Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Kesi ya high court imehukumiwa na judge muhuni latifa mansour ambae ana mahusiano nao na nilivyo appeal wakacheza wakaipeleka Kwa ma judge wao na watunzia heshima.

Wasipojirekebisha kwenye review hakika nitawamwaga uchafu wao wote.
Mkuu usisubiri review usije ukatupiwa jini ukafa tukakosa maelezo yako tunaomba hata kabla ya review wewe weka hapa mkasa mzima, eleza mwanzo mwisho wa mkasa wako ulivyokua, ushaambiwa jamaa wana majeshi ya majini sasa wasije wakakutumia wa kwako tukakosa maelezo yako kimoja emu funguka nini kimekusibu hadi hawa mabwana GSM na Bank Access kudhulumu na kupora Mali zako?
 
Nimeona malalamiko ya mwenzetu kama binaadamu inasikitisha.

Hilo ni dogo Sana nikileta ushenzi waliyonifanyia Mimi hiyo familia ya GSM kudhulumu ardhi yangu kisa imekaa strategic na mahitaji Yao kigamboni basi nchi itazizima hii.

Mimi ni muumini wa serikali kwamba ipo na wapo serikalini watu wenye utu wa kusimamia haki za wanyonge.

Toka nimetoka gerezani Nina mwaka mmoja Kwa kesi ya kubambikiwa mauaji kisa wadhulumu ardhi yangu yenye kituo Cha mafuta na godown yenye value zaidi ya bilioni 7 Kwa kucheza deal na bank ya access na kunibambikia deni kutoka milioni 400 mpaka 1.8b Ili Kuni frustrate na wakauziana kinyemela bila kufata taratibu halali hata Moja na ushahidi wote upo Kwa familia nzima nimeutawanya Kwa serikali mbaya zaidi mahakama yote wameishika na wanasema mahakama zote zinakunywa chai salamander.

Kesi ya high court imehukumiwa na judge muhuni latifa mansour ambae ana mahusiano nao na nilivyo appeal wakacheza wakaipeleka Kwa ma judge wao na watunzia heshima.

Wasipojirekebisha kwenye review hakika nitawamwaga uchafu wao wote.

Tarehe 26/8/2021 baada ya uvamizi na kupora Mali zangu zengine zenye thamani zaidi ya milioni 500 na kutengenezewa kesi mbaya ya mauaji na GSM na vibaraka wake mapolisi na DC.kigamboni f.nyangasa.

Nimekaa gerezani keko from 4/9/21 to 18/3/22.

Nimeandika Kwa uchache tu nasubiria msaada Kwa jitihada ya mwisho tuliyoifanya kama familia kwenda mh.rais mama.

Na sisi ni waarabu wenzao na hatuogopi chochote ni Bora nife kuliko kudhulumiwa na kunyanyaswa kisa tajiri GSM dhulumaat .

Na Wala wasihangaike na Mimi vitisho vyao ni vingi kwangu mimi but siwaogopi na wanajua ninapoishi wajue siko peke yangu kesi hii mama yangu kaka zangu dada zangu na wake zangu na watoto zangu Tisa wote Wana kila evidence needed in their records.

Waziri wa mambo ya ndani na wizara yake yote wote wanajua. lolote likinipata basi watu Hawa ndiyo wahusika.

1.GSM
2.FSM
3.Silent ocean
4.said home shopping
5.na mapolisi wengi majina Nayahifadhi

Maana sijawahi kuona mpaka mawaziri wanajitoa akili kutetea dhulma ya huyu GSM na familia yake.

Tegemeo langu ni Allah(S.W)

Mh.rais Samia mama unaupiga mwingi Sana natumai malalamiko yangu uliyapata in writings and all evidence ndiyo tegemeo nililobaki nasubiri kwako na Kwa waziri mkuu mh.kassim majaaliwa.

Ahsanteni.

Njaa zitafanya binadamu wengi tufe vibaya sana.

Tena mkuu nyinyi waarabu mnaonekanaga mnazo,hivyo mtu kukudhurumu anaona kama hutachukua muda sana kupigania haki yako,poleni sana Mungu awasimamie.

RIP jpm.
 
Hana lolote huyu. Saa 72 zitaisha na hana cha kufanya.
Soma hapa
 
Daaahh....pole sana afu wanajifanya wachamungu kumbe wanafiki kabisaa Hawa mbwa ,wazinzi wanazaa hovyo nje kujifanya
Kweli kesho Kwa MUNGU Kuna Kazi
Ila Hawa endelea kuwasomea alamtara na tabattiyada tu Mungu atawalipa mbonaa

Masiku Yao ni machache sana ya KUFANYA DHULMA
Acheni kuendekeza ushirikina
 
Tanzania ni nchi ya dili kila mahali, hivi Magufuli alivokua anasema ni dili kila mahali alikua anakosea, NI KWELI

MATAJIRI WA TANZANIA NI WIZI TU NA BIASHARA HARAMU ZINAWABEBA

KAMA KWELI MUNGU ATALETA SIRI ZA WANADAMU HADHARANI KUCHEPUKA NA MKE WA MTU HAITAKUA SIRI YA AIBU
 
Asante sana mkuu, kwanza pole sana kwa yanayokusibu lakini pia umeandika kwa uchache sana kinachokusibu tungeomba utuelezee kiundani ni nini kilipelekea hawa wadhulumati kudhulumu mali yako maana hii dhuluma sasa imekua sio nzuri wapo wengi wanaodhulumiwa na hawasemi popote na wengine wanaishia kuzibwa mdomo tu maana kila wanaposema hawasikilizwi na yeyote, sasa basi weka wazi nini kimetokea ni kwanini wakapora na kukudhulumu ardhi yako na kuiuza bila idhini yako?

Na katika madai yako ni nani anaepaswa kulaumiwa Bank ya Access au GSM? Au ni wote kwa pamoja baada ya kukuchezea mchezo mchafu wa kukubambikia kesi?

Emu fafanua kidogo kuna kitu ningependa kujua ilikuaje bank ya Access wakauza ardhi yako kwa GSM bila idhini yako?

Na pia unasema ulibambikiwa kesi ya mauaji na kuporwa Mali zako na Askari wanajua na GSM wanajua, emu tueleze ni nini kilifanyika ni nini hawa watu wanafanya ni uozo gani wanaufanya ambapo watu hawaujui Ila baadhi ya watu km nyinyi ambao mmepitia dhuluma zao mbaya mnaujua kua huyu mtu ni mtu mbaya sana kwa jamii?

Elezea mkuu

GSM sababu hawa wamepitia mgongo wa bank
 
Back
Top Bottom