sasa nyinyi CUF hamna tena -baada ya Seif? Hicho Chama? Hivyo hakuna kiongozi huko? kwenu zaidi ya Seif. Seif -Seif acheni hiyo. CCM wanakwenda na wanabadilika. Sasa Mwiba elewa kuwa Seif hana nafasi CUF inaweza ikawa na nafasi Zanzibar.
Unaposema hakuna zaidi ya Seif sijakuelewa ,labda nikilinganisha na Ilikuwa hamna zaidi ya Nyerere ?
Baada ya Seif wapo tele kwani aliechambua wizi ufisadi unaofanywa na Tanganyika dhidi ya Zanzibar alikuwa Seif ?Shukuruni mmeachiwa Seif kuna wengine hawanywi tende wanakunywa maziko saa nane ,wacheni udhaifu wa kuitolea uvivu Serikali iliyoko madarakani kazi ya wapinzani ni kuibana serikali hata kwa jambo la kweli ni lazima kwa hali yeyote ile hilo hilo la kweli liambiwe japo halipendezi ,itatosha kusulubisha serikali na ndio mbinu za siasa.
Kuna mtu hapa kaandika sera za Chama sijui kwa vile yeye ni kiongozi anaweza akazizungumzia au kama miradi akaifungua , Mimi nakwambia kwa kiongozi alie makini hawezi hata siku moja akafungua miradi ya Chama japo yeye ni mwenyekiti au vyovyote awavyo ,Raisi na Mawaziri wanapoapa hawapi kuwa watakitumikia Chama kwa moyo wake wote ,hakuna hilo ,inawezekana Chama kumwalika Raisi kwenda kufungua miradi iliyotimizwa na Chama huko huko mabondeni lakini sio kwenye miradi ya serikali
Inapotoletwa misaada hapa Nchini kutoka huko mnakokujua nyinyi hailetwi kwa jina la Chama cha siasa ,inaletwa kwa kuipatia au kuisaidia Serikali ya Tanzania na wala si mwenyekiti wa CCM,hilo mnatakiwa raisi na mawaziri wake walifahamu, unapokwenda kufungua tangi la maji na kuwambia wananchi hizi ni sera za Chama chetu inakuwa unawadanganya wananchi ,kuwambia wananchi kuwa bara bara kama mgongo wa ngisi wakati si kweli huko ni kuwadanganya. Yeye ni Raisi alikuwa awe makini na kauli zake,kwani angelisema njia zetu ni mbovu lakini tunajitahidi hivyovyo kidogokidogo mpaka tutamaliza kungekuwa na kosa gani ?, Jamani semeni ukweli ! Uwongo ni dhambi ,lakini jamaa kaingia kwa vishindo mjini kwa watu,ni Raisi anastahili heshima lakini watu wanasema jiheshimu uheshimiwe.
Sasa kuna akina nyinyi mnaobeza viongozi wa CUF naamini kabisa yaliyosemwa ni maneno ya uhakika na ya kweli tupu,hajasingiziwa mtu wala hajazushiwa mtu, Seifu aliposema Kikwete ni mtoto kwake akimaanisha kuwa katika siasa ,Kikwete atakuwa hana ujuzi mkubwa kuliko Seif,Kikwete amemkuta Seif katika siasa tena Seifu ameshapitia sehemu nyeti nyingi tu,hivyo Kikwete hawezi kuzielewa siasa kama anavyozielewa Seif na kwa maana zaidi Seif anayajua mengi zaidi kuliko Kikwete.
Siasa za Kikwete haziwezi kufua dafu mbele ya Seif ,Mr Kikwete ataanguka tu na ndio kama tunavyoona msiojua siasa mtaona Seif ametoa maneno machafu sijui hayafai kuambiwa Raisi lakini Kikwete katika duru za siasa anaisabika amepata pigo kubwa sana kisiasa.Na ameambiwa bado hayo mengine pale si siku au pahala pake ,tayari utaona kuwa Seif amejenga tamaa kwa wananchi wasubiri siku nyengine.
Nendeni mkapumzike na story hiyo hapo ambayo ni latest ,halafu semeni kuna au wanataka kupeleka uarabu au kurudisha maendeleo ,tazameni vipi watu wanawajumuisha watu wengine na kuweka usawa kwa kiasi wawezavyo yaani angalau waonekane na wengine wanajumuishwa kikamilifu bila ya kudharau rangi,dini au kabila au Utaifa wao,wajulikane wapo au wamo.
http://www.thisisleicestershire.co....form-hijab/article-660197-detail/article.html