Salaam kutoka Zanzibar - Hotuba kamili - Msikie SEIF SHARIF HAMAD-Si mchezo

Hakufanya la maana zaidi ya kupandikiza chuki tu kati ya Wapemba na Waunguja. na kati ya Wazanzibari na ndugu zao wa-Bara.Ni mkosoaji mkubwa (mlalamikaji)kuhusu Muungano lakini hakuna lolote analoeleza kuhusu kuboresha Muungano huo.
 

Mfumwa ni wajibu wako kumuweka sawa mpotofu huyu. ANA MACHO HAONI AMEGUBIKWA NA CHUKI BINAFSI, ana masikio lakini anachuja cha kusikia na mwisho ana akili na amepewa elimu ya kupambanua anaendekeza hisia. Ameshindwa kutowa hoja za uhakika kwa anachokitetea UBAGUZI.
Yeye yuko mbele kukemea maovu na ufisadi lakini kwa hili limegusa UARABU na pengine element nyengine. Pengine ungemjuvya kuwa Seif juu ya rangi yake si mwarabu na hilo si geni kwa kule Zenj.
 

Mkuu BUBU ni HATARI SANA kwa KIONGOZI au VIONGOZI hasa wa ngazi za juu Kupoteza BUSARA na HEKIMA wakati wameshikilia dhamana ya uongozi ambayo wakati wote huendana na Maisha ya wale mnao au unaowaongoza. Labda niwasaidie kidogo kwa misemo hii ya Wahenga wanaposema: MDOMO ULIMPONZA KICHWA! Hizo kauli zao za ovyoovyo mara nyingi MADHARA yake huwakuta wengine! Na WAPIGANAPO FAHALI WAWILI ZIUMIAZO NYIKA hivyo wakati wao wanapigania MADARAKA,mishahara minono,marupurupu,magari ya kifahari nk Maumivu na mateso yanakwenda kwa Washabikiwao. Tafadhalini acheni Siasa na Sera za kinazi za Simba na Yanga. MADARAKA YANAKWENDA PAMOJA NA RISPONSIBILITY!!!!!!!! YES??..............YES.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…