Sakata ya Simba na Yanga ni mpango ili kuwapumbaza watanzania wasifatilie yanayoendelea kwenye siasa

Sakata ya Simba na Yanga ni mpango ili kuwapumbaza watanzania wasifatilie yanayoendelea kwenye siasa

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
993
Reaction score
2,045
Mods msiufute huu uzi.

Ukitulia na kutafakari Kwa utulivu hilo swala ya SIMBA na YANGA kusuguana kuhusu huu mchezo wa marudiano utagundua kuwa,

1. Ni mpango uliosukwa kwa makusudi ili kuwafanya WATANZANIA wawe bize kujali huu upuuzi na kujiweka mbali na siasa ambazo kimsingi ndio ukombozj wa Taifa letu.

2. Hili sakata liliundwa ili kuzifanya media zisikose jambo ambalo Kwa juu juu linaonekana ni la msingi lakini ki ukweli ni jambo la kipuuzi sana kwasabab halina tija Kwa Taifa ni upuuzi mtupu.
Media sasa zinashinda na kukesha zikizungumzia swala la Simba na yanga kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.

Mwanasiasa mmoja aliomba Mungu hizi timu zifutike, kwa upande mmoja hayupo sahihi lakini Kwa upande mwingine yupo sahihi kwasabab Simba na yanga ni timu zilizoficha wanasiasa wanaojiita mashabiki, wanasiasa ambao wapo CCM wanazitumiz hizi timu kuteka akili za WATANZANIA.

Ukifatilia utajua kuwa hawa wanaojiita mashabiki Lia Lia wa Simba na yanga ni ma CHAWA na ni wanasiasa ambao wanawezeshwa kifedha na kupewa airtime kubwa ili kusambaza hoja ambazo zinaibua migongano na chokochoko kwa mashabiki wa hizi timu mbili.

Kifupi Taifa kwasasa linapitia kipindi kigumu sana kisiasa na maadui wakubwa wanajulikana na wanashupaza shingo ili kulinda maslahi Yao binafsi na siyo maslahi ya Taifa.
 
Ni hivi, hata ukifuta Simba na Yanga kama watu hawapo tayari kupigana na serikali kisiasa hawatapigana. Hao wanaofatilia Simba na Yanga ni watu wazima na wapo wenye vitambi.
 
Back
Top Bottom