuta ni ya Hovyo, hili ni kosa letu kama Serikali. Hauwezi kuleta crude ukachaji 10%

=> Sitaki itumike advantage ya mwezi wa ramadhani kwa kudai mafuta yanahitajika halafu tuwape chakula hakifai. Ndo maana tukafanya uchunguzi kabla ya kurhusiwa.

=> Double refined ni pipa saba. watayatoa kwa 25% na kupigwa faini ya kudanganya.

=> Kafanyeni marekebisho ya Sheria ya Mafuta. Haiwezekani crued Oil ikachajiwa sawa sawa na Semi refined

=> Kwenye Ofisi ya AG alikuwa na tabia ya kufanya amendment ya Muswada uliotoka bungeni. Yaani wabunge wanapitisha sheria, yeye anaeda kubadilisha na kuweka maneno anayoyataka yeye ndo anampa rais asaini. Ni tabia mbaya ilikuwa.

=> Kaimu kamishina wampe ukamishina wa TRA kamili. (Rais Dkt. John Magufuli amempandisha cheo aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili TRA bandarini hapo baada ya kusimamia vyema mchakato wa kukagua mafuta yaliyokuwa na utata bandarini)

=> Kaimu mkurugenzi wa TBS simamieni masirahi ya serikali bila kudanganya. Ongeeni ukweli kama mambo yalivyo.

=> Mkemia mkuu, nataka sample zote mtakazokuwa mnapewa fanyeni kwa utaratibu kwa kuzingatia maadili yenu. Mkiletewa madawa ya kulevya, kesho msiseme unga wa muhogo. Mkemia mkuu na TBS zingatia maadili yenu.

=> Hawa mliofanya analysisi nawashukuru sana mumesimama kidete.

=> Hakuna tatizo la mafuta, na taratibu zikikamilika mafuta yataingizwa sokoni

Wafanyakazi wa bandarini wameulizwa kama wana chochote cha kumuuliza rais wakasema hamna mwenye swali wala maoni

Nlitamani niende kuchwa chai kwa mama lishe, ana nini? ngoja nikanywe chai. Anaenda kunywa chai kwa mama Lishe.

Amenunua matunda ya Elfu 30.
 
Mhe. Rais Magufuli afanya ziara ya ghafla bandari ya Dar es salaam muda huu. Anakagua matanki ya mafuta ya kula.

Jiwe.jpg
 
Heshima kwenu wakuu,

Rais Magufuli afanya ziara ya kushitukiza bandarini Dar.

Atembelea kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam na kupewa maelezo kuhusu Mafuta kukwama bandarini.
 
Mubashara: Rais Magufuli akiendelea kuhoji maofisa wa Bandari kuhusu mafuta yaliozua utata bandarini na kusababisha upungufu wa mafuta nchini.

 
Back
Top Bottom