Kuna Usemi naupendaga sana uliokua unatumika kwenye harakati za kutafuta uhuru ulikua unasema
" It is Better to die on yo feet rather than to live on yo knees"
Ni Afafhali Ufe Ukiwa Umesimama kwa miguu yako kuliko kuishi maisha ya kuwapigia watu magoti na kuwalamba miguu!
Imagine tungekua bado tunatawaliwa na wakoloni, walete maendeleo ya kila namna Lakini bado tuwe tunafungwa minyororo, tunauzwa kama watumwa n.k.... na hata katika hayo maendeleo kazi ngumu zote ni lazima tungezifanya sisi tena kwa kupigwa mijeledi, kwa jasho kwa damu na vifo
Hayo maendeleo yangekua yanatufaidisha nini sisi?
Uhuru ndo kila kitu, haya yanayotokea Acha Yatokee yanayoendelea Acha yaendelee tutapambana nayo mpaka mwisho wake ukifika mambo yatakua shwari!
Kikubwa tuko huru!
Hata Hamo kama Ameona kule Alikua Anatumia nguvu nyingi lakini Alikua hafaidiki wacha mtu Asimame kwa miguu yake bwana changamoto hazikosekanagi kwenye maisha
Kikubwa yuko huru na kazi zake mziki wake na kipato chake!