- Aibu ni kuyazima na kujidai hayapo, wakati yapo na ndio hasa siasa za Seif, ndio maana Kikwete amesema atalinda Muungano kwa nguvu zote, ninakumbuka siku Mwalimu alipofariki, tulikuwa kwenye mkutano na kiongozi mmoja wa Visiwani ambaye sasa ni waziri wa muungano, aliongea maneno siwezi sahau hata siku moja na ndio siku mawazo yangu yalipobadilika kuhusu Zanzibar na siasa zao, infact at onepoint yule mkuu alikuwa akitoa hotuba huku akitoka machozi kumlilia Mwalimu na kwamba wanaofikiri kufa kwake kutawapa mwanya wa kuichukua Zanzibar ni ndoto tupu, toka siku hiyo mkuu sizitizami siasa za huko kama zamani, lakini samahani kama mtizamo wangu haufikii level yako ya kuficha ficha kuwa hayapo, huku Sumaye a former PM akiandika wazi jinsi udini na urangi ulivyotawala uchaguzi wa rais mwaka 2005.
- Tafuta ile article ya "CCM tumekula nyama ya mtu", utayakuta yote ninayosema wazi hapa!
Thanxs!
Suala la ubaguzi usilikwepe, kama unaona Seif ni mbaguzi hakukufanyi nawe uwabague watu wa rangi tofauti na Nyeusi Zanzibar, nilikuuliza ukiwamaliza hao wenye rangi tofauti utahamia wapi?. Kwanza ni Nyeusi gani unaizungumzia, ukifananisha mjaluo na mrangi. Ama msukuma na mtu wa Sudan Kusini. hapo tena kutakuwa na matabaka ya weusi.
Kuhusu huyo jamaa aliyozungumza baada ya kufariki Mwalimu, mimi siyajui, labda utuwekee hapa. Manake nitaaminije huyo mtu mmoja, tena kwa kukusikia ukisema alisema, na bila kutuambia alisema nini?. Hata mimi najua yaliyo mabaya Seif aliyafanya nyuma na yana mcost sasa, wakati huo alijipendekeza kwa Mwalimu, sasa yamegeuka. Lakini siwezi fikiria bagua mtu kwa rangi, dini, kabila nk. Unapomzungumzia huyo aliyetoa mada (ambaye sasa ni waziri) na kusema eti alisema wasifikiri kufariki kwa Mwalimu kutawapa mwanya wa kuichukua nchi. Sasa hapo huoni hata enzi ya Mwalimu demokrasia ilikuwa inapindwa, na unakubaliana nami bado kwa hiyo kauli inaonesha kuwa bado watapinda demokrasia. Msiba unahusiana vipi na chaguzi. Huyo Waziri huenda alikuwa hamlilii Mwalimu, bali aliona maslahi ya kuondolewa madarakani yanakaribia. Mh. Sumaye alizungumzia CCM, ina maana CCM ndio inaendekeza udini na urangi. Ukiweza nitumie hiyo article ya Sumaye.
Nakubaliana nawe Rais Kikwete anatakiwa kulinda Muungano, manake kaapa kuulinda. Ila hatakiwi kuulinda kwa mizengwe ama kuua watu. Muungano ni wetu wananchi, tuna haki ya kuujadili, bila kutishwa wala mizengwe.
Naomba"-
-muweke huyo waziri alisema nini ili nasi tupime.
-Jaribu kuwa Muungwana kwa kusema uliteleza kuwabagua
Wazanzibar wasio Weusi.
-Jaribu kutofautisha upenzi wa chama (CCM) na maslahi ya nchi, manake kucheza na uchaguzi ni kutafuta matatizo. Na si Zanziba tu, hata Bara.
-Naomba tuache huu mjadala tuangalie hotuba ya Maalim Seif, naona zaidi kama tulitoka nje ya mada, lakini kamautazidi onesha ubaguzi nitaendelea kukuelewesha.