Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Maalim Seif: Kikwete akome kutufitinisha Wazanzibari!7/02/2009
Kauli ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009
Waheshimiwa wananchi wenzangu, sote tunakumbuka kwamba tarehe 27 Januari 2001 nchi yetu ilikumbwa na maafa makubwa. Watanzania wenzetu, hususan Wazanzibari, waliuawa, wengine wakafanywa walemavu wa maisha, wengine walibakwa, wengine wakafungwa, wengine mali zao zikaharibiwa na kuporwa, na wengine wakakimbilia Mombasa kama wakimbizi, kwa mara ya mwanzo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa la Tanzania.
Na hawa (wahanga wa maafa hayo) kosa lao lilikuwa nini? Kosa lao ni kushiriki maandamano ya amani kudai haki zetu. Kimsingi walidai kwamba uchaguzi wa 2000 ulikuwa ni uchafuzi, wakataka urejewe. Wakadai tuwe na katiba mpya Bara na Zanzibar. Wakadai tume huru za uchaguzi Bara na Zanzibar. Lakini kwa watawala, hiyo ilikuwa ni dhambi; kwa hivyo,serikali chini ya usimamizi wa CCM wakaamrisha majeshi: majeshi wanaolipwa kwa fedha za kodi za Watanzania, watumie risasi na silaha zilizonunuliwa kwa fedha za kodi za Watanzania, wawauwe Watanzania wenzao. Na kama alivyosema, Mheshimiwa Duni, baada ya hayo yote kutokezea, Bwana Mkapa anawatunza wale wauaji anawapa vyeo zaidi na Amani Karume anawapongeza majeshi kwa kufanya kazi nzuri.
Waheshimiwa wananchi, mimi napenda tujuwe kuwa msiba huu ni wa wana-CUF peke yao. Msiba huu ni wa Wazanzibari sote. Kuna wengine wenye mtazamo finyu wataona CUF wameshikishwa adabu, lakini wakumbuke Tumbili akisha miti, huja mwilini. Mghani Utenzi amesema wazi wazi kwamba kuna viongozi wa chama cha Afro Shirazi wakubwa tu, nao walipoteza maisha yao. Kwa hivyo, tusiangalie mambo hayo kwa ufinyu kwamba ni CUF.
Huu ni msiba kwa taifa. Wajibu wetu Wazanzibari ni kuwakumbuka wenzetu, tusiwasahau, tuwaenzi. Na kuwaenzi wenzetu ni kuendelea na mapambano yale ambayo yalisababisha damu zao zitoke. Hakuna kurudi nyuma. Yeyote yule ambaye atarudi nyuma kwa namna yoyote ile, huyo ni msaliti na muuaji kama wauaji wenyewe, kabisa. Ni lazima, ni lazima, sote kabisa tuungane kuhakikisha kuwa dhulma katika nchi yetu inaondoka moja kwa moja. Lazima dhulma iondoke. Hakuna mizinga, hakuna bunduki, hakuna rupleni ambayo itaturudisha nyuma katika kudai haki zetu. Tutadai haki zetu mpaka zote zimalizike, lakini tutazipata haki zetu. Lazima tuzipate haki zetu, tusiwasaliti wenzetu.
Waheshimiwa, nasema bado yale yaliyowafanya wenzetu wapoteze maisha, bado madai yetu yapo pale pale. Bado tunataka katiba mpya; hili ni dai ambalo mpaka leo ni halali. Tunataka tume huru ya uchaguzi. La kusikitisha, mimi nilidhani yaliyotokea 2001 watawala watajifunza, lakini bahati mbaya watawala wetu wana vichwa vigumu. Kwao kubwa ni kuhakikisha namna gani wataendelea kubakia kwenye madaraka kwa gharama yoyote ile. Maisha ya binaadamu kwao si kitu, kitu ni wao waendelee kubaki na madaraka, basi.
Wamesahau kuwa waliowaua wenzetu 2001, wengi wao na wao weshakufa. Mwenyezi Mungu hana haraka, lakini anahukumu hapa hapa duniani, akhera ni malipo tu. Nao watahukumiwa, huko akhera kutakwenda hisabu tu basi. Sawa sawa!?
Waheshimiwa, nasema tena nasikitika kuwa watawala hawajifunzi. Na ushahidi kuwa watawala hawajifunzi ni kauli alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, katika ziara aliyoifanya Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Kikwete alisema mengi, lakini mawili makubwa niliyoyashika mimi ni haya: alipokuwa Pemba anawaambia Wazanzibari, kwamba haki ya Wazanzibari ni kuchagua mbunge, mwakilishi na diwani, basi. Lakini ukija kwa uchaguzi wa kumpata kiongozi mkuu wa Zanzibar, Wazanzibari hawana haki hiyo. Hiyo ndiyo kauli ya Kikwete. Na kwa kweli chaguzi za 1995, za 2000 na za 2005 zimeonesha kuwa huo ndio mtindo. Kwa hivyo Kikwete anatwambia kabisa kuwa na 2010, yeye ndiye ataamua nani awe rais wa Zanzibar. Huo ndio ujumbe wa Kikwete.
Waheshimiwa, na hapa nawaomba ndugu zetu wa CCM waifahamu: ingawa Kikwete kasema wapinzani, lakini kakusudia Wazanzibari. Ndugu zetu wa CCM, nyinyi wenyewe ni mashahidi, mwaka 2000 mlikuwa na mtu mlomtaka, mlomchagua nyinyi wenyewe, wana-CCM wa Zanzibar, lakini watawala wa Bara walikuwa hawamtaki. Wakamuweka mtu wanayemtaka wao.
Kwa hivyo, msidhani kauli ile tunaambiwa CUF peke yetu. Hapana, tunaambiwa Wazanzibari kwa ujumla wetu. Inawezekana kabisa na 2010, CCM mkawa na mgombea wenu, lakini madam hamtaki Bwana Kikwete, basi huyo mgombea wenu asahau. Huo ndio ujumbe wenyewe alioutoa Kikwete, kwamba mwenye haki ya kutupatia rais wa Zanzibar ni Kikwete mwenyewe na CCM yake ya Bara. Huo kwa ufupi ndio ujumbe wa Jakaya wa Mrisho wa Kikwete.
Ujumbe wa pili, ambao kautolea hapa hapa Kibandamaiti, ni kwamba ati wako tayari kupambana na wapinga Mapinduzi na akasema watayalinda Mapinduzi yao kwa gharama zozote. Jamani nataka mnisikie vizuri: kauli ya Kikwete na namnukuu: Tutayalinda Mapinduzi Yetu, kwa gharama zozote!
Mimi ninavyojuwa na tunavyoambiwa ni kwamba Mapinduzi yale yalikuwa ni ya Wazanzibari, kwamba kiongozi wa Mapinduzi alikuwa Mzee Abeid Amani Karume na wenzake kina Said Washoto. Tunaambiwa ni Wazanzibari ndio waliofanya Mapinduzi, au sio? Haya Kikwete ni Mzanzibari? Mimi ninavyojuwa na Profesa (Lipumba, ambaye ni Mnyamwezi na kimila ni mtani wa Kikwete) kwamba Kikwete ni Mkwere. Zanzibar haimuhusu shikio wala ndewe. Leo vyereje Kikwete asema: Tutayalinda Mapinduzi yetu! Vyereje!?
Hapo pana mambo makubwa Wazanzibari, lakini leo si wakati wake kuyazungumza. Inshallah siku za mbele tutayafunua moja baada ya moja, kwa nini Kikwete katoa kauli ile. Na kwa kweli anaposema kuwa atapambana na wapinga Mapinduzi, anakusudia wale ambao watampinga mgombea atakayeteuliwa na yeye, Kikwete. Usijali kama wewe ni CCM au CUF, madhali unapingana na mtu aliyemleta yeye, wewe ni mpinga Mapinduzi yao. Ndio maana nasema Wazanzibari tuone kuwa hili suala si dogo. Haambiwi CUF, twaambiwa Wazanzibari kwa ujumla wetu.
Wananchi, jambo la kushangaza, wenzetu watawala hawa watawala wa Bara jambo wanaloliogopa kwa Wazanzibari ni umoja wa Wazanzibari; kwa sababu ndiyo sera yenyewe. Nguvu zao (watawala wa Bara ni) wagawe uwatawale. Mtakumbuka alipokuwa mtawala Mkapa lile linamkera, pale pale hakuweza kujizuia . Pale pale kwenye jukwaa alipopewa nafasi ya kusalimia, akaanza kusema: Tunatoa salamu kwa mababu za hao wapinga Mapinduzi, vijukuu vyao, vitukuu vyao hawatawali hapa. (salamu za Mkapa katika sherehe za mwaka 2002 za Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya Muafaka wa pili wa 2001, CUF ilishiriki katika sherehe hizo kama chama na Mkapa aliogopeshwa sana na namna umma wa Kizanzibari wenye sare za CUF na CCM ulivyokusanyika pamoja kwa mara ya mwanzo kwenye sherehe kama hizo).
Ebo! Wewe badala ya kufurahi kwamba Wazanzibari kwa umoja wao wanasherehekea Mapinduzi kwa mara ya mwanzo, unakasirika. Lakini si ujinga, analijua analolifanya, kwamba lile aliliona inawasogeza Wazanzibari wawe karibu pamoja na hilo watawala wa Tanganyika hawataki kuliona. Na hili, Jakaya Kikwete, kwa hili kashtushwa sana na mshikamano wa Wazanzibari. Kashtushwa sana na umoja wa Wazanzibari. Wazanzibari sasa hivi wamekuja juu kusema kuwa tutalinda nchi yetu, Zanzibar ni nchi na itabaki kuwa nchi mpaka Kiama. Wazanzibari wameshikamana kulinda rasilimali zao, hasa za mafuta. Sasa Kikwete hili linamuuma sana.
Linamuuma sana tu, kwa sababu wao wamo katika kutekeleza mkakati tangu aliouwacha Julius Nyerere kwamba Zanzibar itoweke katika ramani ya dunia. Sasa mshikamano wenu Wazanzibari unawafanya wao wasifanikiwe. Kwa hivyo, alilokuja kufanya Kikwete ni kujaribu kuwagawa tena Wazanzibari kwa kutumia wimbo wa Mapinduzi. Tena, mimi nashukuru Mungu, kasema Mapinduzi yetu, katumia wimbo wa Mapinduzi yao. Mapinduzi yao si Mapinduzi ya Wazanzibari, jamani. Mujuwe hilo!
Kwa hivyo, anataka kutumia wimbo huo atugawe, lakini kachelewa. Kachelewa. Hatugawiki tena ngo! Tena namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete akome, akome, akome! Akome kutuletea fitna katika nchi yetu. Akome, akome kuja kutugawa Wazanzibari. Fanya chokochoko zako huko huko Bara. Namna gani, bwana!?
Tena anajisifu mwenyewe: Miye Zanzibar naijuwa! Waijuwa Zanzibar weye? Wee waijuwa Zanzibar? Ati mwenyewe anaijua Zanzibar kaja 77 akiwa afisa dawati pale Kisiwandui (ofisi ndogo ya CCM, Zanzibar). Wakati huo Maalim Seif tayari ni mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Wakati huo Maalim Seif ni Waziri wa Elimu wa Zanzibar. Wakati huo Maalim Seif ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Wakati huu Maalim Seif ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Yeye (Kikwete) mtoto mdogo tu, nani Kikwete? Nani huyu, kabisa!? Namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete kwamba enzi za kuja na shanga mununue nchi yetu umepitwa na wakati.
Eti CCM imeleta maendeleo. Maendeleo gani? Tumejenga barabara! Barabara ipi mulojenga? Mimi nasema tena, hao vibaraka uliowaweka hawajaleta maendeleo yoyote Zanzibar na sisi Wazanzibari ndio tunaojuwa. Ati umekuja hapa kumtetea Amani Karume kuwa kaleta maendeleo; na mwenyewe bila haya anasema ati Kikwete na Karume ni mama mmoja, baba mmoja, watoto mapacha. Hujasema jipya Kikwete. Na tunajua kwa sababu hiyo, kwa wewe na yeye baba yenu na mama yenu ni CCM ati leo CCM huyo huyo ni baba, huyo huyo ni mama, ni khuntha.
Khuntha CCM imemzaa Kikwete na Karume, ati wanasema ni mapacha. Hatushangai, ndio maana ufisadi unaotokea Zanzibar, watu wanachukuliwa ardhi zao, Kikwete mhm! Kimya, hasemi kitu. Fedha za serikali, kodi zinazokusanywa kutoka bandarini, kutoka airport, kutoka kila mahali zinakwenda nyumba kubwa. Kimwete mhh! Kimya. Lakini hatushangai, CCM inazaa mafisadi, Bara na Zanzibar.
Kwa hivyo ninalosema, Mheshimiwa Kikwete, ujumbe wako Wazanzibari wameupokea, kwamba 2010 kushamuonea choyo Mkapa, nawe wataka kuua. Keshamuonea choyo Mkapa kwamba mikono yake ina damu, na yeye Kikwete anataka mikono yake iwe na damu vile vile. Basi Wazanzibari tunakusubiri njoo! Njoo! Njoo! Wazanzibari tunakusubiri njoo!
Sisi tulikuamini uliposema 2005 kwamba mpasuko wa Zanzibar unakuuma kweli kweli na kwamba utafanya kila njia ili uumalize. Tukakupa mashirikiano yote Kikwete. Wakati napita kwenye matawi kuelezea suala hili, sehemu nyingi nikiulizwa: Hivyo Maalim, unamuamini Kikwete? Nami jibu langu lilikuwa: Simuamini lakini tumpururie, atajinyonga mwenyewe huyu! Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki. Lile ambalo lilikuwemo kwenye moyo wa Kikwete, juzi kalitapika. Sawa sawa? Bila ya siye kushiriki, mwenyewe kalitapika. Wazungu wanasema: the true colors of Kikwete have now come out! Rangi sahihi za Kikwete sasa hivi zinakuja juu. Sawa sawa?
Sasa anajiandaa kutuua tena Wazanzibari. Tunamwambia aje. Lakini tunakwambia, tunakwambia, tunakwambia: Inshallah mara hii, mara hii, mara hii, utakavyoipiga, tutaicheza hivyo hivyo.
Hotuba kamili: Machano Khamis Ali - Mzanzibari ,Makamu Mwenyekiti - CUF
7/02/2009
Ikiwa kuwalinda albino kumemshinda, Kikwete atawezaje kuyalinda Mapinduzi?
Kauli ya Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009
Waheshimiwa wananchi, tumeshamsikia Maalim Seif. Sasa mimi sina makubwa. Ninachosema ni kimoja tu: Basi jiandaeni. Maana yake sio (Maalim Seif) aseme, halafu tufanyiwe, halafu tuje tulaumiane. Ikiwa tunakuja kuuliwa, na siye tunasema tutacheza itakavyopigwa, maana yake ni kuwa akija (Kikwete) atukute tumejitayarisha. Ama sio?
Waheshimiwa, mimi nasema Mheshimiwa Kikwete anaendeleza zile lugha za kisanii tu, kwa sababu hana uwezo yeye wa kuyalinda Mapinduzi. Mapinduzi ya Zanzibar yanalindwa na Wazanzibar wenyewe. Na leo Wazanzibari tukiamua Mapinduzi basi, leo leo yatakuwa hayapo, lakini ni siye siye Wazanzibari ndio tunaoyalinda.
Nasema kama Kikwete anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi, kwanza angewalinda Albino wanaouliwa kama wadudu. Hawa ni binaadamu, wanakufa katika nchi yake, anashindwa kuzuwia. Ataweza kuzuia watu wakitaka kuyapindua Mapinduzi? Kwa hivyo ni usanii tu. Au atwambie, kwa sababu magazeti yanaandika kuwa albino wanakufa kwa sababu ya ushirikina wa watu kutafuta mali na vyeo, ni miongoni mwa hao wanaotafuta vyeo na hivyo anaruhusu wale wauliwe? Kama harusu, hana uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Kwanza atuoneshe mfano, awalinde albino wasiuliwe. Akituonesha mfano kwamba albino hawafi na kawazuia yeye basi tutaamini anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Nawalinde wale.
Kinachosikitisha, ni mtu asiye huruma. Mimi nikifikiri huyu Pinda ndiye aliyekuwa hana huruma, kumbe yeye (Kikwete) ndiyo hana huruma. Pinda kalia Bungeni. Kikwete ashazunguka nchi nzima hii, hajawahi hata kutoa kauli kuwaonea huruma albino. Ana huruma huyu? Albino wanakufa ndani ya nchi yake, tena kule Bara, yeye hana habari nao. Pinda mwenzake kalia, kafika kutoa kauli kinyume na katiba ya nchi na sheria ya nchi, anasema hao wanoua nanyi waueni. Uchungu aliouona wale watu wanavyopoteza maisha. Yeye (Kikwete) hajasema lolote, badala yake kaja Zanzibar anataka kutugawa.
Lakini nataka niwambieni waheshimiwa mufahamu kwamba, sasa hivi Wazanzibari hawagawiki. Juzi nimefatwa ofisini na mtu wa CCM, ananambia Kikwete kachelewa. Nikamuuliza kwa nini, ananambia: Sisi dai letu ni Zanzibari bwana, sio kutuganya tena. Tushachoka. Sisi tunataka nchi. Tutambulie kama nchi. Asitwambie kwamba Zanzibar nini sijui nini. Hapana, atwambie anakubaliana na sisi kuwa hii nayo ni nchi. Akikubali hilo, sawa atakuwa rafiki yetu. Hakukubali hilo, sisi Wazanzibari hakuna CUF hakuna CCM tushaamua, hatutaki tena! Sisi hapo (kwenye msimamo huo) hatuondoki tena.
Halafu (Kikwete) anatwambia: Ooh, CUF wasitegemee kupata serikali. Mtachagua wabunge na wawakilishi. Mie namkumbusha maneno hayo aliyasema baba yake wa taifa, Nyerere. Nyerere alisema atamuona rais wa sita wa Tanzania, alimuona? Hana hakika, basi Kikwete. Haya anayeyajua ni Mungu, sio Kikwete. Kikwete unabahatisha tu, huna hakika. Suala la kuwa 2010 CCM inaondoka au inabakia, hilo anajua Mungu tu, halijui Kikwete. Na kama yeye anapanga hilo, na Mungu anapanga lake. Tungojee.
Tusisitushwe na hilo. Labda nia yake turudi nyuma, tusijitokeze kwa kufikiria yale yale kuwa hawa hawatupi serikali. Tusifike huko. Hapa ndipo tunapoanzia sisi Wazanzibari kulinda haki ya nchi yetu.
Sasa hilo ni moja na dogo. Kubwa nataka muelewe kuwa sisi Zanzibar na Tanzania hatuna tume za uchaguzi. Hawa watu (tume zilizopo) wamewekwa na CCM kuisaidia CCM itawale maisha. Mumesikia Mbeye huko (kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeye Vijijini). Na hapa Zanzibar nataka mutambue muwa huyu mwenyekiti wa sasa tume hii alikuwa ndiye sekreterieti wa tume iliyopita. Uchaguzi uliopita masheha waliwazuia watu wasiandikishwe, Tume ikasema inathubutu masheha kuzungumza nao, masheha hawakwenda kuitikia wito wa Tume; na Tume ikabakia kunyamaza kimya. Hiyo ndiyo tume iliyopita na ndiyo tuliyonayo sasa hivi.
Kwa hivyo hili ndilo suala la kulifanyia kazi. Usije ukategemea kupata haki yako kupitia tume ya uchaguzi, hupati. Jipange, jitayarishe, ona kwamba haki yako unaipata kutokana na uwezo aliokupa Mwenyezi Mungu. Sawa?
Daftari linakuja, vitimbi mtaanza kuviona. Kama kutishwa ndio tushaambiwa hivyo, kama kuuliwa ndio pashaagizwa hivyo. Kwa hivyo, musije mukafikiri haya yanayosemwa yanasemwa kwa 2010, inaweza ikawa yanasemwa kwa wakati huu huu wa Daftari. Wasije wakatufumba, tukaona wao wataanza 2010 kumbe wao wataanza sasa hivi. CCM haaminiki. Akikwambia tukutane Mwembeladu, wewe kamngoje Micheweni.
Tushukuru kwamba CCM wenzake wa Zanzibar hawakubaliani naye. Kwa hivyo, tuungane na wananchi wenzetu wa CCM ambao wanakubaliana na sisi katika kuitetea nchi. Yeye kaja kupandikiza chuki, nyinyi musiwachukie CCM. Wananchi Zanzibar musiwachukie CCM. Tushirikiane nao tujiandikishe kwenye Daftari, twende kwenye uchaguzi tuone ikiwa CCM hii iliyosema Zanzibar si nchi itabakia madarakani.
Hotuba kamili: Juma Duni Haji -Mzanzibari,Katibu Naibu Mkuu - CUF
Wanaoua albino wauawe, walioua Wazanzibari je?
7/02/2009
Kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Mhe. Juma Duni Haji, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009
Sina hakika, lakini juzi nilipokuwa natizama Bunge (vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano), alipoulizwa Mheshimiwa Pinda (Waziri Mkuu) kuhusu mauaji ya maalbino, nadhani ilikuwa tarehe 27 Januari, siku ambayo watu sisi pia waliuliwa, basi namna vile alivyokuwa na huzuni, vile alivyokuwa akilia masikini na mie nikawa ninalia. Lakini kilio cha Pinda na changu kidogo vilikuwa tafauti, maana Pinda alichoambiwa na Kiongozi wetu wa Upinzani Bungeni (Hamad Rashid Mohammed) haoni kuwa si vizuri yule anayedhaniwa kupiga au kuua albino, apelekewe mahkamani, maana (kabla ya hapo) kwa namna alivyoona uchungu, Pinda alikuwa amesema anayeuwa albino naye auliwe.
Nikasema lo, Mashallah! Anayeua albino anaye auliwe, aliyewaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27, afanywe nini? Maana kama ni mwanaadamu na ni uchungu wa roho, roho ya albino na roho ya Mzanzibari ni sawa sawa. Tafauti iliyopo ni kwamba yule aliyemuua albino hajapatikana, bado anasakwa, lakini walowaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27 wanajuilikanwa. Tena wengine, baada ya kuua, Mheshimiwa Mkapa kawatunza vyeo, ati wamefanya kazi nzuri kutuua.
Sasa, kufa ni kufa, roho ni roho. Kamisheni ya Mheshimiwa Hashim Mbita ilishathibitisha yaliyotokea wakati huo wa tarehe 27, basi tungelitegemea angalau wao wakafikishwa mahkamani; maana wanajuilikanwa. Lakini Mheshimiwa Pinda analia kwa uchungu, anasahau kuwa sisi pia tunalia kwa uchungu. Lakini sisi tulipouliwa watu walipewa vyeo. Wanapewa vyeo kwa kutuua? Ee, Mungu we! Hilo ndilo lililonisikitisha.
Sasa kama hilo halitoshi, nikasikitika zaidi kwa Mheshimiwa Kikwete unakuja Zanzibar, badala ya kutusahaulisha yaliyotokea, unatukumbusha? Mashallah, hivo wewe ndo rais kweli weye!?
--------------------------
Hizo ndizo siasa ziliyopo Zanzibar ,hakuna kushughulikia ufisadi wakati waliopo madarakani ndio mafisadi dawa yao ni kampeni ya kung'olewa ,Viongozi wa Upinzani T/Bara mnayaweza hayo -CHADEMA.TLP,SAU,NCCR na vyenginevyo mpira kuelekea uchaguzi MKUU @ 2010 ndio umeanza ,naona mpo na mafisadi mmoja akioza wameoza wote msemo wa kiswahili huo lazima muufanyie kazi kikwelikweli ,hakuna kulala ,tunatahitaji kuona CCM inang'olewa natumai mumefahamu.

Hotuba kamili Seif Sharif Hamadi - Mzanzibari,CUF Katibu Mkuu

Last edited: