- Hapana kama ungekwua mchukia uabguzi ningekusikia maana nilimsikia Sumaye peke yake akilalamika lakini sio wengine kwa sababu ya kuamini kuficha ficha, no inatakiwa yatolewe nje kama ninavyofanya ili yashughulikiwe.
Mkuu FM ES, HUNIJUI, ndio maana huwezi jua wakati Salim anabaguliwa nilipinga ama la. Lakini kwa kusema ukweli nilipinga vibaya mno. Na hili la kubaguliwa Salim halikuanza leo. Wakati yuko AU (OAU) kama Katibu Mkuu alirudi kwa Mwalimu kumuuliza achukue fomu. Hapo ndio hili lilianza, na mwanzilishi ni Mama fulani mtu mzito aliyeko CCM (namuhifadhi jina, bali mme wake kawahi kuwa bosi Nyaraka za Taifa), alifikia kumwambia Nyerere kuwa unataka tutawaliwe na Mwarabu?. Mwalimu kuona mambo yamekuwa makubwa akamwambia Salim usichukue fomu. Hivyo halikuanza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa 2005, bali zamani kidogo.
- Kwa sababu ndio siasa za Seif, hayo maneno ya juu hayawezi kukubalika na sisi wananchi, maana ni matusi sana na hivyo ni vyema akaeleshwa mapema kwamba akielta siasa zake za kibaguzi tunajua sababu na hatuwezi kumpa nafasi.
Maneno ya Seif (kwa uelewa wako kuona kakosea) hayawezi kufanya wazanzibar wote wasio weusi uwabague. Dhambi ya mtu mmoja haifanyi wengine wote waibebe.
- siwezi kujibu hoiaj za hicni namna hii mkuu maana kama wewe hatumii maneno kama shetani sisi tunatumia wka nia njema, Seif aache siasa za Pemba na kutuletea taifa, abaki nazo huko huko Pemba lakini hawezi kumtukana rais wa Jamhuri kwa visingizizio vya sias zake za kibaguzi, majibvu ni kwamba we know him na siasa zake na hatuwezi kumruhusu, Karume alipokuwa akilazimisha wananchi waarabu na wesui kuaona hakuwa mbaguzi ila alikuwa anajaribu ku-deal na ukweli kama mimi sasa,
Nashukuru, ndio uelewa wangu ndio maana natoa hoja za chini, wewe mwenye hoja nzito Mola akuzidishie.
Hivi unataka kusema CCM hawatoi kauli za ajabu. Kikwete alipokuwa Pemba juzi juzi aliwaambia nini kuhusu wapinzani kupata nchi. Na hata Pinda Alhamisi hii iliyopita naye kazungumza hilohilo kuwa wapinzani hawawezi kushika madaraka akiwa Bungeni. Unataka wapinzani wajibu nini?, kama viongozi wanaweza toa kauli ambazo zinaashiria kuwa hawawezi toa nchi hata pale wanaposhindwa. Karume alifanya kosa kubwa sana kulazimisha watu waoane, hiyo ni kuvunja haki za binadamu. Kuoana ni kupendana na si kulazimishana. SASA NIMEKUONA TENA JINSI UNAVYOUNGA MKONO UVUNJAJI WA SHERIA HASA HAKI ZA BINADAMU.
- Hawawezi kuiba kura Unguja kwa sababu hakuna wa kumpigia kura Seif kule Unguja, huwa wanaiaba kura za Pemba tu, ubaguzi upo na ni lazima uemwe wazi, hapa ndicho kinachomsumbua Seif, na hatutampa nafasi kuleta siasa zake za ki-Pemba kwenye Muungano.
Hivi kama unakubaliana nami CUF ilishinda uchaguzi wa 1995, hao watu walitoka wapi?. Na kama unasema CUF hawapati kura Unguja, ulizia kwa nini waliyagawa tena majimbo baada ya uchaguzi wa 1995. Unajua CUF walichukua mpaka jimbo iliyopo Ikulu (Ngome ya CCM), unalijua hilo?. Na mpaka sasa CUF wana mwakilishi Unguja. Kuhusu uizi Pemba huwa wanatumia vikosi vya usalama. Wakati karibia na uchaguzi wanajeshi, askari, zimamoto, KMKM, uwt kibao huhamishiwa zenji, hapo ndio huiba kura toka kambini. Lakini vituo vya raia kwa Pemba wanaiba kiasi kidogo manake jamaa wako ngangari kama walivyokuwa ngangari CHADEMA kwenye jimbo la Mheshimiwa Ndesamburo (Ndesapesa), unajua yaliyojiri kwa hili jimbo?.
Unajitahidi, lakini bado kidogo ingawa pia kuna hoja nzito unazitoa, lakini la ubaguzi wa Seif na hali halisi ya huko linakupa taabu sana ingawa ninajua kwua una background nzuri sana ya CUF
Sijatoa hoja yoyote nzito nje, siwezi kukubali kuwa Seif mbaguzi kwa kushinda Pemba, na CCM wanaoshinda Unguja tu nao sio wabaguzi. Tena CUF huwa wana wawakilishi na Unguja, nani wabaguzi hapo. Hili suala CCM mnatumia Divide and Rule kama wakoloni ni baya sana. Fanyeni maendeleo ya haki kote Unguja na Pemba mtaliondoa jinamizi linalowasumbua, sio kuiba kura.