Sala zenu zinahitajika...

puker

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
1,001
Reaction score
2,010
Ndugu zangu wana Jf.

Nyie ni familia yangu upande wa pili, leo ghafla baada ya kutoka church, hali yangu imebadilika sana....Baridi kali, [emoji1784] viungo vinauma kichwa kinauma sana na kutulia ukinigusa nina moto kama basi.

Mdogo wangu amenipeleka hospital, wakanicheck hawakuona tatizo even Covid19, wamesema nipo good. Ni homa ya kawaida hivyo, nikapewa bedrest na k unitundika chuma za maji mbili.

Hali kidogo ikatulia wameniruhusu nikapewa na Diclopa, nimefika nyumbani hali imebadirika tena now maumivu ya uti wa mgongo yanaongezeka.

Namuamini sana Mungu ila kutokana na maisha niliyopitia, nina mashaka kidogo.

Please ndugu zangu, kwa kila imani nahitaji maombi yenu ya dhati

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Yaani juzi juzi nilipata maumivu ya mgongo kuanzia mchana, yakadumu kwa siku takribani 3 na usiku homa ya kutisha. Yaani kutembea shida napata kizunguzungu na hapo kutembea ni kwa kunyata, usiku kulala hakuna style inayokubali ni maumivu ya kutosha. Tatizo liliisha lenyewe kwa kutumia dawa ya maumivu hizi wanazoziita anti-inflammatory.
 
Pole mkuu,vipi kumbe siku hizi Covid inapimwa na majibu yake unayapata papo kwa papo?
 
Pole mkuu,vipi kumbe siku hizi Covid inapimwa na majibu yake unayapata papo kwa papo?
Walikuwa na ile mashine ya kumulika kwenye paji la uso
 
Ahsante mkuu kwa msaada[emoji120]
 
Pole mkuu..nakuombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akuponye na upate afueni kadiri iwezekanavyo kwa uwezo wake. Urudi ukafanye shughuli zako.
 
Pole sana jipe matibabu ya (changamoto ya upumuaji) kwa tahadhari tu.
Pole
 
Mwenyezi Mungu akuponye ila pia nawe mashaka uliyonayo juu ya hali iyo omba kwa imani yako iyo hali utaivuka
Ahsante kwa ushauri mzuri ubarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…